Tuesday, May 16, 2023

Mwenge Kukagua Na Kuzindua Miradi 23 Bagamoyo Ikiwemo Chalinze

 


Na Tanpresstz.Chalinze

MWENGE wa uhuru umepokelewa na mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge Mei 15 Mwaka huu[u1]  eneo la Ubena Zomozi (Chalinze) kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Morogoro Fatma Mwasa, ambapo utakimbia kwa siku mbili wilayani Bagamoyo na kukagua miradi yenye thamani ya Bilioni 4.7

 

RC.Mwasa (KULIA) akikabidhi Mwenge kwa Rc.Kunenge

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Halima Okash alisema kuwa mbio hizo  zitapitia miradi 23 wilaya ya Bagamoyo kati ya hiyo miradi 14 yenye thamani ya Bilioni 2.4 itapitiwa Halmashauri ya Chalinze na miradi 11 ya sh.Bilioni 2.3 Halmashauri ya Bagamoyo .

RC.Abubakar Kunenge (KULIA) akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo (KUSHOTO) Halima Okash
 

Akipokea Mwenge huo , eneo la Ubena Estate Mkuu wa Mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge, anaeleza kati ya miradi hiyo miradi 55 itakaguliwa,Tisa itafunguliwa ,15 itazinduliwa na 20 itawekwa mawe ya msingi .

 "Miradi hiyo inadhihirisha kazi nzuri inayofanywa na  Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan "

Akiweka jiwe la msingi katika upanuzi wa mradi wa maji Mtambani , mradi ambao unatekelezwa na Wakala wa usambazaji maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA, chini ya mkandarasi mzawa Josan Engineering Group, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa (2023), Abdallah Shaib , alisisitiza kutunza Mazingira na Vyanzo vya maji ndani ya jamii.

 Meneja wa RUWASA Bagamoyo James Kionaumela,alieleza mradi huo una thamani ya milioni 176.3 , chanzo cha fedha ni kutoka fedha za lipa kwa matokeo (PbR) ambazo zilitolewa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya maji.

 Kwa mjibu wa RC. Kunenge ameeleza kuwa Mwenge ukiwa Mkoani hapa utakimbizwa katika Wilaya Saba na Halmashauri 9 za Mkoa wa Pwani umbali wa Kilometa 1,201.95.

 “Mwenge huo utazindua, Kuweka mawe ya Msingi, kukagua na Kufungua miradi yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.4.”Kunenge ameeleza miradi hiyo ni matokeo ya Uongozi Mzuri wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.


 [u1]

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home