Friday, March 9, 2007

siasa inavyoatuathili hapa nchini

G.boy

Siasa ya Tanzania inavyoathiri ukuaji wa kiuchumi hapa nchini

Na M s

Nchi yetu ni moja ya nchi ambazo zipo dunia inayojiendesha kwa kutumia mfumo wa demokrasia ya Vyama vingi iliyoanza kutumika hapa kuanzia mwaka 1992 NA hadi sasa tumekwisha fanya uchaguzi kwa kwa kutumia mfumo huo zaidi ya mara tatu uchaguzi mkuu wa kwanza ulifanya mwaka 95 ukafuatiwa na wa Mwaka 2000 uliorejesha madarakani tena Rais mstaafu Benjamin Mkapa, na uliofanyika mwaka jana uliomwingiza madarakani Rais jakaya Kikwete kutoka chama cha Mapinduzi na kabla ya hapo uliwahi kufanyika baadhi ya majimbo kama majaribio.

Lakini pamoja na kwamba uchauguzi huo umekuwa ukifanyika kikatiba kwa kusimamiwa na tume ya Uchaguzi lakini, Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakilalalamika kwamba chaguzi hizo haziendeshwi kwa uhuru na haki kwa upande mmoja unaweza kusema tangu mfumo huo umeanza kutumika hatujawahi kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki unaweza kuwa wahaki kikatiba lakini ukakosa uhuru au ukawa wa uhuru ukakosa haki ya kufanya hivyo.

Kuwa wa uhuru bila haki ya kuchagua

Uchaguzi unaweza kuwa huru kwa kuendeshwa katika mazingira ya wazi lakini wapiga kura wakanyimwa nafasi ya kupiga kura kutokana na mizengewe inayoweza kuwepo, mfano hapa Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi ya nyuma uchaguzi mkuu uliendeshwa bila kutumia Daftari la kudumu vyama vya upinzani wakalalamika kuwa wamekuwa wakiibiwa kura kutokana na kushindwa kubaini ni watu wangapi wajiandikisha kupiga kura na ni wangapi walipiga, wakifikiri njia hiyo itakuwa bora na kuwafanya washinde kiurahisi.

Lakini kumbe mfumo huo wa kuanzisha daftari la wapiga kura waliutaka bila kufanya utafiti wake wabaini faida na hasara yake waliushikia bango wee hasa chama cha Wanachi Cuf, wakisema kuwa Daftari la kudumu ndio njia pekee ya kuendesha uchaguzi wa uhuru lakini wakati serikali inayoongozwa na CCM ikichelea kuanzisha utaratibu wa kutumia daftari hilo kumbe wao walikuwa wakijifunza njia nzuri ya kuhakikisha wananufaika na hilo daftari kipindi cha uchaguzi.

Inaezwa kwamba kati ya maeneo ambayo CCM ilinufaika kwa kutegemea daftari hilo ni Zanzabar na kwa hapa bara ni ile mikoa ambayo ilikuwa na upinzani wenye nguvu, kutokana na hali hiyo wapiga kura waliandaliwa mazingira uhru wa kupiga kura lakini wengi hasa wanzibar wanalalamika kuwa walinyimwa haki ya kufanya hivyo aidha kwa kunyimwa haki ya kujiandikisha kama wapiga kura kwa madai ya sio wakazi au kutangaziwa mshindi ambao wanaona hakushinda kihalali wanakuwa wananyimwa mtu waliyemchagua kihalali siwezi kutaja baadhi ya majimbo ambayo yanaonekana haki ya wapiga kura iliporowa kutokana na wengi kwenda mahakamani hiyo ndio uhuru bila haki.

Kuwa na haki bila uhuru

Katika chaguzi nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika hapa nchini kwa mfumo huo wa DEMOKRASIA inasemakana kwamba kasoro kubwa ni wanachi wengi kukosa uhuru wa kupiga kura kwani kuanzia kwenye kampeni hutawaliwa na vurugu hadi kwenye uchaguzi, niliwahi kushudia uchaguzi wa serikali za mitaa katika kata moja ya Ilala wapiga kura wakiwa wamefika katikati ya kupiga kura ghafula makachero wa chama kimoja walaibaini kuwa Mgombea wa chama chao walikuwa anakaribia kushindwa ilibidi wazue vurugu na msimizi wa kituo hicho akapigwa ndipo uchaguzi ukaahirishwa ili watu wakajipange upya.

Kutokana kwamba katika maeneo mengine uchaguzi ulikuwa umekwisha fanyika ilibidi siku ya uchaguzi watu wahamishwe kutoka eneo moja kuletwa kwenye kituo hicho na yule mgombea akashinda hiyo ndio Demokrasia ya hapa nchini, kutokana na kutawaliwa na rafu nyingi kwenye uchaguzi wananchi wengi wanasema kuwa wanashindwa kutumia haki yao kuchagua mgombea wanayependa kwa sababu hamna uhuru, mpiga kura mmoja aliwahi kuniambia kunasbabu gani kupiga kura wakati hakuna uhuru wa kuchagu?

Siasa imetuathiri

Wachambuzi wa mabo ya Siasa hapa nchini wanaona kwamba ilikuwa mapema mno kuukubali mfumo huu wa vyama vya siasa kabla hatujajipanga na wananchi pamoja na viongozi wapewe somo la Elimu ya uraia baadala yake tukaukubali hivyo hivyo na sasa umetuathili baada ya kutusaidia kutokana na kuendekeza ubaguzi uhasama na chuki miongoni mwa watanzania.

Watanzania wanafahamika wazi kuwa ni watu waliokuwa wanapendana na wanasikilizana lakini tangu mfumo huo umenza kurumika pamekuwapo na chuki, miongoni mwa wanachama wa chama kimoja kingine ubaguzi wafanyakazi walioko serikalini kupoteza kazi wanapojiunga na vyama upinzani biashara zao kufuatiliwa na mifano mingine mingi ambayo iko wazi ikienda sambamba na usemi wa alikuwa waziri mkuu Fredrick Sumaye aliyesema kwamba ukitaka mambo yako yakunyokee jiunge na CCM.

Wala usemi huo hakuwa wa utani ndio maana toka hapo makundi ya wafanyabiashara wanasiasa wamekuwa wakivikimbia vyama vya upinzani na kujiunga CCM ili mambo yao yawanyooke, kitu kinachodhihirika kwamba kuwa mpinzani ni sawa na muwaasi ni wapinzani wachache hapa nchini wanaoonekana kumdu kufanya biashara wakati ni wanasiasa wengine wameamua kuchagua moja kuwa wanasiasa au wafanyabiashara jambo linalooneka kuwa mwanasiasa wa kambi ya upinzani ni sawa na kujiunga katika kikundi cha waasi wanaotaka kuipindua serikali.

Hali inayozua maswali kama serikali ilikuwa haitaki mfumo wa vyama vingi kwanini ilihurusu hata kama tunaelezwa kuwa ilikuwa ni kwa masilahi ya Taifa vipi taifa likubali kila kitu hata kama kinakwenda kinyume na sheria za nchi yetu, unaweza kuona kwamba maana ya Demokrasia ni kuheshimu maamuzi ya wengi lakini kweli maamuzi ya wengi yanazinatiwa hapa nchini?

Maswali yamekuwa yakihojiwa na Wasomi mbalimbali wa chuo kikuu cha mlimani wanapokuwa wanajadili maana ya Demokrasia kwamba inakuwaje kama maana yake ni kuheshimu maamuzi ya wengi, mfumo huo ukaletwa wakati wananchi wengi waliukataa katika kura za maoni zilizoendeshwa na ile tume maarufu ya Jaji francis Nyalali zaidi ya asilimia 80 hawakuwa tayari kuukubali.

Sasa wasomi wanauliza kama mfumo huo ulikataliwa lakini maoni ya wengi yakapuuzwa badala yake ukaletwa huo mfumo wa kidemokrasia kwanjia ya kidikteta unaweza ukafanya kazi kwa kuheshimu maamuzi ya walio wengi ikiwa hata kuuleta ubabe na udikiteta ulitumika.

Ndio maana kutokana na hali hiyo siasa za ubabe zimekuwa zikitawala kwa sana hapa nchini wananchi wamegawika kwa makundi kuna kipindi mfuasi wa CUF hawasaliamini na wa CCM wakati kabla ya mfumo huo hayo yote hayakuwepo, leo miaka zaidi ya kumi vurumai na matusi imekuwa ni sehemu ya maisha ya wanasiasa.

Hatuna raha na wala hatuufurahii huu mfumo kwasababu hata ukihoji leo hii kwamba huo mfumo umeleta faida gai tulikuwa tukiikosa sijui itazidi hasara ambayo tunaipata kwa kuwa na huu mfumo kwanza tunapoteza roho za watu kila tunapofika kwenye kipindi cha uchaguzi inapotumika nguvu ya dola au vurugu za wenyewe kwa wenyewe yaani wafuasi wa chama kimoja na kingine.

Shughuli na miradi ya maendeleo kukwama kushughulikiwa inapoonekana kwamba wananchi wa eneo hilo wanamuunga mkono mgombea wa chama cha upinzani kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa miaka ya nyuma huko Pemba na Baadhi ya Majimbo ya bara kama Jimbo moja huko Mara waliweka nguzo za umeme wakati wa uchaguzi aliposhwa mgombea wa CCM hizo nguzo zikaendelea kuozea chini hadi hivi karibuni mgombea wa chama hicho aliposhinda kwenye uchaguzi uliomalizika ndio zimeanza kushughulikiwa.

