Saturday, December 13, 2008

Uhuru bila utii ni Wazimu,walisema wahenga

uhuru bila utii ni wazimu na utii bila uhuru ni.........

Na mchambuzi wetu

KUNA usemi usemao kuwa Utii bila uhuru ni sawa na utumwa na uhuru bila utii ni wenda wazimu, msemo huo unaweza kuutumia unapotaka kuelezea hali ya mwenendo wa mambo hapa nchini hasa katika suala zima la maamzi ya kisiasa na kiutendaji serikalini.

Imekuwa ni bahati mbaya kwa baadhi ya watu kuona serikali iliyopo Madarakani inazembea kuchukua hatua za kisheria hasa pale inapodharauliwa na kudhihakiwa kwa kila jambo,inalotenda na kuonekana imekosea

Lakini pia imekuwa ni bahati njema kwa baadhi ya watu kuona Serikali imetoa uhuru wa kutosha ambao sasa wanautumia watakavyo wao bila kujali madhara ya baadaye.

Ni katika mitazamo hiyo tofauti ndiyo tunakuta baadhi ya makundi yameibuka kwenye jamii yetu na kuikosoa serikali waziwazi bila woga wala kificho kwa kutumia uhuru wa Demokrasia tulionao, jambo ambalo ni la msingi kabisa katika katiba.

Pia yapo Makundi yanayotumia uhuru huo vibaya kwa kuikosoa Serikali hadi nje ya mipaka pale matumizi ya kutumia maneno ya kejeli yanayopelekea kukosa nidhamu kwa viongozi wao.

Kufuatia hali hiyo imefikia hatua ya wananchi kuwatendea vitendo visivyokwenda sambamba na maadili ya mtanzania kama vile viongozi kupigwa mawe , kuwazomea na hata kufikia hatua ya kumkejeli Rais anapokuwa kwenye mikutano yake ya hadhara huo ndio tunasema wazimu wa uhuru.

Tukiendelea kunyamaza kwa kushangilia kuona viongozi wanapigwa mawe tunachekelea basi tujue zamu ya viongozi hao ikimalizika kiama hicho kitahamia kwenye makundi mengine kitatukuta na kujikuta tukiwa tumechelewa hivyo kupelekea kila mmoja kujihami kwa silaha yake hali itakayozaa maangamizi kwa Taifa.

Hayo yote yanatokana na ukweli kuwa tunatumia uhuru tulio nao kama wendawazimu, hatujui maana yake tunafikiri kukosa ni nidhamu kwa serikali iliyopo madarakani ndio tutaonekana kuwa tupo huru bila kujua madhara yake baadaye.

Inawezekana kabisa leo baadhi ya wanasiasa hasa wa upinzani wanafurahia kuona Ris wa Nchi akipigwa mawe na wananchi lakini wanasahau kuwa kesho wao watakuwa madarakani na hali hiyo itakapo wakuta je watainyamazia au wataamrisha vikosi vya majeshi vivamie hapo ili kurejesha nidhamu kwa risasi.

Ni katika mtazamo huo ndio narejea katika malumbano yaliyoibuka hivi karibuni kati ya Serikali na mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Regnal Mengi na kufikia hatua mfanyabiashara huyo kupewa siku saba adhibitishe madai aliyotoa kuwa kuna waziri kijana anatishia kumuua na kubambikiwa kodi kubwa kwenye biashara zake ili shindwe kulipa afilisiwe.

Kauli hiyo ya mfanyabiashara raia dhidi ya Waziri ilikuwa nzito na inaweza kuwa kashfa kubwa kwa serikali ikiwa itadhibitika kuwa madai hayo ni ya kweli hasa inapotajwa kuwa katika kikao cha kumjadili Mengi Rais naye alihusika.

Lakini kubwa zaidi linaloonekana kuwa ni matumizi mabaya ya uhuru ni pale watu wanapojaribu kuingilia masuala hayo na kutaka kupotosha ukweli kuwa Mengi na Waziri huyo wanaugomvi binafsi wa kisiasa hivyo kuichanganya jamii.

Wanafikia hatua ya kumuonya Waziri Lawrence Masha kwamba asikurupuke kumpa mfanyabiashara huyo siku saba za kuthibitisha bila kujali kuwa aliyesema hayo sio Masha ni Serikali.

Serikali sio mtu ni tasisi inayosimamia huduma za watu wengi hivyo tamko linapotolelewa halimaanishi ni nani kalitoa ispokuwa ni kwa maslahi ya Umma.

