Mtoto wa miaka 4 adaiwa kubakwa Mogo, Kipawa
Njama za kupotosha ukweli zapangwa atoroshwe.
Na Tanpresstz,Kipawa
![]() |
| mtoto wa miaka 4 anayedaiwa kubakwa |
Taarifa zilizofikia shirika la habari vijijini,Tanpresstz zinahabarisha kwamba kumekuwepo na njama kubwa za kutaka kufifisha tukio hilo lililotokea Disemba mosi 2023 kuripotiwa kituo cha Polisi Staki shari Disemba 2.
![]() | |
| taarifa ya kitabibu iliyopelekwa kituo cha Polisi sitaki Shari ambayo inadai alichezwa tu kwa maelezo aliyopewa mlezi na Polisi. |
“Sisi kama viongozi wa Jumuiya tulipokea taarifa siku ikiwa imepita tulipofuatilia tukakuta huyo mtoto anaugulia maumivu huku walezi wake wakiendelea kumkanda na maji ya moto tukachukua jukumu la kumpeleka Polisi akapatiwe matibabu”anasema Forgeti.
“Mtoto wangu hajawahi kubakwa, nashangaa anayevumisha hayo mambo nikimjua atanilipa anatupa presha mimi na mama yangu kwani watu wanazidi kumiminika hapa, nimeenda hospitali wamesema alichezewa tu na watoto wenzake”alifoka Cesilia Philipo ambaye anadai ni mlezi wa mtoto huyo.
Wakati akiwatuhumu viongozi wa jumuiya ya wazazi
kwamba ndio wanasambaza taarifa hizo, katibu wa shina namba 9 lilipofanyikia
tukio hilo, Geofrey Rugeye anasema baada ya kupata taarifa hiyo alifika kwenye
familia hiyo siku ya Ijumaa jioni akakuta mtoto amelala kwenye mkeka, akawaambia wampeleke kituoni akatibiwe.
“Leo wanakana ,wanajaribu kuficha ukweli Jumamosi
iliyopita tulipokuja hapa walikuwa wanasema bibi yake alipoamka usiku alikuta
mtoto amelala akajiachia huku mbegu za kiume zinatoka sehemu za siri akamuita
mpangaji jirani akaja akadhibitisha kwamba ni kweli kesho nyake wakaanza
kumkanda na maji ya moto”amesema mjumbe kwa masikitiko
Aidha katibu wa Jumuiya ya wazazi tawi la Mogo yeye anasema alikuwa amesafiri aliporudi Ijumaa jioni akaambiwa hiyo familia na mhanga walifika kwake wanataka huyo mtoto awaonyeshe aliyembaka na kumharibu sehemu za siri.
“Mimi nashangaa wanasema kwamba mimi ndio natangaza, wakati wenyewe ndio waliyatoa nje wanaona yameanza kushughulikiwa wanataka kuficha ukweli huku wakipanga kumtorosha muathirika,..hata hiyo ripoti ya daktari hatujui kama ina usahihi”alisema Katibu wazazi.
![]() |
| Sesilia Philipo Mlezi wa muathirika anayekanusha mwanae kubakwa |
Tanpresstz imefanikiwa kuona taarifa ya uchunguzi kutoka kituo cha Buguruni ambayo daktari ameandika kwamba hakuona damu ikitoka kwenye sehemu za siri bila kujali kwamba huyo mtoto ameogeshwa tangu Disemba Mosi hadi leo Disemba 4 damu haiwezi kuonnekana.
katibu wa Jumuiya ya Wazazi anasema kwamba "Wanasema amechezewa tu na watoto wenzake hivi hii inaruhusiwa, ..watoto wenzake wangemchezea akandwe na maji ya moto, au kwasababu mtoto huyo ni wa kambo hana mtetezi? na kuna taarifaa kwamba anataka kutoroshwa"analalama
baadhi ya watu waliozungumza na Tanpresstz bila kutaja majina yao wameomba wadau wa haki za binadamu wamchukue mtoto wampeleke kwenye vipimo zaidi kwani anaonekana kuugulia ndani bila msaada wowote, huku walezi wake wakikanusha taarifa za kubakwa.
Labels: HABARI