Pia kutokana na kwamba nchi yetu haina ukabila siasa za demokrasia zimekuwa zikitumika kuwabagua watu hata kuliko ukabila, inakuwa vigumu ukamkuta mtu ni Mfurukutwa maaru wa CHADEMA au CUF halafu umkute anatumikia shirika la Umma na hiyo ndio jambo baya kabisa ambalo limetuathiri kimaendeleo kuliuko tulipokuwa na chama kimoja kila mmoja alikuwa anathaminiwa mchango wake.

Kwa mfano hapa nchini na hata nje ya nchi Profesa Lipumba anaheshimika kwa elimu yake akienda ng’ambo anaonekana lulu lakini hapa kwetu mchango wake hauthaminiki kwasababu yeye ni mpinzani na kama akipewa nafasi ya Waziri wa Uchumi akafanya maendeleo ataonekana na kwafunika wengine kwa hiyo inakuwa ni lazima abezwe ikibidi ili kuepuka kumpatia nafasi asije akatuzidi kete.

Hapa nchini ninani asiyejua mchango wa Mwenyekiti wa TLP Agoustine Mrema enzi alikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja akiwa kama waziri wa mambo ya Ndani jinsi alivyoushughulikia ujambazi na kutokomeza kabisa na ndiye aliyegundua njia ya kuwaweka wapepelezi mahabusu ili waweze kutoa nje siri za watuhumiwa tangu mfumo huu wa vyama vingi ulipoingia nayeye akaamua kuikimbia CCM Mchango wake umekuwa hauthaminiwi.

hata kipindi hiki majambazi yalipochachamaa yakafanya mambo ya aibu aliomba nafasi katika serikali ya awamau ya nne ili ayashughulikie walimbeza wakaonba kama Mrema akifanikiwa kuyatokomeza ataligeuza zoezi hilo kuwa jukwaa la kisiasa na TLP itapa umaarufu kuliko kawaida jambo ambalo linaweza kuathili siasa za wakubwa, huo ni ubaguzi mwingine ulioletwa na DEMOKRASIA.

Tunaye mwanasiasa na mwanaharakati wa kweli Mchungaji Cristopher Mtikila mpigania katiba isivunjwe isingekuwa ni kutokana na mfumo huu wa kidemokrasia huyu mwanasiasa ndiye alipaswa kuwa mwenyekiti wa tume ya kuratibu maoni ya kuharakisha uundwaji wa shirikisho la Afrika Mashariki pia alipaswa kupewa na nafasi ya kuandaa Rasimu ya katiba mpya kutokana na katiba tunayotumia sasa kuwa ya vilaka.

Lakini hawezi kupewaa hiyo nafasi asije akaitumia kujhinufaisha kisiasa na chama chake cha Democrati Party (DP), huo ndio mfumo mbaya wa DEMOKRASIA ambayo imeletwa na wazungu kwa manufaa ya kutugwa ili wapate kututawala kwa mwanga wa wazi na kufanya biashara kwa kutuuzia masanduku na vifaa vingine vya kupigia kura.

Demokrasia ya vyama vingi imetuathiri kuliko tlivyokuwa awali, kutokana na siasa hii chafu tumejikuta hata tukipuuza yale majukumu mhimu ya kitaifa na kuyageuza majanga kwa mfano Mwenyekiti wa Chama cha TLP aliwa aliwahi kuleta Umeme wa ghalama nafuukwa wananchi wa vijijini lakini chakushangaza kwa sababu yeye ni mpinzani analeta umeme ukazuiliwa eti kwa madai kuwa ni wa ghalama kubwa kwani wao ndio walikuwa wanalipia ghalama hizo wakati ni za mwekezaji.

Hata hivyo mwekezaji hakupaswa azuiliwe kwani umeme alikuwa analeta alikuwa anataka kuuza kwenye soko huria anayetaka angeukubali asiyetaka kwasababu ni wa ghali angaacha pamoja na hiyo, kipindi hiki cha umeme ambao umekuwa wa mgao na giza tororo nchi nzima kama ule ungekuwepo ungeweza kuasaidia mara dufu, leo kila siku shirika la Umeme nchini Tanesco limekuwa lipandisha ghalama za bili lakini hakuna anayezuia kuwa umeme huo ni ghali bei ipunguzwe.

Hizo ndio siasa zetu zinavyotuathili walalahoi ukishakuwa mpinzani basi mchango wako unatupwa kapuni hata kama wewe ungekuwa daktari bingwa na unahitajika lakini ukaamua kufanya kazi ukiwa unafahamika vema kuwa ni wa chama cha upinzani, hautaheshimika wala kuhitajika tena hapo ndio tunajiuliza kama huu mfumo umetusaidia au umetubomoa kipi cha kujivunia katika huu mfumo.

Hata viongozi wa vya vya siasa hapa nchini wanalaumiwa kuwa mchango wao wakiwa kambi ya upinzani haujaonekana kutokana na kwamba wao toka uchaguzi umepita wamekuwa kimya hadi mwishoni mwa wiki walipoamua kudaka hoja ya Rada na kuishikia Bango kwenye maandamo lakini bila hiyo walikuwa hawana hoja na walikuwa wamelala usingizi.

Lakini jambo la Rada linaibukaje hapa wakati Rada ni ya siku nyingi ilinunuliwa na serikali ya awamu ya tatu na sasa inaelekea kuzeeka leo baada ya gazeti moja la uwingereza kulikumbushia sasa limegeuzwa hoja ya kupandia jukwani na ndege ya Rais je.

Hayo yamekwisha pita wananchi wasingependa kukumbushiwa kidonda walichoambiwa ni heri wale nyasi lakini ndege inunuliwe na kweli ikanunuliwa hatukuona mtu anakwenda Mahakamani au anaitisha maandamo ya kuipinga ndege na rada hiyo kama tunavyoshuhudia hata hivyo imefahamika wazi kuwa kuna kikosi huko uingereza cha kuzuia rushwa kubwakubwa CFO kinalishughulikia kisheria wala sio kwa maandamano.

Wananchi wengi sasa hivi wanalia maisha magumu mwaka mmoja uliopita waliokuwa wanaambiwa maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana lakini sasa yamebaki kuwa kitendawili kinachoteguliwa kwa kuambiwa kwamba maisha bora hayaletwi na serikali ila ni kila mtu kwa nafsi yake anatakiwa ayalete maisha bora kwake jambo ambalo hawakuambiwa wakati wa uchaguzi.


Hiyo ndio hoja ilikuwa ya msingi ya kushikia bango na kuwaongoza wananchi nje ya viwanja vya bunge kuiuliza serikali ya awamu ya nne kwamba imeshindwa kurejesha maisha bora hata yale machache yaliyokuwepo kipindi cha Mkapa ambayo yametoweka, kama imeshindwa iweze kuondolewa kwa muda mfupi kama tunavyoshudia katika serikali za wenzetu Rais anajiuzulu kwa kipidi cha miezi sita tu tangu aingie madarakani kwa kushindwa kuboresha maisha na kukuza uchumi.

Tunategemea kama wapinzani wa hapa nchini watakuwa makini na hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu haitamaliza miaka mitano madarakani kabla haijatimuliwa na nguvu ya UMMA kutokana na ugumuwa wamaisha unaowakabili na imani yao kuyzidi kupungua kutoka serikalini.

hatuwezi kuacha kusema ukweli

Siasa

Na g. boy

Kwa hili tuwe wazalendo tuambizane ukweli.

HABARI ambazo imetikisa kwenye vyombo vya habari wiki hii ni kuhusiasa na siasa ya nchi yetu inavyoendeshwa na baadhi ya watu kuitumia kama kitega uchumi maridhwa kufuna kodi za wananchi, pamekuwapo mazungumzo ambayo yameripotiwa kuendelea kwa siri kati ya chama cha wananchi CUF na Chama cha Mapinduzi CCM,ili kupata muafaka wa maelewano kwa upande wa visiwani kunakodaiwa CCM inawafuasi wachache kuliko CUF.

Wakati hayo yakiendelea huko visiwanai kwa upande wa pili huku bara ngomba iliyokuwa inaibwa kwenye vyombo vya habari ni jinsi mbunge na Mjumbe kamati ya haki na maadili ya Bunge alivyolipua bomu linalowahusisha wajumbe wa kamati hiyo na rushwa ili istende haki kwa kesi iliyokuwa mbele ya meza yao.

Hayo ndio yamejiRi kwenye siasa za Tanzania Wikii iliyopita na hayo matukio yote yanahusisha kwa namna moja au nyingine na ubadhirifu wa wazi wa fedha za wananchi, tukianza na mikutano ya viongozi wandamizi wa CCM na CUF kukutana kwa ajili ya kujadili namna ya kumaliza matatizo ya kile wanasiasa wanachokiita Mupasuko wa kisiasa Zanzibar.

Haya mazungumzo yanayoendelea na yamekuwa yakipigiwa debe na vyombo vya habari kuwa yanaelekea pazuri huenda yakazaa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo CUF itapeleka watu wake kuwa miongoni mwa wanaounda baraza la wawakilishi huko zanbari, lakini swali hapa ni kweli yanafaa kuungwa mkono na kila mtanzania? Hapana najua hatuna sababu ya kufanya hivyo!

