SAKATA LA TAJI LA MKOKO; DIWANI AIACHIA CCM LUGOBA
Na Tanpresstz, Lugoba
WAKATI kada wa CCM Agoustine John (Taji la Mkoko) aliyekuwa anatuhumiwa kuwatuhumu viongozi wa kata ya Lugoba, kushiriki kuachia watuhumiwa wanaoharibu miundo umeme ya shule, ‘akichomolewa polisi’ diwani wa kata hiyo anasema litashughulikiwa na chama.
Akiongea na shirika la habari vijijini Tanpresstz, Diwani huyo Rehema Issa Mwene amesema kuwa halizungumzii tena suala hilo, kwani amekiachia chama.
“Mimi sitaki kuliongelea jambo hilo tena litashughuliwa na chama na mimi sio msemaji wake, ukitaka ujue limefika wapi suala langu na Taji waulize viongozi wa kijiji”alisema Diwani
Julai 19,2223 kwenye mkutano wa kijiji cha Lugoba mwanachi huyo alitoa malalamiko yake kwamba vibaka wanavyoingia shule ya msingi Lugoba mara tatu wakiiba na kuharibu miundo umeme ya shule hiyo wanaachiwa kwa maelekezo ya viongozi kata.
Kauli hiyo ilimkera vilivyo diwani wa kata hiyo Rehema Issa Mwene aliyenyenyuka na kumkatisha kisha kumtaka adhibitishe kauli yake ya kuwatuhumu viongozi akiwemo yeye, kama akishindwa kufanya hivyo atalala sero.
“Ngoja siwezi kuvumilia sisi viongozi wa kata tutuhumiwe nikiwepo hapa, kwa kuwa amesema sisi viongozi wa kata asipodhibitisha kauli yake tutapelekana huko polisi atakwenda kuisaidia….sitakubali atakwenda huyu polisi sitakubali kudhalilishwa hadharani tena kwenye mkutano wa hadhara anatutuhumu viongozi kwamba tunaandika vimemo” alisema Diwani
Baada ya mkutano huo Taji alionekana na mtendaji kata Mwenyekiti wa kijiji cha Lugoba Zaituni Kaogo, kituo kidogo cha polisi Lugoba na kuambiwa mkuu wa kituo hicho, hayupo warudi Alhamisi saa tatu asubui.
“leo Alhamisi (jana) nilifika kituo cha polisi kama nilivyoambiwa jana nimeshangaa kumkuta diwani ameisha fika aliponiona akaingia moja kwa moja kwenda kuzungumza na OCS ‘mkuu wa kituo’baadaye na mimi nikaingia nikakuta nahojiwa kwamba kwanini nilitamka kwenye mkutano wa hadhara kuwa polisi waliaachia watuhumiwa kwa vimemo maanake ninawatuhumu kwamba walipokea rushwa,…
…mimi nikajijitetea kwamba mkutano ule ndio sehemu ya kutoa maoni na mimi niliuliza ili nijibiwe kwanini watuhumiwa wameiba mara tatu wakikamatwa wanaachiwa bila kufikishwa mahakamani wakati mtendaji kata yupo, kijiji yupo na diwani hawafuatilii,….baada ya kujieleza diwani ameanza kunilalamikia kwamba natumika kumchafua kisiasa wakati sijamtaja yeye”alisema Taji.
Taarifa zinasema waakati mahojiano yakiendelea viongozi wa Jumuiya ya wazazi CCM, walingia kituo cha polisi na kumuomba mkuu wa kituo awaachie waondoke na mtuhumiwa wakamshughulikie kisiasa.
“kabla sijafika kituoni nilimwambia mwenyekiti wa wazazi kwamba ninakwenda kufungwa wakati natetea elimu ambayo ipo chini ya jumuiya yake kwa hiyo nikitoka nitaongea mengi,…
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kata ya Lugoba Habibu Mzimba alipoulizwa na Mwana Blog alikiri kufika pale kituoni akiwa na katibu malezi (EMMAU) wake nakuomba suala hilo likamalizwe kisiasa.
“ni kweli tulimwambia OCS kwamba suala la wizi shuleni tumeisha lizungumza kwenye vikao vya chama kama huyu alienda kuongea kwenye mkutano wa hadhara tupe tumpeleke kwenye kamati ya maadili, kesi ya kisiasa haiwezi kuisha polisi” amesema Taji
hata hivyo mwanakijiji huyo ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri Jumuiya ya Wazazi amesema anataka ajue kero za kijamii kama hizo nani anapaswa kujibu wananchi bila kupelekwa polisi?
‘ Sitanyamaza’
Taji la Mkoko amesema kwamba hatanyamazishwa huku akiona miundombini ya shule inaibiwa watuhumiwa wanakamatwa wanafikishwa kwa mtendaji au kituo cha Polisi wanaachiwa.
“Mara ya kwanza nikiwa mwenyekiti wa kamati ya shule walienda wakatikisa waya mkubwa unaoingiza umeme shuleni ofisi ya mkuu wa shule ikaungua nilikuwa nimesafiri niliporudi nikawaambia nyaya zilichezewa….
‘Baada ya miezi miwili wale vijana wakaiba tena nyaya zikachunwa wakakamatwa nazo wakafikishwa kwa mtendaji baadaye polisi, wakubwa wakaingilia kesi ikaishia hapo, hawakuishia hapo wakarudi tena wakaiba nyaya walipokamatwa nasikia walipigwa faini kesi ikaishia hapo, juzi wamekuja safari hii wameng’oa hadi saketbreaka shule yetu haina umeme nisiulize”?amehoji Taji
Mwananchi huyo ameendelea kusisitiza kwamba anapaswa kupewa elimu ni maswali gani yanapaswa kuulizwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji ili ajue na nani anapaswa kuulizwa ili asiwauzi wakubwa.
Tanpresstz linaendelea na sakata hili.





