UBADHIRIFU CHUO KIKUU DARUSO UNATISHA
Na Mobini Sarya.
Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo kikuu Mlimani (DARUSO) inayomaliza muda wake, huenda wakafikishwa mahakamani kwa tuhuma za Kuhusika na Ubadhirifu wa Mamilioni ya Shilingi.
Hayo yalibainika jana kwenye kikao cha Mwisho cha Bunge (USRC) la serikali hiyo inayomaliza Muda wake kilichoitwa kwa dharurua na Spika wabunge hilo Kamazima Idd kwa ajili ya kujadili ubadhilifu huo.
Katika kikao hocho wabunge waalisommewa taarifa ya ubadhirifu wa Shilingi Milioni 34 unaodaiwa kufanywa na uongozi wa juu wa DARUSO, kwa kuandaa taarifa mbili tafauti zinazoelezea matumizi na kiasi cha Pesa kilichotumika.
Miongoni mwa ubadhirifu mbaya uliotajwa ni kiasi cha Shilingi milioni 6 zinazodaiwa kuchotwa Machi 3 mwaka 2006, wakati inafahamika kuwa Viongozi wa Serikali hiyo walaikuwa hawajaanza kazi.
Kabla ya kikao hicho kilichoketi kwenye Ukumbi wa TBA chuoni hapo, Spika alisoma Barua ya Rais wa DARUSO anayemaliza muda wake ambaye ndiye ni miongoni mwa wanaotuhumiwa na aliamua kuandika barua hiyo akidai kuwa hatambui hicho kikao kwa Bunge limekwisha vunjwa,
lakini katiaka barua hiyo alisaini kama Rais na kuzua maswali kama bunge limevunjwa kwanini amesaini kama Rais, baada ya Spika kusoma hiyo barua alionya kama kuna watu wameaandaaliwa kufanya fujo watashuighulikiwa kikamaulifu kwa ni bunge lipo kihali hadi Bunge jipya litakapoapishwa.
Katika taarifa iliyosomwa na mbunge mmoja ilionyesha kuwa waziri wa Fedha Mwakarukwa Kaptain alikuwa anapeleka bungeni kiasi kidogo kinachoonyesha matumizi ya Pesa huku kwenye Ofisi ya utawala wanakuwa wamemchota kiasi kikubwa cha Pesa.
Katika taarifa hiyo ulisomwa Waraka ulioonyesha kuwa Machi 2 Mwaka huu Daruso ilipeleka bungeni bajeti inaonyesha matumizi ya Mwaka mzima wa 2006 yalikuwa Milioni 18 matumizi ambayo wabunge waliyakataa kuwa Daruso hawezi kutumia kiasi kikubwa hicho hali iliyowatia wasiwasi wakaanza kufuatilia kwenye ofisi za utawala.
Hata hivyo Bunge hilo linalofahamika kama(USRC) limetupia lawama Utawala wa chuo kikuu ‘Chef Internal Audit’ C.I.A kwa kuzembea hadi Pesa nyingi kiasi hicho zikawa zinachotwa bila kuzibitiwa, jambo ambalo linatia mashaka kama C.I.A haikuhusika kwenye ubadhidhirifu huo.
Wakiachambaua namna ubadhirifu huo ulivyokuwa ukifanyika wametaja kuwa wakati taarifa za CIA zianonyesha kuwa walichota kwa kipindi cha Mwaka mzima shilingi milioni 34 kwenye lipoti waliowakilisha kwenye Bunge USRC na ikakataliwa inaonyesha kuwa ni Milioni 18.
Katika Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Daruso walitoa taarifa kwa USRC kuwa walitumia shilingi 500,000 lakini kwenye ofisi za utawala wa Chuo CIA ripoti inaonyesha kuwa walichota laki 900,000 kwa ajili ya kulipa mafundi lakini cha kushangaza hizo pesa hata mafundi wanadai hawajalipiwa, wakati huo mbunge mmoja alisema kuwa wao waliomba tenda hiyo wakaambia amepatikana mtu wa kurengenez kwa shilingi 300,000.