Tukerejea kwenye kipindi cha uchaguzi uliomalizika kwa nyakati tofauti viongozi waandamizi wa chama cha Cuf walikariri wakisema safari hii wakiibiwa au uchaguzi ukienda mrama watakubali kuketi kwenye meza ya mazumngumzo, na mara kwa mara walisema hakuna muwafaka wa tatu lakini leo hii mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa uchaguzi tunaambiwa kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kati ya katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif na Yusuph Mkamba Katibu mkuu wa CCM haya mazungumzo ni ya nini?

Ni kwa nini imekuwa kila baada ya uchaguzi jamaa hawa wanaketi bila ridhaa ya wananchi wanaanza kutumbua kodi za wazalendo kwa kisingizio cha muafaka kumbe ni njia ya kujipoza taratibu na kufuta jasho lakipindi kirefu cha kuzunguka kwenye kampeni, sasa watanzania tunakuwa tunaambiwa kuwa ni mazungumzo ya muafaka ,muafaka gani wa kila baada ya uchaguzi hivi kwenye uchaguzi huwa mnagombana sasa mnataka muafaka ?

Cuf walitueleza kuwa hawatakuwa tayari kuketi kwenye mazungumzo yatakayozaa muafaka wa tatu leo tunaambiwa tuyaunge mkono mazungumzo hayo yanayoelekea kuzaa muafaka wa tatu je Cuf ilidanganya Taifa au iliposema hayo ilikuwa inamanisha nini? Kwa upande mwingine viongozi mashuri wa CCM visiwani wamesema katu watanzania wasitegemee kuona serikali ya mseto inaundwa visiwani humo.

Aliyasema hayo Naibu waziri kiongozi wa Zanzibar, Juma Shamhuna hawakumwelewa viongozi wengine wakafuata hakueleweka akafuata Rais wa Zanzibar, Amani Karume aliyewambia wanzanzibar wastengee uchaguzi wowote Zanzibar wala serikali ya mseto kwani ilani ya CCM ambayo inawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano haitambui kuwepo kwa serikali ya mseto, kauli ambayo iliwakatisha tama Cuf nakuamua kujifariji kwa kuitisha maandamano ya kumlaani.

Toka hapo hakuna kiongozi wa CCM Zanzibar anayelishughulikia jambo hilo zaidi ya kutumwa Katibu mkuu wa chama hicho kutoka Bara alikwenda huko, kwa ajili ya kuwapoza Cuf hata baada ya kufika huko imedaiwa kuwa aliyekuwa amepangwa kuwa mwenyeji wa Makamba amemkacha jambo ambalo makamba ameshindwa kuvumilia na kulipasua kwenye vyombo vya habari kuwa ametelekwa.

Mwaka 99 vyama hivyo viwili viliketi kwenye mazungumzo yaliyoongozwa na katibu mkuu wa jumuiya ya madola wakati huo chief Emeka Enyauko yaliyozaa muafaka wa kwanza na kuruhusu wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar kuingia kwenye vikao vya baraza hilo hatujui kwenye mazungumzo hayo Cuf waliahidiwa nini au walilipwa kiasi gani hadi wakakubali kuingia kwenyebaraza hilo bila kuunda serikali ya mseto, wakati ushindi ulipatikana kwa 50 kwa 49 dhidi ya CUF.
Na mwaka 2001 vyama hivyo viwili vyenye wananchama wanaozua utata nakushindwa kuelewa ni chama gani chenye wananchama wengi na wenye msimamo unalongana, viliingia tena kwenye mazungumzo baada ya kushudia roho za wazanzibar zikiishia kuzimu huku propaganda nyingi zikitawala kwenye machafuko hayo ,kwani dola inayoonbgozwa na CCM ilitanza kuwa ni watu 21 tu walikufa huku kafu ikisema ni watu 50 huku kikisahau kauli yao ya awali kabisa iliyotolewa na kiongozi wao mmoja aliyekuwa anahijiwa na redio moja akasema Jahazi limezamishwa baharini na kuwa watu walikuwa wanakimbilia Kenya.

Pia kwenye muafaka huo tulichoshuhudia ni kuona muafaka ukisainiwa na uchaguzi ukirejwa kwa upande wa wawakilishi tu si kwa rais wakati machafuko yanatokea Cuf ilikuwa inadai imeibiwa kura za urais na karume hakushina kihalali wala hawakudai za wawakili, wengi tulishangaa tuliposikia uchaguzi ukirudiwa kwa wabunge na wawakilishi tu huku Cuf ikipata pigo la kupoteza baadhi ya majimbo ya watu waliowekewa pingamizi jambo lililowaumiza wananchi wakaamua kupiga kura za maruhani! Huo ndio mchezo wa wanasiasa.

Tangu hapo tumekuwa tukiambiwa kuwa hakuna muafaka wa tatu Zanzibar sasa haya mazungumzo yanayoendelea nin ya nini au ndio kila mmoja kujaribu kujinufaisha kwenye nafasi aliyonayo kisiasa! Kama ni seriukali ya mseto si jambo la kuketi mezani na kugawana pesa za walipa kodi bali lilikuwa ni jambo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa CUF kumtaarifu kuwa wanataka wajumbe watatu kutoka kwenye chama chao wajiunge kwenye baraza la mawaziri na wawakili.

Kwa muda usio zidi siku tatu Cuf ingekuwa imepiga hodi ikulu kupeleka majina mawili kutoka zanzibar moja kutoka pemba na lingine kutoka unguja huku kiki na penati ya majina mawili ya kuchuuja kati ya Mharagande na Lwakatare nani anafaa kuteuliwa kutoka bara kuingia katika baraza la mawaziri wa Tanzania kilikuwa ni kitendo kidogo tu Cuf hawakatai CCM ndio wanakataa na walipaswa wakae wenyewe lumumba au bwawani wakubaline ndipo waandikie Cuf barua sio jambo la kuchikua muda na kutafuna pesa za walipa kodi.

Huo ndio mchezo unaoendelea haya tusuburi tuone kama yale maneno ya Amani kwamba hakuna serikali ya mseto wala kurudiwa kwa uchaguzi yatabezwa kwani ikimbukwe kwamba amani ni makamu wa mwenyekiti wa CCM ambaye ambaye anajaribu kuunda serikali hiyo inayokataliwa na makamu wake je ni nani atakayemsaliti mwenziwe tusubiri tuone kama sio geresha, ikiwa viongozi wakuu CCM Zanzibar wanakataa kuitambua serikali ya mseto na CCM bara inashawishi iwepo je tusubiri kuona mapasuko ndani ya chama hicho kunachoelekea kwenye uchaguzi wa ndani au ni usanii.

nimeanza

.

Mswaada wa Habari unaoitwa uhuru wa habari

Mjadala wa Muswada wa Uhuru wa Habari ni suala la kisiasa, kimaslahi au kitaaluma?

Na Ayoub Rioba


KWANZA naanza kwa kujisalimisha kwa wasomaji. Mimi ni Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ijulikanayo kama MISA-Tan. Hivyo basi natambua jinsi inavyoweza kuwa vigumu kwa watu kutenganisha mawazo yangu kama Ayoub, au mwandishi wa habari, au mhadhiri katika chuo cha Uandishi wa Habari au, kwa upande mwingine, kiongozi wa taasisi inayotetea Uhuru wa Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika. Napenda kuwaruhusu wasomaji wangu kuyasoma mawazo yangu kwa miwani yoyote watakayoichagua.

Nitajitahidi kwa kadri ninavyoweza nijadili hoja yangu kwa urahisi sana, bila kujificha katika kichaka cha wanazuoni, nikiwakalifu na kuwakoga wale wasiojadili maswala haya kwa kutumia mbwembwe na istilahi za kisomi. Nafanya hivyo makusudi ili kutoa mchango mpana katika mjadala huu ambao tokea ulipoibuka umejenga taswira tata machoni pa wadau mbalimbali wa habari wakiwamo wananchi kwa ujumla.
Mjadala huu ni muhimu sana kwa taifa. Watanzania wengi, waandishi kwa watu wa kawaida, wamekuwa wakijadili kwa hoja mbali mbali ama kuunga mkono au kupinga muswada huu. Wapo pia walioujadili muswada huu bila hata kujua maana yake kinadharia na hata kimantiki tu.

Lakini kujadili kwao ni muhimu sana kwani kwa kufanya hivyo tu, wanaupa mjadala uhai zaidi. Napenda nianze hoja yangu kuu kwa kunukuu barua moja iliyochapishwa katika gazeti moja la kila siku hapa nchini ikiuliza swali la msingi sana. Kichwa cha habari cha barua ile kiliuliza: Muswada wa habari ni suala la kisiasa, kimaslahi au kitaaluma?

