Wednesday, July 18, 2007

विकेंदी ही safi

Kanda ya Mashariki kambini Julai 22

WAREMBO watakaoshiriki katika shindano la kumsaka Miss Kanda ya Mashariki wanatakiwa kuripoti kambini Julai 22 mwaka huu, imefahamika juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana waandishi wa habari Dar es Salaam Mratibu wa shindano hilo, Asha Baraka, alisema warembo wote wanatakiwa wataweka kambi katika hoteli ya Landmark ulioko Ubungo jijini.
Asha ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), alisema kwamba warembo hao kuwa ni kutoka katika mikoa ya Mtwara, Morogoro, Pwani na Lindi.
Warembo wanaotarajiwa kushindana ni Saada Hashim, Mariam Msangi, Anna Mkumbo, Rehema Said, Eva Evans, Christian John, Pendo Ernest, Catherine Shirima, Fatuma Kisoki amoja na wengine waliofahamika kwa jina moja kila moja ambao ni Sophia, Clara, Anna na Rehema.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 28, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Landmark, yanadhaminiwa na Kituo cha televisheni cha Channel ten, Vodacom, Redio 88.4 Clouds FM, Redd’s na Landmark.


Respect yampeleka Matonya London

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Kampuni ya Respect Entertainment ya jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kumpeleka msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Issa Shaban a.k.a Matonya nchini Uingereza kwa shughuli ya kurekodi nusu ya albamu yake mpya anayotarajiwa kuitoa baadaye mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mohammed Abdallah Kiumbe ‘Chief’, alisema kuwa amefarajika kampuni yake kutimiza malengo.
“Tumeanza na Matonya, baadaye watafuata wengine. Manaake mara nyingi tumezoea kuwapa shoo za nchi za Kiafrika, lakini sasa tunawavusha bahari kubwa waweze kupata exposure (uzoefu) wa kimataifa.
“Atakuwa huko kwa wiki tatu kabla ya kurudi na kuendelea na shoo kibao za hapa barani kwetu (Afrika),” aisema Kiumbe ambaye amekuwa akimsaidia kwa karibu kinara wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Ally Choki Rwambo.
Alisema kwamba awali kampuni yake ilianza kudhamini kazi za wasanii mbalimbali ambao hawakuwa na uwezo kwa mtazamo wa kukuza vipaji vyao, lakini, sasa imeamua kupanua zaidi wigo wake kwa kudhamini safari ya Matonya kwenda London kurekodi nusu ya nyimbo zake za albamu mpya.


Makamba, Tibaigana wamsifu msanii

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Rajab Makamba na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaamm, Alfred Tibaigana wamemmwagia sifa msanii nyota wa kuigiza sauti za viongozi na watu maarufu Steve Mengele a.k.a ‘Steve Nyerere’ kwa kufanikiwa kutengeneza video ya DVD yenye takriban shoo zake zote.
Akiwa bungeni hivi karibuni, msanii huyo alisifiwa na Makamba alipokutana naye kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma ambapo alimtania kwamba:
“Steve Nyerere unakula mjini kwa kutumia sauti yangu... ni vizuri... lakini, tumia vizuri kipaji chako, kinaweza kukusaidiam:.
Sanjari na Mheshimiwa Makamba,” alisema Makamba.
Kadhalika, Kamanda Tibaigana naye alimdhihaki Steve kwamba hana budi amlipe kwa kuigiza sauti yake huku akiliingizia taifa pato kwa kulipa na VAT pia.
Kama haitoshi, naye alimsifu kwa ubunifu wake wa kutengeneza video hiyo inayoitwa Respect of Nyerere.


Wasanii mahiri ziarani Zambia

KUNDI la ngoma za Asili Afri Arts la mjini Morogoro pamoja na kundi la sarakasi la JKT Makao Makuu yanatarajiwa kushiriki sherehe za sikukuu ya wakulima nchini Zambia zinazotarajia kufanyika kwa siku nne kuanzia Agosti 2, mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa Shirikisho la wasanii Tanzania (SHIWATA), Taalib Kassim alisema mwaliko huo umehusisha pia wanamuziki 11 kutoka makundi mbalimbali ya muziki hapa nchini.
Taalib aliwataja wanamuziki hao na makundi yao kwenye mabano ni pamoja na Mafumu Bilali (African Arts), Said Mabera, Roman Mng’ande, Muhidin Ngurumo (Msondo), Andrew Damas na Hamza Ally (Polisi Jazz).
Wengine ni pamoja na Abdul Salvador ‘Father Kidevu’ (Hisia band), Shabaan Dede, Abbas Jeff (Sikinde), Mwangomolo Mwangomolo (JWTZ) na Sizza Mazongera (Segere Wazazi).
Taalib alisema ziara ya kusherehekea sikukuu hiyo nchini Zambia ni kuonyesha namna Serikali inavyojali SHIWATA na wasanii kwa ujumla.
Aidha Taalib alisema safari ya kwenda Zambia itaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa taratibu zote zimekamilika.

