Laana ya wataafu (EAC) kulitafuna Taifa
Meghji awaambia wastaafu EAC: Wazee tulieni bado tunahakiki mafao yenu
watia kambi Stesheni ya TRL hadi
kieleweke
Na Mobini Sarya.
KWA miaka kadhaa sasa Wazee wastaafu
wa Shirika la Reli lililokuwa chini ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki wanalala
katika stesheni ya Treni Dar es Salaam
wakisubiri rehema za Mwenyezi Mungu
ili waweze kulipwa mafao yao.
wastaafu hao zaidi ya 40 ambao
wanatokea mikoa mbalimbali wakionekana
wamechoka na umri wao kwenda wamesema
walikuja Dar es Salaam miaka mitatu
iliyopita baada ya kuona majina ya
wastaafu yao yakichapishwa kwenye
magazeti kwa ajili ya kulipwa mafao
yao.
Wamesema baada ya kufika Dar es Salaam
walishangaa kuona majina yao hayapo
kwenye orodha ya malipo na
walipofuatilia wakaambiwa wasubiri
ndipo wakaamua kuweka kambi Stesheni
kusubiri Serikali ishughulikie suala
lao.
Ingawa walikuja na vielelezo kamili
baada ya kuona majina yao lakini hata
hivyo waliishia kupigwa kalenda
mwishowe nauli imewashia wameamua
kuishi hapo.
baada ya kuwatembelea katika makazi yao wazee hao
waliniambia kuwa zaidi ya miaka mitatu
sasa wamekuwa wakiishi mahali hapo
huku wakitumia maboksi kama matandiko
ya kulalia wakati wa usiku.
katika mazungumzo yao imebainika kuwa
Wazee hao wanakabiliwa na njaa kali
kwa kukosa chakula na maji ya kuoga na
wala hakuna kikundi chochote cha
watetezi w a haki za binadamu au
wanasiasa waliofika hapo kwa ajili ya
kutoa musaada.
Kero kubwa inayowakabili ni sehemu ya kujisaidia
haja kubwa ambapo wanalazimika kwenda
choo cha kulipia na kutozwa
Sh. 100 kwa kujisaidia mara moja
"Mwanangu tunapoishi hapa matatizo
yetu ni mengi, hatuna chakula wala
maji ya kuoga"Anasema mzee mmoja kwa
uchovu
hata hivyo kinachosikitisha zaidi ni
kuona kwamba wakati serikali ya awamu
ya nne imekuwa ikihubiri kuwa maisha
bora kwa kila mtanzania kwa wazee hao
imekuwa ikivaa miwani ya mbao.
hiyo inatokana na kuwa pamoja na mvua
inakuwa inanyesha wazee hao vikongwe
hubaki kwenye kuta za
majengo ya stesheni bila hata nguo ya
kujifunika wala neti ya kujikinga na
mbu wa malaria.
hapo ndipo yanapozuka maswali je hao
wazee sio binadamu wanaostahili kinga
na maisha bora? serikali na
wanaharakati hawawaoni?
kwa mjibu wa maelezo yao wanasubiri
malipo kamili kutokana na kiasi cha
shilingi bilioni 404/ zilizotolewa na
Malkia wa Uingereza Mwaka
2004.
Fedha hizo zilitangazwa na Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa, kwenye kilele
cha sherehe za Meimosi zilizofanyika
mkoani Mtwara mwaka huo.
wakati nikizungumza nao nilibaini kuwa
wazee hao wamekuwa wakiokota makopo ya
maji majalalani na kuuza ili wapate pesa ya
kununulia sahani moja ya wali.
Mzee Plasdi Marugu(64)kutoka Dodoma
mabaye amepiga kambi hapo kwa miezi
sita sasa anasema awali walikuwa
wanauza makopo hayo kwa kilo shilingi
300 na sasa bei yake imeshuka hadi
shilingi 150 wakati sahani ya chakula
imepanda kutoka shingi 500 hadi 700.
kutokana na mateso wanayoyapata wazee
hao wameanza kufa mmoja mmoja kama
ilivyotokea kwa Laston Mwakabana,
mkazi wa Kyela, Mbeya, ambaye alikuwa
Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia
mafao yake,
hadi amefariki dunia mwezi uliopita
mzee Mwakabana alikuwa analala nje kwa
miaka minne bila msaada wowote. .
wazee hao walisema marehemu alianza
kutapika na kuharisha damu na
walimpeleka Hospitali ambako
aliongezwa damu.
wamesema kuwa marehemu amekuwa
akifuatilia mafao yake jijini kwa
miaka minne bila mafanikio huku akiwa
ameweka makazi yake katika stesheni ya
treni.
wazee hao pamoja na kupata matatizo ya
kulala nje pia wamekuwa kuwa
wakidhulumia haki zao kama John
Herbert ambaye amedai mafao yake
yamepotelea Hazina katika mazingira ya
kutatanisha.
hiyo ni baada ya kukuta hundi yake
imesainiwa na mtu asiyemfahamu.