Waziri kama mtumishi wa Umma ni mteule wa Rais aliyepo madarakani ambaye amechaguliwa na wananchi wa kabila na tabaka mbalimbali hivyo kujaribu kumkashifu waziri ni sawa na kumvunjia heshima mteule wa Rais ambaye ni chaguo mhimu la wananchi.

Ndio maana wengine tunaamini kuwa wakati waziri Masha anampa mfanyabiashara huyo siku saba alikuwa anasimamia majukumu ya umma akiiwakilisha serikali anayoitumikia.

Bila kujali kama Masha ndiye alihusika kupanga njama za kumhujumu Mengi au la ni vizuri watu wakatambua kuwa kama tuhuma hizo zingenyamaziwa na serikali wananchi wangehoji kwanini serikali imekaa kimya.

Kwa kutumia nafasi ya waziri wa mambo ya ndani na usalama wa Raia Masha akaamua kujitokeza kutaka ushahidi wa madai hayo kwa muda wa siku saba ili isije ikaonekana kama ni uzushi ,lakini baadala yake wameibuka watu wakimpinga Masha hapo ndio matumizi ya uhuru yanapokosa thamani.

Siamini kama siku saba ambazo ziliisha wiki iliyopita zilikuwa nyingi kusubiriwa ziishe hadi watu wakaamua kuingilia suala hilo kwani alichofanya Masha sio kumhukumu Mengi bali kuhitaji ushahidi wa kile alichokisema.

Alifanya hivyo akitambua umhimu na umaarufu wa Mengi kwenye jamii yetu, kwa madai kama yale ambayo sio mara ya kwanza Mengi kuyatoa yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye jamii yetu ikitokea jambo baya likamkuta.

Kwa hiyo Serikali ilipaswa iwe makini na kauli ile kwani siku moja baada ya taarifa ile ili lipotiwa na chombo kimoja cha Propaganda kikidai kuwa Mengi akikamatwa walemavu wametishia kufunga barabara za jijini Dar es Salaam, hiyo ndio athari mojawapo.

Kwa kutambua umhimu huo pia endapo Mengi atatoa ushahidi huo serikali itakuwa imejua ni Kiongozi gani ambaye ni wakala wa kutoa taarifa za siri serikalini na kuzisambaza mitaani kwa raia hali inayoweza kuibua matatizo makubwa ya kijamii.

Hivyo basi ni vizuri Serikali ihakikishe inambana Mengi hata kwa kuburuzwa Mahakamani ili akathibitishe ukweli wake huo, kwamba anataka kuwawa na Serikali (Waziri) lakini akishindwa kutoa ushahidi huo atambulike kama ni mzushi.

Serikali isipofanya hivyo jamii nzima itaamini kuwa kweli Serikali ilikuwa inapanga njama za Kuumua Mengi na ikieleweka hivyo watu watakosa imani na serikali yao kwa kuhisi kuwa inahusika kuuwa wapiga kura wake hivyo kuamsha hasira na chuki jambo ambalo sio zuri.

Aidha kama alivyoahidi Masha asipochukua hatua ili jamii iweze kubaini ukweli Umma utamwamini Mengi na utamuonea huruma kwa kitendo hicho hivyo Masha na Serikali anayoitumikia italazimika kuondoka madarakani kwa kashfa hiyo.

Tumezoea kuambia katika matukio mengine kuwa Serikali inayashughulikia mwishowe yanaisha kimya kimya bila wananchi kuambia hatima yake lakini kwahili la Mengi na Serikali wananchi hawatakubali limalizwe kienyeji, ni bora ukweli ukadhibitike hata mahakamani ili anayeumbuka aumbuke.

Taifa lipo kwenye vita ya ufisadi ambao umeitafuna nchi kwa muda mrefu hatuwezi kuchezewa akili kwa kubadilishiwa ‘CD’kama alivyowahi kuomba waziri mmoja ili tuanze kuimba ‘Mengi,Mengi anauwawa, Masha, Masha amempa siku saba’ ili tu muda uende mbele.

