Tuesday, September 11, 2007

MSANII Jhiko Manyika 'Jhiko Man'

Na Mkolo Kimenya

MSANII Jhiko Manyika 'Jhiko Man', amemaliza ziara yake katika nchi za Ulaya kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kuuza kazi zake ikiwa ni pamoja na albamu yake mpya ya Chikondi ambayo nyimbo zake zinatamba katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza na Tanzania Daima, Dar es Salaam juzi, msanii huyo wa muziki wa Afro Reggae, alisema kuwa amefanya maonyesho kadhaa katika nchi za Finland, Danmark na Spain ambako pia ametumia fursa hiyo kukamilisha albu zake mbili ambazo atazizindua baadae mwaka huu.

Manyika alisema kutokana na kazi yake ya Chikondi kuwa sokoni hivi sasa ameamua kusambaza nyimbo mbili ambazo ni Kuagana na Tupendane ambao unabeba jina la albamu yake hiyo mpya ambayo anatarajia kuizindua baadae mwakani.

Alisema albamu yake hiyo ina nyimbo 10 na ameitayarisha katika nchi tofauti kwa kushirikiana na prodyuza Mikko Rossi na bendi nzima ya Suminators ya nchini Spain.

Alisema kuwa licha ya Catherine Mponda pia amemshirikisha kaka wa msichana huyo aitwae Menard Mponda ambaye anaishi nchini humo "huyu bwana amekua na msaada mkubwa katika kukamilisha albamu hiyo" anasema na kuongeza kuwa watu watarajie mambo makubwa zaidi.

Msanii huyo ambaye ana historia ndefu katika muziki wa Reggae nchini, alisema kwa hapa nchini anaisambaza albamu yake kwa kutumia kampuni yake binafsi ya muziki na mazungumzo yanaendelea baina yake na wasambazaji wengine.

mwisho..........

PETER TOSH

PETER TOSH
Mwanga uliofifia kutokana na kusema ukweli
*hasira zake zilikuwa zikimuweka matatani
*alitaka matumizi ya bangi yahalalishwe Jamaica
*kumbukumbu yake Jamaica ni sawa na sikukuu nyingine


LEO katika kona ya mastaa tutakuwa tunamzungumzia mwanamuziki Peter tosh ambaye alikuwa muhamasishaji wa muziki wa Reggae.

Pamoja na kwamba watu walio wengi wamepandikizwa mizizi ya kuamini kuwa muasisi wa muziki huu ni Bob
Marley wakati si kweli bali Bob alijiunga na kundi la The Wailers akimkuta jamaa akiwa amesha utambulisha muziki huo vilivyo.

Isitoshe Bob baada ya kufika kwenye kundi hilo alikuwa mtaalamu wa kuimba na gitaa alikuwa akifundishwa mtaalamu Peter Tosh.

Historia inaonyesha kwamba Peter Tosh hakuwahi kufundishwa gitaa na mtu ila aliwahi kushuhudia mtu akipiga na alipoachiwa ajaribu kucharaza alicharaza kama mtu yule na hapo ndiyo ikawa mwanzo wa kuwa mpiga gitaa.
Septemba 11 ndiyo siku ambayo mwanamuziki huyu atakuwa alikuwa akikumbukwa siku ambayo Jamaica inaifanya kama sikukuu ya kumkumbuka shujaa wao.

Nchini Jamaica mwanamuziki huyu anachuliwa kama mtetezi wa wanyonge na mpingaji wa matendo ya kinyonyaji, unyanyasaji na ubaguzi hasa kwa watu weusi.

Mwanamuziki Peter Tosh alizaliwa Oktoba 19, 1944 akiwa kama muasisi wa kundi la Wailing Wailers kundi linaloamini kuusambaza muziki wa reggae duniani, likiwa kama waanzilishi wa vuguvugu la Kirastafari.

Mwanamuziki huyo alizaliwa Winston Hubert McIntosh, Peter alikulia Kingston, Jamaica kwenye kitongoji cha watu masikini cha Trenchtown.

Baadhi ya vitu vilivyokuwa vikimsababishia matatizo mwanamuziki huyu ni pamoja na hasira na kutoficha ukweli kwa kile kinachomkwaza.