Herbert ambaye wakati wa EAC alikuwa
akifanya kazi Shirika la Reli Tanzania
(TRC), anadai alifika Hazina, lakini
alishangaa kuona nyaraka zinaonesha
kuwa ameshasaini na kuchukua hundi
wakati hajafanya hivyo.
mstaafu huyo alidai baada ya
kukamilisha taratibu zote za
ufuatiliaji mafao Februari mwaka jana
alitakiwa kwenda kuchukua hundi yake,
lakini baada ya kufika Hazina ndogo
iliyopo eneo la Posta ya Zamani, Dar
es Salaam, aliambiwa kuwa tayari
imeshachukuliwa.
hata alipojaribu kufuatilia hatima
yake ili kujua haki yake ya malipo ya
mafao katika ofisi ndogo ya Hazina
alifukuzwa na wafanyakazi.
Herbert ambaye namba yake ya kazi
ilikuwa ni 668859 alianza kazi mwaka
1968 na kustaafu mwaka 1979 mkoani
Tabora.
pamoja na kilio hicho cha wazee Hazina
imekuwa ngumu kutoa ufafanuzi wa
kinachokuamisha wazee hao wasilipwe
maafao yao yaliyotolewa na Malkia wa
Uingereza.
Tatizo lingine ni kwamba hapa
Tanzania, bado hakuna sera maalum
ambazo zinaelekeza jinsi ambavyo wazee
wanavyoweza kuhudumiwa inapofika
vipindi ambapo wanakosa misaada
mbalimbali ya kibinadamu kutoka kwa
familia zao.
Tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo
wazee wengi wakibaki kunyanyasika na
kutelekezwa hata na familia zao, jambo
ambalo baadhi yao hulazimika kuingia
mitaani na kuwa ombaomba.
Serikali itakuwa inakumbuka vema
Oktoba 18, mwaka 2005 ambapo mamia ya
wasimamizi wa mirathi na wajane
waliandamana na kuvamia ofisi za
Hazina jijini Dar es Salaam wakidai
kupigwa danadana katika mafao ya ndugu
zao waliokuwa watumishi wa Jumuiya
hiyo ambayo ilivunjika mwaka 1977.
familia hizo kipindi hicho zilidai
kwamba, wakati mahakama za mwanzo
zinazosimamia mirathi yao,
ziliwaelekeza kwenda kuchukua madai
yao Hazina, ofisi hiyo ilikuwa
ikiwapiga chenga na kuwasababishia
usumbufu bila kujali kuwa walikuwa
wanatokea mikoani.
watu wamekuwa wakijiuliza kuwa ni
lini Tanzania itafikia hatua kuweka
makambi maalum kwa watu wenye umri
mkubwa na kuwahudumia kwa kila hali
hadi wanapokufa kama mateso yenyewe
ndio hayo.
Wazee hao wameitaka serikali
iwape haki zao sasa badala ya kuendelea
kuwazungusha.
wanasema malipo hayo si
hisani ya serikali bali jasho lao
ambalo kuendelea kulizulia ni dhulma.
wakati Jumuiya hiyo inavunjika baada ya viongozi wakuu wa
nchi husika kutofautiana kisiasa iliacha Mashirika yaliyokuwa chini yake kuwa ni ni pamoja na Reli, Bandari na
Ndege.
jumuiya hiyo ambayo makao yake
makuu yalikuwa Nairobi wenzao
wa Kenya na Uganda walishalipwa mara
tu baada ya kuvunjika.
kadri siku zinavyozidi wazee hao
wanaingiwa na
wasiwasi juu ya uwezekano wa kulipwa
haki zao.
Wakati akihojiwa na chombo kimoja cha
habari cha nje, msemaji wa Hazina
alisema mpaka sasa ofisi yake
imeshawalipa wastaafu wasiopungua 700
na kwamba zoezi hilo linaendelea.
kutokana na kelele kuzidi Waziri wa Fedha Zakia Meghji,hivi karibuni
aliwataka wastaafu hao
kutulia wakati Serikali ikihakiki
malipo yao.
