Thursday, July 20, 2023

Mwanakijiji Lugoba anusurika kutupwa sero kisa maoni- Chalinze

Ni kwenye mkutano wa hadhara.

Na Kaisarya wa Tanpresstz



MWANANCHI mkazi wa Kijiji cha Lugoba kata ya Lugoba halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani amenusurika kutupwa sero, kwa kulalamikia uharibifu wa miundombinu unaofanywa na vibaka katika shule ya msingi Lugoba kisha watuhumiwa kuachiwa katika mazingira tatanishi.

Mwananchi huyo, Agoustine John, maarufu kama Taji la Mkoko alikuwa anatoa kero yake kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji cha Lugoba ambapo alilalamikia vibaka wanaong’oa mindo mbinu ya umeme katika shule hiyo kisha kuachiwa baada ya kukamatwa kwa maelekezo ya ‘wakubwa’ wa kata ya Lugoba.

“Kero yangu ni uharibifu wa miundombinu unaofanywa kwenye shule yetu, mara ya kwanza waling’oa vifaa vyote vya umeme, watuhumiwa wakakamatwa lakini wakati wanapelekwa mahakamani faili likapotezwa, kisha wakaiba wakakamtwa tena hadharani lakini waliachiwa kwa vimemo vinavyoandikwa na baadhi ya viongozi wa kata na juzi wemeenda wameharibu tena umeme na kwasasa shule haina umeme wezi tunao mitaani, wanajulikana wakikamatwa na vifaa wanalindwa hata pale kanisa la hapo chini wameiba”alisema Taji

Kauli hiyo ilimkera vilivyo diwani wa kata hiyo Rehema Issa Mwene aliyenyenyuka na kumkatisha kisha kumtaka adhibitishe kauli yake ya kuwatuhumu viongozi akiwemo yeye, kama akishindwa kufanya hivyo atalala sero.

“Ngoja siwezi kuvumilia sisi viongozi wa kata tutuhumiwe nikiwepo hapa, kwa kuwa amesema sisi viongozi wa kata asipodhibitisha kauli yake tutapelekana huko polisi atakwenda kuisaidia….sitakubali atakwenda huyu polisi sitakubali kudhalilishwa hadharani tena kwenye mkutano wa hadhara anatutuhumu viongozi kwamba tunaandika vimemo” alisema Diwani

Hata hivyo huyo mwananchi alikariri kauli yake akihoji kama viongozi hawahusiki mbona hawajawahi kufuatilia hayo matukio na kujua kesi zake zimepotelea wapi na kwanini mafaili hayaonekani.

Jambo hilo lilimuibua tena diwani aliyemuagiza katibu tarafa wa Msoga  kuhakikisha mwanakijiji huyo anafikishwa polisi kuona aliyeandika kimemo kikikosekana abaki sero kwa kuwadhalililisha viongozi wake.

Katibu tarafa Francis Mbegete aliunga mkono kauli hiyo huku akiwataka viongozi wote wa kata kuongozana naye hadi kituo cha Polisi Lugoba kuulizia aliyeandika vimemo, akitajwa pale abaki sero lakini akikosekana mwana kikijiji aliyelalamika abaki sero.

“nawaagiza viongozi wote wa kata tutaongozana kwenda polisi atakayetajwa atabaki sero lakini jina likikosekana mambo yatakuwa kinyume chake nitamchulia hatua aliyetuhumu wenzake”alisema Mbegete.

Hata hivyo mjadala huo ulipunguzwa makali na mwananchi mmoja aliyesiamama nakuomba hekima itumike na maridhiano yafanyike kwa kumsihi Tarafa ajipe muda kufuatilia suala hilo kwani yalikuwa maoni ya kawaida kutolewa hadharani.

“Mimi nadhani busara itumike tu, unajua kuna mambo mengi ya kuhoji kwa hao watendaji kata lakini tunaogopa kama hivi, mwananchi ametoa hija yake inapaswa Katibu Tarafa ujipe muda wa kufuatilia badala ya diwani kujibisha naye, kwanza diwani hakupaswa kabisa kulijibu walitakiwa wataalam wa sheria ndio wajibu”alisema..

Kufuatia ombi hilo Mbegete aliwataka viongozi wa kata wasiende aende mtendaji kata peke yake aongozane na ‘mtuhumiwa’ hadi polisi kubaini wanaonadika vimemo na kumuomba diwani aondoke kabla ya mkutano akaendelee na majukumu mengine.

Baada ya mkutano huo Taji alionekana na mtendaji kata Mwenyekiti wa kijiji cha Lugoba Zaituni Kaogo, kituo kidogo cha polisi na kuambiwa mkuu wa kituo hicho, hayupo warudi Alhamisi saa tatu asubui.

Shirika la habari vijijini Tanpress linaendelea kufuatilia sakata hilo kujua hatima yake, nani aliwaachia watuhumiwa wanaoharibu miundombinu ya umma.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home