Nyimbo za Tosh zilianza kusikika zikipigwa kwenye vituo vya redio vya nchini Marekani tangu akiwa kijana mdogo akifundishwa kuimba na mwalimu wake wa sauti, Joe Higgs.

Katika kuutangaza muziki huo alikuwa peke yake na baadae mwalimu wake huyo alimuunganisha na mwanamuziki Bunny na baadae mwaka 1960 alikuja kumuunganisha na Bob Marley.

Baada ya muunganiko huo walitengteneza kundi lililojulikana kama Wailing Wailers.

Wakiwa ndani ya kundi hilo Peter alimaliza kazi ya kumfundisha Bob kupiga gitaa mwaka 1962.

Ukiwaondoa watatu hao pia kundi hilo lilikuwa na waimbaji wengine wa nyuma kama Junior Braithwaite, Beverley Kelso na Cherry Smith.

Wimbo wa kwanza wa The Wailers ulijulikana kama "Simmer Down" wimbo huop uliwapatia mafanikio ambapo mwaka 1965 waliondokewa na wanamuziki wao akina Braithwaite, Kelso na Smith.

Mwaka 1966 Marley na mama yake walihamia Marekani na kukaa miaka miwili na kurejea Jamaica mwaka 1967 ambapo akina Tosh walikuwa wakiendelea kuwakilisha kundi hilo.

Sifa kundi hili ilikuwa ni kuimba kwa sauti ya juu na kucheza vilivyo mitindo ya ska, ikiwa ni pamoja nakupiga reggae iliyochanganywa na mtindo wa rock na mashairi yao yakiegemea kwenye mitazamo ya kisisa na kijamii.

Bendi ya The Wailers ilikuja kuwa bendi ya kuogopeka kwenye visiwa vya Caribbean.

Kutokana na ubora wake huo ilipata dili ya kusaini mkataba wa kufanya kazi na Chris Blackwell aliyekuwa mmiliki wa studi ya Island Records ambapo waliachia kazi yao ya kwanza wakiwa chini ya studio hiyo mwaka 1973 iliyojulikana kama Catch a Fire, mwaka huo huo waliachia kitu kingine kilichokwenda kwa jina la Burnin'.

Mwaka 1973, Tosh alipata ajali ya gali ambapo alipata hasara ya kumpoteza mpenzi wake katika ajali hiyo huku akipasuka fuu la kichwa.

Lakini shujaa huyu alipona, na baadae alisaini mkataba wa kufanya kazi katika studio za Island Records chini ya rais wa studio hiyo, Chris Blackwell ambapo alifanya kazi hizo akiwa nje ya kundi lake hii ilikuwa ni mwaka 1974.

Wakati anajitegemea

Tosh aliamua kujitoa katika kundi la The Wailers kwa madai kuwa mafanikio makubwa yalikuwa yanakwenda kwa Bob Marley kwa sababu tu baba yake alikuwa ni mzungu.

Tatizo kubwa lililowasababisha Tosh na Bunny kuachana ni kutokana na tabia ya wauzaji wa kazi zao kuwa na tabia ya kumtenganisha Bob na kundi kitendo kilichokuwa kikiwapa maudhi wanamuziki wenzake.

Kwa mfano albamu zao nyingi zilikuwa zikiandikwa Bob Marley & the Wailers, kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa inawezekana ni kutokana na uzungu wa baba yake ndfo maana wanampendelea hawa wazungu kwa kumtukuza mzungu mwenzao.

Tosh alianza kutengeneza wimbo wake mwenyewe kwa jina lake la Peter Tosh na aliiachia albamu yake ya Legalize It ambayo ilitoka mwaka 1976 katika studio za CBS.

Wimbo wa kuuzia albamu hiyo ulikuwa Legalize It ambao ulikuwa ukihamasiha uhuru wa matumizi ya bangi kwa watu wote kama manesi, madaktari, mawakili na wengineo.

Wakati akiwa anaomba uhuru wa bangi Marley alikuwa akitoka na nyimbo zenye ujumbe wa kutaka amani na mapendo kwa kupitia wimbo ‘One Love’.

Huku akitumia mbinu za kijeshi, alitoa albamu nyingine iliyokwenda kwa jina la Equal Rights in 1977.

