Monday, December 3, 2007

Simu sasa kupigwa kutoka angani

ndege ikiwa angani.
Hivi sasa abiria wa ndege wanaweza

kutumia simu zao za mikononi

wanaposafiri katika anga za Ulaya.
Mipango imeandaliwa na nchi wanachama

wa Umoja wa Ulaya kutumia teknolojia

inayowezesha simu za mkononi kupigwa

bila kusababisha athari zozote za

mawasiliano ya ndege.



mfumo huo wa simu jinsi utakavyokuwa ikiwa BINADAMU ataruhusiwa kupiga simu ndge ikiwa angani

Mabadiliko ya teknolojia yatawezesha

abiria kutumia simu za mkononi wakati
Wasimamizi kote barani Ulaya

wameitisha mashauriano kuhusu

uwezekano wa kutumika kwa teknolojia

hiyo.

Endapo itaidhinishwa, huduma hiyo

itawezesha simu kupigwa tokea angani

wakati ndege ikiwa umbali wa mita 3000

juu.

Mashirika ya ndege yatahitaji kuamua

endapo yanataka kutumia teknolojia,

endapo ruksa itatolewa na idara za

usimamizi za nchi husika.

Je mfumo huu unafanyeje kazi?

Kiwango cha ushirikiano kati ya nchi

za Ulaya itakuwa na maana kwamba simu

za mkononi zinaweza kupigwa wakati

ndege zikiruka katika anga za mataifa

ambayo bado hayajaidhinisha

utekelezaji wa teknolojia hiyo.

Kwa wakati huu matumizi ya simu za

mkononi yamepigwa marufuku kwenye

ndege kwasababu ya kuwepo kwa ushahidi

kwamba zinaweza kuingilia na kuvuruga

mawasiliano na mifumo ya kuongozea

ndege.

Utafiti uliochatangazwa mwaka 2003 na

CAA ulipata matokeo kwamba mawimbi ya

simu za mkononi yanavuruga uongozaji

wa ndege kwa takriban nyuzi tano.

Hatua tofauti

Msemaji wa taasisi ya usimamizi wa

mawasiliano nchini Uingereza ya Ofcom,

ameeleza kwamba bado kuna hatua kadhaa

kabla ya idhini ya mwisho haijatolewa

kuwezesha mpango huo kusambazwa

kikamilifu.

Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa

anga ya Uingereza (CAA), na ile ya

Ulaya, European Aviation Safety

Agency, yanafanya kazi kwa pamoja

kuhakikisha kwamba usalama wa ndege na

abiria unazingatiwa kabla ya mifumo

hiyo kuanza kutumika.


Mawasiliano ya simu za mkononi katika

ndege imekuwa kikwazo kwa abiria

wengi.


Taasisi ya usimamizi wa ndege imesema

kwamba teknolojia hiyo inaweza kuanza

kutumika mwaka ujao wa 2008.

Mfumo unaopendekezwa unatumia kituo

cha ndani ya ndege ambacho kinarusha

mawimbi kwenda simu za mkononi za

abiria.

Vituo vya kurushia mawimbi vya simu za

mkononi vilivyoko ardhini vitapokea na

kusambaza mawasiliano kwa njia ya

satellite kuunganisha na vile vya

ndani ya ndege.Simu zitatozwa kupitia

mitandao ya kawaida ya abiria.

Kwa kuanzia mfumo wa simu utakaotumika

ni 2G pekee, japokuwa Ofcom imesema

endapo kutakuwa na mafanikio, kutakuwa

na uwezekano wa kuzindua kwa mfumo wa

kisasa zaidi wa 3G na mingineyo mipya

itakayoundwa siku za usoni.


taarifa hii imeandaliwa kwa msaada wa

bbc