Wednesday, February 3, 2010

Ada ya mtihani ipo palepale

Wizara yawaambia wazazi walipe haraka

*msamaha utaanza baada ya bajeti

Na Moo Jr. Sarya

MATUMAINI ya wanafunzi wa shule za Sekondari kulipiwa ada ya mtihani na serikali kwa mwaka huu yametoweka baada ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kubainisha kwamba mpango huo utaanza rasmi Mwaka kesho.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, Jana Afisa habari wa wizara hiyo Magdalena Kishiwa alisema kuwa wanafunzi wa Mwaka huu wanapaswa kulipa ada ya mtihani kama kawaida.

Kishiwa alisema kuwa ingawa serikali imefuta ada hiyo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanashindwa kufanya mtihani kwa kukosa pesa ,lakini mpango huo utaanza kutekelezeka baada ya Mwaka wa Pesa unaonza julai.

“ni kweli tayari hata sisi tumepokea malalamiko wazazi wakigoma kulipia watoto wao ada kwa madai kuwa serikali imefuta ada ,lakini wajue kuwa Mwaka pesa unaanza julai,kwa hiyo hata hizo pesandipo zitatengwa”alisema Kishiwa

Alisema kuwa wanafunzi watakaochelewa kulipa ada hiyo wakitegemea Serikali watakumbana na faini au kuzuiliwa matokeo yao kwa mjibu wa taratibu za Baraza la mtihani (NECTA).

Afisa habari huyo ameliambia Tanzania Daima kuwa baadhi ya wananchi waliposikia taarifa hiyo walifikiri inaanza mara moja akutekelezwa bila kujua kuwa lazima kwanza itengwe bajeti ya kuwalipia.

Hivi karibuni Waziri wa Elimu na ufundi, Profesa Jumanne Magembe, alitangaza kufuta ada ya mitihani kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari zinazomilikiwa na serikali tu.

Taarifa hiyo ilitolewa siku chache tu baada ya serikali kueleza sababu za kuendelea kushuka kiwango cha ufaulu nchini.
Pia aliziagiza shule zote za sekondari nchini kutumia mfumo wa kitabu kimoja cha kufundishia, utakaowasaidia watungaji mitihani kuwa na mawazo ya pamoja.
.
“Hii ni changamoto nyingine iliyojitokeza katika majadiliano yetu, takwimu hapa zinaonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi 30,000 walitarajia kufanya mtihani wa kidato cha pili lakini walishindwa kutokana na kukosa ada ya mtihani,” alisaema Profesa Maghembe.

Alisema kwa wanafunzi wa kidato cha pili, serikali itatenga bajeti ya gharama za uchapaji mitihani hiyo kupitia ofisi ya mkaguzi mkuu wa shule, ambapo watahiniwa wa vidato vya nne na sita serikali italiwezesha Baraza la Mitihani la Taifa.

Labels:

Friday, February 15, 2008

Ziara ya Bush kuleta madhara na kero ya usafiri jijini



Na Mwandishi wetu. Jijini

WAKATI Jiji la Dar es Salaam, likikabiliwa na tatizo la msongamano wa Magari barabarani, Jeshi la Polisi Mkoani hapa,limetangaza kuzifunga barabara kadhaa kwa nyakati toufauti, kuanzia leo alasiri ili kupisha msafara wa Rais George Bush wa Marekani.

Akizungumza na wandishi wa habari jana ofisini kwake,Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfried Tibaigana alisema kuwa kutokana na ziara hiyo jeshi la Polisi limejipanga kufanya ulinzi madhubuti ili ziara hiyo upite salama,ikiwemo kufunga barabara ili kuzingatia Itifaki.

Tibaigana alitaja barabara zitakazofungwa kuwa ni ya Nyerere itakayofungwa leo saa tisa alasiri kuanzia makutano yake na Pugu hadi barabara ya Gerezani kuingia barabara ya sokoine.

Wakati kesho Feburuari 17 itakuwa Barabara ya Sokoine ,Lithuli,Ocean Road,Kivukoni na nyingine ni Gerezani ,Nyerere hadi makutano ya Kawawa , Uhuru na Kawawa hadi Old Bagamoyo, barabara hizo zitafungwa kuanzia asubuhi hadi jioni.