Waziri Meghji anasema hadi sasa
uhakiki unaendelea ili kuhakikisha
kila mstaafu wa Jumuiya hiyo, analipwa
stahili zake kama inavyotakiwa.
anakili kuwa tangu aingie wizarani,
amekutana na malalamiko mengi kuhusu
mafao ya wastaafu hao, wapo wanaodai
kutolipwa kabisa, wapo wanaodai
wamelipwa kidogo na matatizo mengine lukuki.
"Bado uhakiki unaendelea, ili
kuhakikisha kwamba kila mtu anapata
stahili yake kulingana na sheria na
tunaendelea kuwalipa, hivyo basi yafaa
wakawa watulivu wakati uhakiki
ukiendelea," alisisitiza Bi. Meghji.
Akizungumzia kiasi ambacho Serikali
inatakiwa kukilipa, Bi. Meghji alisema
awali Serikali ilitenga sh. bilioni 50
fedha ambazo katika majadiliano
zilionekana ni ndogo, hivyo
zikaongezwa sh. bilioni 67 na kufikia
sh. bilioni 117.
Wastaafu hao wanapozungumzia juu ya tukio
la kifo cha marehemu Mwakabana,
kilichoshangaza katika vyombo vya
habari, wameshangaa kuwa Waziri Basil
Mramba, aliishia kuchangia shilingi
20,000/ tu kwenye tukio hilo kama
rambirambi na kusafirisha mwili wa
marehemu.
"Nafikiri, kutokana na hali ya tukio
hilo kusababishwa na uzembe wa
serikali walau angekuwa makini
kuonyesha jinsi gani anasikitishwa na
tukio hilo, kama vile angemchangia
Mbunge mwenzake", alidai.
Hata hivyo wazee hao kwa pamoja
wamejumuika kutoa masikitiko yao kwa
jamaa wa marehemu Mwakabana, na
kuikumbusha serikali kutekeleza ahadi
zinazoendelea za kuwalipa mafao yao
yasije yakawafika yaliyomfika mwenzao
ya kufia kwenye jalala la mabehewa
chakavu.
watia kambi Stesheni ya TRL hadi
kieleweke
Na Mobini Sarya.
KWA miaka kadhaa sasa Wazee wastaafu
wa Shirika la Reli lililokuwa chini ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki wanalala
katika stesheni ya Treni Dar es Salaam
wakisubiri rehema za Mwenyezi Mungu
ili waweze kulipwa mafao yao.
wastaafu hao zaidi ya 40 ambao
wanatokea mikoa mbalimbali wakionekana
wamechoka na umri wao kwenda wamesema
walikuja Dar es Salaam miaka mitatu
iliyopita baada ya kuona majina ya
wastaafu yao yakichapishwa kwenye
magazeti kwa ajili ya kulipwa mafao
yao.
Wamesema baada ya kufika Dar es Salaam
walishangaa kuona majina yao hayapo
kwenye orodha ya malipo na
walipofuatilia wakaambiwa wasubiri
ndipo wakaamua kuweka kambi Stesheni
kusubiri Serikali ishughulikie suala
lao.
Ingawa walikuja na vielelezo kamili
baada ya kuona majina yao lakini hata
hivyo waliishia kupigwa kalenda
mwishowe nauli imewashia wameamua
kuishi hapo.
baada ya kuwatembelea katika makazi yao wazee hao
waliniambia kuwa zaidi ya miaka mitatu
sasa wamekuwa wakiishi mahali hapo
huku wakitumia maboksi kama matandiko
ya kulalia wakati wa usiku.
katika mazungumzo yao imebainika kuwa
Wazee hao wanakabiliwa na njaa kali
kwa kukosa chakula na maji ya kuoga na
wala hakuna kikundi chochote cha
watetezi w a haki za binadamu au
wanasiasa waliofika hapo kwa ajili ya
kutoa musaada.
