Tuesday, December 12, 2023

Magreath Sitta;Mafunzo ya Jeshi la Wokovu yamenisadia nisitende maovu

Maadhimisho ya miaka 90 ya Jeshi la Wokovu Territory ya Tanzania yakamilika

Na Nashoni Shadrack, Tanpresstz

Gwaride la maadhimisho ya miaka 90 ya Jeshi la Wokovu
MBUNGE wa Urambo Mashariki, Magreath Sitta, amesema kuwa mafunzo aliyopata katika kanisa la Jeshi la Wokovu alipokuwa Binti mdogo,yamemusaidia asitende maovu, hata baada ya kuolewa na kujiunga na siasa hadi leo.

Akizungumza kwenye kongamano la  Maadhimisho ya Miaka 90 tangu jeshi la Wokovu kuingia hapa nchini Tanzania, Mwaka 1933, Bi Sitta ambaye ni mjane wa Spika wa zamani, marehemu Samweli Sitta, alisema kabla ya kuolewa na mshirika wa Moravian, wazazi wake walikuwa Salvation Army hivyo  alilelewa kwenye kanisa hilo.

Mbunge BI,Samweli Sitta baada ya kukabidhi mchango wa shilingi milioni moja jukwaani katika kongamano la miaka 90 ya SALVATION ARMY
   “Kwa kweli nisema kwamba mafunzo na malezi niliyopatiwa katika kanisa hili yamenisaidia sana nisitende maovu….. yamenisaidia sana hata sasa , ingawa niliolewa Moravian baadaye tulipohamia Dar es Salaam, tukajiunga na kanisa la KKKT nikiwa mtu mzima lakini najivunia kulelewa jeshi la Wokovu”alaisema na Kushangiliwa

Katika maadhimisho hayo ambayo yamefikia tamati Jumapili Disemba 10,2023 makao makuu ,Mgulani Dar es Salaam, yakihudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo kutoka  maeneo mbalimbali ya nchi, Bi Sitta alitoa Shilingii Milioni moja Tasilimu kusaidia shughuli za maadhimisho.

Katika maadhimisho hayo ambayo yalianza Disemba 5 hadi 10 Mwaka 2023, takriban Makadeti 30 waliapishwa kuwa wachungaji na akupewa aagizo rasmi kwenda kwenye vikao (makanisa) mbalimbali kuongoza waumini na kutangaza injili.