Aidha alitaja barabara zingine zitakazofungwa na watumiaji wake kutakiwa akutafuta njia mbadala kuwa ni ya Ali Hassan Mwinyi,Ocean Road , Lithuli na Sokoine zitakazofungwa Jumapili mchana.

Pia siku ya Jumatatu Feburuari 18 ambayo ni kazi Barabara ya Sokoine ,Ohio,Kivukoni,Gerezani na Nyerere hadi makutano ya Pugu zitafungwa saa za Asubuhi na jioni.

Februari 19 ambayo itakuwa siku ya mwisho ya ziara, barabara ya Sokoine kupitia kivukoni,Gerezani na Nyerere hadi makutano ya Pugu zitafungwa saa za asubuhi nakuwalazimu w atumiaji wake kutafuta njia nyingine.

“kama mtakavyoona barabara hizo zitafungwa kwa hiyo ni vema wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri watapitia barabara mbadala ili kuepuka usumbufu”alisema Tibaigana.

Tibaigana aliwataka wananchi wanaoishi Kigamboni na ambao wanatumia Pantoni kuja mjini barabara ya Kivukoni itafungwa katika makutano yake na barabara ya Luthuli,wanatakiwa watumie barabara ya Luthuli , Shaban Robert ,Samora na Pamba Street kupitia Sokoine Drive.

Kwa wale watakaokuwa wanaelekea Kigamboni barabarani itafungwa katika makutano yake na barabara ya Ohio kwa hiyo wanaelekezwa kutumia barabara ya Sokoine ,Pamba na Samora.

Tibaigana alisema kuwa wafanyakazi wa Mahospitali, Mahakama, na Wizara watakaokuwa katika maeneo yatakayofungwa wahusika wataonyeshwa njia ya kuingia sehemu zao na askari watakaokuwa maeneo hayo.

Watu ambao hawafanyii kazi huko lakini wanashida ya kwenda huko wametakiwa kuacha magari yao pembeni na kwenda kwa miguu.

Hata hivyo Taibaigana hakuwa tayari kufafanua saababu ya kufunga barabara kwa ujumla bila kuacha hata upande mmoja wa kutembea magari kama ambavyo wamekuwa wakifanya saiku zote wanapokuja viongozi wa mataifa ya mengine.

Rais Bush anatarajiwa akutua hapa leo saa tisa alasiri katika ziara yake ya siku saba barani Afrika ambapo hapa nchini atakaa siku nne, kabla ya ujio wake yamejitokeza makundi mbalimbali yanayopinga ziara yake hiyo.

Miongoni mwa makundi hayo ni Tasisi za kiislam, ambazo zilitaka kuandamana kwa siku mbili lakini wakapewa siku moja waliyoandamana jana hadi jangwani,Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani (DARUSO) ,

Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu (UDASA) na Chama cha Wananchi Cuf wilaya ya Temeke ambao wote wamezuiliwa na Polisi kuwa jeshi la Polisi litakuwa katika pilika pilika katika ulinzi hivyo kukosa fursa nzuri ya kuongoza maandamano.

Labels:

Wednesday, July 11, 2007

म्बोवे कुम्सोमेशा mtoto

Mwenyekiti CHANDEMA KUMSOMESHA MTOTO HADI MAREKANI.

na Mobini Sarya, Muleba

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ameahidi Kumsomesha mtoto mmoja, Rwechuhura Gozbert na kumgharimikia kila kitu hadi chuo Kikuu, baada ya kumhoji katikati ya mkutano kwanini safarii hakutumia Helcopita.

Katika tukio hilo la aina yake ambalo lilitokea Jumapili iliyopita, kamachumu wilayani Muleba Mtoto huyo wa kike ambaye anakadiriwa kuwa na Umri wa Miaka nane alimkimbilia Mbowe mara tu alipomuona akishuka kutoka kwenye gari akiongozana na viongozi wenzake kwajili ya kuhutubia mkutano wa Hadhara uliokuwa umeandaliwa na umoja wa vyama vya Siasa.

Rwechura baada ya kumuona Mbowe alimkimbilia na kumshika mkono kasha akamsalimia na kumuuliza kuwa Helcopita ikowapi , baada ya swali hilo , Mbowe alishindwa kumjibu , mtoto huyo baadala yake alimbeba juu hadi kwenye meza kuuu walipoketi.

Ilipowadia zamu ya Mbowe kutoa Hotuba alipanda na Mtoto yule jukwani na kuwaambia umati wa watu waliokuwa wammefurika katika viwanja vya Polisi, Kamachumu kuwa hawezi kuhutubia chochote kwani yule mtoto alikuwa amekamilisha hotuba yake.

Akiwa jukwaani alimuuliza yule mtoto kuwa wazazi wake wako wapi , Rwechura aliyekuwa amevalia nguo zilichakaa na mchangamfu alimwambia kuwa baba yake alikuwa anatengeneza Pombe na Mama yake alikuwa anapika chakula.

“ndugu wana wa Muleba siwezi kuhutubia chochote leo kwani hotuba yangu imebebwa na huyu mtoto, maskini , mtoto mdogo bado ananikumbuka mimi , aliponiona tu nashuka kwenye gari alinikimbia na kunishika mkono kasha akaniuliza leo nimeacha wapi ndege, hiyo ndio hotuba yangu kweli huyu mtoto ameniliza nilipomuuliza wazazi wake wako wapi alinijibu kuwa baba yake anatengeza pombe na mama yake anapika hii inaonyesha jinsi nchi yetu ilivyo maskini, ninaahidi kumsomesha kwa kipindi chote cha uhai wangu akita hata marekani atakwenda” alisema Mbowe.

Baada ya maneno hayo alitoa shilingi 20,000 nakumkabidhi huyo mtoto jukwani ili akanunuliwe Nguo kasha akaahidi kuhakikisha kuwa anamsomesha nakumsaidia huyo mtoto kwa kipindi chote cha uhai wake, ili kuona ahadi yake inatekelezwa alimkabidhi huyo mtoto Balozi Cristopher Ngaiza ili awasiline na wazazi wa huyo mtoto kwajili ya kumpeleka Dar es Salaam, kupata elimu.

Labels:

Monday, April 16, 2007

SPIKA STA UMEZOEA KUUZIA ANGALIA USIJE KUPUUZWA

Spika Sitta umezoea kupuuza angalia utapuuziwa,kwa kulea uovu bungeni.

Na Mobini Sarya.

Wiki iliyopita katika kikao cha Bunge kinachoendelea Dodoma Spika wa Bunge Samweli Sita alifanya kile kinachoonekana kama hitimisho la mgogoro uliokuwa umeibuka na kukuzwa akihusishwa na Mbunge wa Mkuranga Adamu Makima.

Katika hitimisho hilo Spika aliendelea kutua uamzi wa kihistoria ambao utaweka kumbukumbu, ilikuwa imepita miezi mitatu tu tangu atoe uamzi mwingine wa kihistoria, alipotamka Bungeni kuwa katika yale Mashitaka mawili yaliyokuwa yamewasilishwa na Mlalamikiwa ,Adamu Malima na Mlalamikaji Mwenyekiti wa Mkampuni ya IPP Regnal Mengi ,hakuna aliyekuwa ameibuka Mashindi.

Kabla ya uamzi wa ke Spika Sita “alisema katika hili watu wengi walitegemea kuona mtu mmoja akiibuka mshindi na Mwingine akishindwa na kupewa adhabu lakini haitakuwa hivyo” alisema Spika, baada ya uamzi wake alisema kuwa angependa kuwakutanisha mlalamiokaji na mlalamikiwa Ofisini kwake ili wayamalize.

Katika uamzi ule watu wengi walidhani kuwa ugomvi ulikuwa umeishia pale kumbe haikuwa hivyo kwani siku chache ililipotiwa kuwa Mbunge Adamu Malima alikuwa hayuko tayari kukutanishwa na Mwenyekiti wa Ipp Mengi Ofisini kwa Spika kwani alikuwa hana ugomvi na Mengi,kama utani mwishowe ikawa kweli kwani Malima hakutia mguu ofisini kwa Spika Bunge liliambiwa .

Baadala yake aliamua kuandika barua ndefu kwenda kwa Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)ambaye yeye ni mbunge anayetokana na chama hicho pamoja na Spika.

lengo likiwa kupata muongozo na utaratibu wa chama ufutwe, akidai kuwa Sita hakumtendea haki katika hukumu yake kwa kumwita muongo kwa madai aliyotoa Bungeni akituhumu vyombo vya habari vya Ipp kuwanyima viongozi wa Serikali muda wa kueleza majanga ya kitaifa.