Mwaka 1978 Tosh alialikwa kwenye onyesho la amani lililokuwa likijulikana kama One Love Peace Concert kwa kuanza Tosh aliwafokea hadhira ‘watazamaji’ waliokuwa wamehudhuria onyesho hilo kwa madai kwamba Serikali hiyo ilikuwa haina amani kwani inawanyima watu wengine uhuru, na kwa upande wa Waziri mkuu aliyekuwa amehudhuria tamasha hilo aliwataka kuhalalishe matumizi ya bangi.

Alipokuwa akizungumza maneno hayo alikuwa akiendelea kupuliza kiko chake cha bangi.

Ilipofika zamu ya kuingia Bob Marley aliwaita waliokuwa mahasimu wawili ambao walikuwa mbwa na paka, Waziri Mkuu Michael Manley na mpinzani wake waliyekuwa wakichuana kwenye uchaguzi wakati huo, Edward Seaga jukwaani na kuwaunganisha mikono ikiwa ni ishara ya kuwataka kumaliza tofauti zao na kufanya kampeni zao kwa amani.

Baada ya kumalizika kwa onyesho hilo Tosh alikamatwa na askari kutokana na kuvuta bangi hadharani.

Baada ya kuachiwa alimaliza machungu yakekwa kuachia kibao kilichojulikana kama shit’stem, kilichokuwa kikiiponda serikali na polisi wa Jamaica.

Tosh alikuwa akina fahari pindi alipokuwa akiyaona makovu yake aliyoyapata kutokana na vipigo toka kwa polisi wakati akiwa katika harakati zake za kudai kila anachoamini kilikuwa haki kupata.


Tosh aliwahi kuingia kwenye mtafaruku na Keith Richards, ambaye alikuwa amempatia nyumba ya aliyokuwa akiishi nchini Jamaica wakati wakiwa wanashirikiana.

Tosh alimdhurumu nyumba hiyo kwa madai kwamba alikuwa anamdai fedha kibao kutokana na nyimbo na maonyesho aliyokuwa akiyafanyana kuwa hakuwa na haki ya kumiliki nyumba Jamaica kwa kuwa alikuwa mzungu.

Wakati Richards aliporudi Jamaica kudai nyumba yake hiyo, Tosh alimtoa mbio kwa machine gun.

Baada ya kasheshe kibao kumkuta hatimaye mwaka 1978 Tosh alijipumzisha kwa kutoka na albamu yake iliyojulikana kama Bush Doctor na mwaka ulifuata aliibuka na albamu iliyojulikana kama Mystic Man.

Alikaa mwaka mmoja bila kutoka na kazi nyingine na mwaka 1981 alitoka tena na albamu iliyokwenda kwa jina la Wanted Dread And Alive.

Kama kawaida yake alipumua tena mwaka mmoja na mwaka 1983 alitoka tena na albamu ya Mama Africa, Tosh albamu aliyoitengenezewa Afrika Kusini ambapo likwenda kujipumzisha na kile alichokiita kukwepa hujuma alizokuwa akifanyiwa nchinin mwake.

Kifo
Mwaka 1987, Tosh alitoka na bonge la albamu lililokuwa na wimbo No Nuclear War wimbo ambao ulikuwa ukiwazuia wamarekani kupigana vita ya Nuklia.

Wimbo huo ulijinyakulia tuzo ya Grammy ya wimbo bora wa Reggae wa mwaka 1987 ikiwa ni pamoja na kupewa tuzo ya kuwa mwanamuziki bora wa miaka yote aliyewahi kutokea.

Baada ya watu waliokuwa wakifanya kazi za mwanamuziki Bob Marley aliyekuwa amefariki waliona mwanamuziki huyo analiua soko la Bob hatimaye zikafanyika njama za kutaka kumuua huku wimbo wake huo ukipigwa marufuku kucghezwa nchini Marekani.

Septemba 11, 1987 watu watatu ambao walikuwa wakiongozwa na rafiki yake waliyewahi kukutana naye jela, Dennis 'Leppo' Lobban, ambaye alikuwa mmoja wa watu ambaye alimsaidia kwenye kesi yake ikiwa ni pamoja na kumtafuta kazi mara baada ya kutoka jela kutumikia kifungo chake.

Leppo na wenzie walifika nyumbani kwake na kumuua mbwa wake na kuingia ndani ambapo walimkuta Tosh akicharaza gitaa na kuanza kumdai fedha.

