Sunday, June 1, 2008

MZEE Mpema;Kada wa TANU anayejitosa kumaliza mgogoro wa CCM,CUF



.
*Asema siasa chafu zilianza enzi ya Nyerere

Na Mwandishi wetu

WAKATI Chama cha Wananchi CUF kikigoma kurejea kwenye Mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa Kisiasa Zanzibar,kati yake na CCM, Mzee mmoja amejitokeza nakutaka kuwa mpatanishi atakayekutanisha mahasimu hao wawili aweze kuleta maelewano.

“unapotaka kuwapatanisha wanaogombana kwanza unakutana na upande mmoja unausikiliza na kupima kiwango cha hasira kisha unatoa ushauri kuwa kushusha hasira zile ili iwe rahisi kukutana na upande wa pili vingenevyo watapigana mbele yako” ndivyo anavyoaza kwa kusema Mzee huyo ambaye aliwahi kuwa Kada maarufu wa Chama cha TANU,

Mzee Paul Mpema aliyezaliwa 1924 ambaye amezungumza na Tanzania Daima wiki hii nakushauri atafutwe msuluhishi haraka ili awapatanishe mahasimu hao wawili wa kisiasa Zanzibar.

Mzee Mpema alikuwa akizungumza na Tanzania daima kwenye mahojiano maalum, nyumbani kwake Kigamboni alisema kuwa yuko tayari kuwakutanisha, katibu mkuu wa CUF Maalim Seif na Rais wa Zanzibar Aman Karume ili kumaliza mgogoro huo unaoweza kuleta ,maafa.

Mzee huyo amesema kuwa kwa uzoefu wake alionao kwenye mambo ya siasa ni vigumu vyama hivyo vikafikia kutokana na chuki, dharau waliyojingea kwa kipindi kirefu hivyo kila mmoja hamwamini mwezike.

Alisema kuwa tatizo la mpasuko Zanzibar linazidi kuwa kubwa kutokana na ufahamu mdogo wa Viongozi wa CCM na CUF ambao kila mmoja anasumbuliwa na tatizo la unazi wa kiitikadi.

“CCM inasumbuliwa na Ukereketwa kutokana namatatizo waliyonayo viongozi wake kukumbatia Ukeretwa kila Mwanaccm anapokuwa anazungumzia Mgogoro wa Zanzibar anatanguliza ukeretwa hivyo hata akikosea anajiona yuko sahihi”alisema mzee huyo nakuongeza kuwa tatizo la CUF ni ufurukutwa hivyo ni wananchama wake wanajihisi wanadhulumiwa kila uchaguzi’

Kutokana na ufurukutwa uliojengekeka miongoni mwa Viongozi wa CUF wamekuwa wakilalamikia CCM kuwadhulumu kila uchaguzi ingawa na CCM haitaki kukubali makosa kutokana na Ukereketwa wake.

Anakumbushia kuwa hata yalipofanyika mauwaji kule Zanzibar Mwaka 2001, CCM haikutambua kuwa ni kosa lao limesababisha mauwaji hayo, hata CUF katika kujihisi kuwa imedhulumiwa haikutafuta njia iliyobora kudai haki baadala yake ikaamua kutumia Ubabe wa jino kwa jino CCM ikajibu kwa Dola damu ikamwagika.

Mpema anasema kuwa kama CUF wangetumia njia iliyo bora kama Mahakama kutafuta haki yasingetokea ,lakini wakabaki wanatumia maneno kuwa tutaingia barabarani bila kuwa na silaha huku wakitambua kuwa CCM inadola inayoweza kuwadhibiti.

akizungumzia Mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kwa miezi kumi na nne anasema yameshindwa kupata ufumbuzi kutokana kuwa ya kinafiki na kufanywa siri ya watu wawili ambao ni mahasimu bila kushirikisha vyama vya upinzani ili kuwa mashahidi na kinachozungumzwa.

“CUF na CCM kujifungia wawili eti wanatafuta muafaka wakati wanachukiana ni unafiki hivyo ni vema akatafutwa mpatanishi akawakutanisha wote wawili.. …hata mimi nipo tayari kuwa mshuluhishi wakinichagua kuwapatanisha viongozi hao ili kumaliza mgogoro huo ambao tayari CUF wameonyesha kutumia mbinu zozote kufanikiwa huku CCM ikijivunia dola”anaonya Mpema

Mzee Mpema anasema kuwa hata kama sio yeye atakuwa mpatanishi ni vizuri tasisi mbalimbali zikajitosa kupatanisha vyama hivyo, ingawa yuko tayari kufanya hivyo ,kutokana na uzoefu wa kutatua migogoro aliona kwani anaamini vyama hivyo haviwezi kupatana bila kuwepo msuluhishi kutokana na unafiki wake ambapo wakikutana kwenye vikao hawaaminiani.