Mwisho

Jebby afyatua Wamadaha

Victor Masangu

MKALI wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika miondoko ya ‘Bongo fleva’ Jeneby Mbaraka ‘Jebby’ baada ya kimya kirefu ameachia kibao chake kipya kinachotambulika kwa jina la ‘Wamadaha’.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, Jebby alisema ya kuwa wimbo huo tayari ameshakamilisha kuurekodi na umeshaanza kusikika katika vituo mbali mbali vya redio hapa nchini.
“Mtu wangu nafahamu wapenzi wangu walikuwa na maswali mengi juu ya ukimya wangu, lakini nilikuwa najiweka sawa ili niweze kutoa kitu ambacho kitaweza kufanya vizuri katika anga hiii ya muziki kwani kumekuwa na ushindani mkubwa na ongezeko la wasanii katika kila pande,” alisema Jebby.
Jebby alisema kwamba wimbo huo utakuwa ni tofauti ukulinganisha na zile za awali zilizotangulia kwani ameamu kuongeza vionjo zaidi ili kuweza kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake.
Msanii huyo aliyejipatia umaarufu katika anga ya muziki kutokana na wimbo wake wa Swaiba ambao ulionekana kufanya vizuri katika kila pande pamoja na ule wa Marehemu ameacha orodha ambao tayari ameshakwisha uweka ndani ya luninga..

Mwisho

ACB yamwaga zawadi Dar
BENKI ya Biashara ya Akiba (ACB), imewakabidhi zawadi washindi sita wa droo ya pili ya bahati nasibu, ikiwa ni mojawapo ya shughuli za shamrashamra ya kusheherekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye ofisi za Makao Makuu ya benki hiyo inayojulikana kwa jina la Tawi Branch iliyopo Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa benki hiyo, Godfrey Masawe, aliwataja washindi hao kuwa ni mshindi wa kwanza Lotti Zakaria aliyejinyakulia fedha taslimu sh 400,000.
Mshindi wa pili ameibuka Kissensi Mussa aliyepata zawadi ya jokofu na mshindi wa tatu Zaina Kitimla ameondoka na Televisheni aina ya LG.
Wengine ni Ngowi Grace aliyekuwa mshindi wa nne na kupata zawadi ya deki aina ya LG, wakati mshindi wa tano Boniface Mariki alipata feni huku mshindi wa sita Hamoud Yahaya alijishindia zawadi ya pasi.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao, Meneja wa Tawi Branch, Vincent Anthony aliwataka watu kundelea kufungua akaunti katika benki hiyo ili waweze kushinda zawadi ya gari aina ya Toyota Corolla katika droo kubwa ya mwisho inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.

MWISHO.

uchumi

UCHUMI
Mwisho wa ubaya CCM ni Aibu Kigoma.

NA Mobini Baranyikwa.

Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa iliyojaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa na wingi wa Raslmali za kutosha kuwafaa wakazi wake.

lakini kwa makusudi na bila sababu za maana mkoa huo ambao upo mgaribi Mwatanzania umeachwa bila kuendelezwa na umekuwa kama umetelekezwa.

baadhi ya hazina ya utajiri unaostirika hapo ni, aina mbalimbali za madini yanayopatikana Kongo, Ardhi nzuri ya rutuba inayostawisha kila aina ya mazao kama michikichi inayotoa mafuta ya mawese, mihogo, tumbaku, Miwa, Pamba ,ndizi, Mahindi na aina mbalimbali za mistu ya miti.

ukifika kigoma wilayani kasulu ukapita njia inayoelekea Burundi utajiionea jinsi mkoa huo unavyopendeza uoto w a asili milima na mabonde yenye vijito vinavyotiririka majira majira yote ya kiangazi.

“ni uwanda muzuri sana unafaa kustawisha miti ya kila aina kama ile ya kutengeneza karatasi na njiti za kibeti sijui kwanini serikali haifanyi hivyo” alisema mtu mmoja aliyekuwa amekaa karibu nami tukiwa kwenye gari tunaelekea kijiji cha Mayovu kasulu.

eneo hilo lina hekari za vilima Tambarare ambazo kama serikali ingeamua kupanda miti kila inaadhimisha siku ya mazingira duniani nchi yetu ingewedza kuwa na msitu mkubwa wa kujivunia kwa kupanda miti zaidi ya milioni 50.

kigoma ni miongoni mwa sehemu Afrika mashariki na kati zenye kubeba historia na kumbukumbu kamili ya wakoloni waliolitawala bara letu la Afrika.

ni mkoa ambao hadi kufikia mwanzoni mwa karne ya 19 tayari ulikuwa umekwisha jengeka hasa katika eneo la Kigoma ujiji kulikuwa tayari miundombinu imara kama Bandari, Reli na Barabara.

ni mji ambao leo hii wakazi w ake wanajutia wakoloni kuondoka kwani leo hii baada ya jiji kama la Arusha au Mwanza tungekuwa na jiji la Asili Ujiji lakini sasa mji umekuwa kama maghofu na makambi ya wakimbizi.

kwani mji huo ndio ulikuwa kituo
kikuu Afrika ya kati ambapo watumwa kutoka nchi za maziwa makuu walikuwa wanakusanyikia pale Ujiji kabla ya kupelekwa Tabora na hatimaye Bagamoyo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda ulaya.