Uamzi wa Malima kumwandikia Katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba barua ya kuomba chama kujadili swala hilo kilionekana kutaka kulidhalilisha Bunge kwa kutoa mambo yahusuyo Bunge yakajadiliwe nje pia kilitafusiliwa kuwa ni mbinu za kutaka kumng’oa Sita katika kiti chake cha Usipika.

Habari hizo zilikuwa zianakolezwa na uvumi kuwa Malima alikuwa anatumia bila kujua wakubwa Serikalini kama chambo kumyumbisha Sita baada ya kupeleka Kashifa ya madai kuwa kamati ya maadili haki na madaraka ya Bunge iliyokuwa inachunguza Mashitaka ya Mengi na Malima imehongwa ili ismtendee haki Mengi, madai yaliyoibuliwa na Mbunge wa CHADEMA,Philemon Ndesamburo.

Uamzi wa Sipika kuikabidhi Tasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa ,TAKURU’ unadaiwa kuwakera viongozi wengi hasa walioko kwenye mtandao jambo ambalo litapelea wahusika kuitwa kuhojiwa na TAKURU akiwemo Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Kwa mara nyingine tena Sipika Sita ameamua kutoa uamzi ulioweka historia duniani na baada ya kusema bungeni kuwa hukumu pekee anayopaswa kukumbana nayo Mbunge huyo kwa kupeleka mambo ya Bunge nje yakajadiliwe ni kumuuza kwani hata yeye amechafuliwa na kusononeshwa lakini imempasa kumpuuza huku akiwaomba wabunge wampe Malima ushauri nasaha.

Lakini pamoja na kwamba Malima alikuwa amefanya kosa kupeleka kujadili masuala ya bunge nje pia alikuwa na hoja, alikuwa na hoja kwa sababu alijua fika kuwa kama kweli anakosa alitakiwa apewe adhabu sawa na wabunge wengine waliowahi kupewa adhabu akiwemo mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo,aliposema kuwa Waziri ‘mstaafu’ Fredrick Sumaye aliwahi kuwaabia wananchi kuwa wakitaka mambo yao yawanyookee wahamie CCM huku akitumia gharama za Serikali.

Pamoja na kwamba mbunge huyo alitoa uthibitisho ukiwemo ushahidi wa magazeti yaliyoandika siku hiyo lakini hiyo hakutosha kumuepusha na adhabu ya kufungiwa asihudhurie vikao kadhaa vya bunge, kama ilivyokuwa kwa Ndesamburo, Malima alitegemea kuwa kama Bunge limemkuta na tuhuma za kusema uongo angepewa adhabu lakini akasshangaa kuona anaitwa akapatanishwe na mtu ambaye hajawahi kugombana naye!

Tunajiuliza ni kwanini kama Malima alikutwa na hatia ya kulidanganya Bunge letu Tukufu, hakuchukuliwa hatua ya kusimamishwa Vikao kadhaa au kama Busara ilitumika ni kwanini hakutakiwa kukanusha na kumuomba Radhi mwenyekiti wa Ipp ,Reginal Mengi kwa tuhuma alizomtupia zilizokuwa zinalenga kumchonganisha na viongozi wa kitaifa?mbona akina John Cheyo,Zito Kabwe pamoja na Mbunge wa Tarime walilazimishwa kukanusha tarifa zao hata kama zilidhibitishwa kama yule wa Tarime au alilenga kuwadhalalisha wapinzani waonekane hawana hoja? ,

Zaidi swali lililokuwa linaulizwa na kushangaza ni kwa nini Spika hakutumia Busara zake mapema, kuwapatanisha kabla Taifa halijapoteza shilingi milioni 100 kwa kuketi vikao 60 kwa ajili ya kusikiliza shitaka hilo kisha baada ya kutoa uamzi Spika aupuuzie na kusema anakwenda kuwapatanisha.

Spika amefanikiwa kupuuza swala la Malima limeonekana kama limekwisha lakini tunafahamu kuwa bado halijamalizwa kwani limepuuzwa likatupwa kapuni baada ya kushughukiliwa nah ii inatokana kwamba wahusika hawajafahamu chanzo cha tatizo hilo au kama wanakijua wameamua kukipuuza na wao, kwani Malima na Sita hawajahi kugombana leo kwanini iwe hivyo? kuna jambo linafunikwa, wao wanatolewa sadaka tu.