Kwa kuonyesha kuwa alikuwa ameshajua nia yao Tosh aliwaambia kwamba anajua hawakuwa shida na fedha bali mnataka kuniua fanyeni mnavyotaka.

Baada ya kutamka maneno hayo Leppo alichomoa bastola na kumpiga Tosh na hatimaye mwanga wa mshumaa wa watetezi wa wanyonge Jamaica ukatoweka na upepo baharini.

Baada ya kumpiga risasi na kufa walitokomea ambapo inasemekana kuwa wauaji wawili waliuawa na wananchi wenye hasira.

Wakati wasanii hao wakiuawa, kiongozi wao, Leppo alijisalimisha polisi na kufikishwa mahakamani na kutiwa hatiani katika moja ya kesi iliyoendeshwa na kutolewa hukumu kwa muda mfupi katika historia ya Jamaica kwani alihukumiwa kwa dakiaka 11 pekee akihukumiwa kunyongwa, lakini hukumu yake hiyo ilibadilishwa mwaka 1995 na kuwa kifungo cha maisha.

Hapo ikawa mwisho wa maisha ya mtetezi huyo wa haki baada wauaji hao kukatisha maisha yake kwa kumuua nyumbani kwake.

Wengi wanaamini kwamba Tosh aliuawa kwa njama za Serikali za kutaka kumnyamazisha na wapo walioamini inawezekana walipanga kumuua ili kunusuru soko la muziki la Bob Marley ambaye alikuwa ameshafariki.

Mwanae Andrew Tosh ndiye aliyerithi kazi ya baba yake ya kuimba muziki wa reggae.

Mwisho

Makala hii imeandaliwa na Shabani Matutu: anayepatikana kwa barua pepe:kimyamatutu@yahoo.com.

WANAWAKE ambao wamekuwa wakijifungua kwa matatizo

Na Mobini Sarya

WANAWAKE ambao wamekuwa wakijifungua kwa matatizo yanayowalazimisha kufanyiwa upasuaji huenda wakawa wamepata faraja baada ya mtu mmoja kudai kuwa amepata dawa ambayo mwanamke anazaa bila matatizo.

Mganga huyo Musa Yusuf kutoka Ntonya Bagamoyo ameliambia Tanzania Daima katika mahojiano maalum kuwa amepata dawa inayojulikana kama FourtPower Arobaini kamili inayomwezesha mwanamke ambaye angeza kwa kupasuliwa ‘Oparesheni’ kama mtoto amekaa vibaya kujigeuza kwa nusa saa na kuzaa bila matatizo yoyote.

Dawa hiyo ambayo ni mchanganyiko wa madawa 40 ambayo ananunua madukani inadaiwa kuwa imeweza kuponya watu wengi ambao wangefanyiwa upasuaji au walikuwa wamekaa na mamba kwa muda mrefu bila kujifungua.

“Lengo la tiba hii ni hawa wanaopasuliwa kwa sababu mimba imekaa vibaya wasiumizwe tena kwani kumpasua ni sawasawa na kusema kuwa wataalam wamekosa mbinu kabisa yoyote , sasa imepatikana kwanini wapasuliwe wakati kuna mbinu na uwezo”alisema Musa

Aidha mganga huyo amesema kuwa baada ya kuvumbua dawa hiyo nakuonyesha maajabu ya kutibu ikiwamo magonjwa mengine aliomba kibali kwa mganga wa wilaya Bagamoyo ili aruhusiwe kutibu ndani ya Hospitali lakini akambiwa aende Mhimbili ambapo amekuwa akizungushwa na sasa wamemwambia ili kuithibitisha lazima iende kwanza kwa mkemia mkuu.

“nilikwenda katika kitengo cha mizizi Hosptali ya Taifa Mhimbili (MNH) ili waihakiki wanipe kibali cha kufanya kazi popote wakanishauri niende kwenye vyombo vya habari nikajitangaze kwani wao watanichelesha kutokana na mlolongo uliopo”alisema Musa.
mwisho

Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu.