Kero kubwa inayowakabili ni sehemu ya kujisaidia
haja kubwa ambapo wanalazimika kwenda
choo cha kulipia na kutozwa
Sh. 100 kwa kujisaidia mara moja
"Mwanangu tunapoishi hapa matatizo
yetu ni mengi, hatuna chakula wala
maji ya kuoga"Anasema mzee mmoja kwa
uchovu
hata hivyo kinachosikitisha zaidi ni
kuona kwamba wakati serikali ya awamu
ya nne imekuwa ikihubiri kuwa maisha
bora kwa kila mtanzania kwa wazee hao
imekuwa ikivaa miwani ya mbao.
hiyo inatokana na kuwa pamoja na mvua
inakuwa inanyesha wazee hao vikongwe
hubaki kwenye kuta za
majengo ya stesheni bila hata nguo ya
kujifunika wala neti ya kujikinga na
mbu wa malaria.
hapo ndipo yanapozuka maswali je hao
wazee sio binadamu wanaostahili kinga
na maisha bora? serikali na
wanaharakati hawawaoni?
kwa mjibu wa maelezo yao wanasubiri
malipo kamili kutokana na kiasi cha
shilingi bilioni 404/ zilizotolewa na
Malkia wa Uingereza Mwaka
2004.
Fedha hizo zilitangazwa na Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa, kwenye kilele
cha sherehe za Meimosi zilizofanyika
mkoani Mtwara mwaka huo.
wakati nikizungumza nao nilibaini kuwa
wazee hao wamekuwa wakiokota makopo ya
maji majalalani na kuuza ili wapate pesa ya
kununulia sahani moja ya wali.
Mzee Plasdi Marugu(64)kutoka Dodoma
mabaye amepiga kambi hapo kwa miezi
sita sasa anasema awali walikuwa
wanauza makopo hayo kwa kilo shilingi
300 na sasa bei yake imeshuka hadi
shilingi 150 wakati sahani ya chakula
imepanda kutoka shingi 500 hadi 700.
kutokana na mateso wanayoyapata wazee
hao wameanza kufa mmoja mmoja kama
ilivyotokea kwa Laston Mwakabana,
mkazi wa Kyela, Mbeya, ambaye alikuwa
Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia
mafao yake,
hadi amefariki dunia mwezi uliopita
mzee Mwakabana alikuwa analala nje kwa
miaka minne bila msaada wowote. .
wazee hao walisema marehemu alianza
kutapika na kuharisha damu na
walimpeleka Hospitali ambako
aliongezwa damu.
wamesema kuwa marehemu amekuwa
akifuatilia mafao yake jijini kwa
miaka minne bila mafanikio huku akiwa
ameweka makazi yake katika stesheni ya
treni.
wazee hao pamoja na kupata matatizo ya
kulala nje pia wamekuwa kuwa
wakidhulumia haki zao kama John
Herbert ambaye amedai mafao yake
yamepotelea Hazina katika mazingira ya
kutatanisha.
hiyo ni baada ya kukuta hundi yake
imesainiwa na mtu asiyemfahamu.
Herbert ambaye wakati wa EAC alikuwa
akifanya kazi Shirika la Reli Tanzania
(TRC), anadai alifika Hazina, lakini
alishangaa kuona nyaraka zinaonesha
kuwa ameshasaini na kuchukua hundi
wakati hajafanya hivyo.
mstaafu huyo alidai baada ya
kukamilisha taratibu zote za
ufuatiliaji mafao Februari mwaka jana
alitakiwa kwenda kuchukua hundi yake,
lakini baada ya kufika Hazina ndogo
iliyopo eneo la Posta ya Zamani, Dar
es Salaam, aliambiwa kuwa tayari
imeshachukuliwa.
hata alipojaribu kufuatilia hatima
yake ili kujua haki yake ya malipo ya
mafao katika ofisi ndogo ya Hazina
alifukuzwa na wafanyakazi.
Herbert ambaye namba yake ya kazi
ilikuwa ni 668859 alianza kazi mwaka
1968 na kustaafu mwaka 1979 mkoani
Tabora.
pamoja na kilio hicho cha wazee Hazina
imekuwa ngumu kutoa ufafanuzi wa
kinachokuamisha wazee hao wasilipwe
maafao yao yaliyotolewa na Malkia wa
Uingereza.
Tatizo lingine ni kwamba hapa
Tanzania, bado hakuna sera maalum
ambazo zinaelekeza jinsi ambavyo wazee
wanavyoweza kuhudumiwa inapofika
vipindi ambapo wanakosa misaada
mbalimbali ya kibinadamu kutoka kwa
familia zao.
Tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo
wazee wengi wakibaki kunyanyasika na
kutelekezwa hata na familia zao, jambo
ambalo baadhi yao hulazimika kuingia
mitaani na kuwa ombaomba.