Ni malize kwa kumuomba mzee Mengi atue ushujaa wake ule ule aliotumia kwenye vyombo vya habari kutoa madai yake na sasa autumie kuthibitisha kama alivyosema siku saba ni nyingi ili tuweze kumwamini vingenevyo tutajua anazusha mambo ili aonewe huruma.
Kwa sisi wananchi tunapaswa kuepuka uchochezi wa wanansiasa dhidi ya viongozi wa Serikali kwani kufanya hivyo kutatufanya tupigwe na adhabu ya Mungu kwani Serikali za Dunia zipo kwa kumwakilisha yeye. .ukiona nimetia chumvi tia na wewe maji kadri uonavyo kisha onja ladha yake.

kwa maoni tutumie

Tuesday, December 9, 2008

Chama kipya cha waandishi chaanzishwa Tanzania Correspondent Journalist .TCJ

]

na Ripota Wetu

WAANDISHI WA Habari wasio na ajira ya kudumu kwenye vyombo vya habari (Correspondent) wameanzisha chama kipya kitakachotetea haki na maslahi yao kwenye vyombo wanavyofanyia kazi.

Chama hicho Tanzania Correspondent Jounalist (TCJ) kitazinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika baada ya Disemba 6 Mwaka huu wajumbe kupitisha katiba kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano wa kupitisha katiba Mwenyekiti wa Muda Sir Mobini Sarya alisema kuwa chama hicho kitakuwa na lengo la kusaidia wanachama wake kupata ajira, kuwatetea pale wanapopata misukosuko ya kikazi na kuwaendeleza kielimu.

Sir Mobini alisema kuwa ni muda mrefu sasa wandishi wamekuwa wakinyonywa na w aadishi wa habari bila kujali mafanikio ya kujituma kwao sasa wameamua kuanzisha umoja, ifuatayo ni Hotuba ya Mwenyekiti huyo;…….

……. Hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kupitia rasimu ya katiba iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama cha ma-Correspondent Sir Mobini Sarya, disemba 6 mwaka 2008.

Ndugu wajumbe mliofika hapa kwenye ukumbi huu wa idara ya habari na MAELEZO, awali ya yote napenda kuanza kuashukuru kufika kwenye mkutano huu ambao baadhi ya watu walifikiri hautafanikiwa, lakini ni jambo jema kubwa na la kufurahisha kuona tulipofikia leo.

Ndugu wajumbe mliofika kwenye mkutano huu ni jambo la kufurahisha na kuwashukuru zaidi hasa ninapoona kuna watu wapo tayari kutetea maslahi yao wakiwa huru kwa kutumia chombo huru walichoanzisha.

Leo tunakwenda kupitia katiba ambayo itafanikisha kusajiri chama cha waandishi wa habari wasio na ajira ya kudumu kwenye vyombo vya habari, licha ya kufahamika kuwa sisi ndio wenye jukumu zito la kuchapa kazi hasa katika kutafuta habari.

Lakini ni sisi tunaofahamika kuwa ombaomba wa nauli baada ya wamiliki wa vyombo vya habari MOAT kuonekana kama wamewasahau waandishi Correspondent, kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa tumetelekezwa.

Tunaweza kusema hivyo kwa kuona watu wakifanya kazi kwenye media miaka mitatu hadi sita bila kupatiwa ajira wakati katika sekta zingine mtu akifanya kazi miezi sita anakuwa tayari ndani ya ajira.

Limekuwa ni jambo la kushangaza kuona wandishi wa habari hawakumbukwi wala maslahi yao hayazingatiwa licha ya kufahamika kuwa Correspondent ndio hutumwa haraka haraka kwenye tukio linapotokea tafauti na waajiriwa ambao wamezoea kukaa ofisini wakisubiri semina za Bagamoyo.

Wakati leo tunapitisha katiba hii tutakuwa tumefungua ukurasa mpya wa kuanzisha harakati za ukombozi kwa waandishi wa habari nchini, kwani tungependa chama hiki kiwe na mwanasheria wake ili kuweza kukabiliana na dhuluma yoyote inayotokea kwenye Media.

Kwa sababu wandishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu bila kuajiriwa huku wakijituma lakini bila kujali jitihada hizo wajiri wamekuwa wakichukua hatua za kuwapunguza kazi na kuwafukuza bila hata kinua mgongo huku stori zikizimwa kama hakuna jambo lolote.

Tungependa kuwaona wandishi wote wakijiandikisha kwenye chama hiki ili wanapokuwa wamepata tatizo kama hilo sheria za kazi ziweze kuchukua mkondo wake na watu waweze kulipwa haki zao.

Sisi wote bado tutakuwa tunakumbuka jinsi baadhi ya makampuni ya habari yalivyo punguza waandishi wa habari bila kufuata sheria ambazo zinataka mwajiri atoe taarifa kabla ya kuchukua hatua hizo, wala hakuna aliyelipwa.