‘Sisi tunashangaa inawezekana hata kiasi cha pesa kilichotumika kwenye website ni chini ya laki tatu kwani sisi tuliomba hiyo tenda kwa kiasi hicho tukaambia amepatikana wa bei ya chini iweje leo tuambiwe walitumia laki
tisa?” alihoji
hasira zilidi kuwaka ukumbuni humo baada ya waziri mmoja kudai kuwa alikuwa anatumia pesa zake zaidi laki mbili kwa ajili ya mawasilino kwa maelezo kuwa atalipwa lakini hajalipwa huku katika ubadhirifu inaonyesha shilingi 3,000,000 zilitumika katika Mawasilino lakini kwenye bunge waliambiwa ni 560,000.
Katika uchunguzi huo ripoti moja ya bunge ilionyesha kuwa viongozi wa vitengo vya Daruso walitumia 550,000 lakini kwenye ripoti ya CIA inaonyesha kuwa ni shilingi 1,100,000 na kwenye stationari inaonyesha kuwa walitumia 920,000 huku wakidanya bunge kuwa walitumia 568,000.
Ubadhirifu mwingine uliobanika ni kiasi cha shilingi milioni 3000,000 zinazodaiwa kutumiwa na wabunge kwa mawasiliano kumbe ni uongo huku kwenyeb taarifa ya wabunge wakidai ni shilingi 1,032,000 pesa ambazo wabunge walisema lazima wazilipwe.
Baada ya wabunge kusomewa mlolongo wa
Ubadhirifu walinza kuchangia mmoja moja hatua za kuwachukulia viiongozi hao ambao waligoma kuhudhuria hicho kikao huku wengi wakionyesha nia dhabiti ya kutaka wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria na kitaaluma.
“Spika ni vigumu Serikali kujisafisha na hili kwanza tumedanganywa na kuonekana wajinga kwa kuturetea ripoti ambayo siyo inabidi tuwachukulie hatua zinazopaswa ikiwemo kutangazwa kwenye mbao za matangazo wafahamike kuwa wao ndio wabadhirifu sio sisi”alisema mmoja.
Baada ya kila mmoja kuchangia kwa jazba kuonyesha jinsi walivyiokerwa na wizi huo kikao kiliaziamia kwam kupiga kura ya pamoja kuwa Uongozi wa chuo utaarifiwe kwa hatua za kisheria , wapewe siku saba wawe wamelipa pesa hizo, vyeti vyao vya uongozi na Elimu ya chuo kikuu vizuiliwe, Akaunti zao zifungwe, chuo kikuu kiwaandikie Ripoti mbaya kwenye vyeti vyao, na wapashwe kizimbani.
Wanaotuhumiwa katika ubadhirifu huo ni rais anayemaliza muda wake Mwita Magesa, Waziri Mkuu wake Mathias Renatus na Waziri wa Fedha Mwakarukwa Kaptain ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kudanganya, kutoa taarifa za uongo, kujaribu kutoa rushwa ili wasichunguzwe na kuiba mali za umma M.34.
Uongozi mpyab unaotarajiwa kuaopishwa keshokutwa umeombwa kulishughulikia swala hili kikamilifu ili liweze kuwa funzo kwa wengine kwa ni Daruso imechafuliwa kwa kudaiwa kula pesa wakati walikuwa wengine walikuwa wanatumia pesa zao mfukoni.
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtmypk9RABCvNqwT3GVPCFK8-Dx6lwGxRUsy-IjdulqbHPyycUoE6LvJKvlO2cPhWdLzz63MPoS9QoKUVtzNfA_EFMH8hMf5i2T_9rW6FuLMbR-c7UMjhyC5lGPtMcoxu2DaG14U_2hGGC/s1600-h/pesa1.jpg">
HZI PESA NDIZO HUPINDISHA SHERIA NA KWELI
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_H2RdBqI04kZm8eFmvGr-AP0CJdlX6a23U00mSSIPlCYwzhg-EeklbgcGMnmOqeLLJRxJntbl7oNkrw4NI-vif8Asr8b-3ngVVf8nEWWy6q_0g0GpSsRewaTKd33hN87Vp1mCA1GDjCHV/s1600-h/pesa.jpg">
Na Mwandishi Mwetu
SHERIA za nchi zimedharauliwa, Mahakama Kuu imebakwa na nchi imevuliwa nguo na kubaki uchi huku utawala wa sheria ukibaki na aibu kubwa isiyositiriwa, na iliyoweka historia katika taifa letu, huku watawala wakibaki na kigugumizi wasipate la kujibu baada ya kuonekana mtunga sheria ndiye mvunja sheria.