POLISI MJINI MOSHI WAKIONYESHA WANDISHI WA HABARI SILAHA AMBAZO ZILIKUWA ZITUMIKE KWENYE KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI AMBAO WALIUWAWA KATIKA MAJAMBAZI 14 RAIA WAKENYA

Na Ratifa Baranyikwa

JESHI la Polisi limepokea hundi ya sh milioni tano toka benki ya Exim kwa kufanikisha kuyaua majambazi 14 yaliyokuwa yamejiandaa kuvamia benki hiyo tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro yakitokea Kenya

Akikabidhi hundi hiyo jana Makao makuu ya Polisi Jijini Dar es Salaam mbele ya Maofisa waandamizi wa Polisi na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Exim, Sabetha Mwambenja alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na benki hiyo mahususi kwa askari wa Moshi waliofanikisha kuyaua majambazi hayo.

“Tumetoa milioni tano kama shukrani kwa askari ya kule Moshi waliofanikisha katika tukio lile, sasa hivi kama si Jeshi la Polisi tungekuwa tumepoteza pesa na Vijana wetu kule” alisema

Alisema kuwa benki ya Exim ipo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi pia ametoa wito kwa Taasisi za fedha kungalia jinsi ambavyo wanaweza kuunganisha juhudi na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Inspekta Jenelari wa Polisi nchini (IGP) Said Mwema, Mkurugenzi wa Utawala na fedha, Kamishna wa Polisi (CP) Clodwig Mtweve amesema kuwa Jeshi la Polisi linazishauri Taasisi za fedha kuangalia maeneo ambayo ndio chanzo cha kupanga ujambazi.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Ajira na kuzishauri taasisi hizo kuwa makini na watu wanaoingia nao mkataba wa ajira kwani katika uchunguzi wao wamebaini kuwa uhalifu mwingi unatokana na vyanzo vya ndani.

Aidha amewataka kuwaweka mashushushu ndani ya Mabenki ambao si lazima wakafahamika na kwamba Jeshi hilo lipo tayari katika kutoa mafunzo kwa mashushu hao.

“Jeshi la polisi linashauri waunde Intelligence ndani ya Mabenki na si lazima wakafahamika, waje washirikine nasi tutawafundisha , pia suala la ulinzi nalo ni muhimu tunapendelea kamera ambazo zimewekwa kwenye mabenki ziwe connected moja kwa moja na Polisi” alisema

Hata hivyo Mtweve ameziomba Taasisi za fedha kulisaidia Jeshi hilo vifaa mbalimbali ambavyo vitafanikisha katika kupambana na uhalifu

“ Mipaka yetu ya kutoka Tanga mpaka Mara haiku salama kabisa ndugu zetu hapa juzi juzi walitupa piki piki lakini kwa maeneo ya kule piki piki si salama tunahitaji mawasiliano kama magari watu waone kama hili ni changamoto kwao” alisema Mtweve.

Akiongelea tukio hilo , Mtweve alisema kuwa katika tukio hilo la kufanikisha kuyaua majambazi hayo Jeshi la Polisi halikuwa peke yake bali lilishirikiana na Timu aliyounda Rais, Jakaya Kikwete ambaye aliunda timu ya kufanikisha kukamata wahalifu.

“Katika tukio hili Polisi hatukuwa peke yetu kama mlivyosikia, Rais alisema ameunda timu ya kufanikisha kukamata wahalifu, timu hiyo ndio imefanikisha” alisema.

Alisema kuwa sasa hivi Jeshi la Polisi lina falsafa ya Polisi jamii na Polisi shirikishi ambapo mkakati huo umekuja baada ya kuona polisi peke yake haitoshi hivyo ameitaka jamiii kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu.

MWISHO.

Arobaini kamili Neema

CHUO CHA WITS KILICHOOPO JOHANNESBURG AFRIKA KUSINI AMBAPO SEHEMU YA WANAHABARI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI YA AFRIKA WALIPOKUTANA KUJIFUNZA NAMNA YA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI


Arobaini kamili Neema wa wajawazito wanaojifungua kwa matatizo ya upasuaji

Na M.S

“LENGO langu ni kuwasaidia hawa akinamama wanaopasuliwa kwasababu mtoto amekaa vibaya tumboni ,kumfanyia upasuaji mama mjazito kwasabu ameshindwa kuzaa ni kuonyesha kuwa umekosa mbinu yoyote” ndivyo anavyoanza kueleza Musa Yusuf ,mganga aliyegundua dawa ya kusaidia mjamzito anayehitaji uparesheni ajifugue bila kufanyika.

WANAWAKE ambao wamekuwa wakijifungua kwa matatizo yanayowalazimisha kufanyiwa upasuaji huenda wakawa wamepata faraja baada ya mtu mmoja kudai kuwa amepata dawa ambayo mwanamke anazaa bila matatizo.

Mganga huyo Musa Yusuf kutoka Ntonya Bagamoyo ameliambia Tanzania Daima katika mahojiano maalum kuwa amepata dawa inayojulikana kama FourtPower Arobaini kamili inayomwezesha mwanamke ambaye angeza kwa kupasuliwa ‘Oparesheni’ kama mtoto amekaa vibaya kujigeuza kwa nusa saa na kuzaa bila matatizo yoyote.


“nilikwenda katika kitengo cha mizizi Hosptali ya Taifa Mhimbili (MNH) ili waihakiki wanipe kibali cha kufanya kazi popote wakanishauri niende kwenye vyombo vya habari nikajitangaze kwani wao watanichelesha kutokana na mlolongo uliopo”alisema Musa.

Mganga huyo katika mahojiano yake na Tanzania Daima alisema kuwa katika utafiti wake wa miaka sita amefanikiwa kugundua dawa inayojulikana kama ‘MS Fourty power 2007 Arobaini kamili’ ambayo inamaanisha kwamba; M.S inamaana ya jina lake Musa Yusuf na Fourty power 2007 ni mwaka ambao ameanza kuitangaza rasmi dawa hiyo baada ya kuonyesha mafanikio na Arobaini kamili ni mchanganyiko wa aina za madawa arobaini.

“Lengo la tiba hii ni hawa wanaopasuliwa kwa sababu mimba imekaa vibaya wasiumizwe tena kwani kumpasua ni sawasawa na kusema kuwa wataalam wamekosa mbinu kabisa yoyote , sasa imepatikana kwanini wapasuliwe wakati kuna mbinu na uwezo sasa tunao kwanini wapasuliwe wanaumizwa ..unapompasua huyo mama na huna uhakika na nyumbani kwao kama kuna watu watakao mhudumia kwa kipindi chote ”anasema

mganga huyo nakuongeza kuwa baada ya kuvumbua dawa hiyo nakuonyesha maajabu ya kutibu ikiwamo magonjwa mengine aliomba kibali kwa mganga wa wilaya Bagamoyo ili aruhusiwe kutibu ndani ya Hospitali lakini akambiwa aende Mhimbili ambapo amekuwa akizungushwa na sasa wamemwambia ili kuithibitisha lazima iende kwanza kwa mkemia mkuu.

Baada ya Madaktari wa Mhimbili kushuhudia uwezo mkubwa wa dawa hiyo jinsi inavyofanya kazi kwa muda mfupi yaani nusu saa tu Mtoto aliyekaa vibaya tumboni anajigeuza na kuzaliwa bila matatozo walimwabia “Sisi bwana tutakuzungusha wakati hii dawa ingeweza kusaidia na kuokoa maisha ya watu wengi kwani hadi twende kwa mkemia mkuu halafu turudi hapa ndio upewe kibali utakuwa umechelewa ,tunakushauri uongee na wagonjwa kupitia vyombo vya habari” aliwakariri.

Dawa hiyo ambayo ni mchanganyiko wa madawa 40 ambazo ananunua madukani inadaiwa kuwa imeweza kuponya watu wengi ambao wangefanyiwa upasuaji au walikuwa wamekaa na mimba kwa muda mrefu bila kujifungua kwani mara tu anapopewa nusu kijiko ,ikiwa ni unga unaochanywa na maji ya kawaida anakuwa akimaliza kunywa tu mtoto anakuwa tayari kuzaliwa .

Musa anasema kwamba dawa hiyo ya Arobaini kamili sio kwamba inamsaidia mama mjamzito tu bali hata wanayama wengine ambao mimba zimekaa vibaya na magonjwa mengine ni kama ;mtu amekula kitu kibaya kimemkwama moyoni au amemeza sumu yoyote akikorogewa akanywa inaishiwa nguvu , kama miguu inawaka moto au inakufa ganzi ,kama mtu amehehuka akili au kuingiliwa na mashetani ,kama amegongwa na nyoka chango kwa kina mama likiwa limezidi akinywa nusu kijiko tu linakwisha.

