Chama kipya cha waandishi chaanzishwa Tanzania Correspondent Journalist .TCJ
]
na Ripota Wetu
WAANDISHI WA Habari wasio na ajira ya kudumu kwenye vyombo vya habari (Correspondent) wameanzisha chama kipya kitakachotetea haki na maslahi
Chama hicho Tanzania Correspondent Jounalist (TCJ) kitazinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika baada ya Disemba 6 Mwaka huu wajumbe kupitisha katiba kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano wa kupitisha katiba Mwenyekiti wa Muda Sir Mobini Sarya alisema kuwa chama hicho kitakuwa na lengo la kusaidia wanachama wake kupata ajira, kuwatetea pale wanapopata misukosuko ya kikazi na kuwaendeleza kielimu.
Sir Mobini alisema kuwa ni muda mrefu sasa wandishi wamekuwa wakinyonywa na w aadishi wa habari bila kujali mafanikio ya kujituma kwao sasa wameamua kuanzisha umoja, ifuatayo ni Hotuba ya Mwenyekiti huyo;…….
……. Hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kupitia rasimu ya katiba iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama cha ma-Correspondent Sir Mobini Sarya, disemba 6 mwaka 2008.
Ndugu wajumbe mliofika hapa kwenye ukumbi huu wa idara ya habari na MAELEZO, awali ya yote napenda kuanza kuashukuru kufika kwenye mkutano huu ambao baadhi ya watu walifikiri hautafanikiwa, lakini ni jambo jema kubwa na la kufurahisha kuona tulipofikia leo.
Ndugu wajumbe mliofika kwenye mkutano huu ni jambo la kufurahisha na kuwashukuru zaidi hasa ninapoona kuna watu wapo tayari kutetea maslahi
Leo tunakwenda kupitia katiba ambayo itafanikisha kusajiri chama cha waandishi wa habari wasio na ajira ya kudumu kwenye vyombo vya habari, licha ya kufahamika kuwa sisi ndio wenye jukumu zito la kuchapa kazi hasa katika kutafuta habari.
Lakini ni sisi tunaofahamika kuwa ombaomba wa nauli baada ya wamiliki wa vyombo vya habari MOAT kuonekana
Tunaweza kusema hivyo kwa kuona watu wakifanya kazi kwenye media miaka mitatu hadi sita bila kupatiwa ajira wakati katika sekta zingine mtu akifanya kazi miezi sita anakuwa tayari ndani ya ajira.
Limekuwa ni jambo la kushangaza kuona wandishi wa habari hawakumbukwi wala maslahi
Wakati leo tunapitisha katiba hii tutakuwa tumefungua ukurasa mpya wa kuanzisha harakati za ukombozi kwa waandishi wa habari nchini, kwani tungependa chama hiki kiwe na mwanasheria wake ili kuweza kukabiliana na dhuluma yoyote inayotokea kwenye Media.
Kwa sababu wandishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu bila kuajiriwa huku wakijituma lakini bila kujali jitihada hizo wajiri wamekuwa wakichukua hatua za kuwapunguza kazi na kuwafukuza bila hata kinua mgongo huku stori zikizimwa
Tungependa kuwaona wandishi wote wakijiandikisha kwenye chama hiki ili wanapokuwa wamepata tatizo kama
Sisi wote bado tutakuwa tunakumbuka jinsi baadhi ya makampuni ya habari yalivyo punguza waandishi wa habari bila kufuata sheria ambazo zinataka mwajiri atoe taarifa kabla ya kuchukua hatua hizo, wala hakuna aliyelipwa.
Lakini pia ikumbukwe kuwa ni mwaka mmoja sasa tangu serikali itoe tamko la wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa wafanyakazi wao mshahara wa kima cha chini laki mbili lakini hakuna aliyefanya hivyo wameendelea kuvunja utaratibu huo bila kuulizwa.
Wanatumia mwanya huo kwa kutambua kuwa hakuna chama au chombo kinachoweza kuwaunganisha waandishi wakadai haki zao leo kitu hicho kinazaliwa hivyo litakuwa jukumu la kwanza kufuatilia tamko
Ndugu wajumbe mliofika hapa, pia ikumbukwe kuwa chama chetu bado ni kichanga hakijapata uongozi, waliopo wanajitolea kuhakikisha moto huu tuliouwasha hauzimiki ni vizuri leo mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali ili kuleta mabadiliko.
Litakuwa jambo jema kama tutashuhudia wachapakazi wapya wakijitokeza kugombea nafasi ambazo tutazipitisha wenyewe kwenye katiba hii ili waweze kutoa mawazo
Yapo majukumu kadhaa na mazito yanayowakabilia viongozi watakaochaguliwa leo, kwanza ni lazima viongozi watakaochaghuliwa leo wawe ni watu wenye moyo wa kujituma kwani chama chetu bado hakijawa na ofisi wala vyanzo vya mapato.
Hivyo inahitaji wakati mwingine viongozi wanachagia wenyewe kutoka mfukoni mwao ili kufanikisha suala lolote, ikiwa ni pamoja na shughuli za uchapaji, kazi hiyo nimekuwa nikiifanya mimi mwenyewe pamoja na kuwa ombaomba lakini nashukru kuwa nimeweza kufanikisha kila kitu.
Nimejitahidi kuhakikisha angalau
Viongozi wa namna hiyo wakijitokeza wataweza kufanikisha shughuli hii ngumu kufikia kikomo, kwani tunataka kabla ya kusajili chama tuwe kwanza na ofisi hivyo viongozi watakaopatika leo wanapaswa kulishughulikia
Ingawa chama chetu bado hakijapatiwa jina lakini nilipendekeza kiitwe TAJOA yaani Tanzania Journalist Association au Tanzania Correspondent Journalis TCJ wote tupo hapa leo ni wajibu wetu kuchagua jina jema na
Pia
Hivyo tunawataka waandishi ambao hawajajiunga watambue kuwa Serikali inakusudia kupitisha msuada wa vyombo vya habari ambao utawaondoa waandishi wote wasio kuwa na elimu angalau miaka miwili hivyo chama hiki kitasadia watu
Lakini pia hivi karibuni umezinduliwa mfuko wa vyombo vya habari TMF hiki chombo kimeweka bayana kuwa hakitatoa pesa kwa mwandishi yoyote bila kudhaminiwa na Press Club yake, Mhariri wake hivyo kumbe bado kuna umhimu wa kuwa mwanachama hiki chama, ambacho naamini baada ya muda kitasambaa mikoani.
Nimalizie kwa kuwashukru wajumbe mliofika hapa kwa lengo la kujadili rasimu ya katiba hii na hatimaye kuwapata viongozi wa chama chetu, niwashukru tena na tena wale ,mlioacha shughuli zenu mkaamua kulipa kipaumbele suala hili.
Ahsanteni
Mwenyekiti wa Muda.
Labels: Nawapenda wote mnaosoma hapa

<< Home