ni katika miaka hiyo biashara ya chumvi kutoka Uvinza ilikuwa inafanyika hadi leo hii kigoma Ingekuwa kitovu cha biashara Afrika ya kati na ungekuwa na miundombinu imara zaidi.

kutokana na Serikali kushindwa kutumia Raslimali za mkoa huo kwa manufaa ya watu wa kigoma hata pale historia inapotajwa, wakazi wake wamekuwa wakiona kuwa wametelekezwa na kufananaishwa na wakimbizi huru ndani ya nchi yao.

utakuta serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi CCM inatenga PESA za kwenda kununua wananchama wa vyama vya siasa wakiwemo viopngozi waliochaguliwa na wnanchi kihalali lakini sio kwa ajili ya kutenga pesa kwa ajili ya kusaidia mkoa huo.

ukweli huo unafahamika baada ya Rais Mwenye majukumu ya kukomboa nchii alipokwenda kigoma na Kupokea vbiongozi wa Serikali za mtaa waliokuwa wanahamia CCM huku akiwa amefanya Ziara ya kiserikali kitendo ambacho ni sawa na rais kuvunja katiba kwa kushiriki kuvunja serikali iliyochaguliwa na wananchi.

ingawa wenyeviti wanne wa vyama vya Siasa waliofanya ziara yao hivi karibuni Kigoma walifaniwa kuwarejesha baadhi ya viongozi waliokuwa wamehama lakini, ikiwa mkurugenzi wa uchaguzi atashindwa kukubaliana nao utaitishwa uchaguzi mdogo hali itakayolazimu zitumike pesa zingine.

lakini hiyo haikuishia hapo kwani siku chache baada ya viongozi hao kuondoka hapo kigoma kuelekea Kagera Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Mkamba alifika kigoma na kudaiwa kununua kijiwe kimoja maarufu kama Urusi ambacho kinawafuasi wengi wa CHADEMA.

Baadhi ya viongozi wa kishna hicho wakiwasiliana na viongozi wa Upinzani walipokuwa Mkoa wa Kagera waliwaambia kuwa wamepewa shilingi milioni 16 kwa ajilinya kushusha tu Bendera ya CHADEMA na kupandisha ya CCM ili kumfurahisha Makamba na chama chake.

aliposikia habari hiyo Mwenyekiti wa CHEDEMA Freema Mbowe alinukuliwa akisema kuwa ‘CCM inatukumbusha huko nyuma kwa kufanya biashara ya wanachama sawa na wakoloni waliponunua w atumwa’


hiyo ndio hali ya siasa na kijamii KIGOMA , hadi leo hata baada ya uhuru biashara ya watu inafanyika , kiongozi anaandaa bajeti anakkwenda kigoma kununua w atu wala sio kununua mawese ambayo yanazalishwa huko na Serikali imeshindwa kuwatafutia wakulima soko la uhakika.

hali inavyoonekana katika mkoa wa Kigoma inadhihirisha ule usemi unaosema kuwa kufa kufaana kwani kama leo yasingekuwepo Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa huduma katika makambi ya wakimbizi na jamii ya watu wa Kigoma leo kigoma ingekwa Pori la watu waliotengwa.

ni kutokanakana na mashirika hayo kama UNHCR, UNICEF ,WF na mengine yameweza kushirikiana kwa kujenga na kukarabati Barabara zote katika wilaya za Kasulu, Kibondo na KIGOMA Pamojana na viwanja vya ndege ambazo zinatua katika eneo hilo kwa ajili ya misaada ya wakimbizi.

zaidi ya hapo Wakazi wa Kigoma wanasema hata pato lao linategemeana na bajeti ya mashirika hayo yanapokuwa yametenga bajeti kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi , kwa mfano zinaweza kutengwa shilingi bilioni 2 kwenda kwa wakimbizi hizo pesa zitatumika kununua chakula , vyakula , vifaa vya ujenzi wa mahema hata watoto kununuliwa nguo na wale waakimbizi w enyewe hufanya biashara kutokana na hali hiyo pesa huwa kwenye mzunguko ambao huwafikia wakazi.

kitu kingine kinachoonekana kuwa kigoma imesahauliwa na mzunguko wake wa hela ni mdogo ni jinsi hata pesa za eneo hilo zilivyotafauti na eneo lingine, tafauti kwa maana ya uchafu na kuzeeka, pesa za kigoma ni ushahidi mwingine kuwa mkoa huo upo kama kisiwa ukipeleka noti mpya pale ukaiwekea alama baada ya mwaka ukirudi unaweza kuipata.

kutokana na mawasilino ya kutoka eneo moja kwenda jingine wananchi hawana desturi ya kusafiri kutokana na miundombinu nmibovu inayosababisha kupanda kwa nauli kwa kiasin kinachowashinda wakazi kumudu.

wananchi hao wanazidi kutengwa mno na Sehemu nyingine ya Tanzania hata kwa habari na mawasilino magazeti yanafika kule baada ya wiki moja tangu yasomwe kwa maana nyingine ni kwamba wanapekewa mabaki yaliyosomwa sehemu nyingine.

kwa mfano tulifika kigoma siku ya jumanne tukakuta magazeti ya ijumaa ndio yanasomwa hadi tunaondoka alhamis tunaacha wanasubiri Treni iwaletee magazeti mengine.

ukiondoa kiwanda cha kuzalisha Chumvi cha Uvinza ambacho kimetoa ajira kiasi hakuna tena kiwanda katika eneo hilo hata cha kusindika Minofu ya Samaki ambazo zinapatikana katika ziwa Tanganyika lenye kina kirefu Barani afrika na hazina ya samaki wa kila aina.