Upo umuhimu wa kujaribu kujibu maswali ya barua ile, iliyoandikwa na mwandishi aliyejitambulisha kama Alisea Mbogela, kwani iliuliza maswali mazito na muhimu sana. Kwangu mimi hakuna utata wowote kwamba suala la Muswada wa Habari laweza kuwa la kisiasa, kimaslahi binafsi na kitaaluma pia. Ni suala linalogusa vyote alivyovitaja Alisea.
Huenda tu nirejee baadhi ya yale aliyoyasema Alisea kwa kumnukuu: “Ingawa mimi si mwandishi wa habari, na ingawa napenda sana kusoma habari mbalimbali ili kwenda na wakati, kuna vitu vitatu vinanishangaza kama si kunitatiza anaeleza mwandishi huyo’.
La kwanza linalomtatiza ni ukweli kwamba Dr. Sengondo Mvungi aliwania urais mwaka juzi kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, na kwa upande mwingine Anthony Ngaiza akawania ubunge katika Jimbo la Muleba Kaskazini kupitia TLP. Alisea anasema ana wasiwasi kuwa kwa vile wawili hao walishindwa katika uchaguzi basi wanaweza kuwa wanatumia nafasi hii kuipinga Serikali iliyoko madarakani.
La pili mwandishi pia anauliza kwamba katika kila mikutano mbona ni hao wawili tu wanaozungumza? Hakuna wadau wengine? Mbona hawasikiki?
La tatu, anauliza, wale waandishi wanaounga mkono muswada, ni kweli wanaunga mkono kwa dhati? Nahoji hivyo kwa sababu duniani kote, hakuna urafiki kati ya Serikali na waandishi wa habari, anasema Alisea na kuongeza kuwa ndiyo maana anashawishika kuamini kuwa malumbano haya kuhusu muswada wa habari, yanaweza kuwa yameegemea zaidi ama kwenye siasa na au maslahi binafsi badala ya taaluma.
Alisea ana haki kabisa ya kutatizwa na masuala yote haya. Aliyeisoma barua ya Alisea kwa makini, atagundua kuwa mwandishi yule ana uwezo mzuri wa utambuzi wa mambo kuliko inavyojidhihirisha katika barua ile. Anauliza maswali muhimu kwa kujaribu kuonyesha kwamba hana anakoegemea. Na kwamba huenda ni kutokana na kuonekana kutokuwa na pa kuegemea ndiyo maana anatatizwa.
Kwanza kabisa tuanze na tatizo la kwanza la muswada kuonekana wa kisiasa. Tukianza na sera, miswada yote inapotungwa na hata inapofikia kuwa sheria, yote haya hufanyika kwa kufuata taratibu zinazoratibiwa na kuamuliwa kisiasa.
Hivyo basi suala la muswada kuwa la kisiasa halina utata. Hili la Dk. Mvungi na Ngaiza kuwa waliwahi kuwania nafasi za uongozi kupitia vyama vya upinzani halitoshi kushamirisha hoja ya kusema suala la kupinga muswada ni la kupinga serikali iliyo madarakani. Hoja hii ni changa mno, sawa sawa na ile ya kusema kama hauko nasi basi uko na adui yetu.



Dk Mvungi ni Mhadhiri mwandamizi wa sheria kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliwahi kuwa mwandishi wa habari. Dk. Mvungi pia amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari na ana ufahamu mkubwa wa masuala ya vyombo vya habari na sheria zinazobana uhuru wa habari. Pale Dk Mvungi anapochepuka na kuingiza siasa katika suala la kitaaluma basi apingwe, na kuhojiwa kwa mizani ya hoja.
Anthony Ngaiza ni mwanahabari wa siku nyingi, lakini pia ni mwanataaluma katika habari. Aliwahi kuwa Mratibu wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ) wakati huo, na amekuwa mhariri wa magazeti kadhaa yaliyoheshimika sana kabla hajawa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). Anapokuwa anaingiza siasa katika hoja zake basi apingwe kwa mizani ya hoja na siyo taswira tu ya yeye yuko upande gani au anaamini katika nini.


Lakini kila mtu ana haki ya kuchagua kuwatazama watu hawa kama anavyotaka. Alisea anaweza akachagua kumtazama na kumhukumu Dk Mvungi pale tu alipoamua kutumia haki yake ya Kikatiba kugombea urais wa nchi kutumia tiketi ya chama cha upinzani. Alisea anaweza pia akafumbia macho ukweli wa sifa zingine zote alizo nazo Mvungi, ikiwa ni pamoja na haki zake na majukumu yake kama raia.
Anaweza pia akachagua kumtazama na kumhukumu Ngaiza pale tu alipoamua kutumia haki yake ya kikatiba kugombea nafasi ya siasa kupitia chama cha upinzani na akafumbia macho ukweli kuhusu sifa na haki zingine zote alizo nazo Ngaiza kama raia.
Hawa wawili ni Watanzania wenye haki sawa kabisa na Mtanzania mwingine yeyote ya kutimiza wajibu wao kama raia, hasa pale wanapokuwa na nafasi na ufahamu zaidi kuhusu suala husika, kama hili la uhuru wa habari.
Katika suala la pili la kudai ni Dk Mvungi na Ngaiza tu wanaoongoza upingaji wa Muswada, huenda ni kutokana na Alisea kuchagua kufumba macho, na hivyo kushindwa kabisa kuwaona akina Mohamed Tibanyendera (ambaye si mwanasiasa, bali mwanasheria kutoka MISA-Tan).


Wengine ni Rose Haji (ambaye si mwanasiasa, bali Mkurugenzi wa MISA-Tan), Ananilea Nkya (Ambaye si mwanasiasa, bali Mkurugenzi wa TAMWA), Ayub Rioba (Ambaye si mwanasiasa, bali Mwenyekiti wa MISA-Tan), Pili Mtambalike (ambaye si mwanasiasa, bali ni Afisa Programu wa MCT) wakishiriki katika mchakato wa kuwaunganisha wadau wengine zaidi kuujadili muswada huo ili kuongeza uelewa wa jamii kwa ujumla.
Kuchagua kuwaona Dk Mvungi na Ngaiza peke yake katika mchakato huu huenda kukawa kwa bahati mbaya au la, au yote mawili.
Hivi sasa kuna wadau mbalimbali wakiwamo wanasheria, wanataaluma zingine, wanasiasa, na hata wananachi wa kawaida wanashirikishwa katika kutoa mawazo yao kuhusu Muswada huo.

Lakini pia ipo hoja ya msingi sana hapa kuhusu ujenzi wa demokrasia. Mwandishi wa barua ile, huenda bila kutambua, ni kama anahitimisha kwamba wadau wote wanaoshiriki kuupinga Muswada ule watakuwa waligombea nafasi katika upinzani kama walivyo Dk. Mvungi na Ngaiza na wakashindwa na hivyo basi wanaamua kupinga muswada wa serikali kuikomoa!
Upo ukweli kwamba kinachojadiliwa pale ni hoja za kinadharia ina dhana juu ya umuhimu wa uhuru wa habari na wala si sera za vyama. Na hili pia linatusukuma kuona umuhimu wa kushamirisha uelewa miongoni mwa wananchi wetu kuhusu ukweli kwamba upinzani si uhalifu. Na kutoa hoja za kupinga serikali si kosa la jinai na ndiyo maana wanaopinga hawajakamatwa kupelekwa mahakamani.

Ndani ya CCM yenyewe kuna demokrasia inayoruhusu watu kupingana. Kutofautiana
kimawazo, kimaoni na kifikra. Serikali peke yake isiyoweza kupingwa ni ya Mwenyezi Mungu asiyekosea daima.
Suala la tatu lililomtatiza mwandishi wa barua ile ni baadhi ya waandishi wa habari kuonekana wanaunga mkono muswada ule katika namna iliyoonyesha urafiki wa karibu kati ya wao na serikali.
Kwanza kabisa kama nilivyokwishasema hapo juu, kila raia wa nchi hii anao uhuru wa kuwa na maoni yake na kuyatoa bila kushurutishwa. Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawapa uhuru wa kufanya hivyo.
Na huenda mjadala (wengine wanauita malumbano) usingekuwa na mchango mkubwa wa mawazo mbalimbali kama ilivyo sasa kama wote tungekuwa upande mmoja tukikubaliana kwa kila jambo. Ni ukuku huo huo wa kutaka kukubaliana katika kila jambo unaotusukuma wengine kuupinga muswada huo kupelekwa Bungeni kama ulivyo.


Mwandishi Alisea anazungumzia kama kuna maslahi binafsi yanayosukuma baadhi ya waandishi wanaojadili Muswada huu. Uzoefu wa hulka ya binadamu unatuonyesha kuwa binadamu wote duniani, madhali bado wangali hai, wanayo maslahi wanayoyapigania, ukubwa wa maslahi, aina za maslahi, mbinu za upiganiaji, nguvu za upiganaji, na hata viwango vya malipo ya upiganiaji maslahi hutofautiana kulingana na kila binadamu anavyojithamanisha mwenyewe au anavyoithamanisha jamii yake kwa ujumla. Hili linahitaji mjadala mpana zaidi.
Alisea anaenda mbali zaidi. Anasema duniani kote hakuna waandishi wa habari wanaokuwa na urafiki wa karibu na serikali. Labda nitoe tu mfano wa nchi ambayo ni rafiki ya Tanzania kabisa. Naamini Alisea angefanya utafiti asingezungumza hivyo. Leo hii Zimbabwe kuna makundi mawili makuu ya waandishi na uandishi wa habari.


Yapo magazeti yanayomilikiwa na watu binafsi ambayo hutoa mawazo binafsi na hata yale yanayopinga baadhi ya sera za serikali na utekelezaji wake. Haya ofisi zake hupigwa mabomu mara kwa mara na waandishi wake kukamatwa na kushikiliwa na polisi kila mara.
Na upande mwingine yapo yale ambayo kazi yake ni kuimba nyimbo za kumsifu Rais Robert Mugabe na mkewe Grace muda wote. Wakati mwingine huandika habari na makala za kupinga yale yaliyoandikwa na magazeti binafsi kuibua uovu na kashfa mbalimbali.
Ilitokea siku wananchi 16 wakauawa na polisi katika vurugu za siasa, lakini yale magazeti tawala yakawa na habari kuu ukurasa wa mbele zikielezea masuala ya Rais Mugabe na Grace walivyohudhuria sherehe moja hivi. Na kipo kisa cha waandishi wa pande mbili hizi ambao waliwahi kuchapana makonde kwa sababu tu mwandishi wa kambi ya upinzani aliandika makala iliyomuudhi mwandishi wa kambi tawala.
Mwandishi wa kambi tawala akamfundisha adabu pale pale na baadaye kumuitia polisi ambao walienda kumuweka ndani huku damu zikimchuruzika. Siasa za Zimbabwe zinafahamika kwa wengi.

Tukiiongelea zaidi Zimbabwe huko wanayo Sheria ya Uhuru wa Habari ambayo aliyekuwa Waziri wa Habari wa nchi hiyo, Profesa Jonathan Moyo, aliipigania sana hadi ikatungwa. Profesa Moyo (Mungu ailaze akili yake mahala pema peponi) ni msomi aliyekuwa akifundisha katika chuo kikuu cha Harare na baadaye kuingia katika siasa.
Kabla ya kuingia katika serikali, Profesa Moyo anakumbukwa jinsi alivyokuwa mwiba kwa uongozi wa Mugabe kwa kukosoa na kupinga tabia zilizoenda kinyume na maadili ya demokrasia.
Lakini baada ya kuingia madarakani aliweka usomi wake kando kwa sababu ya maslahi na akafanya mambo ya kijinga kweli kweli hata mwishowe Mugabe akamdharau. Akamtimua. Profesa Moyo akakimbilia katika upinzani alikokutana na joto la moto aliouwasha kwa kutunga sheria kandamizi kwa uhuru wa habari.
Waziri Muhammed Seif Khatib, tunaweza kusema, ni mpenda uhuru wa habari. Asingekuwa mpenda uhuru wa habari, na kusingekuwepo uhuru wa habari nchini, Khatib asingethubutu kuandika baadhi ya maudhui anayoyaandika katika makala zake, hata kama yuko chama tawala.

Kesho yake angeamka akajisoma makala yake mwenyewe na kwa vile ndiye waziri wa habari, akaamua kulifungia gazeti la Mzalendo. Pamoja na kuwa na sheria kandamizi mkononi mwake, yeye na Mkurugenzi wa Maelezo, Kassim Mpenda, hawakutaka kuzitumia kufungia vyombo vya habari hovyo, au kutoandikisha magazeti fulani kwa kuyahisi vibaya wakati huu wa mpito kuelekea demokrasia ya kweli.
Wawe wamefanya hivyo kwa ushauri au imani yao katika misingi ya demokrasia, bado ni dhahiri kuwa historia itawakumbuka kwa kulinda uhuru wa habari pamoja na kuwepo sheria mbaya za kikoloni ambazo Tume ya Jaji Francis Nyalali alikwishashauri zifutwe.
Kwa hiyo namchukulia waziri Khatib kama mwandishi mwenzetu. Mbali na kuwa mwandishi wa gazeti kongwe la Mzalendo, yeye pia ni mmiliki wa Kituo cha Radio visiwani Zanzibar.


Tunamtarajia sana atusaidie katika mchakato huu wa kuunda sheria ya uhuru wa habari itakayoshamirisha uhuru na siyo afuate nyayo za Profesa Jonathan Moyo alipokuwa waziri. Naamini kabisa katika hili Waziri Khatib na timu ya wataalamu mahiri waliopo MAELEZO watatuunga mkono kwa faida ya demokrasia ya nchi yetu na vizazi vijavyo.
Sasa nirejee katika hoja za msingi kuhusu Muswada. Ninamshukuru sana Alisea kuuliza kama muswada ni swala la taaluma pia. Muswada huu unahusu moja kwa moja dhana ijulikanayo kote duniani kama uhuru wa habari. Kwa kifupi tu nieleze kuwa historia ya binadamu kutaka kuwa huru ni ya muda mrefu kama ilivyo ile ya baadhi ya watu kutaka kuwakandamiza wengine.
Kuanzishwa kwa vyuo vikuu kule Timbuktu Mali na hata kule Alexandria kulikuwa na lengo moja la kusaidia kuweka huru fikra za mwanadamu. Kwa mfano: Binadamu anaweza akazaliwa akakua akiamini, kwa mujibu wa mila zake, kwamba kila akiugua basi karogwa. Huyu anaamini hivyo siyo kwa sababu anaona raha kuogopa uchawi, la hasha. Anaamini hivyo kwa sababu tu fikra zake hazijawekwa huru.
Mchezo wa kuhurisha fikra ulianza zamani. Katika vitabu vya wanazuoni na

wanafalsafa tunasoma, kwa mfano, kuhusu wagiriki akina Sokrates, Plato, Aristoto na wengineo, walivyoanzisha mchezo wa kuhuisha na kuhurisha fikra. Sokrates kwa mfano, alianza kwa kuhoji kila jambo, kila imani.
Kuhoji ni mwanzo wa kujua. Asiyehoji hawezi kujibiwa. Atajibiwa na nani? Sokrates aliwaambia wagiriki wenzie kwamba binadamu anayekubali kuishi bila kuhoji ana matatizo. Ni kama aliyekufa. Yeye alihoji hadi akachukiwa. Wakamuandalia mashitaka. Wakamhukumu kufa. Hao hao waliomhukumu kufa, wakapanga kumtorosha asiuwawe. Yeye akakataa. Akasema hachezi michezo ya kitoto ya kutoroka jukumu lake la kiraia la adhabu ya kifo. Siku yake ilipofika akaomba sumu yake akainywa akafa. Kama alivyofanya Saddam Hussein na kamba yake shingoni.
Historia ina undugu wa karibu sana na watu kama Sokrates, mwingine aliitwa Galileo Galilei. Yeye alipenda kuhoji. Katika kuhoji akajibiwa. Akatambua kuwa dunia haikuwa tambarare tu kama meza. Akawaambia watawala kuwa dunia ilikuwa duara ikijizungusha katika muhimili wake na kwamba vyote vilivyomo vilishikiliwa na nguvu ya uvutano. Watawala wakampinga.

Wakajua kama amekuja na ukweli ule basi nguvu yao ya kutawala kwa mafundisho ya mapokeo itakuwa inatishiwa uhai. Wakaamuru auwawe. Badala ya kuchukua hatua za kuua ujinga alioufichua, wakachagua kuua ukweli. Ukweli usiokufa kamwe.
Ukaja wakati ambapo elimu ya kuhoji ilianza kusambaa duniani kote, hasa baada ya teknolojia ya maandishi na uchapaji kuruhusu utoaji wa nakala nyingi. Jinsi machapisho yalivyosambaa zaidi ndivyo sayansi na teknolojia vilivyoanza kukua kwa kasi.
Kufikia karne ya 16, tayari watu Ulaya walikwishaanza kuhoji kwa kuandika, maovu waliyokuwa wakiyafanya watawala. Wakati huo zilitungwa sheria kali sana za kuwabana raia wasithubutu kuhoji. Adhabu za faini kubwa na hata kifo ziliwekwa kwa yeyote aliyethubutu kumsema vibaya, kumkejeli au kumtukana Mfalme, kwa mfano.
Lakini bado watu wengi waliendelea kuhoji huku wakijua watauwawa. Kwao ilikuwa bora kufa na fikra zinazoishi kuliko kuishi na fikra zilizokufa. Kadiri waliohoji walivyokuwa wakizidi kuuwawa, upinzani dhidi ya uimla ukazidi kuongezeka pia. Ndiyo maana wanafalsafa wengi wa karne ya 16 hadi 19 walikazania sana umuhimu wa uhuru wa kujieleza, uhuru wa kujua wanaongozwaje na uhuru wa kujiamulia mambo.


Jambo la ajabu, ambalo wakati mwingine tunashindwa kuliona wazi, ni kwamba kipindi ambacho Ulaya iliendelea kwa kasi kubwa kilikuwa ni kati ya Karne ya 16 na 18. Hiki kilikuwa kipindi cha uamsho ambacho uhuru wa kujieleza na kuhoji ulitolewa jela.
Watu walihoji, wakajua. Walivyojua wakawa huru. Wakafikiri. Wakatambua. Wakabuni. Wakaumba. Wakaunda. Wakatawala dunia.
Thomas Jefferson, mwanafalsafa maarufu na aliyewahi kuwa rais wa marekani alitambua mno umuhimu wa uhuru katika maendeleo ya binadamu. Mawazo aliyoyaweka katika Katiba ya Marekani yamechangia kulifanya Taifa hilo kuwa na nguvu za ajabu duniani.
Haikuwa ajabu basi pale Wamarekani walipoamua kuweka bayana katika badiliko la kwanza la Katiba yao, kwamba si Bunge lao wala chombo chochote kile kitaruhusiwa kutunga sheria iwayo yote itakayochezea uhuru wa habari.
Wamarekani wanayo mapungufu mengi kwa sababu nao pia ni binadamu. Lakini ni taifa ambapo watu wengi duniani wanataka kukimbilia huko. Mafanikio yao, kwa kiasi kikubwa, yametokana na kuitumia vyema dhana ya uhuru.
Somo jingine kubwa kuhusu suala la uhuru wa habari, au uhuru wa maoni, kujieleza na