Lakini pia ikumbukwe kuwa ni mwaka mmoja sasa tangu serikali itoe tamko la wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa wafanyakazi wao mshahara wa kima cha chini laki mbili lakini hakuna aliyefanya hivyo wameendelea kuvunja utaratibu huo bila kuulizwa.

Wanatumia mwanya huo kwa kutambua kuwa hakuna chama au chombo kinachoweza kuwaunganisha waandishi wakadai haki zao leo kitu hicho kinazaliwa hivyo litakuwa jukumu la kwanza kufuatilia tamko hilo.

Ndugu wajumbe mliofika hapa, pia ikumbukwe kuwa chama chetu bado ni kichanga hakijapata uongozi, waliopo wanajitolea kuhakikisha moto huu tuliouwasha hauzimiki ni vizuri leo mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali ili kuleta mabadiliko.

Litakuwa jambo jema kama tutashuhudia wachapakazi wapya wakijitokeza kugombea nafasi ambazo tutazipitisha wenyewe kwenye katiba hii ili waweze kutoa mawazo yao katika kuandikisha chama.

Yapo majukumu kadhaa na mazito yanayowakabilia viongozi watakaochaguliwa leo, kwanza ni lazima viongozi watakaochaghuliwa leo wawe ni watu wenye moyo wa kujituma kwani chama chetu bado hakijawa na ofisi wala vyanzo vya mapato.

Hivyo inahitaji wakati mwingine viongozi wanachagia wenyewe kutoka mfukoni mwao ili kufanikisha suala lolote, ikiwa ni pamoja na shughuli za uchapaji, kazi hiyo nimekuwa nikiifanya mimi mwenyewe pamoja na kuwa ombaomba lakini nashukru kuwa nimeweza kufanikisha kila kitu.

Nimejitahidi kuhakikisha angalau napata pesa ya kuchapisha nakala za katiba ili kuwapatia wajumbe wazipitie pia nimejitahidi kuhakikisha mambo yote yanafanikiwa kwa kusukuma na kufanya kampeni na wenzangu hadi leo tumeweza kupata ukumbi wa kufanyia mkutano.

Viongozi wa namna hiyo wakijitokeza wataweza kufanikisha shughuli hii ngumu kufikia kikomo, kwani tunataka kabla ya kusajili chama tuwe kwanza na ofisi hivyo viongozi watakaopatika leo wanapaswa kulishughulikia hilo mapema.

Ingawa chama chetu bado hakijapatiwa jina lakini nilipendekeza kiitwe TAJOA yaani Tanzania Journalist Association au Tanzania Correspondent Journalis TCJ wote tupo hapa leo ni wajibu wetu kuchagua jina jema na kama haya yote hayafai basi tunaweza kuangalia lingine.

Pia kama mnavyojua chama chetu ni kwa ajili ya wanachama wasio na jira mbao watapata frusa ya kusomeshwa na kuhudhuria semina mbalimbali za kuwajengea uzoefu hasa kwenye nyanja ya habari za uchunguzi.

Hivyo tunawataka waandishi ambao hawajajiunga watambue kuwa Serikali inakusudia kupitisha msuada wa vyombo vya habari ambao utawaondoa waandishi wote wasio kuwa na elimu angalau miaka miwili hivyo chama hiki kitasadia watu kama hao kupata elimu hiyo.

Lakini pia hivi karibuni umezinduliwa mfuko wa vyombo vya habari TMF hiki chombo kimeweka bayana kuwa hakitatoa pesa kwa mwandishi yoyote bila kudhaminiwa na Press Club yake, Mhariri wake hivyo kumbe bado kuna umhimu wa kuwa mwanachama hiki chama, ambacho naamini baada ya muda kitasambaa mikoani.

Nimalizie kwa kuwashukru wajumbe mliofika hapa kwa lengo la kujadili rasimu ya katiba hii na hatimaye kuwapata viongozi wa chama chetu, niwashukru tena na tena wale ,mlioacha shughuli zenu mkaamua kulipa kipaumbele suala hili.

Ahsanteni sana.

Mwenyekiti wa Muda.

Labels:

Katiba ya chama cha -TCJ

Katiba ya chama cha -TCJ

SEHEMU YA KWANZA

1.Jina la Chama litakuwa -TANZANIA CORRESPONDET JOURNALIST

(TCJ)

2.Anuani ya Chama- S.L.P. DAR ES SALAAM.

