
MIMI NI KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 23 MTANZANIA NAKAA JIJINI DAR ES salaam kwa muda kutokana kwamba ndipo nafanyia kazi zangu.
nilizaliwa miaka 23 iliyopita katika Familia ya wakulima na wafugaji wilayani Tarime mkoani Mara kaskazini Mwa Tanzania, tangu nimezaliwa sikumbuki nisiku gani niliamka toka asubuhi hadi jioni nikiwa na furaha, isipokuwa nachofahamu nikuwa kila siku kwangua ni huzumi tu.
nimekuwa nikipata huzuni kwangu mwenyewe kwa kukumbwa na ugumu wa maisha yanasabisha nashindwa kupata hata riziki ya kutwa wakati mwingine hujikuta nikiambulia maji au chuisi inayouzwa mitaa ya Posta kwa bei ya chini.
lakini pia kinachokuwa kinaniskitisha kikubwa ninapofuatilia natukio ya ulimwengu kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya habari, kama tukio liliotangazwa kuwa aliyekuwa Mtawala wa Iraq Bw. Sadam Hussein ameuwa kwa kunyongwa baadala ya kudaiwa kuwa aliwauwa wananchi wake mwaka 1982 lilinisononesha sana.
nilijiuliza maswali mengi kuwa watawala wa hii dunia wameuwa watu wangapi mbona wapo hawajashitakiwa? karibu kila matawala anayeingia madarakani hujaribu kuzima wakosoajo wake kwa kuwauwa lakini pia huyo Sadamu Hussein inasadikiwa kuwa Silaha alizotumia kuwauwa WAKURD 102 ALIPEWA NA MAREKANI, SWALI HAPA LINI KIONGOZI WA MAREKANI RAIS GEORGE BUSH ATAFIKISHWA MAHAKAMANI NA HATIMAYE KUWEKEWA KITANZIA KAMA WANAVYOSEMA WAO AUWAYE KWA UPANGA NA YEYE ATAUWAWA?
SIO HIVYO TU BUSH AMEUWA MAELFU WAKATI SADDAM AMEUWA ELFU ZAKE ANAPASWA KUWAWA KWA KUUWA MAELFU YA AKINAMAMA NA WATOTO KULE AFGANSTAN NA IRAQ.
Pamoja na hayo mimi huwa muda mwingi nahuzunika napopata taarifa kwamba mtu au jamii fulani imenyanyaswa hata na serikali yake iliyoiweka madarakani ndio maana wakati mwingine huwa napingana waziwazi na jinsi serikali inaposimamia sera ya kuwahamisha wananchi kwa nguvu kutoka maeneo inayosema hayaruhusiwa kama wamachinga na wachimabaji wadogo wadogo migodini.
pia mimi sijaoa wala sina mwenza ndoto zangu kama zingetimia siku moja nimepanga kuowa watoto wawili mapacha niwafanye kuwa wake zangu,napenda sana siku moja kuwaowa mabinti wanaofanana, nitamshukuru mtu yeyote atakayefanikisha azima hiyo kwa kunijulisha walipo mabinti hao, sifa kuu lazima wawe wanafanana sana nitaendelea kuweka mawasiliano wazi.
vilevile kwa imani mimi ni mkristo wa dhehebu la wasabato lakini huwa nakerwa na migogoro ya makanisa hata kwenye kanaisa letu ipob kwani kwa sasa hivi limegawanyika makundi mawili wapo wanaokubali mwanamke awe kiongozi wapo wanaokataa.
elimu yangu ni kidato cha nne ninahitaji au natafuta mfadhili popote pale alipo aweze kunisomesha nirudie mtihani wa kidato cha nne ili niweze kuendelea vema na masomo, kitaaluma ni mwaandishi wa habari , naishi kwenye nyumba aliyojenga baba bado sijawa na uwezo wa kujenga nyumba kwani kipato changu ni kidogo.
Labels: SOMA maisha yangu jinsi yalivyo jaa utata