kupata habari, lilipatikana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Wakati moshi wa mabaki ya moto ulioteketeza asilimia kubwa tu ya maisha, viwanda, majengo na miundombinu ya Ulaya ukiendelea kufuka. Wazungu kutoka nchi 50 mbalimbali, huku wakiwa na makovu ya vita waliamua kukutana jijini San Fransisco, Marekani mwaka 1948. Kule wakatizamana. Wakashangaana. Wakaulizana: kulikoni tuuane hivi? Ni kwa nini binadamu tunaoonekana kuwa na akili kuliko viumbe vingine vyote duniani, wakiwamo waafrika, tuwe wa kwanza kufanya maangamizi ya kijinga kabisa katika historia ya dunia?
Jibu walilolipata ni moja tu. Vita ile ilikuwa ni matokeo ya ubabe. Ukandamizaji. Wachache kuziba midomo ya wengi ili waendelee kufanikisha maslahi ya kundi fulani. Kwamba baadhi ya binadamu waliamua kutumia ubabe kutimiza matakwa yao binafsi na kwa kuzuia kabisa sauti za waliowapinga. Wajumbe wa mkutano wa San Fransisco wakatambua kuwa endapo nchi zile zilizoanzisha vita zingelikuwa na utaratibu ulioruhusu mawazo

mbadala kusikika, basi wasingefika kule.
Wakagundua kwamba haki ya kutoa maoni au kuhoji na kujua ni haki anayozaliwa nayo mtu. Wakagundua pia na haki zingine nyingi za msingi zilizokuwa zikivunjwa kufikia hatua ya kusababisha vita. Wakaziainisha zote. Wakatoa tamko. Tamko la Haki za Binadamu duniani.
Na sisi Afrika tukaja na tamko letu pia. Tamko hilo lilikuwa limekopi karibu haki zile zile za Tamko la Dunia. Lakini kama kawaida yetu, tulikopi tu. Tukadesa vipengele vile. Tukakariri kwa ajili ya kujibia mitihani ya wazungu, basi! Katika nchi moja moja, tukaingiza vipengere vya haki za binadamu katika katiba. Tanzania iliziingiza haki zile katika katiba mwaka 1984.
Nasema tulidesa kwa sababu kwa miaka takriban 50 sasa bara la Afrika ndilo linaongoza kwa kuvunja haki za binadamu. Bara hili linaongoza kwa kuwa na watawala wanaowakandamiza watu wao kupita viwango vya ubinadamu. Watawala wasiojua kuongoza kwa ubunifu wala kwa haki; Watawala wanochukua madaraka na kuzigeuza nchi zao kuwa kama kampuni binafsi wakiwapora raia wao na kuwaacha maskini wa kuhurumiwa; Watawala wanaoua yeyote anayethubutu kuhoji au kuwapinga; Watawala wanaofurahi kuwa vibaraka wa mabwana wa kikoloni wanaoahidi kuwalinda madarakani; Na ni kwa sababu hiyo tu, Afrika imebaki nyuma. Imebaki kichekesho.
Njaa haiishi. Vita haviishi. Bara linanuka. Kipindupindu hakiishi. Kwa sababu watu wake wamekubali kula kinyesi. Hawahoji.
Lipo jambo moja kubwa na zuri kuhusu Tanzania. Ni kweli hii ni nchi ambayo ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa ambayo kwa kiwango kikubwa ilifunga uhuru wa habari

na uhuru wa maoni. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 1990, tulibadili katiba kuruhusu vyama vingi.
Papo hapo tukawa tumefungulia maoni mbadala katika vyombo vingine vya habari ambavyo havikuwa vya serikali. Katika kipindi hicho, Tanzania ilishuhudia maoni yaliyokuwa jela yakifanya vurugu katika vichwa vya habari vya magazeti na redio. Walishuhudia uandishi wa habari uliochokonoa yale ambayo hayakuwahi kuandikwa.
Walishuhudia uandishi wa habari uliowasema viongoziwakuu katika namna ambayo haikuwahi kutokea. Tanzania tuna bahati sana. Tumshukuru sana Mungu kwamba aliyekuwa rais wa pili alikuwa ni Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Mtu rahim. Mpole. Mvumilivu. Rais Mwinyi hakukimbilia kufungia vyombo vya habari eti tu kwa vile vilimkosoa, au hata wakati mwingine kumtukana. Alivumilia.
Na alipohojiwa baada ya kustaafu ni vipi alivumilia uhuru wa habari kiasi kile alitoa jibu kama mzazi.
‘Nilijua wahariri na waandishi wale wana watoto nyumbani. Na kwa kuniandika vile waliuza magazeti. Na kwa kuuza, waliweza kupata fedha za kuwapa watoto chakula na hata kuwapeleka shule’alijibu Mzee Mwinyi.
Nilipomhoji mzee Mwinyi wakati wa kuadhimisha miaka 40 ya uhuru wa Tanganyika, nilimuuliza msingi wa falsafa yake ya ruksa. Jibu alilolitoa Mzee Mwinyi lilipaswa kuwa msingi wa sheria yeyote ya mambo ya habari tunayoiandaa sasa. Alisema: Binadamu yeyote yule anazaliwa huru. Msingi mkubwa wa kuishi kwetu na kustawi kwetu ni uhuru.


Muongo mmoja na nusu umetimu sasa tokea tulivyoanza mageuzi ya kisiasa na uchumi wa soko huria katika nchi hii. Tanzania bado ni nchi iliyoshikamana na yenye amani. Ingawa kumekuwapo matukio na vijimambo vya hapa na pale vilivyoonyesha kutikisa umoja wetu, hakika vimekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kupima uimara wa umoja wetu.
Pamoja na mapungufu yote yanayoonekana katika vyombo vya habari; pamoja na hawa tunaowaita makanjanja, ambao ni raia wa Tanzania pia, bado kuwa na uhuru wa habari ni muhimu mno kuliko kuwa na sheria inayokandamiza uhuru huo.
Katika kuhakikisha waandishi wa habari wanajidhibiti wenyewe, mwanzoni mwa miaka ya 1990 waandishi wa Tanzania walijiunga pamoja na kupinga jitihada za Serikali kutaka kupeleka Muswada kama huu wa sasa Bungeni. Serikali ilisikiliza. Muswada ule haukwenda. Waandishi wa habari tukiwa na wadau wengine tukaunda baraza la habari huria.


