maelezo ya shindano jipya
Utangulizi
MOBINDAY Tanzania Culture, Beauty and Promotion ni kampuni iliyodhamiria kurejesha heshima ya Tanzania kwa kuandaa tamasha la utamaduni litakalokuwa linatambulisha hadhi na utamaduni wa kila kabila.
Tamasha hilo litakalojulikana kama Shindano la Kumtafuta Malkia wa Utamadauni wa Taifa (SHIKUMATA), litakuwa likifanyika kila mwaka na kutanguliwa na mashindano madogo madogo kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini katika ngazi za tarafa hadi kanda.
Tamasha hilo litakaloanza rasmi mwaka huu, limetayarishwa kwa lengo la kuulinda na kuuenzi utamaduni wetu na wa Mwafrika kwa ujumla, kwani ninaamini kuwa utamaduni wetu ni bora na muhimu kuliko wa mataifa mengine.
Msingi wa tamasha lenyewe
Kampuni ya Mobinday Tanzania Culture, Beauty and Promotion, iliyosajiliwa kihalali kwa Msajili wa Makampuni (BRELA), imeanzisha shindano la kitaifa linalojukana kama 'Mrembo wa Utamaduni wa Taifa'.
Shindano hilo litakuwa likianzia kwenye ngazi za tarafa (vitongojini), kwa kuwashindanisha warembo wa kabila moja.
Mrembo atakayeibuka mshindi kwa kuonyesha uelewa wa kulitangaza kabila lake vizuri nje, hasa katika mila na utamaduni, ndiye atakayekwenda ngazi ya jimbo (wilaya). Hapo ndipo kinyang’anyiro cha kuhusisha kabila na kabila kitakapoanza.
Wakati huo mashindano hayo yatakuwa yanasimamiwa na mawakala watakaokuwa wamepewa kibali maalumu na kampuni ya Mobinday inayoandaa tamasha la kitaifa.
Kila shindano la kuanzia ngazi ya chini kabisa, litakuwa linachukua mshindi kutoka wa kwanza hadi wa tatu.
Hawa watakuwa wanashiriki ngazi inayofuata hadi ngazi ya kanda.
Ni vizuri kila jimbo la ubunge likawa na mshindi atakayeshiriki mashindano ya wilaya au mkoa. (Wakala atakuwa na wajibu wa kuchagua waamuzi wa shindano).
Vigezo vinavyotumika kwa mshiriki au mshindi
* Mshiriki awe Mtanzania anayefahamu vizuri mila na desturi za kabila lake.
* Mshiriki anatakiwa awe jasiri wa kuweza kusimama na kutetea mila na desturi za kabila lake na jamii imuelewe.
*
Mshiriki awe tayari kukabiliana na changamoto hasa za makabila ya watani wao(kama yatakuwapo).
* Mshiriki afahamu vema lugha ya kabila lake na ya Kiswahili kama lugha ya taifa, kwani ndizo zitakazotumika katika shindano.
* Mshiriki awe na umri usiozidi miaka 25.
* Jamii na familia anayotokea iwe imempa baraka zote za kushiriki mashindano. (Wakala atakuwa na mamlaka ya kumtoa mshiriki kutoka kwenye shindano atakapobaini kuwa ana matatizo ya kijamii).
Dhima
Lengo la shindano hili ni kutangaza mila na tamaduni za makabila mbalimbali kwa kuyaenzi na kuyahifadhi.
Sote tunafahamu kwamba kuna makabila yaliyo hatarini kutoweka.
Kwa hiyo mshiriki atakayetokea katika mojawapo ya hayo awe tayari kuyatetea na kuhakikisha anatangaza tatizo hilo kwa jamii ili wasaidiwe.
Vigezo vya kushinda
Ili mshiriki awe mshindi na kutangazwa kuwa mrembo wa utamaduni wa Tanzania atatakiwa aeleze namna atakavyoisaidia jamii yake.
Je, mavazi aliyovaa mshiriki yanaitambulishaje jamii yake, yanavutia au ameiga?
Ni kwa jinsi gani mshiriki ameweza kujieleza mbele watu na kujibu maswali anayoulizwa kuhusu kabila lake, mila na desturi.
Mshiriki anatakiwa ashiriki katika mashindano ya utangulizi kabla ya shindano kubwa la kumpata mshindi wa jumla.
Kila mrembo atapita katika jukwaa liliotayarishwa na kuonyesha mavazi yanayovaliwa nyumbani - jina la vazi, muda wa kuvaa vazi hilo na sehemu vazi kama hilo linapovaliwa.
Mrembo atakapokuwa jukwaani ataeleza historia ya kabila lake, lilikotokea, liliko hivi sasa na kama kabila hilo limesambaa katika mikoa mbalimbali; aina ya maisha wanayoishi na utamaduni wao kwa ujumla.
Mrembo aeleze ubora wa utamaduni wa kabila lake na kuutetea kwa swali lolote atakaloulizwa huku akionekana mchangamfu mwenye uso wa furaha.
Mrembo aonyeshe mavazi ya ubunifu. Vazi litakaloonekana zuri litatangazwa kuwa la taifa kwa kipindi cha mwaka mzima. Katika kila hatua mshindi atapata alama mwishowe zitakajumlishwa na waamuzi na kisha aliyepata kura nyingi atatangazwa mshindi wa jumla.
Baada ya mshindi kupatikana
Baada ya kuwa mshindi kuonekana kuwa amekidhi vigezo vilivyohitajika na kuwazidi wenzake kwa alama, atangazwa kuwa ndiye Malkia wa Utamanduni wa Taifa.
Kuanzia muda huo, mila na tamaduni za kabila lake zitaanza kutangazwa kwenye vyombo vya habari huku aina ya mavazi yake yakichaguliwa kuwa ‘mavazi ya kitaifa kwa mwaka mzima’ hadi atakapopata mrithi.
Mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapewa zawadi mbalimbali zitakazokuwa zimependekezwa na waandaaji wa tamasha na kwa mwaka husika.
Mshindi atawezeshwa kwa kila hali kufanya shughuli zake atakazotaka ikiwa ni pamoja na kuutangaza utamaduni wao.
Umhimu wa tamasha
Shindano hili linaihusisha serikali kwa maana ya taifa kwa kutoa mchango wa kulinda maadili ya nchi na kuyafanya makabila mbalimbali yanayochukiana kuacha vita na kushindana kwa utamaduni, jambo litakaloleta mshikamano na amani pamoja na kuwapatia watu mbalimbali ajira.
Vile vile shindano hili litatumika kulinda na kuendeleza mazingira ikitiliwa maanani kwamba kuna makabila mbalimbali yenye mila zisizoruhusu kukata miti ovyo.
Jambo hilo litaisaidia serikali na kuitangaza nchi kwa kushirikiana na vituo vya utamaduni.
Shindano litakuwa likiboreshwa kadiri miaka inavyokwenda na kadiri inavyowezekana. Na hili litatokana hasa na jinsi jamii itavyolipokea.

<< Home