Thursday, October 2, 2008

AKIMU AMFUNGA MTOTO WA MIAKA 3

Hakimu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

HAKIMU mmoja wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma anatuhumiwa kukiuka utawala bora kwa kutumia madaraka yake vibaya, kumweka Mtoto wa Miaka mitatu rumande bila hatia akitaka akabidhiwe mtuhumiwa wake.

Hakimu huyo Dora Musuya anadaiwa kuamuru askari wa Kituo cha kati mjini Dodoma kumshikilia Joel Michael (3) hadi wazazi wa mtoto huyo ambao hata hivyo walikuwa safarini watakapo mpelekea, binti aliyekuwa anamtuhumu kumwibia pesa zake na kujificha kwenye nyumba ya familia hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa masikitiko makubwa baba wa mtoto huyo, Michael Kilango alisema kuwa Hakimu huyo alifikia hatua hiyo miezi miwili iliyopita baada ya kuvamia nyumba yake saa sita usiku akiwa na askari wa tatu pamoja na mme wake ambaye alimtaja kwa jina la Mushi nakuwaamsha wapangaji wa nyumba hiyo kisha kumkamata mtoto huyo na mlezi wake, Rehema.

Wakati askari hao wakifanya tukio hilo wazazi wa mtoto huyo walikuwa safarini, hivyo mtoto huyo alilala kituo cha Polisi kwa siku mbili hata pale ndugu walipojitokeza kumtoa, Hakimu aliweka shinikizo akidai kuwa anataka kwanza apelekewe mtuhumiwa wake aliyekuwa amemwibia pesa na kukimbilia kwenye nyumba hiyo.

“Huyu Hakimu alikuwa anaishi na shangazi yake mdogo ambaye baadaye alidai kuwa alimwibia pesa sh.100,000 na cheni akakimbilia kwangu kwa sababu mke wangu wana undugu naye,mimi na mke wangu tulikuwa safari, ilipofika usiku yule hakimu akakodi maaskari wakavamia nyumbani kwangu akiwa amelewa na walipomkosa mtuhumiwa wakamchukua mwanangu hadi watakapompata mtuhumiwa ndipo wamwachie”alisema Michael

Alisema kuwa hata hivyo baada ya yule mtoto kuanza kuugua kwa kuumwa na Mbu ilibidi wamwachie na baba yake akawa amerudi akampeleka hospitali nakuanza kufuatilia taratibu za sheria ambazo amekuwa akisumbuliwa na kuzuiwa kufungua kesi.

“Baada ya hapo nilikwenda kituo cha Polisi nifungue Malalamiko, mkuu wa kituo akakataa kuchukua maelezo yangu nakuniambia kuwa shukuru mwanao ameachiwa, nikaenda kwa msajili wa mahakama akaniambia niende kwa Hakimu mkuu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma ambaye hata hivyo nilipomuona alishindwa kunisadia zaidi ya kunitaka niende popote”alilalamika Michael

Michael anasema kuwa anaamini ameshindwa kupatiwa msaada wa sheria kutokana na uhusiano wa kibiashara alionao huyo hakimu na mapolisi hao aidha inadaiwa kuwa hata mgahawa wa Polisi unamilikiwa na Mme wa Hakimu huyo alipoulizwa alisema…………