Baraza hilo, pamoja na kubezwa na baadhi ya wadau wachache, limekuwa na mafanikio makubwa tu. Zaidi ya asilimia 97 ya maamuzi yake yanafuatwa. Tayari viongozi wa kitaifa, akiwamo makamu wa rais wa zamani, Hayati Omar Ali Juma mashauri yao pale yakasikilizwa. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya aliwahi kupeleka shauri lake pale likasikilizwa. Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye aliwahi kupeleka shauri lake pale. Watu wa kawaida kabisa kama Neema, binti mmoja ambaye aliandikwa vibaya katika michoro ya gazeti moja alipeleka shauri lake pale na likasikilizwa na gazeti likamlipa kifuta machozi shilingi milioni mbili. Wapo wengine wengi tu kama Neema.
Lakini pia wapo ambao walipeleka mashauri yao pale na hawakuridhika, hivyo ikawabidi kupeleka kesi mahakamani. Hii ni kawaida kabisa. Na ndiyo maana Baraza la Habari Tanzania halimfungi mtu kupeleka suala lake mahakamani endapo hakuridhia uamuzi wake. Kuwepo kwa baraza huru kumesaidia sana kupunguza kesi ambazo zingefilisi magazeti haya endapo zingepelekwa mahakamani. Kule mahakamani nako kesi hukaa muda mrefu kabla mtu hajapata nafuu aliyoihitaji baada ya kudai kukashifiwa.
Leo Muswada mpya unapendekeza tuwe na Baraza lenye meno! Baraza litakaloamua nani
awe mwandishi na chombo gani kinafaa au kutofaa kuwa hewani au mtaani. Maudhui gani yaonyeshwe au kuchapishwa n.k.
Hiyo, wataalamu wa masuala ya habari si wanaonya kabisa si kazi ya serikali. Serikali yoyote inayotaka kuwajibika kwa wananchi inahitaji kukosolewa. Inahitaji kukosolewa na wapinzani lakini pia inahitaji kukosolewa na vyombo vya habari.
Serikali hiyo ikiwa na madaraka ya kudhibiti vyombo vya habari basi itakuwa inaua demokrasia. Kawasome, Dennis McQuail wa Uingereza (2005), John C. Merrill wa Marekani (2000, 2004), Kaarle Nordestreng wa Finland (2006), Francis Nyamjoh wa Cameroon (2003), Guy Berger wa Afrika ya Kusini (2000), Prof. Karikari wa Ghana (1998), na wengineo wengi.
Kwanini tudhani kwamba wale wanaoitwa makanjanja ndio wanaoharibu uandishi wa habari? Kwani vyombo hivi vya habari havina wahariri? Kwani makanjanja ndio wahariri wanaoruhusu kila kinachochapwa au kurushwa hewani? Je kuwadhibiti makanjanja kwa kutumia sheria ndiyo njia pekee inayofaa kuboresha uandishi wa habari? Je kila aliye na digrii atakuwa mwandishi mzuri na anayefuata maadili? Yapo wapi majibu ya maswali haya?
Kwani katika uandishi wa habari pekee ndiko kwenye makanjanja? Huko katika siasa hakuna makanjanja? Huko kwa wanaosaini mikataba ya kutia Taifa hili hasara hakuna makanjanja wenye vyeti vikubwa tu? Tuna miaka 45 ya uhuru na bado takwimu zinaonyesha hapa kwetu watu maskini wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku wanazidi kuongezeka.
Umaskini huo umesababishwa na makanjanja wa kwenye vyombo vya habari? Je ni hatua gani za kisheria zimechukuliwa dhidi ya makanjanja wa kisiasa ambao wamelitia Taifa hili katika umaskini?
Kujenga hoja kwamba ni lazima tuwadhibiti makanjanja kwa sheria ni kutafuta visingizio vya kutunga sheria za kikoloni kwa lengo la kulinda au kuendeleza maslahi ya watu binafsi au ya kundi fulani.
Hoja kubwa kuliko zote ni kwamba hapa tulipofika si pa kurejea tena katika sheria za kikoloni zilizokuwa na lengo la kumkandamiza, kumdhibiti na hata kumdhalilisha mwananchi wa Afrika.
Lengo likiwa kumnyamazisha asipige kelele wakati wao, mbwana, wakipora rasilmali za Afrika. Leo hii hata ripoti zinazoandikwa na CIA ya Marekani kuhusu Tanzania zinakiri kuwapo kiwango kizuri cha uhuru wa habari nchini na hata kutoa mfano kwamba gazeti la serikali la Daily News pia mara kwa mara huandika habari za kukosoa serikali.
Hiyo ni hatua kubwa mno katika demokrasia ya nchi yetu. Na ni sifa kubwa (tena ya dhati) kwa viongozi wa nchi. Kwa nini tudhani ipo haja ya kurudi katika siasa za kikomunist katika kudhibiti vyombo vya habari na utoaji habari, huku tukiwa na juhudi kubwa za kuedeleza uchumi wa kibepari kwa upande mwingine?.
Kwanini sheria za kuwavutia na kuwalinda wawekezaji (wengi wageni) ziwape haki, uhuru mkubwa na kuwalinda zaidi wao (Hata pale ambapo wanafaidika zaidi kuliko sisi) na iweje leo tukae chini kutaka kudhibiti uhuru wa kupata habari na uhuru wa kuandika habari kwa raia wetu wenyewe?
La mwisho, ninahofu moja kubwa kwamba mtu yeyote anayezungumzia kutunga sheria ya kubana uhuru wa habari ama kuzuia wananchi wasijue mambo kadha wa kadha muhimu ya uendeshaji wa nchi au kudhibiti ni nani awe mwandishi na ni nani asiwe, anajaribu kulilenga jua kwa manati. Dunia ya sasa haina magazeti, radio na televisheni peke yake.
Watanzania asilimia kubwa sasa wana ama mawasiliano ya simu au barua pepe. Humo hutumiana ujumbe mbalimbali kuhusiana na yale ambayo sheria haziwezi kuruhusu yaandikwe magazetini. Kuanzia nani kahusika katika mikataba fulani mibovu hadi nani kalipwa nini na ziko wapi. Zipo blogu katika mtandao wa intaneti ambako watu huwasiliana yale ambayo hayaandikwi hadharani kwa kuhofia sheria. Lakini maudhui yale hunakiliwa kule na kuletwa mitaani ambako watu wengi zaidi husoma.
Ushauri wangu mkubwa kwa serikali ni kwamba kwa sasa ielekeze nguvu nyingi sana katika sheria ya rushwa. Hilo ndilo tatizo kubwa sana linalosababisha umaskini wetu kuongezeka, elimu kushuka, huduma hospitalini kudorora, njaa kutuandama kila mwaka, kukosa umeme wa uhakika, wakulima wa korosho, pamba na kahawa kuendelea kunyonywa na matajiri, n.k.
Hayo yote hapo juu hayasababishwi na makanjanja au kuvuja kwa siri za serikali, zikiwamo taarifa kuhusu mikataba na wawekezaji au IPTL au manunuzi tata ya NBC au Rada au Ndege ya Rais, au mikataba mibovu ya madini au utata ulioigubika Richmond. Huu ndio ukweli tusiotaka kuuzungumza wazi kwa sababu tu tumeanza kupoteza mwelekeo kama Taifa na tumefika mahala ambapo utashi, matakwa na maslahi binafsi yanaweza kutusukuma kuhalalisha utungwaji wa sheria ambayo kamwe hatuihitaji katika karne hii.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Mungu waongoze viongozi wetu katika suala hili la sheria ya uhuru wa habari.
ayubrioba@hotmail.com
mwisho

Wednesday, March 7, 2007

Tambwe Hiza Siasa sio Kubadili Vyama watakucheka

Tambwe siasa sio kuhama vyama ,huo ni mchezo sio siasa

Siasa ni kuvumiliana na kujifunza


Tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uliporejeshwa mwaka 1992 na vyama vingi kuanzishwa hapa nchini, watu wengi walijikuta wakijitumbukiza kwenye vyama hivyo hata kama hawakuwa wanasiasa ili mradi anao uwezo wa kuongea akawavutia wasikilizaji, basi yeye alijihesabu kuwa tayari ni mwanasiasa hata kama hakuwa na taaluma hiyo.

Watu wengi walijikutwa wakiwa wanasiasa hata kama ilikuwa haimlazimu kuwa hivyo ili tu apate nafrasi ya kusikika au kupqatia masilahi ndio maana ,hata kabla ya kutimiza miaka kumi ya kurejea Demokrasia nchi watu namna hiyo ambao wengine wanafahamika kama pandikizi na kanyaboya walianza kurudi walikotokea na kutupa mzigo wa lawama wanakotoka.

Katika watu hao wengine walitoka CCM wakijua hawawezi kupata nafasi kwenye chama hicho kikongwe hasa baada ya Kusheeni wanasiasa wa kila aina ,wasomi, wajanja na wataalamu wa Propaganda ,ikabidi wakimbilie kwenye vyama vya Upinzani wakifikiri kuwa wangeweza kutimiza azima yao mapema.

Miongoni mwao alikuwamo Agoustine Mrema aliyekimbia CCM, dakika za Mwishoni na kuhamia chama cha NCCR-Mageuzi ili kuwahi Ikulu ,Mrema alifikiri kuwa kwa kutumia kambi ya upinzani angeliweza kutimiza haja yake ambayo iulikuwa ni kuingia Ikulu tu, lakini alishindwa kutimiza hiyo haja yake baada ya kushindwa na Mpinzani wake kutoka CCM ,Benjamin Mkapa.

Lakini kutokana kuwa Mrema hakuwa na taaluma ya siasa kufahamu kuwa vitisho,kashifa na matusi hatimaye kifo ni sehemu ya mchezo wa Siasa alijikuta akijenga uadui kutoka kila upande hata wale waliomkaribisha na kule alikotoka ,ndivyo siasa ya Mrema ilivyomalizika akizani kuwa ukiitwa mwanasiasa lazima uwe na cheo! Hatimaye akakihama chama kukwepa mapinduzi ya vijana.

Mrema kuhama chama chama na kukimbilia TLP ilifuatiwa na mlolongo wa wanasiasa kukimbia vyama kurudi CCM kule walikotokea huku wakiacha nyuma mzigo wa lawama kuwa kambi ya upinzani haina lolote imejaa Ubabaishaji , huku wakisahau kuwa hata wanakoelekea ni watu kama waliwaacha huko nyuma, ambao wametulia ndani ya chama bila kulilia madaraka.

Lakini kumbe kambi ya upinzani ilikuja kufahamika kwamba kambi ya upiunzani ni chuo cha kuzalisha wanasiasa ,kama zilivyo timu za mpira wa miguu ndogo kama Moro utd, kutafuta vipaji akionekana anangara kwenye ligi kuu, Timu kubwa za Yanga na Simba zina

FITNA ZA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA KAMA ZILIVYOPIKWA

Fitina za uchaguzi mkuu 2005

Toleo namba 328 la Ijumaa, Januari 6- 12 mwaka 2006, HAJA lilichapisha habari ya yenye kichwa cha habari cha
MBOWE APENDELEA WACHAGA VITI MAALUM CHADEMA
*Apangua maoni ya Kamati Kuu
*Wengi wajiandaa kurejea CCM

Habari hiyo iliandikiwa na Mwandishi Wetu, ilisema
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,amelaumiwa vikali kwa kufanya chama hicho kuwa tawi la wachagga na kupitisha maamuzi ya kuwapa upendeleo wa wazi.

Ufuatiliaji wetu ndani ya shughuli za chama hicho umebaini kuwa asilimia 80 ya wanachama walioteuliwa viti maalum ni kutoka mkoa wa Kilimanjaro tofauti na ilivyopendekezwa na Kamati Kuu.

Wabunge hao wanadaiwa kupenyezwa kwa upendeleo wa ukabila ni Anna Anna Komu, Grace Kiwelu, Khalima Mdee, Lucy Suzana Lyimo ambao wote ni kutoka mkoa wa mwenyekiti Mbowe.

Ili kupoteza lengo, inadaiwa Mbowe alitumbukiza jina la Bi Mhonga Said wa Kigoma kuhalalisha uteuzi huo.

Inadaiwa kuwa mmoja wa walioteuliwa ni motto wa kigogo wa CHADEMA ambaye amepewa fadhila kwa niaba ya baba yake-mfadhili wa CHADEMA.

Kutokana na sakata hilo, kundi la wanawake wanaodaiwa kuhangaikia chama kwa muda mrefu lakini wameachwa bila maelezo wamepanga kuanika hadharani maovu yote ya vigogo wa CHADEMA, ikiwemo ubabe, ufuska, udikteta na ukabila kinyume na jina la chama hicho.

“Sisi majina yetu yamekatwa kwa kuwa sio wachaga na hatuna sura nzuri za urembo lazima wakubwa waonje joto ya jiwe kwa kutufanya ngazi,” alidai mwanamke mmoja kutoka Zanzibar.

Aidha wanadai idara zote nyeti zimeshikwa na watu wa Kilimanjaro hata bila kuwa na ujuzi.

