Wednesday, July 12, 2023

KARDINALI Rugambwa siyo mrithi wa Pengo- Paroko

 

Na Mobini Kaisarya, Tanpresstz.chalinze

kardanali  mteule Rugambwa kushoto akiwa na PAPA

KAMA uliokuwa unafikri kwamba uteuzi wa Askofu mkuu mwandamizi Protase Rugambwa kuwa Kardinali, anakuja kuchukua mikoba ya Askofu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es Salaam, Kardanali Pengo, utakuwa umekosea.

Ni kwamba hadi sasa kardinali Pengo hajastaafu nafasi yake hiyo bali alichostaafu ni majukumu ya Askofu mkuu  wa jimbo nafasi ambayo ili chukuliwa na Mhashamu Yudas Thedeus,baada ya kutimiza miaka 75 kwa mjibu wa kanuni za kiaskofu.

Akizungumza na shirika la habari vijijini TANPRESSTZ, Paroko wa kanisa Katholic Parokia ya Lugoba, Chalinze, Paulinus Ponda aliweka wazi kwamba ‘Pengo bado hajastaafu ukadinali ataendelea na majukumu yake hadi atakapofikisha miaka 85’

Padre Ponda aliombwa na Tanpresstz kuelezea anavyomfahamu Kardinari mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Papa, Julai 9 Mwaka huu,

“siwezi kumuelezea kiundani Kardinali Rugambwa kwasababu sijawahi kufanya naye kazi, lakini ninachojua amewahi kuwa Katibu mkuu wa idara ya kikatoliki  ya kueneza injili duniani baadaye akateuliwa kuwa askofu wa jimbo la Kigoma”amesema Padre Ponda.

Hata hivyo baadaye aliteuliwa kuwa askofu mkuu na Balozi wa Papa hivyo kumwakilisha Papa katika nchi  mbalimbali alizofanya kazi kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa jimbo kuu Tabora na siku chache baadaye akatangazwa na Papa kuwa miongoni mwa makardinali wapya wanaotarajiwa kuapishwa Septemba 30 Mwaka 2023.

Baada ya kuteuliwa nafasi hiyo watu wengi wamekuwa wakisema kuwa huyo ni mrithi wa Pengo baada ya kustaafu, kumbe majukumu ya Kardinali yanadumu hadi miaka 85 ambapo kadinali hustaafu majukumu ya kiofisi na hundelea kuwa kardinali anayetunzwa hadi kufa.

Hivyo kwasasa Tanzania imebahatika kuwa na makardinali wawili huku Rugambwa akitarajiwa kuteuliwa tena kuwa askofu mkuu wa jimbo kuu la Tabora endapo aliyepo sasa atastaafu kutokana na umri wake.

Hata hivyo kwa mjibu wa kanisa katoliki kiongozi mkuu hapa nchini ni rais wa maaskofu (TEC) , sio kardinali ambaye kazi yake ni kumshauri Papa na kuwa miongoni mwa wajumbe wanaomchagua Papa, kwani Papa pia lazima awe miongoni mwa Makardinali.

      

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home