Vyama 13 vimechukua fomu uchaguzi mdogo Mbeya
Vyama 13 vimechukua fomu uchaguzi mdogo Mbeya
na Mwandishi wetu, Mbeya
JUMLA ya wagombea 14 kutoka vyama mbalimbali wamejitokeza kuchukua fomu yakushiriki kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya.
Akitoa taarifa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo Misana Kwangwalu amesema taratibu za uchukuaji fomu zilianza Agosti 13, 2023 na kukamilika Agosti 19, 2023 ambapo vyama 14 vimejitokeza kuchukua fomu lakini chama kimoja hakikurejesha fomu.
Misana Kwangwalu amevitaja vyama vilvyochukua fomu kuwa ni pamoja na AAFP, DP, UDP, CCK, UPDP, ACT, TLP, CCM, ADC, NLD, NRA, UMD, ADA TADEA na CHAMA MAKINI chama pekee ambacho hakikurejesha fomu ni NRA.
Uchaguzi huo utafanyika Septemba 19, 2023 ili kujaza nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,Francis Mtega aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na trekta akielekea shambani kwake Julai Mosi, 2023.
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua, Bahati Ndingo kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.
Kwa sasa Bahati ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Francis Mtega aliyefariki Julai Mosi kwa ajili ya pikipiki na gari jimboni humo.


0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home