Hayo matukio yote yamekuja baada ya aliyekuwa kiongozi wa umma kushitakiwa kwa kosa la kuua kisha kuachiwa kwa dhamana ndani ya siku 120, kwa madai kuwa aliua bila kukusudia na kuwaacha watu wakijiuliza maswali mengi kuhusu jinsi kiongozi huyu alivyoshughulikiwa haraka na kutoka kama kweli taratibu zilifuatwa.
Aibu imekuwa kubwa zaidi na isiyofutika baada ya kiongozi huyo aliyewahi kuwa mbunge na mtunga sheria za nchi kupitia Jimbo la Ilala na baadaye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kupitishwa kwenye mlango wa majaji wakati anaingizwa Mahakama Kuu kupewa dhamana, kitu ambacho hakijawahi kutokea, huku akipewa ulinzi sawa na rais.
Katika kuonyeha kuwa ‘mtunga sheria ndiye mvunja sheria’ na sheria za hapa Tanzania hutungiwa ‘wendawazimu’ tu huku wenye akili wakizivunja, ndugu wa mtuhumiwa wa mauaji waliwageuza waandishi wa habari waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo kuwa ndio watuhumiwa na kuanza kuwaadhibu mithili ya vibaka, wakisaidiana na askari polisi!
Matukio hayo waliyoyafanya si mara yao ya kwanza, ilikuwa ni kuendeleza ufedhuli waliokuwa wameanza nao tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, pale walipoanza kuwazuia waandishi wa habari wasifanye kazi zao, kwa kuwatukana na kuwamwagia maji ya upupu, na siku zingine kumfunika mtuhumiwa kanga au kumletea kofia aina ya ‘pama’ ili ajifunike kuepuka aibu ya jamii, baada ya ‘kumuua bila kukusudia’ dereva wa daladala, Hassan Mbonde, ambaye uhai wake ulikatishwa na risasi zilizotua kichwani.
Katika kesi hii inayomkabili kiongozi wa umma, tusingependa kuijadili kutokana na kuwa ipo mahakamani, lakini jinsi mwenendo wake unavyokwenda na matukio yaliyoambatana nayo, hiyo kesi hakuna kizuizi chochote kinachoweza kuzuia isiandikwe wala kuzungumzwa mitaani, kwani hadi sasa kila mmoja anayeifuatilia anajua kinachofanyika au kuendelea.
Mwenendo mzima wa kesi umekuwa ukiacha maswali mengi kuliko majibu, huku kila kukicha haki na sheria vikikiukwa kwa uwazi bila kuhojiwa, na hali ilianza kushangaza katika Mahakama ya Kisutu pale ndugu wa mtuhumiwa walipofanikiwa kumfunika kanga ili asipigwe picha huku polisi wakichekelea, maswali yaliyoibuka hapa ni kwamba ndugu zake walipataje nafasi ya kumkaribia mtuhumiwa wa mauaji kiasi hicho ikiwa mahabusu wa kawaida tu ndugu zao wanazuiliwa kuwasogelea pale wanapofikishwa mahakamani?
Je, katika hili polisi walikuwa wanajua wajibu wao kwa kuwaruhusu ndugu wa mtuhumiwa wa mauaji kumsogelea, wangewezaje kumzuia mtu mwingine ambaye angejipenyeza kama ndugu wa mtuhumiwa kumbe akiwa na lengo la kumchoma kisu mtuhumiwa, ilikuwaje polisi katika Mahakama ya Kisutu waendele kuwashuhudia ndugu wa mtuhumiwa wakiwafanyia waandishi vitendo vya dharau hadi pale hakimu alipoingilia kati na kusema wazi kuwa polisi walikuwa wamezembea kupita kiasi?
Kama kuna mkono wa mtu unatumika katika kesi hii, basi ulianza kutumika kikamilifu katika Mahakama ya Kisutu na polisi walilishwa limbwata wakawa kama chatu aliyemeza mzoga na kulala asijue la kufanya huku wakiangalia bila aibu vitendo vya uvunjwaji wa sheria za nchi.
Kama hiyo haitoshi, inafahamika wazi kuwa mbele ya pesa hakuna kinachoshindikana, hali ilikuwa mbaya zaidi walipomfikisha mtuhumiwa Mahakama Kuu, kwani waliamua kutumia mlango unaotumiwa na majaji pekee kwa kumpitisha mtuhumiwa, wakati wanajua kuwa huo mlango hata mfanyakazi wa mahakama hiyo haruhusiwi kupita, mlinzi wa mahakama alipojaribu kuwazuia wakamnyanyasa kwa kumsukuma, hadi wakafanikiwa kutizima azima yao.
Kitendo kilichowakasirisha majaji wa mahakama hiyo na kuamua kumtaka Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, atoe maelezo, ndani ya muda ambao mtuhumiwa alipewa dhamana katika Mahakama Kuu na ndugu zake waligeuza eneo hilo kuwa uwanja wa masumbwi kwa kuwaadhibu waandishi mbele ya Mahakama ya haki huku wakiimba kuwa nchi hii ni yao, kama waandishi walikuwa hawawajui watajua sasa, na kuwajeruhi waandishi kadhaa.
Baada ya kuangalia mwenendo mzima wa hii kesi, wananchi wameingiwa na hofu kama kweli haki itatendeka kuhusiana na kesi hii.
Siku chache tu baada ya Ditopile kushikiliwa na polisi kwa kuua dereva Novemba 8 mwaka jana, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Rais Kikwete amekiri kuwa Dito alikuwa mwanamtandao wa kuaminika, amesononeshwa kwa tukio hilo, na hajui afanye nini, akasema anaachia sheria ifanye kazi yake.
Kutokana na Tanzania kuwa na mfumo mbaya wa sheria za kulindana kumesababisha mtuhumiwa wa mauaji kubadilishiwa kesi nje ya Mahakama Kuu kupitia dirisha la nyuma na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia kwa muda wa siku 120 tu.
Huku watu waliokamatwa kwa kuhisiwa tu wengine kwa makosa madogo madogo wamesota jela na wengine kufia mahabusu bila kesi yao kusikilizwa wakiambiwa kuwa upepelezi bado haujakamilika, na kunyimwa dhamana bila maelezo ya msingi huku wakinyimwa nafasi ya kuonana na ndugu zao, wapo wanaolalamika kunyimwa huduma ya matibabu kutoka kwa ndugu zao.
Kuachiwa kwa dhamana kwa mtuhumiwa wa mauaji kwa upande wa pili kumefungua njia ya ukombozi na mapinduzi kutokea magereza, tukio hilo limehitimisha yale manung’uniko ya muda mrefu kuwa magereza Tanzania ni sehemu ya kuwatunzia walalahoi huku wenye nguvu wakiachiwa bila kutiwa hatiani hata kama kuna ushahidi wa wazi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa kwa kukusudia.
Hapa Tanzania imekuwa ni kawaida kwa tajiri anayetenda kosa, mfano la kuua kuambiwa kajeruhi, lakini mlalahoi akijeruhi anaambiwa kaua, kibaka anauawa, mzururaji anaandikiwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kunyimwa dhamana wengine kubambikiziwa kesi wasizozijua huku wakiambulia kipigo cha maumivu ili wakubali makosa bandia.
Mgomo wa siku kadhaa wa mahabusu uliotawala katika magereza ya maeneo mbalimbali nchini, umeashiria mwanzo mpya wa mapinduzi ya haki na ni mwanzo wa aibu kubwa kwa taifa kama letu linalojivunia utawala bora wa sheria na kulinda haki za binadamu.
Wiki za hivi karibuni zimegubikwa na aibu kubwa kwa taifa, mahabusu wakitaka haki ambayo wameikosa siku nyingi, wapo waliokamatwa kwa kuiba kuku wamekaa rumande kwa muda mrefu wakiambiwa upelelezi bado haujakamilika, lakini wengine wanakamatwa kesho yake kwa mauaji au kulawiti watoto wanadhaminiwa.
Tumesikia katika gereza la Isanga, Dodoma wafungwa waliokamatwa kwa kosa la unyang’anyi baada ya kukaa rumande bila dhamana sasa wamebadilishiwa kesi na kuwa ya kuua na kule Serengeti Polisi walikamata madumu ya maji wakadhani ni mafuta ya dizeli wakambambikizia mwananchi mmoja wakakaa naye kituo kikuu cha polisi kuanzia asubuhi hadi jioni bila dhamana wakitaka rushwa hadi mwenye madumu alipojitokeza jioni na kuomba madumu yake, polisi wakashtuka kuwa kumbe ndani kulikuwa na maji.