Wakati mkoa huo unayorutuba na eneo la kutosha kwa ajili ya kuzalisha tani za vyakula za kutosha kama zao la Mhogo kwa ajili ya kuweka akiba ya kujilinda na Njaa inayotishishia eneo la Ukanda wa Afrika mashariki kutokana na kukabiliwa na ukame wa mara kwa mara, serikali yetu haina habari hiyo.

Ni jambo la kushangaza kuona serikali ikitoa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo kwa baadhi ya mikoa kama Mbeya na kuacha mkoa Kigoma ambao sio tu kusahauliwa kila nyanja bali hata bei ya pembejeo za kilimo ni ghali kutokana na usafiri wa kwenda huko.

Wakazi wa Kigoma wanasema kuwa hawashindwi kulima mazao mengi kama Mbeya bali kikwazo ni kwamba wapi watauza mazo yao, kwa mfano zao kama la Nyanya linastawi huko lakini nyanya ni zao linalofahamika kuwa likishaiva halivumili kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu wafanyabiashara huogopa kwenda kuchukua huko.

Hali kama hiyo ilitakiwa serikali kujenga kiwanda cha kusindika Nyanya na kusafirisha zikiwa tayari kwenye makopo kwenda Sokoni kama Mwanza ,Arusha , Dar es Salaam na nchi za kongo na Burundi, kiwandahichon licha ya kumsaidia mkulima kupata soko la Nyanya wananchi wengi wangeajiliwa.\

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, na Mwanauchumi aliyebobea Pro.Ibrahimu Lipumba baada ya kuutembelea mkoa huo alisema kuwa kama Serikali ingekuwa na Mkakati wa kusaidia wananchi wa Kigoma ingehamasisha Kilimo cha Mhogo kwa wingi ili uuzwe China.

Lipumba alisema Nchi ya China kwa Mwaka inahitaji zao la Mhogo tani Milioni moja kwa ajili ya kuchanganya na Petroli ili kuepuka uharibifu wa Mazingira unaotokana na Moshi wa Magari, kutokana na zao la mhogo tungeweza kubadilishana na pembejeo za Kilimo kama matrekta na majembe.

Vile vile wakati umoja wa mataifa unaagiza chakula kutoka nje kwa ajili ya kulisha wakimbizi nchi yetu kupitia mkoa wa kigoma ingeweza kuzalisha chakula mbalimbali kama ndizi, Viazi na mahindi kwa ajili ya kuwauzia.

Kutokana na hali hiyo Kigoma ingeweza kunufaika kwa kujengewa sekondari bora kila kata na Walimu wazuri wenye uzoefu tafauti na sasa ambapo, watoto wa kigoma wanapata bora elimu sio elimu bora.

Katika swala hilo la Elimu Kigoma iko Nyuma sana hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia kutoa takwimu za kushangaza pale aliposema kuwa, Mkoa wa Kilimanjaro wenye wakazi Milion 1.4 unasekondari zaidi ya 270 wakati kigoma yenye wakazi M. 1.6 inasekondari 80 tu kati ya hizo ikiwamo moja ya seminari.

Hata katika uwiano wa kiutawala kigoma inaonekana kusahauli
iwa pale inapoonekana mkoa huo ukiwa na wapigakura zaidi ya milioni moja hauna hata Waziri mmoja kuna manaibu waziri wawili, wakati Kilimanjaro yenye Wapigakura chuni yake inamawaziri zaidi ya watatu na manaibu waziri .

hali hiyo inatafsiriwa kisiasa na wakazi wa mkoa huo kuwa kama wammetengewa sawa na wakati Fulani wapemba waliwahi kulalamika kuwa pamoja na kisiwa cha pemba kuwa na wabunge wengi hakuna waziri anayetokea kule.

Kutokana na hali hiyo wakazi wa Kigoma wanaona Ziwa Tanganyika kama Kikwazo kinachowabana waendelee kuwa chini ya utawala wa Tanzania vingenevyo huenda wangekuwa Kongo kutokana na wanavyotengwa.

Wakitoa maoni yao wanaona kuwa ni bora wangekuwa sehemu ya kongo kwani Seerikali ya Tanzania huakumbuka wakati wa Uchaguzi tu ndio magari ya wakubwa yenye namba za STJ huonekana zaidi ya hapo kigoma ni kama hame.

Hali kama hiyo inaonekana tunapotaza kwa undani miundombinu tatizo kama la umeme kwa Kigoma ni sawa na Kilema kwani tangu tupate uhuru karne ya 20 hadi leo karne ya 21 hawajawahi kupatiwa Umeme wanategemea Jenereta za muda tu.