Aidha aliyataja magonjwa mengine kuwa ni ngiri kwa wanaume ,ikimshika akanywa nusu kijiko inamchukua dakika tano kuwa amepona ,kwenda hedhi bila kukoma , inauwezo kuponya kidonda ndugu na kusimamisha damu inayochuruzika ,meno kama yanauma mtu akiimung’unya mdomoni anauwa vijijidudu vyote ,Kambako yaani kama makamasi yameganda kichwani akiinusa tu yanaporomoka kukosa hamu ya kula ,kusafisa mkojo ,gesi kujaa tumboni.


Maajabu ya dawa hiyo ni kwamba inaweza kuponya mtoto aliyezaliwa analia tumbo lakini hatari kwa yoka ukimwanga kwenye shimo lake anatoka nje na kufa hataki harafi yake “ kwa maana nyingine hii ni kama X-Lay ukipimwa ugonjwa hospitali ukawa hauonekani ukinywa hii dawa utapona au ugonjwa utaonekana”anasema mzee huyo.

Lakini mzee huyo anatangaza biashara au ana lengo gani? “mimi sifanyi biashara kama unavyoniona ni mtu wa kawaida hata nauli ya kunitoa Bagamoyo hadi hapa inanipa shida lakini lengo langu ninataka kumpata mfadhili atayeniwezesha kuwafikia waagonjwa wote wanaohitaji tiba hii waaliokwama Mahospitali ,kwani unakuta kuna mtu amekaa hopitali kwa muda mwingi hata miezi 15 bila kuzaa

Namtaka mfadhili ili aniwezeshe kumuona Mkemia mkuu wa Serikali aweze kudhibitisha dawa yangu niweze kuanzia hospitali ya mhimbili kuokoa maisha ya akinamama wanaochanwachanwa wakati wa oparesheni kwani sasa wataweza kiaujifungua bila tatizo, ikiwa nitampata mfadahili atanisaidia kununua chupa za kuweka hayo madawa au nipewe mashine iliyoko Keko jijini Dar es Salaam ili nizalishe vidonge vingi kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania” anasema mzee huyo.

Akielezea jinsi utafiti wa dawa hiyo ulivyofanyika anasema kuwa Mwaka 2000 alijiunga na chama madaktari wa asili (MAACO) na akaanza moja kwamoja kutafiti dawa itakayowasaidia akinamama baada ya mama yake kuwa amekufa kwa tatizo hilo baada ya kuipata alianza kutembea anawapa wagonjwa na kila mgonjwa alimwambia amepona ugonjwa fulani hapo ndipo alipouweka katika orodha ya magonjwa yanayotibiwa na dawa hiyo.

Baada ya hapo akaomba kibali kwa serikali ya kijiji cha Kikaro Tarafa ya Miono ili aweze kuokoa maisha ya watu baada ya kupewa akaenda kwa mganga wa wilaya mganga huyo nakuongeza kuwa baada ya kuvumbua dawa hiyo nakuonyesha maajabu ya kutibu ikiwamo magonjwa mengine aliomba kibali kwa mganga wa wilaya Bagamoyo ili aruhusiwe kutibu ndani ya Hospitali lakini akambiwa aende Mhimbili ambapo amekuwa akizungushwa na sasa wamemwambia ili kuithibitisha lazima iende kwanza kwa mkemia mkuu.

Musa anasema kuwa magonjwa haya yanayosimbuwa watu yanaweza kutibiwa na miti shamba mtu akapona kabisa ikiwa serikali itaweka utaratibu mzuri wa kuwatambua ,akitolea mfano dawa yake anasema kuwa kama sheria zingekuwa sawa leo hii angekuwa anaokoa maelfu ya akinamama wanaopoteza maisha yao kwa kushindwa kujifungua salama.

Mzee huyo anayeonekana wa makamo ambaye na mtu wa kawaida huenda anatembea na utajili mkubwa ikiwa atapatikana mfadhili amsaidie kupata japo mashine ya kuzalisha dawa hiyo zaidi nakuuzwa kimataifa kwaani ikiwa dawa hiyo kama anavyosema imeweza kuzalisha akinamama bila kufanyia upasuaji huenda ni neema nyingine kwa Taifa letu.

0753 399579 .,, 0782 62 97 65,,,0787 62 97 65