Wednesday, March 16, 2011

majina ya waliochaguliwa kidato cha tano yatangazwa

wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi leo imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi vya serikali.

majina hayo yametangazwa na waziri wa elimu Dk.Shukuru kawambwa kufuatia kukamilika kwa uchaguzi uliofanyika mara baada ya kutangazwa ,matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.
Dk.Kawambwa ametaja idadi ya wanafunzi hao wanaojiunga na kidato cha tano mwaka huu kuwa ni 36366, wasichana wakiwa ni 11210 na wavulana wakiwa ni 25156.

kwa upande wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi ni 916 wakiwemo wasichana 861.

aidha Dk.Kawambwa amesema kuwa vigezo vilivyotumika kuwachagua wanafunzi hao ni pamoja na umri usiozidi miaka 25 awe amefaulu alama 3 na ufaulu wa daraja la kwanza hadi 3.
pia wanafunzi waliochaguliwa kwenye fani ya ufundi wanatakiwa wawe wamefaulu masomo yaPCM kutokana na sifa hizo wanafunzi 29 wamekosa nafasi kwa kufuka umri huo.

Waziri kawambwa amesema kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti April 3 Mwaka huu katika shule walizopangiwa kabla majina ya awamu ya pili hayajataangazwa.

kamati ya umeme yazinduliwa

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Jairo amezindua kamati ya wataalamu ya kusimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme .
Akiitangaza kamati ya wataalamu ya kusimamia utekelezaji wa mradi wa STIGLER`S GORGE mbele ya waandishi wa habari katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawati 2100 za umeme ambapo juhudi hizo zilianza miaka ya 1970 kwa kufanya upembuzi yakinifu kwa msaada wa Serikali ya Norway.
Kwa mujibu wa Gairo Mradi huo ambao upo chini ya Wizara ya Nishati na Madini sasa umeundiwa kamati ya wataalamu ya kusimamia utekelezaji wake ili kuendeleza uzalishaji wa nishati ya umeme nchini .Zaidi anaelezea utekelezaji wa sera na sheria za nishati na madini unaosimamiwa na wizara ya nishati na madini. CLIPP.
akitaja umuhimu wa mradi huo katibu jairo amesema ni matarajio yake kuwa Wizara ya Nishati na Madini itatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuandaa njia bora za kusimamia uendelezaji wa mradi na kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua kwa lengo la kuendeleza mradi bila kuathiri mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini.
Ili kufanikisha mradi huo serikali imeunda kamati ya kuusimamia iliyochini ya wizara ya nishati na madini ikiongozwa na mhandisi Bashir J.Mrindoko,Theophillo Bwakea, Leonard Masanja na Bw.Joram Kangete
Wajumbe wengine ni kutoka Ofisi ya Rais Tume ya mipango, Wizara ya maji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kilimo chakula na ushirika na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
Pia kamati hiyo imejumuisha wajumbe kutoka ewura na tanesko.
Kama mradi huu wa STIGLER`S GORGE utafanikiwa na megawati 2100 za umeme kuzalishwa, Tanzania itakuwa imetokomeza kabisa tatizo la umeme na itakuwa na uwezo wa kuuza nishati hiyo kwa nchi nyengine.