Alipofanya ziara ya kiserikali Rais Jakaya Kikwete Katika mkoa huo mapema Mwaka huu alisema kuwa Serikali inajaribu kuiunganisha Kigoma na Sehemu ya Nchi kauli ambayo imetafsiriwa kuwa kumbe Kigoma haikuwa Sehemu ya nchi.

Katika ziara hiyo Rais Kikwete alisema kuwa Serikali inampango wa kuleta umeme Kigoma kutoka Tabora au kuzalisha katika Maporomoko ya mto Malagalasi , kasha itajenga uwanja wa Ndege wa Kimataifa lakini katika Bajeti ya 2007/2008 pesa iliyotengwa ni milioni 100 kwa ajili ya viwanja viwili, Mwanza na Kigoma.

Hali kama ya Barabara wananchi wanashukuru uwepo wa Vita ya nchi za jirani kutokana na wakimbizi wanaoingia nchini kunasababisha mashirika ya umoja wa Mataifa kuweka moramu na kuzikarabati ili kurahisha kipita.

Mtoto mmoja wa miaka 16 mkazi wa Manyovu wilayani kasulu anayesoma darasa la saba alipoulizwa kama aliwahi kuona Lami alishangaza watu kwenye mkutano aliposema ameiona Bujumbura Burundi tu.

Ikiwa Serikali itaamua kuwekeza katika Mkoa huo kwa nguvu zote ikianza kwa kutenga pesa kila bajeti kwa ajili ya kujenga barabara za lami na kujenga mtambo wa umeme katika maporomoko ya mto malagalasi mkoa huo utakuwa kitovu cha uchumi nchini.

Hakuna mkoa hapa Tanzania unaoweza kushindana na mkoa wa Kigoma kwa pato la wananchi wake ikiwa miundombinu kama Reli,bandari na Umeme itaboreshwa na mazao kusafirishwa bila taabu uchumi wake utakuwa ajabu.

Bandari ya Ujiji nayo kama ingekuwa imeboreshwa, inatumika lkikamilifu Mkoa wa Kigoma ungekuwa Dubai ndogo ya Afrika kutokana na mji huo kuwa katikati ya nchi za afrika ya kati, kama Burundi,Kongo kishaza, kongo brazaville ,Rwanda

na Afrika ya kati na kwa upande wa kusini zambia, ikiunganishwa na ziwa Tanganyika huku ukiungawanishwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa Barabara na reli.

Ni rahisi zaidi nchi hizo kuagiza na kuchukuliwa bidhaa zao hapo Ligoma zikiwa zimekwisha pakuliwa katika bandari ya Dar es Salaam kuliko kuzifuata wenywe Dubai ya kiarabu.

Ni jambo la kushangaza kuona kiogozi aliyekabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi anasimama anasema kuwa anatangaza vita ya wamachinga ambao wanajitafutia riziki pamoja na familia zao anasema hataki kuwaona mitaani bila kuwajulisha wapi waende.

Lakini kama busara na hekima zitatumika vijana wengi ambao ni machinga na wapiga debe gharama za kupambana nao mitaani wakati mwingine wanageuka kuwa vibaka na kutudhuru, zitumike kununua pembejeo za kilimo na kuwapeleka kuzalisha mazao ya kilimo kigoma.

Yale makambi ya wakimbi yanayofungwa wakati wakimbimbizi wakirejea kwao yatumike kwa ajili ya vijana wanaokwenda kuanzisha mpango wa kilimo ni uti wa mgongo na baada ya muda vijana wengi watakuwa wamepata amtaji nakuondokana na tabia ya kupiga debe mjini.

Wakati sereikali ikigombana na wanachi wake kwa kubeba viwanja vinavyojengwa maghorofa ujenzi huo uelekezwe kigoma mji ambao ni wa Kihistoria kwani pale kuna kila kitu,Kigoma unafaa kuwa mji wa kibiashara na kitaliii na kilimo kwa ajili ya kuwalisha watu wake.

Nchi kama za kongo na Burundi zifungue balozi zake huko zijengwe kumbi kubwa za mikutano ya kimataifa kwa ajili ya kuendeshea mazumzo ya Amani afrika eneo la maziwa makuu.

Viwanda vya kuzalisha bisukuti kutokana na ndizi ,Sukari kutokana na Miwa ,pamoja na kiwanda cha kuchambua pamba na Kahawa vijengwe huko kwa ajili ya kuwapa wakazi wake ajira, serikali ihamasishe kilimo cha mpunga katika bonde la mto malagalasi.

Kigoma imesahauliwa unakila sababu ya kuwa kitovu cha biashara afrika ya kati ikiwa miundombinu utaboreshwa na wafanyabiashara wenye mitaji kuhamasishwa kufungua maduka na mahoteli makubwa, kwa mfano mji kama wa Kibondo bila hoteli ya UN hakuna hoteli kubwa ya kulala.

Ili kuwanutia wafanyabiasha wa Afrika ya kati makontena yote yanayokwenda nje yakipitia Bandari ya Dar es Salaam yapakuliwe haraka na kwenda kulipiwa ushuru kigoma wakati yanavuka ili kuwarahisishia wafanyabiashara usunbufu wa mzigo wao kuchelewa bandarini.