Kesi hii ya Ditopile imetufanya tufahamu kuwa kumbe kuna wananchi na ‘walanchi’, tumefahamu kwamba kuna watu wameua lakini hata mahabusu wengine hawakufika, miongoni mwao ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoani Dar es Salaam (RCO), Abdallah Zombe, upelelezi wake ulikamilika ndani ya siku 150 yeye yupo rumande.
Mwingine ni mtoto wa Balozi Rupia aliyetuhumiwa kwa kosa la mauaji na kuachiwa baada ya siku tisa.
Aidha, mtoto wa Kingunge Ngombale-Mwiru pia inadaiwa aliwahi kuua, lakini hata hakufika mahakamani, na mtoto wa Sumaye naye alituhumiwa kwa mauaji lakini wote hawa wanatesa uraiani.
Kutokana na mwenendo usiofaa wa kuendesha kesi nchini, wananchi wote wanapaswa kuungana kupinga haki kutolewa kwa kubaguana, pia tunapaswa kuungana na mwanaharakati Christopher Mtikila, kuiomba mahakama kufuta nafasi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, kwani inaonekana ipo kwa ajili ya kuwalinda vigogo wachafu, kama kuna sheria mbaya ya nchi hii inapaswa kulaaniwa ni sheria inayomtambua Mwendesha Mashitaka (DPP).
Mwendesha Mashitaka ni mtu anayebaka haki za majaji kutokana na kupewa uwezo wa kuruhusu kesi iende mahakamani au isiende na kupewa uwezo wa kuibadili kama anavyopenda, na hii nafasi ilianzishwa na wakoloni ili kujilinda dhidi na ufedhuri waliokuwa wanawafanyia Waafrika, hata walipokabidhi madaraka, wamewaachia watawala wetu ndio wanaitumia kujilinda wakituhumiwa kuwa wamekula rushwa, wanamkimbilia mwendesha mashitaka anawabadilishia kesi.
Mkurugenzi wa Mashitaka anaingilia uhuru wa mahakama na kuwafanya majaji wawe vibaraka wake kama yeye alivyo kibaraka wa viongozi wa serikali, haiwezekani abadilishe mashitaka yawe ya kuua bila kukusudia nje ya mahakama halafu anawapelekea majaji wa Mahakama Kuu wagonge muhuri wa kumpa dhamana mtuhumiwa bila kuona kesi yake kwanza kama ni hivyo basi hata dhamana angetoa yeye.
Sheria hii anayoitumia DPP kama angekuwa anaitumia kwa wananchi wote kusingekuwapo msongamano wa wananchi mahabusu, kwani wengi wametenda makosa bila kukukusudia, tangu waandishi wamepigwa na kuharibiwa vifaa vyao polisi wameshindwa kuwachukulia hatua wale waliohusika, kitu kinachotushawishi tuamini kuwa lile tukio liliratibiwa kikamilifu na polisi.
Kesi hii imetufundisha mambo mengi, imetuonyesha jinsi ndugu wa watawala wanavyotenda makosa kwa makusudi wakitegemea kuwa watasaidiwa na wakubwa wao, na jinsi walivyoweza kuidhalilisha serikali ambayo imechaguliwa na wananchi, lakini hii haitavumilika siku zote, waandishi wameonyesha nia ya mapambano, pia mahabusu wamebipu, tunawasubiri wananchi waungane na wanaharakati kufanya maandamano ya kupinga kubaguliwa wanyonge na kukandamizwa haki zao.
Wiki ijayo nitaeleza jinsi mwendo mbaya huu wa kesi ulivyoanza kujionyesha kuwa mnyonge hana haki, nitaonyesha jinsi kiongozi wa nchi anavyotakiwa awe asiyekuwa na ubia na mtu kwenye madaraka yake.
Kwa mara ya kwanza historia ya taifa letu imetiwa doa kubwa na viongozi wenyewe serikalini, watuhumiwa wahukumiwe kulingana na sheria si utashi wetu kisiasa!
Web.www.mobinday.blogspot.com email.mobinsons@yahoo.com
Mwisho