Serikali itakuwa inakumbuka vema
Oktoba 18, mwaka 2005 ambapo mamia ya
wasimamizi wa mirathi na wajane
waliandamana na kuvamia ofisi za
Hazina jijini Dar es Salaam wakidai
kupigwa danadana katika mafao ya ndugu
zao waliokuwa watumishi wa Jumuiya
hiyo ambayo ilivunjika mwaka 1977.
familia hizo kipindi hicho zilidai
kwamba, wakati mahakama za mwanzo
zinazosimamia mirathi yao,
ziliwaelekeza kwenda kuchukua madai
yao Hazina, ofisi hiyo ilikuwa
ikiwapiga chenga na kuwasababishia
usumbufu bila kujali kuwa walikuwa
wanatokea mikoani.
watu wamekuwa wakijiuliza kuwa ni
lini Tanzania itafikia hatua kuweka
makambi maalum kwa watu wenye umri
mkubwa na kuwahudumia kwa kila hali
hadi wanapokufa kama mateso yenyewe
ndio hayo.
Wazee hao wameitaka serikali
iwape haki zao sasa badala ya kuendelea
kuwazungusha.
wanasema malipo hayo si
hisani ya serikali bali jasho lao
ambalo kuendelea kulizulia ni dhulma.
wakati Jumuiya hiyo inavunjika baada ya viongozi wakuu wa
nchi husika kutofautiana kisiasa iliacha Mashirika yaliyokuwa chini yake kuwa ni ni pamoja na Reli, Bandari na
Ndege.
jumuiya hiyo ambayo makao yake
makuu yalikuwa Nairobi wenzao
wa Kenya na Uganda walishalipwa mara
tu baada ya kuvunjika.
kadri siku zinavyozidi wazee hao
wanaingiwa na
wasiwasi juu ya uwezekano wa kulipwa
haki zao.
Wakati akihojiwa na chombo kimoja cha
habari cha nje, msemaji wa Hazina
alisema mpaka sasa ofisi yake
imeshawalipa wastaafu wasiopungua 700
na kwamba zoezi hilo linaendelea.
kutokana na kelele kuzidi Waziri wa Fedha Zakia Meghji,hivi karibuni
aliwataka wastaafu hao
kutulia wakati Serikali ikihakiki
malipo yao.
Waziri Meghji anasema hadi sasa
uhakiki unaendelea ili kuhakikisha
kila mstaafu wa Jumuiya hiyo, analipwa
stahili zake kama inavyotakiwa.
anakili kuwa tangu aingie wizarani,
amekutana na malalamiko mengi kuhusu
mafao ya wastaafu hao, wapo wanaodai
kutolipwa kabisa, wapo wanaodai
wamelipwa kidogo na matatizo mengine lukuki.
"Bado uhakiki unaendelea, ili
kuhakikisha kwamba kila mtu anapata
stahili yake kulingana na sheria na
tunaendelea kuwalipa, hivyo basi yafaa
wakawa watulivu wakati uhakiki
ukiendelea," alisisitiza Bi. Meghji.
Akizungumzia kiasi ambacho Serikali
inatakiwa kukilipa, Bi. Meghji alisema
awali Serikali ilitenga sh. bilioni 50
fedha ambazo katika majadiliano
zilionekana ni ndogo, hivyo
zikaongezwa sh. bilioni 67 na kufikia
sh. bilioni 117.
Wastaafu hao wanapozungumzia juu ya tukio
la kifo cha marehemu Mwakabana,
kilichoshangaza katika vyombo vya
habari, wameshangaa kuwa Waziri Basil
Mramba, aliishia kuchangia shilingi
20,000/ tu kwenye tukio hilo kama
rambirambi na kusafirisha mwili wa
marehemu.
"Nafikiri, kutokana na hali ya tukio
hilo kusababishwa na uzembe wa
serikali walau angekuwa makini
kuonyesha jinsi gani anasikitishwa na
tukio hilo, kama vile angemchangia
Mbunge mwenzake", alidai.
Hata hivyo wazee hao kwa pamoja
wamejumuika kutoa masikitiko yao kwa
jamaa wa marehemu Mwakabana, na
kuikumbusha serikali kutekeleza ahadi
zinazoendelea za kuwalipa mafao yao
yasije yakawafika yaliyomfika mwenzao
ya kufia kwenye jalala la mabehewa
chakavu.

<< Home