Rais wetu JK,huruma yako ni maumivu kwetu.
Na jack mwambi
KUNA simulizi moja kila ninapoikumba huwa inanifurahisha,kwamba mwanafalsafa mmoja aliwahi kutoa mfano kwamba walikuwepo wavulana watundu wanacheza karibu na bwawa la maji,wakitupa mawe humo.
Kumbe ndani ya bwawa mle kulikuwa na vyura, waliokuwa wanaumia kwa yale mawe mwishowe wakashindwa kuvumilia wakaamua kutamka kwa uchungu’Nyie wavulana kumbukeni kuwa mchezo wenu ni umauti kwetu’ hapo ndio wale wavulana wakashtuka mwanafalsa haendelei hatujui kilichotokea baadaye.
Lakini kisa hicho kinatufundisha nini ‘watoto wa mamantilie’ tanzania hasa baada ya Rais wetu na amiri jeshi mkuu wa ulinzi na usalama Jakaya Kikwete kutangaza rasmi kuwa amewasamehe wakwapuaji wa mali ya umma?
Ambao walijipenyeza hadi kwenye hazina yetu ya kutunzia pesa na kujitotea mabilioni ya shilingi bila ridhaa yetu kisha leo hii wanatamkiwa kuwa wamesamehewa ‘dhambi zao’ili mradi warudishe kile tu walichoiba Benki kuu (BOT)bila hata kuweka Riba yoyote.
Kwa kuwa wengine hatuna ushahidi wa kutosha hatuwezi kutamka kwa uwazi kuwa Rais wetu amewaogapa hao wanaoitwa siku hizi Mafisadi bali tunachosema ni kuwa Rais wetu Kikwete ametumia huruma mno.
Tunamwambia Rais kuwa huruma yake ni maumivu kwetu tena wakati mwingine ni mauti kama yale waliyokuwa wanayapata wale vyura hadi wakaamua kusema ‘nyie wavulana mchezo wenu ni mauti kwetu’
Rais kikwete anapaswa kutambua kuwa wapo vijana zaidi na zaidi wametupwa gerezani kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuiba na wengine bado hawajahukumiwa wanasota gerezani leo unapowasamahe majambazi wa Umma unatupa maumivu makali sisi wazazi ambao watoto wetu wanasota gerezani kwa kuiba kuku au simu.
Insakuwaje wasamehewe watu ambao walikaa pamoja wakaunganisha makampuni ,wakapanga namna ya kuingia hazina na kuchota pesa ambazo zilikuwa kwenye akaunti ya madeni ya nje EPA zaidi ya shilingi Bilioni 133 halafu leo useme wamesamehewa, wajitwishe utajiri wao waende zao!.
Rais wetu kauli uliyotoa siku ya alhamisi 21 Agousti Mwaka huu bungeni kuwa umewapa muda hadi Oktoba 31 Mwaka huu wawe wamerudisha kiasi cha pesa kilichosalia (ambacho hata hivyo hajafahamika vema baada ya takwimu kujikanganya) imetushangaza sana.
Tunajiuliza hivi kumbe mtu akiiba kiasi kikubwa cha pesa husamehewa bila hata kuweka riba tafauti na sisi ambao tunahangaika kwenye mabenki kutafuta mkopo bila mafanikio wakati mwingine wanatupa kwa masharti magumu yanayoshinda wengi?
Rais Kikwete huruma yako imewasononesha, kuwaumiza mawakili na wanasheria wa taifa hili, wameondoka mbele ya Televisheni alipokuwa wanatazamana na kusikiliza hotuba yako wakiwa mikono mitupu! Wanajiuliza tangu lini wewe ukawa hakimu na ukahukumu bila kusikiliza pande zote mlalamikaji na mdaiwa?
Wanasema umewatosa kwenye sekta ya ajira wanahoji ilikuwaje uwasamehe mafisadi wenye pesa bila kuwafikisa mahakamani ili pesa faida waliyochuma wagawane na mawakili wakati wa kuwasimamia kesi na hapo ungekuwa umeongeza ajira ya uhakika wanasheria kadhaa.
Wanajiuliza utawala bora katika serikali yako uko wapi maana hii ni mara ya pili sheria kukiukwa kwa uwazi mara ya kwanza wanadai ni kipindi kile mtuhumiwa wa mauwaji alipopitishwa kwenye mlango wa majaji mahakama kuu inayotoa haki na waandishi wa habari wakapigwa bila msaada wowote unaoonyesha utawala wa sheria.
Licha ya kwamba wananchi hawajasahau hilo umekuja nahii ya kuwasamehe wahujumu uchumi, hapo ndipo tunapojiuliza kuwa kweli nchi hii inautawala wa sheria?

Labels: Tuma picha za mwanao kwa ajili ya saalam na Birthday

<< Home