“Mwaka 2000 walifikia Muafaka lakini CCM ilishindwa kutekeleza madai ya CUF na Mwaka huu wametuambia kuwa wamefikia muafaka lakini hakuna anayeamini kama kweli madai ya CUF ni ya kweli kwani walifanya siri katika kipiondi chote walichokuwa wanazungumza …
katika ufahamu wangu hawa watu walitakiwa wapate msuluhishi akae nao awapatanishe kabla maafa hayajatufikia” anasema mzee huyo nakusema kuwa kilichopo Zanzibar ni mgogoro sio mpasuko wa kisiasa kama wanavyouita wanasiasa

Akizungumzia mgogoro ulioibuka katika kisiwa cha Pemba anaonya kuwa kutokana na msimamo ulioonyeshwa na wakazi wa kisiwa hicho wakitishia kujivika mabomu Serikali ya CCM isipojirekebisha na kutafakari kwa kina madai yao wanaweza kusababisha mauwaji makubwa nchini.

“tumefikia sehemu mbaya wale wanaotaka kujifunga mabomu watauwa hata wasio kuwemo”nakuwataka chama cha CCM kuacha ulevi wa Madaraka na kuitafakari kauli hiyo ya wapemba kutaka kujilipua huku akionya kuwa kauli hiyo ilitolewa baada ya CCM na CUF kushindwa kufikia muafaka jambo ambalo limerudisha hata maendeleo ya jamii nyuma.

Mzee huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Somangira Kigamboni na Makamu mwenyekiti Wilaya ya Temeke anasema kuwa kama watamwitaji anaouwezo wa kuwakutanisha Viongozi mahasimu Rais Amani Karume wa Zanzibar na katibu Mkuu wa Cuf Seif Shaarif Hamad ili kumaliza kabisa mgogoro huo kwani inaonekana wanashindania uhai wa watu.

“unapotaka kuwapatanisha wanaogombana kwanza unakutana na upande mmoja unausikiliza na kupima kiwango cha hasira kisha unatoa ushauri kuwa kushusha hasira zile ili iwe rahisi kukutana na upande wa pili vingenevyo watapigana mbele yako” anasema mzee Mpema (84) ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke anasema siasa za chuki hazikuanza leo.

Anasema kuwa wakati akiwa kijana wa TANU tawi la Kigoma wao ndio walikuwa wanamsaidia Mwalimu Julias Nyerere kueneza chama hicho kwa watu wakifanya kampeni kwa siri kwa kumuogopa Gavana wa kiingereza.

Anasimulia kuwa Mwaka 1961 uliitishwa uchaguzi mkuu chini ya Serikali ya Mwingereza ambapo vyama viliwili vilikuwa vinaongozwa na waafrika vilikuwa mahasimu kama ilivyo sasa kwa CCM na CUF vyama hivyo vilikuwa ni TANU ya Mwalimu Nyerere na Congress cha Zuberi Mtemvu.

Katika uchaguzi huo ambao nafasi ya juu iliyokuwa inagombewa ni uwaziri mkuu, Chama cha Tanu kiliamua kutumia mbinu chafu kumpaka matope mgombea wa Congress ili asichaguliwe na wananchi.

“mbinu iliyotumiwa na Nyerere kumshinda Mtemvu kirahisi ni kutumia karatasi ya kupigia kura kumchora Simba baadala ya picha halisi ya Mtemvu na Nyerere akachorwa amekaa amekipakata kitufe cha nchi….vijana wa Tanu tukaanza kupita usiku nyumba hadi nyumba tunawaambia wananchi wasimchague Simba atawatafuna bali wamcague Nyerer ndiye alikuwa Mlezi”

Mzee huyo anasema kuwa mbinu hiyo ilitumika kumpa ushindi mkubwa Mwalimu Nyerere lakini baada ya uchaguzi Mtemvu alibaini mchezo huo akaamua kupinga lakini Serikali ya Tanu chini ya Mwalimu Nyerere akiwa Waziri Mkuu iliwatia mbaroni wafuasi wa Congress kwa kuwaita Wahaini.

“Baada ya Mtemvu kufahamu kampeni hizo wafuasi wake wakaanza kudai uchaguzi huru ,Nyerere akawaita Wahaini akaanza kuwakamata waliosalimika walikimbilia nje waliobaki wakasweka ndani jela zikajaa mahabusu ,Serikali ikajitapa ‘tunataka kujenga jela zaidi ili waishie gerezani’na Mwaka 1962 Nyerere alipotawazwa kuwa Rais akapiga marufuku vyama vingi ili kuwavunja nguvu.

Mzee mpema anamaliza kwa kusema kuwa hakushangaa kusikia hivi karibuni wapemba waliojitokeza kudai Serikali ya Shirikishi wakiitwa wahahaini hata hivyo anasema amesikitishwa na kauli zilizotolewa na wapemba kuwa wapo tayari kujilipua huku serikali ikidharau kuwasikiliza madai yao ambayo kimsingi yanamantiki na yanaweza kuleta madhara makubwa kwenye jamii yasiposikilizwa na kutekelezwa nakumaliza kwa kusema Mwenye hekima hakosi Busara.

Mobinsons@yahoo.com .. …0712 17 16 23



Labels: