Thursday, October 2, 2008

AKIMU AMFUNGA MTOTO WA MIAKA 3

Hakimu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

HAKIMU mmoja wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma anatuhumiwa kukiuka utawala bora kwa kutumia madaraka yake vibaya, kumweka Mtoto wa Miaka mitatu rumande bila hatia akitaka akabidhiwe mtuhumiwa wake.

Hakimu huyo Dora Musuya anadaiwa kuamuru askari wa Kituo cha kati mjini Dodoma kumshikilia Joel Michael (3) hadi wazazi wa mtoto huyo ambao hata hivyo walikuwa safarini watakapo mpelekea, binti aliyekuwa anamtuhumu kumwibia pesa zake na kujificha kwenye nyumba ya familia hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa masikitiko makubwa baba wa mtoto huyo, Michael Kilango alisema kuwa Hakimu huyo alifikia hatua hiyo miezi miwili iliyopita baada ya kuvamia nyumba yake saa sita usiku akiwa na askari wa tatu pamoja na mme wake ambaye alimtaja kwa jina la Mushi nakuwaamsha wapangaji wa nyumba hiyo kisha kumkamata mtoto huyo na mlezi wake, Rehema.

Wakati askari hao wakifanya tukio hilo wazazi wa mtoto huyo walikuwa safarini, hivyo mtoto huyo alilala kituo cha Polisi kwa siku mbili hata pale ndugu walipojitokeza kumtoa, Hakimu aliweka shinikizo akidai kuwa anataka kwanza apelekewe mtuhumiwa wake aliyekuwa amemwibia pesa na kukimbilia kwenye nyumba hiyo.

“Huyu Hakimu alikuwa anaishi na shangazi yake mdogo ambaye baadaye alidai kuwa alimwibia pesa sh.100,000 na cheni akakimbilia kwangu kwa sababu mke wangu wana undugu naye,mimi na mke wangu tulikuwa safari, ilipofika usiku yule hakimu akakodi maaskari wakavamia nyumbani kwangu akiwa amelewa na walipomkosa mtuhumiwa wakamchukua mwanangu hadi watakapompata mtuhumiwa ndipo wamwachie”alisema Michael

Alisema kuwa hata hivyo baada ya yule mtoto kuanza kuugua kwa kuumwa na Mbu ilibidi wamwachie na baba yake akawa amerudi akampeleka hospitali nakuanza kufuatilia taratibu za sheria ambazo amekuwa akisumbuliwa na kuzuiwa kufungua kesi.

“Baada ya hapo nilikwenda kituo cha Polisi nifungue Malalamiko, mkuu wa kituo akakataa kuchukua maelezo yangu nakuniambia kuwa shukuru mwanao ameachiwa, nikaenda kwa msajili wa mahakama akaniambia niende kwa Hakimu mkuu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma ambaye hata hivyo nilipomuona alishindwa kunisadia zaidi ya kunitaka niende popote”alilalamika Michael

Michael anasema kuwa anaamini ameshindwa kupatiwa msaada wa sheria kutokana na uhusiano wa kibiashara alionao huyo hakimu na mapolisi hao aidha inadaiwa kuwa hata mgahawa wa Polisi unamilikiwa na Mme wa Hakimu huyo alipoulizwa alisema…………

Dk.Slaa ,Sitta, chunga domo lako

Pole mama hawa ndio wanasiasa wetu

Na Mwandishi Wetu

“Kauli hii ni nzito,ni ya kihuni imenishtua na inalenga kunidhalalisha mimi mwenyewe na familia, Staki malumbano naye nasubili kikao cha familia ndicho kitakachotoa majibu ,nimekwishawasiliana na wanafamilia, wamefadhaika mno” hayo ni maneno ya uchungu aliyatoa wiki hii mjane wa Marehemu Chacha Wangwe akieleza kushtushwa na kauli za wanasiasa wetu.

Bi Mariam Wangwe amejikuta akidhalalishwa na wanasiasa wetu tunaowatarajia kutuongoza katika siku za usoni baada ya kutoa rai yake kama raia akitaka kifo cha Mme wake ambaye alikuwa Mbunge wa Tarime kichunguzwe, lakini matokeo yake ameambulia kashifa za nguoni.

Ni vizuri ifahamike kuwa moja ya sifa mhimu anayopaswa kuwa nayo kiongozi akaheshimika kwenye jamii na isimchoke ni kutokuwa mnafiki anayebadilika kimsimamo na kuogopa kukosolewa.

Hata kiongozi wa Dini anaposimama mbele ya jukwaa kuanza kuwakemea waumini wake waache dhambi ya uzinzi na zinaa, anapaswa kutambua kuwa hiyo dhambi itakapomkuta mke wake awe tayari kuikemea bila uoga kama alivyokuwa akiwakemea wengine.

Mfano huo hauna tafauti na viongozi wa kisiasa ambao muda mwingi huutumia kuwashutumu wapinzani wao kwa kuwaporomoshea makashifa kibao ,sawa na viongozi wa dini wanavyomkemea shetani kila wakati ili aonekane mbaya wanadamu wamuasi.

Kwa kuwa viongozi wa kisiasa ni mahodari wa kuibulia maadui zao kashfa ili wachafuke hatuimaye waachane na siasa ni vizuri na wao yanapowakuta wawe tayari kukabiliana nayo kwa hoja sio kwa vitisho vivyokuwa na maana.

Ninaandika hivyo kutokana na kauli tata zilizotolewa wiki iliyopita na wanasiasa wawili machachari ambao ni mabingwa wa kutupa makomboro ya wenzao kwenye vyombo vya habari, Spika wa Bunge Samweli Stta na yule katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa.
Viongozi hawa wawili ni miongoni mwa viongozi wachache ambao jamii ya watanzania inawategemea kuweza kumrithi Rais Jakaya Kikwete mara atakapoondoka madarakani, lakini kwa mshangao wa wengi wamekuwa wapayukaji wanaokosa sifa maridhwa za kuwa viongozi wa Taifa hili.

Dk.Slaa ambaye aliwahi kuwa Paroko anatajwa kuwa ni miongoni mwa viongozi wa kambi ya upinzani wenye ushawishi atakayegombea urais wa jamhuri hii mara baada ya kuondoka Kikwete, pia Spika Stta ambaye aliwahi kuwa mwanasheria wa serikali anatajwa miongoni mwa wana-CCM wenye nia na tama ya kumrithi Kikwete.

Lakini kwa nyakati tofauti wanasiasa hawa wamekuwa mabingwa wa upayukaji wanaotoa maneno yasiyo na staa wala ueledi kwenye jamii jambo linalowapunguzia nafasi ya kuwa viongozi tegemeo.

Jambo moja la umhimu kuliko mifano mingi ambayo ningeitoa hapa ni kwamba wiki iliyopita wanasiasa hao wamekaririwa wakimkemea na kumdhihaki mjane wa Marehemu Chacha Wangwe aliyekuwa mbunge wa Tarime.

Marehemu Wangwe alifariki Dunia Julai 28 usiki akitokea bungeni Dodoma kuja Dar es Salaam, akiendeshwa na kijana mmoja anayetajwa kuwa Deus Mally waliyejuana naye muda mufupi kabla ya mauti kumkuta.

Tangu kifo hicho kitokee yameibuka maneno mengi na maswali yasiyo na majibu huku kukiwepo taarifa kuwa mado majibu ya ripoti mbili zilizochunguzwa mwili wa marehemu juu ya kifo gani alifariki hajifunguliwa bado.

Ikumbukwe kuwa awali marehemu alifanyiwa uchunguzi na mganga mkuu wa Dodoma baadaye akapelekwa wilayani Tarime akazikwe alipofika huko, ndugu na wananchi wa jimbo wakasema hawaridhiki na namna mpendwa wao alivyofariki wangependa afanyiwe uchunguz tena.jambo lilikubaliwa.

Msemaji wa familia hiyo Prof.Samweli Wangwe akiongoza jopo la watu kadhaa walipeleka mwili wa Marehemu kuchunguzwa upya kwenye hosipitali ya wilaya ya Tarime kisha jioni hiyo hiyo wakaenda kuzika kimya kimya, waliohudhuria mazishi hayo kwa wingi ni mapolisi na ndugu waliokuwa wanalala kwenye msiba pekee.

Licha ya Prof.Wangwe ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM kutoa taarifa kuwa wamegundua hakupigwa risasi tafauti na madai ya awali lakini taarifa za uchunguzi huo hazikutolewa hadharani na hadi leo ripoti hiyo imefungwa pamoja na kuendelea kuwepo madai kuwa alionekana amechomwa na kitu chenye ncha kali.

Wakati ripoti hizo zikiwa zimefungwa na familia kutokupewa taarifa rasmi juu ya kilichomuua ndugu yao, Prof. Wangwe alifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nakuaambia kuwa bado wanamashaka na kifo kile, wangependa polisi wafanye uchunguzi zaidi ni hapo yalianza kuibuka maswali ya ripoti hizo.

Lakini baadaye polisi yenyewe ilisema kwa haraka kuwa ilishamaliza uchunguzi wao hivyo haina sababu ya kuendelea kufanya uchunguzi,majibu hayo hayakuridhisha familia ndio maana baada ya miezi miwili mjane wa Marehemu, Mariam Wangwe ameona bunge ni chombo pekee alichoelekezea matumaini yake.

Akaomba wa Spika Sitta aunde tume kuchunguza kifo hicho kama ambavyo amewahi kufanya katika suala la mkataba tata wa Richmond ,ambao tayari ulikuwa umekwisha chunguzwa na Tasisi ya kupambana na Rushwa (TAKUKURU)ikadai kuwa ni safi lakini bunge lilipounda tume ikabainika madudu.

Kwa matazamo huo ndio maana huyo mama alifikia hatua ya kuomba Spika Sitta mtu anayejitapa kuwa anafanyakazi kwa kasi yenye viwango aunde tume kuchunguza mkasa huo lakini kwa mshango wa wengi, Sitta amelipuka na kumwonya mama huyo asikurupuke kumpelekea mzigo huo kwani kufanya hivyo ni kugongana na vyombo vingine vya sheria.

Wakati Sitta akilipuka ,Dk. Silla naye naye ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa anayeongea bila kupima athali za maneno yake kwenye jamii kwani amemkana mama huyo kuwa sio mke wa marehemu!

Maneno ya kashfa na dharau alizotoa huyo Paroko hayakutegemewa kutolewa na kiongozi aliyekuwa anaheshimika kama yeye, tulitarajia kuwasikia wale tuliozoea kusikia wanaitwa waropokaji.

Slaa alipaswa kunyamaza au kutoa hoja za busara kuliko kuanza kumshambulia huyo mama ambaye bado anauchungu wa kupotelewa na Mme wake aliyekuwa tegemeo la familia.

Kwanza ukimuuliza Sipaka Sitta sababu ya kuidhinisha bunge likaunda tume ya kuanza kupita mkataba huo ambao ulikuwa umekwisha chunguzwa na Takukuru sijui kama takuwa na jibu lolote la kutupa.

Leo analipuka kama mwenzake kwa kumtolea huyo maneno yanoonyesha kuwa kumbe hata ile tume huenda aliiunda kwa shinikizo maalum, kama sivyo kwa nini kifo cha mbunge ashindwe au kwanini atoe majibu ya hovyo?

Sitta amewahi kunukuliwa akiwaita wapinzani wake kuwa ni wanasiasa wanaoendekeza siasa za maji taka ,wakati Dk.Slaa aliposikia habari za kupigwa kwa Mwanasheria wa NCCR-Mageuzi Dk.Sengondo Mvungi baada ya kukemea wafuasi wake yeye akachochoea kwa kusema ni domo limemponza.

Kwanza Slaa akijua kuwa yeye ni kiongozi wa Dini anayejua maana ya ndoa na familia ni kwanini amekurupuka na kutoa kauli inayoonyesha kama kumtaliki mke wa marehemu hivyo kumweka kwenye kundi la kutengwa.

Jambo lingine amefikia hatua ya kumtishia huyu mjane kuwa anyamaze asije akamtobolea siri, jamii ya watanzania inapenda kujua ni siri gani hizo Slaa anazojua nakuzitunza?

Leo kama Slaa anafikia hatua ya kupambana na mke wa marehemu kwenye majukwaa ya kisiasa ni jambo linaloonyesha wazi kuwa ule usemi usemao ngoma ikilia sana hupasuka umefika kikomo.

Kwa maneno hayo aliyoyatoa mwanasiasa huyo sio ya kuvumilia kwa mwanaharakati yoyote yule anayependa haki, leo anapoibuka mtu mwenye akili timamu na kutoa maneno yenye kukatisha tamaa yanayoweza kuvuruga familia tutarajie nini:?

Huyu Slaa ndio wapinzani wanajivunia kuwa wanakiongozi ambaye atasimama kugombea urais kipindi kijacho, je tumtarajie mtu kama huyo anayetoa maneno yasiyo na staha kuongoza jamii ya watanzania au tumtazamie mwingine.

Slaa na Spika Sitta wamekosa sifa ya kuwa viongozi wa jamii ,wameoneka ni watu wa kutoa maneno yenye kinyaa sawa na wapiga debe wa vijiweni , Sitta kama hawezi kuunda tume angesema wazi kuliko kutoa shutuma ambazo zimemdhalalisha hata yeye mwenyewe.

Tukimuuliza kwanini aliunda tume ya kuchunguza mkataba wa Richmond, wakati tayari ulikuwa umeishapitiwa atakuwa na lakujibu? ,mbona kwenye uchunguzi wa kifo cha Wangwe Polisi wameishafunga uchunguzi na wamesema kuwa ni kosa la usalama wa barabarani?

Je Spika anashindwa nini?au amerika na majibu hayo si angeleza kwa utaratibu, pole sana mama Wangwe hawa ndio wanasiasa wetu wasio na huruma, wanakula hata nyumbani kwa wajane, uliwategemea sasa wameonekana wazi ni mbwa mwitu wasiojificha. Unafiki wao umeonekana

Sunday, September 28, 2008

FOMU YA KUJIUNGA NA TASISI YETU

TASISI YA KAYA NA FAMILIA (TAKAFA)

OMBI LA HATI YA KUJIUNGA NA TAKAFA

JALADA NA…………….
PICHA YA MUOMBAJI

ADA;-Tsh.12,000/=

MAELEZO MHIMU

1.Ombi hili lijazwe na muombaji mwenyewe anayetaka kuwa mwanachama

2.FOMU IJAZWE KWA HERUFI KUBWA (HABARI BINAFSI)

JINA LA UKOO……….……..JINA LA KATI………………….JINA LA MWISHO
MAHALI PA KUZALIWA KIJIJI/MTAA……………………..KATA/SHEHIA…………

WILAYA……………………MKOA………………….NCHI………………JINSIA
MKE ………………MME

UREFU WA MITA…….. SENTIMETA… RANGI YA MACHO ……..RANGI YA NYWELE…….

ALAMA YA PEKEE MWILINI………

TAREHE YA KUZALIWA …………………….MWEZI………….MWAKA…………..

KAZI………………………………..

HABARI ZA NDOA.. SINAMKE………..NINANDOA………….MFIWA…………..MTALAKA…………

JINA LA ZAMANI……………………………….ANANUANI YA POSTA……………………….

SIMU……………………….BARUA PEPE………………………..FAKSI…………………….

MAHALI UNAPOISHI..MTAA/KIJIJI………………. NYUMBA NAMBA………………………

KATA /SHEHIA…………..WILAYA…………………..MKOA………………

Labels:

Rais wetu JK,huruma yako ni maumivu kwetu.

Na jack mwambi

KUNA simulizi moja kila ninapoikumba huwa inanifurahisha,kwamba mwanafalsafa mmoja aliwahi kutoa mfano kwamba walikuwepo wavulana watundu wanacheza karibu na bwawa la maji,wakitupa mawe humo.

Kumbe ndani ya bwawa mle kulikuwa na vyura, waliokuwa wanaumia kwa yale mawe mwishowe wakashindwa kuvumilia wakaamua kutamka kwa uchungu’Nyie wavulana kumbukeni kuwa mchezo wenu ni umauti kwetu’ hapo ndio wale wavulana wakashtuka mwanafalsa haendelei hatujui kilichotokea baadaye.

