Monday, December 4, 2023

Mtoto wa miaka 4 adaiwa kubakwa Mogo, Kipawa

Njama za kupotosha ukweli zapangwa atoroshwe.

Na Tanpresstz,Kipawa

mtoto wa miaka 4 anayedaiwa kubakwa
VITA ya ukatili wa kijinsia inazidi kuwa ngumu kutokana na matukio ubakaji kufichwa na familia za wahanga likiwemo lililotokea mtaa wa Mogo kata ya Kipawa kwa mtoto wa miaka 4 kubakwa.

Taarifa zilizofikia shirika la habari  vijijini,Tanpresstz zinahabarisha kwamba kumekuwepo na njama kubwa za kutaka kufifisha tukio hilo lililotokea Disemba mosi 2023 kuripotiwa kituo cha Polisi Staki shari Disemba 2.

taarifa ya kitabibu iliyopelekwa kituo cha Polisi sitaki Shari ambayo inadai alichezwa tu kwa maelezo aliyopewa mlezi na Polisi.

Akizungumza na Tanpresstz Katibu Elimu,Malezi na Mazingira (EMAU) Tawi la Mogo kupitia Jumuiya ya Wazazi (CCM) Forget Chakupewa anasema kuwa tukio hilo walilipata siku zikiwa zimepita huku muathirika akiwa ndani.

“Sisi kama viongozi wa Jumuiya tulipokea taarifa siku ikiwa imepita tulipofuatilia tukakuta huyo mtoto anaugulia maumivu huku walezi wake wakiendelea kumkanda na maji ya moto tukachukua jukumu la kumpeleka Polisi akapatiwe matibabu”anasema Forgeti.

 
Hata hivyo juhudi za kupotosha ukweli zilianza baada ya Polisi kutoa fomu namba 3, PF3 kwa lengo la kwenda kumpima hospitali ambapo mjumbe wa shinda alitakiwa kuongoza msafara lakini aliyenda peke yake mlezi wa mtoto ambaye sasa anakanusha mtoto wake kubakwa,

“Mtoto wangu hajawahi kubakwa, nashangaa anayevumisha hayo mambo nikimjua atanilipa anatupa presha mimi na mama yangu kwani watu wanazidi kumiminika hapa, nimeenda hospitali wamesema alichezewa tu na watoto wenzake”alifoka Cesilia Philipo ambaye anadai ni mlezi wa mtoto huyo.

Wakati akiwatuhumu viongozi wa jumuiya ya wazazi kwamba ndio wanasambaza taarifa hizo, katibu wa shina namba 9 lilipofanyikia tukio hilo, Geofrey Rugeye anasema baada ya kupata taarifa hiyo alifika kwenye familia hiyo siku ya Ijumaa jioni akakuta mtoto amelala kwenye mkeka, akawaambia wampeleke kituoni akatibiwe.

“Leo wanakana ,wanajaribu kuficha ukweli Jumamosi iliyopita tulipokuja hapa walikuwa wanasema bibi yake alipoamka usiku alikuta mtoto amelala akajiachia huku mbegu za kiume zinatoka sehemu za siri akamuita mpangaji jirani akaja akadhibitisha kwamba ni kweli kesho nyake wakaanza kumkanda na maji ya moto”amesema mjumbe kwa masikitiko

Aidha katibu wa Jumuiya ya wazazi tawi la Mogo yeye anasema alikuwa amesafiri aliporudi Ijumaa jioni akaambiwa hiyo familia na mhanga walifika kwake wanataka huyo mtoto awaonyeshe aliyembaka na kumharibu sehemu za siri.

“Mimi nashangaa wanasema kwamba mimi ndio natangaza, wakati wenyewe ndio waliyatoa nje wanaona yameanza kushughulikiwa wanataka kuficha ukweli huku wakipanga kumtorosha muathirika,..hata hiyo ripoti ya daktari hatujui kama ina usahihi”alisema Katibu wazazi.

Sesilia Philipo Mlezi wa muathirika anayekanusha mwanae kubakwa

Tanpresstz imefanikiwa kuona taarifa ya uchunguzi kutoka kituo cha Buguruni ambayo daktari ameandika kwamba hakuona damu ikitoka kwenye sehemu za siri bila kujali kwamba huyo mtoto ameogeshwa tangu Disemba Mosi hadi leo Disemba 4 damu haiwezi kuonnekana.  

katibu wa Jumuiya ya Wazazi anasema kwamba "Wanasema amechezewa tu na watoto wenzake hivi hii inaruhusiwa, ..watoto wenzake wangemchezea akandwe na maji ya moto, au kwasababu mtoto huyo ni wa kambo hana mtetezi? na kuna taarifaa kwamba anataka kutoroshwa"analalama  

baadhi ya watu waliozungumza na Tanpresstz bila kutaja majina yao wameomba wadau wa haki za binadamu wamchukue mtoto wampeleke kwenye vipimo zaidi kwani anaonekana kuugulia ndani bila msaada wowote, huku walezi wake wakikanusha taarifa za kubakwa.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home