Arafa Kikwete kuibeba Taasisi ya Women Talk Chalinze
Mke wa mbunge wa Chalinze ajitosa vita ya ukatili wa kijinsia, Women Talk Group wamkaribisha awe mshauri wao.
Na Mobini Sarya,Tanpresstz
![]() | |||
| Bi Arafa Kikwete ambaye ni mke wa Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma, Ridhiwan |
Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti wa taasisi hiyo,Kulwa Mwakapande kwenye kongamano la wanawake linaloandaliwa na taasisi hiyo kila Mwaka maeneo ya Chalinze mkoa wa Pwani.
![]() |
| Bi, Arafa Ridhiwan Kikwete |
“Tunayo ombi kwako na kwa mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,ili tuweze kutimiza malengo yetu tunaomba kupatiwa eneo maalum ,kwa ajili ya kuweka makazi ya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kutimiza ndoto zao”alisema maadam Mwakapande
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo lililofanyika Disemba 2,2023,Lugoba alikuwa ni Bi.Arafa Ridhiwani Kikwete ambaye ameipongeza taasisi hiyo kwa shughuli zake za kusaidia makundi maalumu wakiwemo watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
“Nileeteni mahitaji yenu, ni vitu gani mnataka mkatoe msaada na mimi nitawasaidia kwa kushirikiana na mme wangu (mbunge wa Chalinze) kipindi hiki shule zinaelekea kufungwa na nyie mnasema mnasaidia wanafunzi ni vyema nikapata mahitaji yenu mapema ili tuweze kuwasaidia”alisema Bi.Arafa Kikwete.
Aliwaasa akinamama hao kuzingatia kikamilifu malezi ya watoto yanayostahili ili kupunguza ukatili wa kijinsia ‘tusiache jukumu letu, msingi wa kulea watoto tusimuachie mtu mwingine’aliwaasa.
Akisoma risala mwenyekiti wa kongamano hilo, Kulwa Mwakapande kuwa umoja wao ulianzishwa Mwaka 2021 ukiwa na wanawake 50 wakiwa na lengo la kuwakutanisha wanawake ili kujadili mambo yao na kuwagusa akina mama na watoto wenye mazingira magumu kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
“Tulikuwa na lengo la kuwakutanisha akina mama ili kujadili mamabo yetu na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na sasa hivi wanawake wameongezeka na kufikia 200 huku tukiendelea kusambaa kata zote za Chalinze”alisema Maadam Mwakapande.
Aidha katika kutekeleza malengo yao wamefanikiwa kutembelea vituo vya watoto yatima kama vile Hope Disability na KULEANA kinachosimamiwa na Askof.Rommy, huku wakifanikiwa kuandaa maadhimisho ya Mtoto wa AFRIKA yaliyofanyika Juni 14,2023 Halmashauri ya Chalinze.
“Pia tumeweza kufanya makongamano ya wanawake kwa miaka miwili mfululizo yaani 2021 na 2023 na kuwapatia wanawake 15 tuzo kutokana na kujituma kwao huku tukianzisha kundi dogo ndani ya kundi kubwa linalojulikana kama ACTIVE MAMAZ ambalo limesajiliwa na kufungua akaunti kwa lengo la kujiwekea akiba ya 50,000 kila mwezi”alisema Maadam Mwakapande.
Labels: HABARI



0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home