Ziara ya Bush kuleta madhara na kero ya usafiri jijini

Na Mwandishi wetu. Jijini
WAKATI Jiji la Dar es Salaam, likikabiliwa na tatizo la msongamano wa Magari barabarani, Jeshi la Polisi Mkoani hapa,limetangaza kuzifunga barabara kadhaa kwa nyakati toufauti, kuanzia leo alasiri ili kupisha msafara wa Rais George Bush wa Marekani.
Akizungumza na wandishi wa habari jana ofisini kwake,Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfried Tibaigana alisema kuwa kutokana na ziara hiyo jeshi la Polisi limejipanga kufanya ulinzi madhubuti ili ziara hiyo upite salama,ikiwemo kufunga barabara ili kuzingatia Itifaki.
Tibaigana alitaja barabara zitakazofungwa kuwa ni ya Nyerere itakayofungwa leo saa tisa alasiri kuanzia makutano yake na Pugu hadi barabara ya Gerezani kuingia barabara ya sokoine.
Wakati kesho Feburuari 17 itakuwa Barabara ya Sokoine ,Lithuli,Ocean Road,Kivukoni na nyingine ni Gerezani ,Nyerere hadi makutano ya Kawawa , Uhuru na Kawawa hadi Old Bagamoyo, barabara hizo zitafungwa kuanzia asubuhi hadi jioni.
Aidha alitaja barabara zingine zitakazofungwa na watumiaji wake kutakiwa akutafuta njia mbadala kuwa ni ya Ali Hassan Mwinyi,Ocean Road , Lithuli na Sokoine zitakazofungwa Jumapili mchana.
Pia siku ya Jumatatu Feburuari 18 ambayo ni kazi Barabara ya Sokoine ,Ohio,Kivukoni,Gerezani na Nyerere hadi makutano ya Pugu zitafungwa saa za Asubuhi na jioni.
Februari 19 ambayo itakuwa siku ya mwisho ya ziara, barabara ya Sokoine kupitia kivukoni,Gerezani na Nyerere hadi makutano ya Pugu zitafungwa saa za asubuhi nakuwalazimu w atumiaji wake kutafuta njia nyingine.
“kama mtakavyoona barabara hizo zitafungwa kwa hiyo ni vema wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri watapitia barabara mbadala ili kuepuka usumbufu”alisema Tibaigana.
Tibaigana aliwataka wananchi wanaoishi Kigamboni na ambao wanatumia Pantoni kuja mjini barabara ya Kivukoni itafungwa katika makutano yake na barabara ya Luthuli,wanatakiwa watumie barabara ya Luthuli , Shaban Robert ,Samora na Pamba Street kupitia Sokoine Drive.
Kwa wale watakaokuwa wanaelekea Kigamboni barabarani itafungwa katika makutano yake na barabara ya Ohio kwa hiyo wanaelekezwa kutumia barabara ya Sokoine ,Pamba na Samora.
Tibaigana alisema kuwa wafanyakazi wa Mahospitali, Mahakama, na Wizara watakaokuwa katika maeneo yatakayofungwa wahusika wataonyeshwa njia ya kuingia sehemu zao na askari watakaokuwa maeneo hayo.
Watu ambao hawafanyii kazi huko lakini wanashida ya kwenda huko wametakiwa kuacha magari yao pembeni na kwenda kwa miguu.
Hata hivyo Taibaigana hakuwa tayari kufafanua saababu ya kufunga barabara kwa ujumla bila kuacha hata upande mmoja wa kutembea magari kama ambavyo wamekuwa wakifanya saiku zote wanapokuja viongozi wa mataifa ya mengine.
Rais Bush anatarajiwa akutua hapa leo saa tisa alasiri katika ziara yake ya siku saba barani Afrika ambapo hapa nchini atakaa siku nne, kabla ya ujio wake yamejitokeza makundi mbalimbali yanayopinga ziara yake hiyo.
Miongoni mwa makundi hayo ni Tasisi za kiislam, ambazo zilitaka kuandamana kwa siku mbili lakini wakapewa siku moja waliyoandamana jana hadi jangwani,Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani (DARUSO) ,
Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu (UDASA) na Chama cha Wananchi Cuf wilaya ya Temeke ambao wote wamezuiliwa na Polisi kuwa jeshi la Polisi litakuwa katika pilika pilika katika ulinzi hivyo kukosa fursa nzuri ya kuongoza maandamano.

<< Home