3.Idadi ya waanzilishi………

4.Eneo la shughuli za chama litakuwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

5.Makao makuu ya chama yatakuwa katika jiji la Dar es Salaam.

6.SEHEMU YA PILI

MADHUMUNI YA CHAMA

Madhumni ya chama hiki yatakuwa kama ifuatavyo

a)kukuza /kuendeleza kielimu na kuimalisha ushirikiano wa wanachama wake wote.

B)kudai/kutetea maslahi ya wanachama wake katika sekta ya ajira.

c)kuhakikisha kwamba mwanachama anasaidiwa kwa hali na mali wakati wote anapopatwa na matatizo ya ajira.

Dkubadilishana mawazo katika juhudi za kujiendeleza kitaaluma na kiuchumi

E)kukutana na kuelezana matatizo yanayowapata wanachama katika sehemu zao za kazi.

F)kuhakikisha waajiri wanafuata sheria za kazi katika sehemu za kazi

7.0.SEHEMU YA TATU

1

A.HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA

1.Mwanachama anayo HAKI ya;.

i.Kuchagua/kuchauliwa kwa mjibu wa katiba

ii. atakuwa na haki ya kutoa mawazo yake kwenye mikutano halali.

iii.haki ya kukosoa na kukosolewa katika vikao.

iv.haki ya kupata msaada wa kisheria kwa mjibu wa katiba

v.haki ya kuendelezwa kitaaluma.

2.Mwanachama anawajibu wa’

a. wajibu wa kulipa michango yote ,kutekeleza maamzi yatakayoamriwa na chama.

b.kuhudhuria vikao halali vya chama .

c.kulinda na kutetea maslahi ya chama

d.kutii i na kuheshimu viongozi wa chama waliochaguliwa kwa mjibu wa katiba

e.kutunza Rasirimali za chaman a

f.hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa yule atakayezembea kulipa michango na mafao ya chama.

B.AINA ZA WANACHAMA

A. wanachama wasisi/waanzilishi

B. wanachama waliojiunga.

C.wanachama wa Heshima

I.wanachama waasisi/ waanzilishi- Ni wale walioasisi chama

II.wanachama waliojiunga/washirika- Ni wale waliojiunga baada ya chama kusajiliwa

2

III.wanachama wa heshima- Ni wale waliopata uanachama kwa kutunukiwa

- Ni wale wasisi wanaoajiriwa na kuachana na masuala ya chama

.

8 .0 SIFA ZA MWANACHAMA

1.awe mwandishi wa habari

2.awe amepitia kwenye chuo chochote cha habari

3.awe na chombo cha habari .

4.awe anatoa michango ya chama

8.1 UKOMO WA MWANACHAMA

1.Kifo

2.kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila taarifa.

3.kutolipa ada miaka mitatu mfululizo

4.kujiuzulu/kujiondoa mwenyewe kwa maandishi

5.kupata Maradhi ya akili.

9.0. SEHEMU YA NNE

9.1.A..MUUNDO WA VIONGOZI

KUTAKUWEPO NA NAFASI YA MWENYEKITI,MAKAMU M/KITI ,KATIBU MKUU, KATIBU MKUU MSAIDIZI NA MWEKAHAZINA PAMOJA NA MWEKA HAZINA MSAIDIZI na WAJUMBE-4.

9.02 WAJUMBE- watakuwa wanachaguliwa na wanachama kutoka kila Mkoa 9.03.MATAWI- kila Mkoa lazima pawepo na tawi lenye uongozi.

9.02 MKUTANO MKUU-ndio wenye maamzi ya mwisho ya chama

B.KAZI NA MAJUKUMU YAO

MWENYEKITI

A.ni Kiongozi wa Chama Taifa

B.ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za Chama.

C. anaitisha mkutano kwa kushirikiana na Katibu Mkuu.

3

MAKAMU M/KITI

A.ni msadisi wa Mwenyekiti

B.anakaimu wakati mwenyekiti hayupo

KATIBU MKUU

A.ni mtendaji mkuu wa shughuli za chama

B.ni msemaji wa Chama

C.anaadaa mikutano

D.

KATIBU M.MSAIDIZI

A.ni msadizi wa Katibu mkuu

B.anakaimu ka katibu mkuu hayupo

C.ni mtendaji wa shughuli za kila siku

MWEKA HAZINA

A.anapokea pesa na kutunza benki

B.anakusanya michango ya wanachama

C.anahusika kutoa pesa Benki

MWEKA HAZINA.MSAIDIZI

A.ni msaidizi wa Mwekahazina

B.anakusanya michango ya wanachama

C.MUDA WA KUKAA MADARAKANI

i.viongozi wote watakuwa wanakaa madarakani mwaka miaka 3

ii.watakuwa wanachaguliwa na Mkutano Mkuu

D.KAMATI ZINAZOUNDA CHAMA

I.kutakuwa na kamati tatu zinazoundwa na mkutano mkuu

1.kamati ya utendaji

2. kamati ya maadili na nidhamu

3 kamati ya uchumi na mipango

E.KAZI NA MAJUKUMU YA KAMATI HIZO

1.KAMATI YA UTENDAJI

4.

i. .inao uwezo wa kumfuta mtu uanachama anapovunja katiba

ii inasikiliza rufaa za malalamiko

iii.kumtafuta mwanasheria wa chama

2.KAMATI YA MAADILI NA NIDHAMU

i.inasikiliza migogoro ya wanachama

ii.inatoa adhabu kwa wanaokiuka katiba

iii.inalinda na kutunga kanuni za chama

3.KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO

i.inatafuta vyanzo vya MAPATO

ii.inabuni na kuendesha miradi ya chama

iii.inatafuta pesa za kuwawezesha wajumbe

9.03 TUME YA UCHAGUZI

I.Tume ya uchaguzi- itakuwa inasimamia uchaguzi wowote ndani ya chama

II.Wajumbe wa tume-wanatakiwa wasiwe na nafasi yoyote ndani ya chama.

III.Wajumbe wa tume-watakuwa wanachaguliwa na mkutano mkuu.

IV.Muda wa tume- ni miaka mitatu

9.03 KAZI YA MWANASHERIA

1.kusimamia masuala ya kisheria yanayohusu chama

2.kusimamia haki na masilahi ya wanachama mahakamani.

10.0 SEHEMU YA TANO

MAPATO YA KUENDESHA CHAMA

a.yataokana na michango ya wanachama

b.pesa za wafadhili mbalimbali

c.harambee

d.miradi ya chama

10.01.MIKUTANO YA CHAMA

Itakuwepo mikutano mitatu ya chama ambayo ni

a.Mkutano wa mkuu wa Mwaka

b. Mkutano wa dharura

5.

10.03 TARATIBU ZA MIKUTANO HIYO

a.itakuwa inaitishwa na Katibu Mkuu pamoja na Mwenyekiti.

b.lazima zaidi ya 1/2 ya wajumbe itimie

11. SEHEMU YA SITA

11.01 JINA LA CHAMA,ALAMA, ANUANI NA MHURI

11.02 JINA la Chama litakuwa linajulikana kama – T.C.J

11.3 ANUANI………….DSM

11.4 ALAMA/NEMBO ZA CHAMA-ni mikono miwili imeshikiliwa kalamu

Na maiki pamoja notebook.

11.5, ENEO ZILIPO OFISI-DAR ES SALAAM.

12.0 SEHEMU YA SABA

12.1 DIRA YA CHAMA NA MTAZAMO

Dira-kuhakikisha kila mwanachama anapata haki na maslahi stahiki

Dhima-kulinda misingi ya taaluma bila ubaguzi

12.2 SIFA ZA KUWA KIONGOZI

I.awe Mwanachama Hai.

II.awe mwanachama kutoka tawi lolote la chama

III.awe muadilifu /hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai

IV.Viongozi wote watakakuwa wanachaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu

12.0 SEHEMU YA NANE

12.1 MABADILIKO YA KATIBA-inaweza kubadilishwa katika mkutano mkuu wa Mwaka ikiungwa mkono na zaidi ya1/2 ya wajumbe.

13 .SEHEMU YA TISA

13.1 LUGHA ZA CHAMA ZITAKUWA MBILI

Kiswahili na kiingereza

14.0 SEHEMU YA KUMI

14.1 MATAWI YA MIKOA

6.

i.kila Mkoa utakuwa na uongozi uliokamilika ambao ni Matawi yanayounda TCJ

ii.wandishi wa habari mikoani kupitia Malawi hayo watakuwa wanachama wa T.C.J

iii.kila Tawi litakuwa linatoa wajumbe wanaingia kwenye mkutano mkuu

1. Majina ya watu waliohusika kupitisha kusajili katiba ni ……..

Labels: