Matukio ya Richmond kama mchezo wa kuigiza
Februari 28, 2006: Rais Jakaya Kikwete anatangaza mkakati wa kupata megawati 105 kutoka katika mitambo ya kukodi ya Ubungo na Tegeta.
Machi 31, 2006: Rais Kikwete anaeleza utaratibu wa kupata mitambo ya kukodisha umekamilika na uingizaji wa mitambo hiyo ungefanyika wiki chache zilizofuata baada ya kukamilisha taratibu za manunuzi.
Machi 31, 2006: Rais anasema mitambo hiyo ya kutumia gesi ingefungwa baada ya miezi miwili hadi mitatu.
Juni 23, 2006: Mkataba kati ya Serikali/Tanesco na kampuni ya Richmond Development unasainiwa na kuipa kampuni hiyo jukumu la kweka mitambo hiyo ya dharura ndani ya miezi mitatu ili kukabili natizo la uhaba wa nishati hiyo.
Agosti 25, 2006: Mtambo wa kuzalisha umeme Songas unaharibika na hivyo kuongeza makali zaidi ya umeme kufuatia kushindwa kuzalisha megawati 40. Mgawo unaongeza saa kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 5.00 usiku.
Septemba 15, 2006: Tanesco inahusisha mgawo kwa sekta ya viwanda. Sasa viwanda vinakosa nishati hiyo kwa siku tatu kwa wiki.
Septemba 29, 2006: Waziri wa Nishati na Madini, Dk Ibrahim Msabaha anatangaza kuwa
kampuni ya Richmond kutoka Marekani itazalisha megawati 22.
Septemba 30, 2006: Waziri wa Nishati na Madini, Dk Msabaha anaeleza kuwa kampuni ya Richmond ingeleta mitambo yake na kuanza uzalishaji mwezi Oktoba.
Oktoba 4, 2006: Inatangazwa kuwa Richmond ingeanza kuzalisha umeme Oktoba 20, ikiwa
nyuma ya muda uliokuwa umekubaliwa awali.
Oktoba 8, 2006: Jenereta za Richmond zinatangazwa kuwasili, lakini hazikuletwa.
Oktoba 10, 2006: Gazeti la "The Citizen" linaandika kuhusu utata wa kampuni ya Richmond kufuatia kutofahamika huko Texas Marekani ambako inaelezwa ndipo makao yake makuu.
Oktoba 15, 2006: Wakati utata kuhusu Richmond unaendelea, Rais Kikwete anapangua baraza lake la Mawaziri na kumuondoa Dk Msabaha katika Wizara ya Nishati na Madini na kumsimika Nizar Karamagi.
Oktoba 20, 2006: Richmond inakana kuvunja vipengele vya mkataba na Tanesco kufuatia kushindwa kuanza uzalishaji wa umeme. Hata hivyo taarifa inatolewa kuwa mitambo yake bado iko njiani.
Oktoba 21, 2006: Mitambo ya awali ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Richmond inawasili uwanja wa JK Nyerere, Dar es Salaam.
Oktoba 27, 2006: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahoji juu ya usiri wa gharama za umeme wa kukodi utakaozalishwa na makampuni ya Richmond na Aggreko.
Oktoba 30, 2006: Waziri Mkuu, Edward Lowassa anawaomba wabunge wa CCM wasiibue hoja ya Richmond bungeni. Wabunge hao wanaitii wito na kuliacha suala hilo.
Oktoba 30, 2006: Awamu ya pili ya mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Richmond inawasili uwanja wa JK Nyerere, Dar es Salaam.
Novemba 19, 2006: Wananchi wanalalama kuhusu utata wa uzalishaji umeme kutoka kampuni ya Richmond.
Novemba 23, 2006: Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi anaeleza waandishi wa habari kuwa umeme wa Richmond ndio rahisi kuliko makampuni yote yanayozalisha umeme nchini. Hata hivyo haelezi kuhusu maana ya urahisi huo.
Novemba 24, 2006: Waziri Karamagi anaikana Richmond na kudai kuwa ndani ya wamiliki wa kampuni hiyo hakuna mkono wa mtoto wa kigogo.
Desemba 1, 2006: Rais Kikwete anakwepa kuzungumzia uzembe wa kampuni ya Richmond licha ya kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa hoja hiyo imo katka hotuba yake aliyotakiwa kuitoa siku ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, kitaifa ikiadhimishwa mjini Musoma.
Desemba 10, 2006: Richmond bado inazidi kushindwa kuingiza umeme katika gridi ya taifa, licha ya Waziri Karamagi kuahidi kuwa ingefanya hivyo mwanzoni mwa Desemba.
Desemba 11, 2006: Richmond inalalama kwa kuibua madai yanayoituhumu Tanesco kuwa inawahujumu kwa kuwapatia gesi iliyochanganyikana na mchanga.
Desemba 12, 2006: Richmond na Tanesco zinamhusisha Mkemia Mkuu kuchunguza gesi iliyotolewa na Tanesco kwenda Richmond.
Desemba 15, 2006: Bado umeme megawati 20 hazijazalishwa na magazeti ya Mwananchi na The Citizen yanaandika waliohusika kuandaa mkataba wa Richmond huku Rais akishauriwa kuingilia kati kuufuta lakini haonyeshi kufanya hivyo.
Januari 28, 2007: Wabunge wanadhamiria kupeleka Richmond Bungeni, busara na uzalendo wa Spika inaonekana ndio ngao pekee kwa wakati huo.
Februari 11, 2007: Hoja ya Richmond inagonga mwamba bungeni baada ya kuwasilishwa kwa kuchelewa.
Aprili 15, 2007: Suala la Richmond kupelekwa tena Bungeni baada ya kushindikana kwa vikao viwili vilivyopita.
Novemba 13,2007: Bunge la Jamhuri ya Muungano linaridhia kuundwa kwa Kamati teule ya Bunge Kuichunguza Richmond.
Novemba 16, 2007: Waziri Mkuu Lowassa anaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati Teule akiwa Bungeni Dodoma.
Desemba 05, 2007: Kamati ya Richmond yaeleza nia yake ya kuwachimba wamiliki wa kampuni hiyo
Desemba 13,2007: Kamati yaeleza kuwashtukia watu waliotoa maelezo ya uongo. Majina yao ywekwa kapuni lakini yaahidi kuwaita na kuwahoji kwa mara ya pili.
Desemba 31, 2007: Kamati yakabidhi rasmi ripoti yake kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta.
Februari 01, 2008: Spika anaaga kwenda nchini Marekani na kumpoga 'Stop' Naibu wake Anna Makinda akimtaka kutogusa hoja ya Richmond.
Februari 03,2008: Wabunge wanakataa semina ya Karamagi na kudai ripoti ya Richmond
Februari 04: Spika anaahirisha ziara yake nchini Marekani ili kusimaia hoja hiyo Bungeni.
Februari 05: Wabunge wa CCM wanakaa na kujipanga kwa ajili ya kuikabili hoja hiyo mara itakapowasilishwa Bungeni.
Februari 06, 2008: Makati ya Mwakyembe yawasilisha rasmi hoja hiyo katika kikao cha wabunge mjini Dodoma.

Labels: SAKATA LA MALIMA

<< Home