Tunapenda kuelezwa sababu ya Mengi kukwaruzana na Malima na sababu ya vyombo vya Ipp kuhusishwa,na ni nani anayedaiwa kutoa Rushwa ,kwa malengo gani na sababu ya Mfanyabiashara Mwingine maarufu kuhusishwa kwenye kamati hii baada ya majibu hayo mnaweza kutuambia kuwa sasa limekwisha.

Wananchi wanapenda kumwaasa Sita kuwa pamoja na Falsafa yake hiyo mpya ya kupuuza masuala mhimu asiendelee kuitumia kupuuza vitendo viovu kama rushwa na Ubadhirifu bungeni asije akapuuzwa nay eye kisha imani kwa wananchi ikapungua.

Tahadhari hiyo inatolewa baada ya wasiwasi kuanza kuwaingia wananchi kuwa huenda Spika naye anamapungufu makubwa ndiyo maana anajaribu kutimiza kile kinachofahamika kuwa nilinde nikulinde, wasiwasi huo unatokana na jinsi anavyoshughulikia mambo kadhaa bungeni, kwanza alianza kwa kupuuzia tuhuma zilizokuwa zinawakabili wabunge kadhaa wa Bunge la Tanzania, zikiwemo za kughushi elimu yao.

Spika alikaririwa akisema kuwa endapo mbunge angeweza kubainika kuwa alighushi vyeti angemshughulikia ,lakini pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kutumia gharama kubwa kusafiri hadi nchini Uganda kuhakikisha kama kweli mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza, Samweli Chitalilo na kubaini kuwa alidanganya lakini hapo pote Sita ameshindwa kuchukuwa hatua na kupuuza ushahidi wa Polisi kuwa hawezi kuufanyanyia kazi.

Hadi wananchi wenyewe wameamua kumpuuza Spika na kumburuza mbunge wao huyo kortini kitu ambacho ni aibu kwa Spika Sita kushindwa kumtimua mbunge huyo na kusababisha wananchi wa jimbo la Chitalilo kuingia Gharama ya kumfikisha Mahakamani.

Lakini hiyo kama haitoshi imeibuka Kashifa nyingine kubwa na Mbaya inayolihushu Bunge letu linalotegemewa na wananchi, kashifa hiyo imeibuka baada ya kubainika kuwa wabunge wa kadhaa wa Bunge hili wakati wanakula kiapo walidanya bungeni kwa kutaja majimbo tafauti wanayotokea hali ambayo immesababisha kuendelea kuibia bunge, pesa za Umma kwa muda mrefu hadi walipokuja kufahamika,

Pamoja na kwamba wamefahamika kuwa walikuwa wanawaibia Wananchi kodi zao, kwa kulipwa mara mbili ya mahitaji yao lakini Spika amepuuzia hayo madai ameshindwa kuwachukuliwa hatua zozote zaidi ya kuwata tu warejeshe pesa walikuwa wammejichotea ingawa hatuna uhakika ni kiasi gani wameweza kurudisha hadi sasa.

Wabunge hao wanaodaiwa kuhujumu mali ya Nchi ni wale ambao wamechaguliwa kwa viti Maalum ili kuwakilisha makundi yaliyooko kwenye jamii,wakiwamo vijana, wabunge hao inasemekana kwamba wengi wao kutokana na kutokuwa na jimbo wanakaa Dar es Salaam, lakini kule bungeni wamedanganya kuwa wanatokea katika mikoa ya pembezoni mwa nchi ambayo miundombinu yake ni mibovu,\

kwa hiyo walikuwa wanachukuwa kiwango kikubwa cha pesa Marambili hadi tatu ya wabunge wanaotokea Dar es Salaam,mikoa mingine yenye miundombinu bora,hali kama hiyo inaonekana kama ni wizi ulioshamiri bungeni ,tena wa wazi jambo ambalo Spika alitakiwa kulitollea mfano kwa kuwaadhibu wahusika lakini a=mewapuzia na kuwataka warejeshe Pesa bila hata riba!

Spika Sita angalia Falsafa yako hiyo itakuponza unapuuzia vingi utapuuziwa kwani utakuja kupuuzia visyopuzwa, kama alivyokufanya Malima, kama awali ungemchulia hatua usingesononeshwa ,tunakuomba upuuzie yote lakini usipuuzie Rushwa na Mali zetu za NSSF na PSPSF tutazungumza zaidi.

Mobinsons@yahoo.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com website ;www.mobinday.blogspot.com.

Labels: