NECTA yafungia Shule za TWIBHOKI NA GRAIYAKI mtihani- Serengeti
Na Mwandishi Wetu, Tanpresstz
SHULE za mchepuo wa kiingereza TWIBHOKI na Graiyaki English Medium za Serengeti mkoani Mara zimefungiwa kufanya mtihani wa Darasa la Saba, baada ya kubainika vituo vyake kupanga udanganyifu wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, Mwaka 2023.Akitoa taarifa hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani nchini (NECTA) DK.Said Mohamed alinukuu kifungu cha 4(8) cha kanuni za mtihani Mwaka 2016 nakusema adhabu hiyo itaendelea hadi hapo baraza litakapojiridhisha kuwa ni maeneo salama kwa uendeshaji wa mitihani ya Taifa.
“Baraza limefungia vituo vya mitihani viwili ambavyo ni Twibhoki chenye usajili namba PS0904095 na Graiyaki (PS0904122) vyote vya Halmashauri ya Serengeti mkoani Mara, vilivyothibitika kupanga kufanya udanganyifu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE)2023 kwa mjibu wa kifungu cha 4(8) cha kanuni za mtihani Mwaka 2016” alisema DK.Mohamed
Aidha Dk.Mohamed ametaja shule zilizopewa onyo kuwa ni MOTHER OF MERCY PS0203133, St.Marys Mbezi Beach ,PS0203088, za Halamashauri ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam, CHARM MORDEN (PS0103111) kutoka Halashauri ya Karatu mkoani ARUSHA pamoja na MOROTONGA (PS0904042) ya Halmashauri ya Serengeti mkoani Mara.“Baraza limeziandikia barua za onyo shule hizo nne ambazo zilijaribu kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani, vituo vyao vitakuwa chini ya uangalizi wa Baraza la mtihani hadi hapo baraza litakapojiridhisha kuwa vituo hivyo ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya Taifa alisema Dk.Mohamed.
Katika taarifa hiyo iliyoambatanishwa na matokeo ya darasa la saba mwaka 2023 inaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 1,397293walisajiliwa kufanya mtihaniwa kumaliza elimu ya msingi wakiwemo wasichana 742690 (53.15%) na wavulana 654,603 (46.85%) kati ya watahiniwa waliosajiliwa wenye mahitaji maalum, walikuwa 4,599 sawa na asilimia 0.33.



0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home