Serikali ikizingatia haya nini kitauzuia mkoa wa Kigoma usiwe jiji la utalii na kitovu cha kibiashara huku vijana ambao walikuwa wapiga Debe na machinga wakiwa wamejikita katika mashamba wakizalisha, mazao mbalimbali na Mikirosho ambayo inahitajika nje kwa ajili ya kutengenezea mafuta ya mashine.

Waswahili husema mtu anayetenda jambo baya kwa hila mwisho wake mbaya, CCM na serikali yake iache kuwafanyia wakazi wa kigoma mchezo wa Siasa kwani mwisho wake ni Aibu kigoma.

Mwandishi wa makala haya anefanya ziara mkoani kigoma hivi karibuni
www.mobinday.blogspot.com 0753 399 579 , 9717 328 102

वातोतो वाबलिलिया elimu



hata mnyama kama huyu anahaki ya kupata mahutaji yake . huyu ni simba akiwa amejihifadhi katika mbuga ya serengeti inayotarajiwa kujengengwa mahiteli na uwanja wa ndege wa kimataifa wanyama kama huyu hawapendi kelele wataalam wa wanyama wanasema simba watatoweka wakihama kelele za ndege

LINI MTOTO WA TANZANIA ATAPATA HAKI YA KUSOMA

Na Ratifa Baranyikwa

PAMOJA na kuwepo kwa sheria, sera na mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa watoto wa Tanzania wanapata haki ya elimu kama ambavyo Serikali ya awamu hii imetilia umuhimu wa hali ya juu, lakini bado kuna baadhi ya watendaji wa serikali ambao wanatweza haki hii.

Watendaji hawa, hasa wa Halmashauri za wilaya wao hujiona kama miungu mtu, linapokuja suala la utekelezaji hapo hufanya vitu kwa maslahi ya kisiasa na si kwa maslahi ya wananchi ambao wamewapa dhamana ya kuwaongoza.

Elimu ni haki ya msingi ya binadamu, haki hiyo inatambuliwa na sheria ambazo tumejiwekea sisi wenyewe

Taarifa ya hivi karibuni za kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) zinashtusha kama si kusikitisha ambapo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Henry Shekifu anakanusha suala la watoto zaidi ya 500 kukosa elimu baada ya shule waliyokuwa wakisoma kufungwa kupisha eneo la hifadhi na watoto hao kuahidiwa ahadi hewa za kupatiwa shule nyingine.

Inashangaza kusikia Mkuu wa Mkoa anapinga kitendo hicho ambacho kinathibitishwa na wananchi huku akiwakingia kifua watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) ,Harold Sungusia na baadhi wa maofisa wa kituo hicho ambao wapo wilayani humo watoto hao waliokuwa wakisoma shule ya Lendrok iliyoko kijiji cha Loltepesi kata ya Sunya hawajaenda shule tangu zifunguliwe Januari mwaka huu na hivyo kusababisha kubaki nyumbani wakiendelea na shughuli nyingine tofauti na masomo.

Shule waliyokuwa wakisoma watoto hao Halmashauri iliamuru kuvunjwa kupisha hifadhi lakini wananchi walipinga suala hilo mahakamani wakisaidiwa na LHRC na Mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Ardhi ilizuia zoezi la kuwaondoa wakazi wa eneo hilo sanjari na kuvunja shule hiyo mpaka itakapoamriwa na mahakama hiyo.

Kwa maana hiyo shule ya Lendrok ambayo imejengwa kwa nguvu shirikishi za wananchi hadi kukamilika kila kitu kuanzia viti,choo ilipaswa kuendelea kuwahudumia wanafunzi wale mpaka hapo mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho.

Kiu ya wananchi ambao ilitakiwa waungwe mkono na Serikali haikuishia hapo walidiriki hata kuchangishana kumlipa mwalimu

Kinachosikitisha zaidi baada ya kuwepo kwa mpango wa kuvunja shule hiyo ambayo ilisajiliwa kisheria kwa namba za usajili MA/03/02/77 ni ahadi za watendaji wa Halmashauri ya Kiteto kwamba watoto hao wangehamishiwa shule iliyo karibu na Kijiji hca Lobosoit ambayo nayo inaelezwa kuwa ina wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili na kwamba madarasa ya shule hiyo yapatayo matatu hayana paa, wala viti na vyoo.

Sasa Kitu cha kujiuliza Halmashauri wakati inasema itawahamishia watoto hawa katika shule ya Lobosoit hawakujua kuwa shule hiyo ina madarasa matatu tena ambayo hayajakamilika? Watoto hao ambao walikuwa mpaka darasa la nne wangesoma kwenye madarasa gani?

Hata hivyo tunaelezwa kuwa hakuna kumbukumbu yoyote inayoonesha kuwa baada ya uamuzi wa kuifunga shule ya Lendrok watoto walifanyiwa utaratibu wa uhamisho na serikali ya wilaya kwenda Loibosoit.

Mkuu wa Mkoa anapinga huku akiwatetea watendaji wa halimashauri ambao kwa uzembe tu na kwa maslahi ya kisiasa wamekwamisha watoto zaidi ya 500 kutokwenda shule bila kufanya mipangilio thabiti.

Nauliza hivi kama walijua shule hiyo inatakiwa kuvunjwa kwanini mazingira mengine hayakuandaliwa? Huu ni uzembe.

Tunahitaji ufafanuzi kuhusu sh mil 16 ambazo Halmashauri inadai ilitenga kwa ajili ya kujenga shule ambayo ingesaidia kupunguza tatizo la wanafunzi ambao wamesimama masomo kwa takribani miezi saba.

Pia tunaelezwa watoto wapatao 300 ambao walipaswa kuanza darasa la kwanza nao wameshindwa kuanza kutokana na tatizo hilo utafiti wa LHRC unaeleza kuwa inaonekana wapo wanafunzi na watoto zaidi ya 1000 ambao wanapaswa kuwa shuleni kwa sasa na hawapo kwa sababu ya shule kufungwa, kuvunjwa na nyingine kutokamilika na pia kukosa walimu katika eneo hilo na Halmashauri ikifahamu tatizo hilo


Idadi hiyo ni kubwa sana Matokeo yake leo hii kila kukicha tunaongelea ndoa za utotoni, Vifo vya akinamama wajawazito ambao wengi pia husababishwa na ndoa hizo, unyanyasaji wa kijinsia, umaskini na hii ni kutokana na uzembe wa baadhi ya viongozi ambao hukwamisha maendeleo yetu.

Hivi kwa akili ya kawaida watoto hawa ambao wamesimama kimasomo kwa miezi hiyo yote kweli watakuwa na shauku ya kurudi shuleni na hata wakirudi hivi kweli wataendelea vizuri? Nahisi nina maswali mengi kuliko majibu

Watoto hawa wataishia kuolewa mapema, huku wengine wakipiga vita ndoa za utotoni wengine ndio wanatoa mianya ya ndoa hizo.

Kwa mantiki hiyo badi kama ni uzembe wa baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Mkoa wa Manyara basi wawajibishwe na Kama uzembe huu ni wa Serikali kuu basi Serikali iwajibike kwa hili hasa kwa kutoandaa mazingira mapya.


MWISHO.

Monday, July 16, 2007

नि उवेकेज़ाजी ओ उपोराजी?

Mitaji ya wawekezaji haiwezi kuodoa umaskini wa ujinga wetu.

Na Mobini Sarya

DUNIA ipo kwenye mapambano ya kupata maendeleo lakini Afrika ipo vitani kwa ajili ya kupambana na umaskini na ujinga ambao umelikwamisha bara hili lisiendele katika nyanja na maendeleo na tekinolojia ingawa limejaliwa malighafi na kila kitu.

Wakati Dunia ikiwa katika vita ya maendeleo Tanzania inaoneka kushindwa kabisa hata ile hatua ya kupambana na ujinga na umaskini , Mapambano ya ambayo yalitangazwa na Rais wa kwanza Mwalimu Nyerere saa chache baada ya kujipatia uhuru kutoka kwa Wakoloni Mwaka 1961.

Askari waliopaswa kupambana katika vita hiyo wamekuwa wakipungua nguvu kila kukicha, wakistaafu na wengine wakifa kama hayati Mwalimu Nyerere alikuwa kamanda wa vita hiyo huku askari wakiendelea wakiendelea kutumia silaha zile zile za mwaka 61.

Siku chache zilizopita niliandamana na viongozi wanne wa vyama vya siasa, TLP,CUF ,CHADEMA na NCCR-Mageuzi katika ziara yao ya Mikoa miwili Kigoma na Kagera wakiwapa wananchi Elimu ya Uraia nikiwa Kagera wilayani Ngara katika mkutano wa Hadhara wananchi walisoma risala ya kushangaza.

Katika mkutano huo uliofanyikia viwanja vya Posta na kuhudhuria na watu mbalimbali katika Risala hiyo iliyosomwa mbele ya Mwenyekiti wa CHEDEMA, Freeman Mbowe ,NCCR-Mageuzi James Mbatia ,CUF Prof Ibrahim Lipumba na Chama cha TLP Agoustne Lyatonga Mrema,

wananchi walisema kuna mgodi eneo la kabanga ambao shughuli zake zimekuwa zikendeshwa kinyemela kwa muda mrefu huku shughuli hizo zikifanywa kwa usiri mkubwa huku wakiwa na taarifa kuwa madini mbalimbali yakiwemo Dhahabu yanachimbwa eneo hilo.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alishangaza zaidi aliposema kuwa anaifahamu huo mgodi wa kabanga kwani umeanza kudaiwa kufanyiwa utafiti tangu anasoma shule ya msingi miaka 34 baadaye wakati huo wawekezaji walikuwa wanatafiti madini ya Nikel lakini baadaye ulipatikana utitili mwingine wa madini.

Mbatia anasema wakati huo ndege zilikuwa zinatua kila jumatatu na ijumaa kuchukua kile kile wanachoita sambuli ya madini na kupeleka ulaya kwa ajili ya kupima wakati wanasema hayo hakuna kiongozi yeyote wa Serikali katika eneo hilo aliyejitokeza kupina hayo madai lakini yalipofika kwenye gazeti serikali imeyaona kuwa sumu.