Lakini kisa hicho kinatufundisha nini ‘watoto wa mamantilie’ tanzania hasa baada ya Rais wetu na amiri jeshi mkuu wa ulinzi na usalama Jakaya Kikwete kutangaza rasmi kuwa amewasamehe wakwapuaji wa mali ya umma?

Ambao walijipenyeza hadi kwenye hazina yetu ya kutunzia pesa na kujitotea mabilioni ya shilingi bila ridhaa yetu kisha leo hii wanatamkiwa kuwa wamesamehewa ‘dhambi zao’ili mradi warudishe kile tu walichoiba Benki kuu (BOT)bila hata kuweka Riba yoyote.

Kwa kuwa wengine hatuna ushahidi wa kutosha hatuwezi kutamka kwa uwazi kuwa Rais wetu amewaogapa hao wanaoitwa siku hizi Mafisadi bali tunachosema ni kuwa Rais wetu Kikwete ametumia huruma mno.

Tunamwambia Rais kuwa huruma yake ni maumivu kwetu tena wakati mwingine ni mauti kama yale waliyokuwa wanayapata wale vyura hadi wakaamua kusema ‘nyie wavulana mchezo wenu ni mauti kwetu’

Rais kikwete anapaswa kutambua kuwa wapo vijana zaidi na zaidi wametupwa gerezani kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuiba na wengine bado hawajahukumiwa wanasota gerezani leo unapowasamahe majambazi wa Umma unatupa maumivu makali sisi wazazi ambao watoto wetu wanasota gerezani kwa kuiba kuku au simu.

Insakuwaje wasamehewe watu ambao walikaa pamoja wakaunganisha makampuni ,wakapanga namna ya kuingia hazina na kuchota pesa ambazo zilikuwa kwenye akaunti ya madeni ya nje EPA zaidi ya shilingi Bilioni 133 halafu leo useme wamesamehewa, wajitwishe utajiri wao waende zao!.

Rais wetu kauli uliyotoa siku ya alhamisi 21 Agousti Mwaka huu bungeni kuwa umewapa muda hadi Oktoba 31 Mwaka huu wawe wamerudisha kiasi cha pesa kilichosalia (ambacho hata hivyo hajafahamika vema baada ya takwimu kujikanganya) imetushangaza sana.

Tunajiuliza hivi kumbe mtu akiiba kiasi kikubwa cha pesa husamehewa bila hata kuweka riba tafauti na sisi ambao tunahangaika kwenye mabenki kutafuta mkopo bila mafanikio wakati mwingine wanatupa kwa masharti magumu yanayoshinda wengi?

Rais Kikwete huruma yako imewasononesha, kuwaumiza mawakili na wanasheria wa taifa hili, wameondoka mbele ya Televisheni alipokuwa wanatazamana na kusikiliza hotuba yako wakiwa mikono mitupu! Wanajiuliza tangu lini wewe ukawa hakimu na ukahukumu bila kusikiliza pande zote mlalamikaji na mdaiwa?

Wanasema umewatosa kwenye sekta ya ajira wanahoji ilikuwaje uwasamehe mafisadi wenye pesa bila kuwafikisa mahakamani ili pesa faida waliyochuma wagawane na mawakili wakati wa kuwasimamia kesi na hapo ungekuwa umeongeza ajira ya uhakika wanasheria kadhaa.

Wanajiuliza utawala bora katika serikali yako uko wapi maana hii ni mara ya pili sheria kukiukwa kwa uwazi mara ya kwanza wanadai ni kipindi kile mtuhumiwa wa mauwaji alipopitishwa kwenye mlango wa majaji mahakama kuu inayotoa haki na waandishi wa habari wakapigwa bila msaada wowote unaoonyesha utawala wa sheria.

Licha ya kwamba wananchi hawajasahau hilo umekuja nahii ya kuwasamehe wahujumu uchumi, hapo ndipo tunapojiuliza kuwa kweli nchi hii inautawala wa sheria?