Dc Bagamoyo awasihi wananchi kujitokeza mbio za mwenge
Na Tanpresstz.Chalinze
MKUU wa wilaya (DC) ya Bagamoyo mkoani Pwani Halima Okash amewasihi wananchi wa halmashauri ya Chalinze kujitokeza barabarani kuupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kupokelewa asubuhi ya Mei 15 Mwaka huu eneo la Bwawani ukitokea mkoani Morogoro.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Lugoba jumatano iliyopita aliwasihi wananchi hao kujitokeza kujipanga barabarani wakati mwenge utakapokuwa unapita huku wakiushangilia.
“ulipo mwenge ndipo alipo Rais hivyo nawaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi mjipange barabarani kuupokea wakati mwenge utakuwa ukipita kukagua na kufungua miradi ambayo ipo kwenye kata hii ukiwemo wa pikipiki na maabara ya kisasa, …mkijitokeza mtakuwa mmeniheshimisha sana” alisema Dc.Halima Okash
Mkuu huyo aliwakumbusha wananchi hao kuwa mwaka jana halmashauri ya Chalinze iliongoza kwa ubora wa mapokezi ya mwenge hivyo nakuwataka kipindi hiki tena wajitahidi kubakisha kombe la ushindi nyumbani.
“tumieni hata kamati za ufundi ….najua nyie ni wataalam, ushindi lazima ubaki kama mwaka jana Chalinze tulichukua ushindi mwaka huu tujitahidi kufanya vizuri zaidi,”alisisitiza huku akitania wakazi wa kijiji Lunga
Mwenge wa uhuru wenye kauli mbiu ya kulinda mazingira utawasili mkoa wa Pwani jumatatu na kukesha katika kata ya Msata jimboni Chalinze kisha kuzunguka wilaya mbalimbali za mkoa wa Pwani kwa kuzindua miradi kadhaa.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home