Miaka miwili ya JK Ikulu na Tuzo ya Vasco Dagama
MWEZI huu Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imetizima Miaka miwili Ikulu tangu ichaguliwe Disemba 14 Mwaka 2005 nakubakiza Miaka miwili na siku 120 pekee kabla ya kuanza tena kwa mchakato wa kuwatafuta wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Wakati Rais Kikwete akitimiza miaka miwili Ikulu mambo yanaoonekana kumwenedea kombo kila kukicha huku Nyota yake iliyongara 2005 ikififia.
Itakumbukukwa kwmaba wakati anawania kuingia Ikulu alikuwa na kauli mbiu yake nzuri ya Maisha bora kwa kila mtanzania huku akiongozwa na falsafa yake ya Ari mpya, Nguvu mpya na kasi Mpya.

JK, Rais wa jamhuri ya TZ akiwa na wahuni wa marekani aka BOYS II MEN yaani wavulana wanaunda kundi la Mzuki Marekani, hiyo ni siku aliyopewa tuzo na wafanyabiashara , baada ya kutumbuzwa na mziki.
Kikwete alikuwa mgombea pekee aliyefanikiwa kuwajaza matumaini makubwa watanzania, wakamwamini na kumpa kura wakidhania kuwa Tumaini jipya la watanzania lilikuwa limerejea huku akipigiwa pambio na wachungaji wa makanisa kuwa ni chaguo la Mungu.
Hata hivyo kwa kipindi hicho alichokaa Madarakani hayo matumaini yameanza kutoweka huku yeye akionekana kutojali kelele zinazopigwa kwa utawala wake kuwa umeshindwa kusimamia vema uchumi wan chi unaoendelea kudidimia na maisha ya wananchi kuwa magumu.
Jambo pekee ambalo sasa Rais Kikwete anaweza kujivunia katika kipindi hiki alichokaa madarakani kama mafanikio yake ni jinsi alivyofanikiwa kuizunguka Dunia kwa ziara zake za mara kwa mara nje ya Nc hi ambazo zimemletea matunda na umaarufu binafsi wa kuweka rekodi kama Rais wa kwanza duniani kufanya ziara nyingi kwa kipindi kifupi.
Kutokana na ziara hizo Mwezi huu akiwa katika ziara zake za kitalii nchini Marekani hatimaye amefanikiwa kutwaa ‘Tuzo ya Msafiri ,Mvumbuzi wa Dunia kutoka Ureno,Vasco Da Gama’ tuzo hiyo ametunikiwa na wafanyabiashara wenye asili ya Afrika waishio nchini Marekani wanaojulikana kama Leon Sullivan.
Waziri wa Mambo ya nje Berndard Membe aliwaambia wandishi wa habari kuwa Leon Sullivan wamemtunukia heshima hiyo Rais Kikwete kwa kukubali mkutano wao ufanyike hapa nchini mjini Arusha ambapo washiriki takribani 3,000 wanatarajiwa kuhudhuria.
hali kadhalika, Sullivan imempa tuzo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye alikuwa Waziri wake wa mambo ya nje kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo Asha-Rose Migiro eti kwa maelezo kuwa ni kutambua juhudi alizozifanya kuimarisha amani kwenye eneo la Maziwa Makuu kipindi alichokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 2006.
Mimi sina ugomvi na Membe najua anazungumzia anachotumwa, wala sihitaji kuzungumzia tuzo ya Migiro najua ni kama kiini macho maana haingii akili kuwa kwa kipindi kifupi ambacho alishika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje aliweza kweli kutoa machango wa kuleta suluhu ya Amani katika ukanda huu wa maziwa makuu? Au wameshindwa kutuamabia kuwa wamempa hiyo kama zawadi baada ya kuwafanikishia kuwakutanisha na huyo Mvumbuzi JK?.
Dhumni la kumpa JK tuzo hiyo sio heshima ni fedheha kubwa kwa Ris kupewa tuzo kama hizi katika kumbi za Starehe akituumbuizwa na kundi na wanamziki wa Marekani Boys II Men (sawa na bongofleva wa hapa) huku akiacha matatizo lukuki hapa nchini, jambo linaloibua maswali mengi.
Tuzo aliyopewa Rais Kikwete kwenye Klub ya usiku inaonekana kumdhalalisha kutokana kwamba imeanza kuibua maswali mengi miongoni mwa jamii wakitaka kujua hiyo tuzo inamaana gani na nini chimbuko lake kwani hatuwezi kuamini maneno ya kirejareja kuwa ametunukiwa kutokana na kukubali kuiruhusu nchi yake iandae mkutano huo hii ni danganya toto.
Kwa sababu suala hapa si kukubali mkutano ufanyike hapa nchini kwani kusingekuwapo kipingamizi chochote, inamaana wanataka tuamini kuwa walikuwa wamekosa sehemu ya kufanyia huo mkutano, ni nchi ngapi walizokuwa wamejaribu wanakataliwa hadi Tanzania ndio iliyowakubalia tu? au wanataka tuamini kuwa ilikuwa kazi ngumu Tanzania kuwakubalia?
