Kibajaji na mjamzito wa Tanzania
Uchambuzi
Na Mobini Sarya
Ni bunge la kumi katika utawala wa awamu ya nne, kipindi cha pili cha Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ni katika kipindi hiki ambapo bunge la kumi chini ya Spika wa kwanza Mwanamke,Mhe.Anna Makinda linaendelea katika kikao chake mjini Dodoma.
Katika kikao hicho macho na masikio ya wananchi yameelekea bungeni kusikia na kutazama yanayojiri huko.
Kila Mtanzania akiulizwa atoe maoni yake kuhusu mtazamo wake wa kile kinachoendelea mjini Dodoma atakuwa na maoni ya tofauti.
Lakini swali moja ambalo kila mmoja anaweza kujiuliza kichwani mwake ni kwamba ‘je wabunge wa Tanzania hasa wa sasa wanamwakilisha nani?.
Yale yanayojadiliwa bungeni ni kwa manufaa ya wabunge au wananchi ambao waliwatuma kama wawakilishi wao?.
Kawaida mbunge ni mteule aliyechaguliwa na wananchi kama mwakilishi wao anayepaswa kutumwa Serikalini kuwakilisha mahitaji ya wananchi waliomchagua.
Sehemu muhimu na ya kwanza anayopaswa kuwaikilisha ni mahitaji ya wananchi wake bungeni,ambapo bunge ni sehemu pekee inayopitisha bajeti na kuwauliza mawaziri wanaoiwakilisha Serikali maswali.
Kwa hiyo kabla mbunge hajaenda bungeni anapaswa kufanya mkutano na wakazi wa jimbo lake ili wampe kile atakachokiwakilisha bungeni kwa niaba yao.
Hata hivyo tofauti na matarajio hayo wabunge sasa wamegeuza bunge kama sehemu ya kuwakilisha maslahi yao binafsi, bila kujua kuwa wao ni ‘watumishi’ wa jimbo.
Katika kikao cha pili cha bunge la kumi kinachoendelea Mjini Dodoma, wabunge wamekuwa wakijadili hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Novemba Mwaka jana.
Miongoni mwa mambo ambayo Rais Kikwete aliyazungumza kwenye hotuba hiyo na ambayo yamekuwa yakijadiliwa na wabunge ni Serikali kukusudia kusambaza Pikipiki za matairi matatu yaani Bajaj nchi nzima.
Serikali ilitoa taarifa hiyo kwa mara ya kwanza kwenye hotuba ya bajeti ya Mwaka 2010/2011, ambapo Waziri wa Afya wakati huo,ni Prof.David Mwakyusa alisema zitasambazwa bajaj 400 ili zitumike kama ‘ambulace’ya kusafirisha wajawazito kwenda hospitalini.
Hilo ni moja ya mambo yanayoyojadiliwa kwenye hotuba hiyo huku wabunge wengi wakionekana kuunga mkono mpango huo wa kusambaza bajaji kama ambulace ya kuwakimbiza akinamama wajawazito kwenye vituo vya afya.
Ni mbunge mmoja wa jimbo la Ngorongoro ndiye ameonekana kuwakilisha mawazo ya wananchi wa jimbo lake pale alipo kataa bungeni ‘msaada huo’kwa kutamka kuwa bajaji sio usafiri muafaka katika jimbo lake.
Mbunge huyo alijenga hoja kuwa katika jimbo lake na baadhi ya majimbo mengine,kuna milima na mabonde ambayo bajaji haiwezi kumudu kupita kwenye njia hizo kumwaisha mama mjamzito hospitalini pamoja na kuwabeba watu wengine wa kumsaidia mjamzito huyo.
Wakati wabunge wengine wakipigia makofi ‘msaada’huo wanaoona kama ni mkombozi atakayesaidia kupunguza vifo vya akinamama na watoto, wao wameendelea kuvuna mamilioni ya Pesa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka bungeni zimeeleza kuwa kila mbunge amezoa shilingi Milioni 90 kwa ajili ya kununua gari ya usafiri wao.
Bunge la Tanzania linawabunge 360 ikiwa ni pungufu ya majimbo 239 yanayowakilishwa na wabunge wote wa kuchaguliwa.
Kwa hiyo, wabunge kupokea Milioni 90 kwa ajili ya kununua magari yao huku wakipongeza mpango wa Serikali kusambaza bajaji za Shilingi mil.tatu kwa ajili kuwabeba wajawazito ni dharau kwa wapiga kura.
Na hii inatia shaka kama wabunge wetu wanawakilisha mawazo ya wapiga kura wao bungeni.
Akizungumzia dharau hiyo mbunge wa Arusha mjini,Godbless Lema ameshangazwa na kitendo hicho kwa kile alichosema “hali hii ni mbaya ,siku moja tutafanya maandamano bungeni inashangaza kuona tumepewa Milion.90 za magari kwa wabunge wote huku bungeni tunajadili bajaji kuwa ambulace kwa akinamama”.
Wabunge hao ambao wengine hata suala la barabara za lami ni kitendawili kwenye majimbo yao wamekubaliana na mpango huo kama vile hawajui kuwa hizo bajaji matumizi yake ni kwenye lami tu.
Kama wabunge wengi wangekuwa wanawakilisha mawazo ya wapiga kura wao,wangewauliza mpango huo na bila shaka wangetambua kuwa haufai kabisa.
Ni bora watumie hizo Milion.90 kununua ambulace kwa ajili ya wajawazito kama kweli wao ni wawakilishi wa wananachi halafu wajitafutie usafiri mwingine wa gharama nafuu.
Litakuwa ni jambo kuwakejeli wananchi wao, hasa wazazi kama mbunge ataingia Kijijini akiwa na shangingi la milioni 90 huku nyuma akiburuza bajaji kwa ajili ya ambulance ya wagonjwa.Hapo ndipo yanapoibuka matabaka ya watawala na watawaliwa hivyo kuweka pengo kubwa kati ya wananchi na viongozi.
Aidha wabunge hao kwa sasa wanaonekana kama malaika walioshuka kutoka mbinguni hivyo kutosimamia masuala yanayotuhusu wapiga kura wao.
Wabunge hao wameomba bima ya afya itakayowawezesha kutibiwa nje ya nchi au katika hospitali binafsi hawataki huduma katika hospitali za Serikali maana haziwafai kulingana na hadhi yao.
Wao ni akina nani? wametoka wapi? wamesahau kuwa ni watumishi wa jimbo?wanataka wakatibiwe nje watajuaje matatizo yaliyoopo kwenye hospitali hizo ili wawakilishe matatizo hayo Serikalini ziboreshwe?.
www.mobinday.blogspot.com