Amri ya Dc Bagamoyo kuanza kutekelezwa leo Msoga
Na tanpresstz. Chalinze
AGIZO la Mkuu wa Wilaya (DC) wa Bagamoyo Halima
Okash , kuitaka kamati ya ulinzi na usalama kushirikiana na Afisa Ardhi
Chalinze kuvunja nyumba zilizojengwa kwenye mpaka wa kijiji cha Mundutulieni na
Diozile ndani ya siku saba litaanza kutekelekezwa leo Alhamisi Tanpresstz
linaripoti.
Akizungumza na shirika la habari vijijini
Tanpresstz, Deo Damian Mfilu ambaye ni Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Chalinze jana
Jumatano amesema kuwa amri hiyo ya Mkuu wa Wilaya itaanza kutekelezwa leo kwa
kuzitambua kwanza nyumba hizo na mipaka yake kisha ziwekewe alama na walengwa
kupewa amri ya siku saba kuondoka.
DC HALIMA OKASH
“Zoezi la kuvunja nyumba hizo linaanza mara moja kesho ‘leo’ kwa kuzitambua kwanza na kuziwekea alama kisha kuwapatia notisi wamiliki, kwasababu nyumba hizo zipo kwenye kijiji cha Mindu na Diozile wale waliojenga Diozile hawana tatizo zitakazovunjwa ni waliojenga eneo la Mindu ndio wenyeji wanawalalamikia hawawataki”amesema Mfilu.
agizo hilo limetolewa Juni 13 mwaka huu na DC, kwenye ziara yake ya kujitambulisha kwa wakazi wa kata ya Lugoba na kupokea kero zao katika ukumbi wa Lugoba sekondari.
Amri ya kuvunja nyumba hizo ambazo zipo kati ya kijiji cha wafugaji, Mindutulieni kata ya Lugoba na kijiji cha wakulima Diozile kata ya Msoga limetokkana na ombi lililotolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ambaye ni diwani wa kata ya Msoga, Hassan Mwinyikondo kutaka DC aingilie kati mgogoro huo.
“Hapa mnatoa kero za ardhi mnafurahia Dc kutoa wiki wiki moja watendaji kumaliza migogoro ya mpaka lakini hawa watafungwa tu na hiyo mgogogo hawataiweza kuna mgogoro hapa juu ya migogoro hamtaki kuusema, kuna watu hawajulikani wapo Lugoba au Diozile wameingia na kuanzisha makazi bila kibali na sasa wameanza kutengeneza kijiji chao, hawatatambuliki popote walishapewa masaa 48 kuhama wakakaidi….mnanyamaza”alisema Mwinyikondo.
Kufuatia kauli hiyo Dc.Okash alimwagiza pale pale Afisa Ardhi, Deo Damian Mfilu kwa kushilikiana na kamati ya ulinzi na usalama kwenda kuvunja nyumba hizo ndani ya siku saba wakiwa na silaha za moto na matinga tinga.
“Yaani wamepewa masaa 48 wakagoma kuhama sio mimi naagiza kamati ya ulinzi na usalama kwa kushilikiana na Afisa Ardhi wa wilaya wepewe notisi ya siku 7 huku mkiandaa magari ya kwenda kuvunja na mabati yatakayopatikana yapelekwe kwenye taasisi za umma kama mashule …mkurugenzi atoe gharama za kununua rangi ya kwenda kupuliza x tuone anayejitokeza na mishale”alisema DC Okash.
Hata hivyo alionya tabia ya viongozi kunyamazia wavamizi hadi mwaka ndi wanaanza kulalamika, “mtu anaingia eneo anakaa wiki ,mwezi hadi mwaka una mwangalia anajenga halafu unakuja kulalamika , kuanzia sasa wavamizi waondolewe ndani ya siku saba” DC.
Habari hii imechapwa Na mobini sarya

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home