Tumekwishambiwa w azi kuwa wapo wajumbe 3000 hawa ni wengi tena wafanyabiashara kwa nchi yoyote ile wangetaka wangeruhusiwa kwa sababu mkutano wao mmoja tu ni sawa na kuwekeza kiwanda, lakini ukweli ni kwamba kinachoonekana hapa kama Kikwete amepewa Tuzo hiyo kama zawadi ya ‘shanga’ili kuruhusu hao wafanyabiashara kupata nafasi kiurahisi ya kugawana maliasili zetu.
Habari zimeanza kusemwa kuwa huo mkutano ambao unatarajiwa kufanayika hapa nchini Juni 2008 ni sawa na ule uliofanyika Mwaka 1884 kule Berlin Ujeruman wakati Wakoloni walipokaa kuligawana bara letu la Afrika na ndicho kitakachofanyika kwa hawa Leon Sullivan.
Wasiwasi huo umezidi kutanda kutoka Arusha hadi Serengeti ambako kunaelezwa huo mkutano utakuwa sawa na biashara ya mwisho ya kuuza nchi kwa Marekani, baada ya kuwa Sehemu kubwa katika Mbuga ya Serengeti imekwisha waangukia wamarekani.
``Tayari tumeshaanza kuunda kamati mbalimbali ili kuweza kuhakikisha kwamba kila kitu kinakamilika kwa wakati kabla ya mkutano huo kuanza mwezi Juni,`` alisema Membe.
Kutokana na hali hiyo Rais Kikwete ameamua kutumia mapumziko ya Disemba wakati akijipongeza kwa kutimiza miaka Miwili Ikulu kwenda kupumzika katika hizo mbuga za Serengeti kunakoelezwa kuwa amekwishajikatia maeneo ya vitalu vya uwindaji.
Ambako sasa anatembelee miradi yake ambayo anatarajia kuionyesha kwa hawa Sullivan watakapookuja hapa nchini ili aweze kupata wakuingia naye ubia wa uwekezaji.
Mbali na mafanikio ya kupata hiyo tuzo ya Ziara tayari kuna mafanikio mengine anayodaiwa kuyapata baada ya kuwa ameamua kufuata nyayo za Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alipoamua kuunda Kampuni na Mke wa iliyojulikana kama ANBEN.
Kwani nay eye anadaiwa kuunda SAKI ambayo imejikita katika kutafuta wawekezaji wa Hoteli za Kitalii na vitalu vya uwindaji Serengeti ndio maana hatoki huko kila Mwaka lazima apate likizo ya kujichimbia humo akiangalia miradi yake inavyokwenda.
kwa hili hatutasubiri atoke madarakani kama Mkapa tunataka maelezo, kwani tayari amekwishaingia ubia na wamarekani ambao wanataka kuanza kujenga uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa mbugani humo ili utumike kuwatorosha wanyama na madini kiurahisi.
Watanzania tuombe huo uwanja utumike kutupora maliasili zetu tu usije ukaingia kwenye kashifa ya kutumika kusafirisha silaha kwenda Somali , Sudan na DRC ya Kongo ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ,hatutakuwa na chakueleza ulimwengu kwani tumeamua kuanzisha uwanja wa kibinfsi katikakati ya Mbuga.
Rais Kikwete ameamua kutumia muda wake mwingi kufanya ziara nje bila sababu huku akifurahia kuitwa Vasco Da Gama anayetalii Dunia kwa kuendelea kukimbilia marekani kila wakati hadi wakosoaji wake wameanza kusema kuwa hata ikifanyika ‘Kitcheni Party’ huko nje lazima aende.
Watu wengi wanajiuliza maswali wanashindwa kupata hasa wanapaotafakali kwa kipindi cha miaka miwili nini alichofanya Ikulu, ameshindwaje kukaa na w ataalam tulio nao ili kujadiliana namna ya kulitoa taifa katika umasikini, huko nje anakwenda kufanya nini, kwa kipindi cha miaka kumi alichokaa wizara ya mambo ya nje hakuweza kujitambulisha?.
Je maisha bora aliyowahidi watanzaniab yatakuja lini, tuseme kwamba hana huwezo wa kuongaza nchi hadi kwenye kilele cha mafanikio mpaka apewe msaada na wamarejani.
Iko wapi ile ahadi ya Maisha bora wananchi wakaichukue,ni kweli hadi sasa viongozi wa Dini wanaamini kuwa ni chaguo la Mungu? Kikwete anampango wa kugombea tena urais 2010? Haya maswali yanahitaji majibu.
Kama lengo la Ziara zake ni kujitambulisha nje ajitambulisha Mara ngapi Marekani kwanini hakutumia mkutano kati ya Nchi za Ulaya na Afrika Uliofanyika Lisbon Ureno akajitambulishe kwa jumla baadala yake akaukacha nakuamua kukimbilia marekani alikotoka miezi michache iliyopoti.
kumbe anakwenda kutunukiwa tuzo ya uvumbuzi wa Dunia Vasco Dagama? Haya maswali na mengine yanatakiwa kujibiwa na malengo ya huo mkutano LEON, Mwisho ni Vipi Rais wetu akatumbuizwe na BOYS II Men awaache hapa Ottu Jazz Band wanamsondo ngoma?
www.mobinday.blogspot.com.. mobinsons@yahoo.com

<< Home