Tuesday, July 25, 2023

LHRC YATOA MAPENDEKEZO, UTEKELEZAJI WA RIPOTI YA HAKI JINAI

NA MOBIN KAISARYA
Adv.Anna Henga

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepitia na kufanyia uchambuzi ripoti iliyotolewa na Tume ya  Haki Jinai iliyoundwa na Rais Samia Hassan, nakuja na mapendekezo matano namna ya kufanyia maboresho tasisi zinazoguswa.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Julai 25, Manispaa ya Kinondoni, mkurugenzi wa kituo cha LHRC, Dk.Anna Henga ameyataja mapendekezo yanayotakiwa kuboreshwa kuwa ni; upelelezi na uchunguzi,dhamana,adhabu ya kifo ,utitiri wa vyombo vyenye taswira ya kijeshi na kuanzishwa kwa chombo huru kitakacho shughulikia malalamiko ya wananchi.

“kwa mda mrefu LHRC imekuwa ikipigania uwepo wa mfumo wa huru unaojitegemea juu ya uchunguzi na upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini kutokana na ukweli kwamba mfumo wa sasa kuwa sehemu ya jeshi la polisi nchini”alisema Hengan a kuongeza kuwa kitendo hicho huchochea ubambikizi wa kesi.

Akizungumzia dhamana anasema kuwa “LHRC imekuwa ikipigania juu ya mahakama kupewa mamlaka ya ninani anastahili kupewa dhamana kwa mazingira gani badala ya kuamriwa na sheria ya makosa gani yanastahili dhamana’’

Kituo hicho kimeishauri serikali kuifanyia marekebisho adhabu ya kifo, kwani kwa mjibu wa tume adhabu ya kifo ni ya kikatili sana, inayotweza  utu wa mtu na iliyo kinyume na haki za binadamu.

Pendekezo lingine ni utitiri wa vyombo vyenye taswira ya kijeshi, kama TANAPA,TAWA,TFS pamoja na mamlaka zingine, hivyo kituo hicho kinaishauri serikali kurudisha majukumu yote ya ukamataji mikononi mwa jeshi la Polisi.


Kituo hicho pia kimeangazia kuanzishwa kwa chombo huru kitakachoshughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi la polisi kutoenenda kwa mjibu wa sheria “LHRC inapigania uwepo wa chombo huru ‘Police Oversight Body,kitakachoshughulikia malalamiko na baadhi ya vitendo vya askari Polisi.

Mkurugenzi huyo ametoa wito vyombo husika vya haki jinai kuanza kutekeleza mapendekezo ya tume hasa yale yasiyohitaji bajeti ya fedha kubadilisha sheria wabadili tabia tu, “wadau wa haki jinai watoe elimu kwa wananchi juu ya kutii sheria bila shuruti ili kuepuka mgogoro na vyombo vya dola”alisema Adv.Henga

Pia ameshauri tasisi zisizoghuswa na mapendekezo ya tume ziandae mpango kazi ‘Action Plan’juu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyogusa taasisi zao.

“kuwe na mfumo wa kufanya tathimini ‘Monitoring and Evaluation’ juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya tume, serikali ipeleke miswada ya sheria katika Bunge la Septemba katika mapendekezo ambayo yanahitaji mabadiliko ya sheria.

January 13 Mwaka 2223 Rais Samia Suluhu Hassan alizindua Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za haki jinai nchini, chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Mohamed Chande Othuman, ambazo ni Polisi,magereza, TAKUKURU, Ofisi ya Mashtaka na Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya.       

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home