Serikali kupitia wizara ya nishati na Madini imetumia kodi za wananchi, kuja juu na kumshutumu mwandishi na gazeti zima kupitia kwenye matangazo yake eti kwanini habari ile iliandikwa bila kuwauliza wao utafikiri mwandishi kaibua.

Katika taarifa yake wizara ya Nishati ilidai kuwa habari iliyoandikwa katika gazeti bila kupata taarifa za kitaalam ililenga kuchochea wananchi kupinga uwekezaji huo wa miaka 34 bila tija, nakuwashauri wahariri na wandishi kufanya itafiti wa kina ‘kama wa mwekezaji kwa muda mrefu’kabla ya kuandika makala au habari kwa umma.

Nakumaliza hasira kwa kusema habari au makala zilizoandikwa bila takwimu au taarifa sahihi zinapotosha baadala ya kuelimisha ufafanuzi huo unaoonekana kuwa shutuma ulitolewa na Kamishna wa Madini Dalaly Kafumu.

Ukisoma ufafanuzi uliotolewa na Kamishna kisha ukalinganisha na madai ya wananchi walioyatoa katika gazeti la Tanzania Daima Julai 9 mwaka huu utabaini kuwa mgodi wa kabanga ambao wizara inasema sio mgodi bali ni eneo la utafiti, kuna jambo ambalo wakubwa wanalificha.

Wananchi walisema kuwa eneo linapatikana madini aina ya Platinum, Nikel ,Uranium,Dhahabu n.k na limefanyiwa shughuli kwa miaka 34 kiinyemela kwa makampuni kadhaa yanayodai kuwa yanadai kuwa yanafanya utafiti huku yakuuziana mikataba kienyeji.

Madai hayo yanadhibitishwa na wizara inaposema kuwa historia ya utafutaji madini katika eneo hilo ilianza Mwaka 1974 wakati ukifanywa na wizara ya maji, nishati na madini chini ya mradi wa utafutaji madini ‘Project no.URT-73/030 uliokuwa unafadhiliwa na shirika la maendeleo UNDP uchunguzi huo uligundua maeneo 48 yanayoonyesha kuwepo madini aina ya Nickel,shaba, Cobalt,chrome na Zink.

Katika eneo hilo wataalam walikadiliwa kuwepo na Nickel tani milioni 26 zenye asilimia 0.7 za nickel, baada ya ugunduzi huo wizara ya nishati inasema makampuni mbalimbali yamekwisha fanya utafiti eneo hilo ambayo ni

Romenex/Sutton Resources, Sutton Resources/BHP ,Anglo America/Sutton Resources na Barrick Gold Corporation /Falconbridge na sasa yaliyopo ni Barrick Gold Corporation kwa Kushirikiana na Xstrata Nickel.

Hapo baada ya wizara kudhibitisha madai alichokikosea mwandishi nini kutoa taarifa kutoka sehemu moja kwenda nyingine au kuiamsha Serikali ilazimike kutoa ifafanuzi kwa Umma kwa sababu tangu madini hayo ,mbalimbali yapatikane serikali haikuwahi kutoa taarifa zozote kwa umma na isingetoa kama habari hizomsingeandikwa.

Lakini wananchi bado wanamashaka ni madini gani hayo ambayo kwa miaka 34 yanafanyiwa utafiti na bado udongo wake unakwenda kupimiwa ulaya bila kinu chake kuanzishwa hapa nchini, kwa maneno yake yenyewe wizara ya madini imezibitisha kuwa kuanzia mwaka 2003 pekee hadi sasa wamesafisha nje tani 13.2 za miamba inayokisiwa kuwa na madini sawa na wastani wa tani 2.6 kwa mwaka!

Katika maelezo hayo ya kushangaza serikali inasema kuwa ili uchimbaji wa Nickel uwe na faida kibiashara unahitaji kuchimba tani milioni 1 za miamba kwa mwaka kwa hiyo kuchukua miamba kiasi cha wastani wa tani 2.6 kwa mwaka hauwezi kuzalisha nikel kibiashara.

Wizara inashindwa kuambia umma kama sio kibiashara hizo tani 2.6 kwa mwaka anakula nani wakishauza uko nje kwani anatuambia kuwa kabla ya kusafirisha nje hizo tani hupeleka kwenye ofisi za madini kanda ya ziwa kukaguliwa na kupewa kibali cha kusafisha nje ya nchi (export Permit) ,lakini hatuambiwi baadaye kama helejeshwa hiyo tani hapa nchini.

Tunadhani majibu yaliyotolewa na wizara yalikuwa mepesi yanayiolenga kuwafurahisha baadhi ya watu hasa katika kipindi hiki cha bajeti, kwani baadala ya kuwafafanulia wananchi waelewe kinachofanyika hapo unaelekeza shutuma kwa mtu asiyehusika,

ni vema taarifa za migodi mingine zikatolewa kwani huo sio wakwanza kuna mwinge huko geita tulisikia kampuni ilifanya utafiti kwa miaka 23 hadi mkuu mmoja alipoingilia katu weka wazi kama wa North Mara makampuni kubadilisha mikataba kinyemela na faida iliyopatikana katiaka mgodi wa Buhemba Mara.

www.mobinday.blogspot.com 0753399579

Labels: