OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA-(NPS) YAFUNGULIWA CHALINZE
Ofisi ya mashtaka (NPS) yafunguliwa-Lugoba
Na Mobini Kaisarya-tnpress
WAKAZI wa Chalinze wilayani Bagamoyo, mkoani, Pwani wameanza kunufaika na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini, baada ya kufungua ofisi yake hapa, Tanpresstz inakuhabarisha.
Akizungumza na shirika la habari vijijini (TANPRESSTZ) Mkuu wa Mashtaka Wilaya ya Chalinze (DPO) Janeth A.Magoho ameweka bayana kuwa ofisi hyo, itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika masuala ya haki jinai.
“tangu aprili Mwaka huu ofisi hii imefunguliwa lakini tumeanza kufanya kazi rasmi Julai Mosi Mwaka 2023, kikubwa tunahusika na uandaaji wa mashtaka mbalimbali yanayohusika na makosa ya jinai na kuendesha kesi mahakamani ndio maana tunaitwa waendesha mashtaka, kwasasa tunaanzia mahakama ya wilaya”amesema DPO Mahogo.
Ametakaja majukumu mengine ambayo ofisi hiyo inahusika nayo , “lakini mbali na hivyo pia tunahusika na upelelezi kwa kushilikiana na Polisi Chalinze, sisi ni wataalam wa sheria tunawapa muongozo polisi namna ya kukamilisha upelelezi kwa haraka”anasema
Bi. Magoho anasema kwamba kazi ya Polisi kwasasa ni kukamata mtuhumiwa kupeleleza kabla kesi haijaenda mahakamani wanaichunguza ‘lazima kwanza tujirizishe kwamba upelelezi huu umefuata utaratibu’
Majukumu mengine ambayo wanahusika nayo ni kuhakikisha kwamba zile Hakijinai upande wa watuhumiwa zinafuatwa,wanapokuwa polisi wanatendewa haki hata kama ni watuhimiwa ikiwemo kupata dhamana kwa yule anayestahili.
“kama kosa linadhaminika mtuhumiwa anaweza kudhaminiwa wakati polisi inaendelea na uchunguzi na kama kuna mlalamikaji , anasumbuliwa na polisi hawataki kufungua kesi yaketunapokea malalamiko hayo na kufuatilia, pia ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba mtuhumiwa anachukuliwa maelezo ndani ya masaa manne tangu amekamatwa” amesema DPO.
Aidha ofisi ya waendesha mashtaka inaweza kuondoa shtaka mahakamani endapo wataona kwamba halikidhi vigezo vya kisheria “Sisi kama waendesha mashtaka tunayo mamlaka kwa kutumia kifungu 91 (1)cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo 2022 kama tunaona changamoto kwenye kesi tunaweza kuifuta au kuiondoa mahakamani”anasema DPO Magoho
Anasema kuwa kwa muongozo wa sasa upelelezi wa kesi unapaswa kufanyika ndani ya siku 90 huku ofisi yake ikiwa na majukumu mengine ya kuhakikisha mashahidi wanafika mahakamani na kulipwa posho ya kujikimu.
“tunawajibu wa kuwalipa posho mashahidi pindi wanapofika mahakamani kutoa ushahidi wao, mwanzoni mahakama ndio ilikuwa inawalipa, hii ni ofisi mhimu sana kwa wana Chalinze mtu akiona haki zake zinavunjwa inabidi akimbilie kwetu tumpatie ushauri wa kisheria”anasema
Kutokana na ofisi hii mhimu kufunguliwa hapa Chalinze wananchi wameanza kunufaika na mambo ya msingi yanayotakiwa kufuatwa kwenye kesi, kama kutobambikiwa kesi, dhamana kuchelewa na sasa kesi zinaenda haraka.
Pia ushauri wa kisheria unatolewa bure elimu ya Haki jinai kwa wananchi wanaofika ofisini kwao zilipokuwa ofisi za Halmashauri zamani, Lugoba, kuhakikisha kwamba mashauri ya kawaida yanamalizika ndani ya miezi 6 na yale makubwa yasizidi siku 180.
Lakini majukumu mengine ambayo wanayafanya ni kutembelea vituo vyote vya polisi ambavyo vina selo na magereza zenye mahabusu wanaotoka Chalinze (Ubena na Bagamoyo) kuona hali ya mahabusu na kusikiliza malalamiko yao, ‘ili mwenye kudhaminika atoke na sisi kuendesha kesi zao kwa haraka’.
“lengo kubwa ni kupunguza msongamano mahabusu”anasema DPO huku akiwakaribisha wananchi ofisi wake kupata elimu ya hakijinai.
Labels: HABARI


0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home