Kigogo mmoja aliyehamia CHADEMA kutoka CUF ndiye anayetuhumiwa kumpotosha Mbowe na kumshinikiza ateue watu wengi wa kabila moja kwa maslahi binafsi.


HOJA la Ijumaa, Machi 10- 16, 2006, katka ukurasa wake wa tano, kwenye Makala ya Siasa liliandika makala yenye kichwa kifuatacho

VIONGOZI WA MIKOA TUPO TAYARI KUINUSURU CHADEMA
*Uteuzi wa viti maalum, wabunge haukueleweka
*Waliochangia helikopta walifidiwa kwa kupewa ubunge viti maalum

Makala hiyo ilipambwa na picha nne, ya Mbowe, Dk. Kaborour, Dk. Slaa na Bob Makani. Makala hiyo ilianza kwa kusema
Mhariri
AMA kweli Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimo kwenye mtihani mzito wa kusambaratika, kutokana na uongozi usiofaa hususan makao makuu.

Mambo yanaendeshwa visivyo, wanachama na viongozi wa mikoa wanadai mkutano mkuu maalum uitishwe au Baraza Kuu ili kumjadili Mwenyekiti wao wa taifa na Katibu Mkuu wake.

Mambo ambayo yanaleta majonzi ni pamoja na viongozi kuendesha chama kama kampuni, baya zaidi ambalo wanachama wana hasira nalo ni pamoja na
(a) Ubaguzi wa ukabila ndani ya vitengo vya makao makuu
(b) Mbowe kutokuwa muwazi kuhusu fedha za kukodi helikopta
(c) Kutoa upendeleo safari za nje ya nchi
(d) Kuteua wabunge viti maalum kutoka mkoa mmoja
(e) Kumsusia Dk. Kabourou kwenye kampeni kule Kigoma
(f) Kutoa upendeleo wa misaada ya kampeni na kubagua wagombea
Haya ni baadhi ya mambo ambayo takribani mikoa 23 inataka maelezo

Viongozi wa mikoa wanalalamika kwamba hawakuona faida ya mgombea wao wa urais (Mbowe) kutumia helkopta kwa sababu alikuwa hawapigii debe wagombea wa udiwani na ubunge ila aliwabagua wagombea kulingana na mahusiano yao. Kuna madai kwamba mwenyekiti alitoa msada kwa wagombea ambao ni rafiki zake wa damu.

Ili kuonyesha ubaguzi wa wagombea walimchangia mgombea ubunge fedha nyingi za kampeni ambazo zilimwezesha kushinda. Chama kimewaangiza wengi kwenye matatizo ya madeni kutokana na maagizo ya makao makuu kwamba kitawakopesha fedha na walete hati zao za nyumba.

Baadhi ya wagombea wanaolalamikiwa kwamba walipewa upendeleo ni pamoja na Erasto Tumbo (Kisesa), Damas Mbogoro (Songea Mjini), Victor Kimesera (Kiteto Manyoni) wakati Bob Makani alipata msaada kidogo sana.

Viongozi wa mikoa wanataka kujua kwanini Mbowe, Slaa, Zitto Kabwe, Shaibu Akwilombe na Grace Kiwelu walishiriki kuhujumu maamuzi ya kamati kuu ambayo tayari ilishateua wabunge wa viti maalum?

SIRI YA HELIKOPTA
Nao wanachama na viongozi wa mikoa mbalimbali wameshitushwa na kitendo cha kufanya mktaba wa siri na kigogo mmoja ambaye alimkopesha sh 50,000,000 kwa makubaliano kwamba motto wa tajiri huyo lazima awe mbunge.

Binti huyo ni motto wa kwanza wa Kigogo wa CHADEMA na makubaliano hayo yametekelezwa ili kumfariji kwa mkopo alioutoa. Lakini yamejitokeza malalamiko zaidi kwamba tajiri huyo mwaka 2000 alipewa nafasi ya upendeleo ambapo mke wa motto wake (MKWE), alipewa ubunge wa viti maalum kwa mizengwe iliyoambatana na takrima.



HOJA, Machi 24 hadi 30 2006, katika ukurasa wa 7. Ilichapisha makala yenye kichwa cha habari kifuatacho
CHADEMA YAFICHA UGONJWA YASHINDWA KUFICHA ‘KIFO’
Kwa muda mrefu, Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) kimekuwa kutokana na chama hich o kuasisiwa na wazee wa mkoa wa Kilimanjaro.

CHADEMA imekuwa inasemwa na kwamba,viongozi wake wa kitaifa hawaheshimu maamuzi ya kikao na kundi la vigogo wa chama hicho kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini hufikia maamuzi mazito ndani ya chama ambayo ni ya kibinafsi.

Mkutano wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA wa hivi karibuni, umekata mzizi wa fitina na kuweka hadharani uozo uliotanda kwenye chama hicho ambao unanuka ufisadi , ukabila, udini na ukanda na viongozi kutoheshimu maamuzi ya vikao vya kikatiba ya chama.

Kamati Kuu ilifikia uamuzi wa kumuwajibisha Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karatu Wilbrod Slaa kwa kuwatuhumu kwamba walitumia madaraka yao vibaya katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mwingine ambaye Kamati Kuu alinusurika kuwajibishwa na Kamati Kuu ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CHADEMA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kigoma Vijijini, Zitto Kabwe ambaye anadaiwa ni kibaraka wa Mwenyekiti Mbowe ambaye alimburuza katika zoezi la kuteua wabunge wa Viti Maalum.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ambaye pia ni mtendaji wa makao makuu ya CHADEMA amefichua kwamba, orodha ya majina ya wabunge wa Viti Maalum ilitayarishwa na kitengo cha wanawake wa chama hicho wakaipeleka Kamati Kuu lakini ikatupw kapuni na Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Wilbrod Slaa wakatengeneza taarifa yao.

Majina ya wabunge wav Viti Maalum hupendekezwa na vikao vya kitengo cha Wanawake wa CHADEMA,


Hoja la Ijumaa, Machi 24-3- 2006
Gazeti namba 336

Lilikuwa na kichwa cha habari cha
MBOWE AHOFIWA KUPINDULIWA NA DK. AMAAN KABOUROU
*Mikoa 23 yataka ang’olewe
*Dk. Slaa naye yupo matatani
*Watendaji makao makuu wagawanyika

WIKI moja tu baada ya kulipotiwa kuwepo kwa mtafaruku wa chini chini ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA unaotaka mwenyekiti wa chama hicho kujihuzulu kutokana na tuhuma za kuendesha chama binafsi.

Imebainika kwamba bado mambo si shwari ndani ya chama hicho kwani sasa Mbowe anamwona makamu wake , Dk .Amani Walid Kabourou kama mwiba unaoweza kumchoma na kumuangamiza kisiasa wakati wowote.

Kuwa kwa namna yoyote ile Mbowe lazima aondolewe katika uongozi wa chama hicho na nafasi yake kukaimiwa na makamu wake Dk. Kabourou.

Wamesema kiongozi huyo amethibitika kuwa na mapungufu makubwa ya kiuongozi ambayo si tu yamesababisha mgawanyiko baina ya viongozi.

Bali pia yamewagawa baadhi ya watendaji wa chama hicho na hata wengine kufikia hatua ya kudharauliwa na kupuuzwa zikiwemo taarifa za mapendekezo yao kuchanwa na kutupwa katika mapipa ya takataka.

Wajumbe hao wamesisitiza kwamba, ingawa hoja yao yakumtaka Mbowe ajiuzulu haikufanikiwa katika kikao kilicho malizika cha kamati kuu,lakina sasa wanajiandaa kuwasilisha mapendekezo mapya katika kikao cha baraza kuu la chama hicho lililopanga kafanya kikao chake mwezi aprilmwaka huu.

“katika kikao hicho lazima tutataka tupate majibu ya kwanini Mbowe na wapambe wake wasijiuzulu wakiwemo wabunge wa viti maalum ambao wameteuliwa bila ridhaa ya vikao halali vya CHADEMA”wameeleza wajumbe hao walioomba majina yao yahifadhiwe.

Wamezidi kubainisha kwamba,hatamapendekezo ya Mbowe na wapambe wake kutaka katiba ya chama hicho ifanyiwe marekebisho kwa kufuta baadhi ya ngazi za uongozi hawatayakubali na kama atathubutu kuwalazimisha basi huo ndio utakuwa mwaanzo wa kifo cha kisiasacha chama hicho.

Katika mabadiliko hayo ya katiba, Mbowe na kundi lake wanataka kamati kuuya CHADEMA ivunjwe na muundo wa utawala makao makuuwanataka ribadilike

Imeelezwa na wajumbe hao kuwa,lengo kuu la Mbowe ni kutaka kuwang’oa wenyeviti na makatibu wote wa mikoa.Hatua hiyo imelengwakuchukuliwa baada ya kubainika kwamba mikoa.23 inatakaMbowe na katibu mkuu wake Dk. Wilbrod Slaa wajihudhulu au wafukuzwe.

Kilichomalizika hivi majuzi hatua iliyo mfanya Mbowe kutoka nje ya kikao kwa muda ili kutafakari hatua hiyo na baadaye kurejea akionekana mwenye jazba.

Dk. Slaa anatuhumiwa kwa kutowajibika na kufikia hatua ya kukasimu madaraka yake kwa watendaji ambao kikatiba na kiprotokali hawakustahili kukabidhiwa madarakahayo.

“pamoja na kwamba makao makuu wapo watendaji ambao wameajiriwa na kulipwa mishahara.Lakini Dk. Slaa hawapi kazi.Anapoondoka ofisini anatakiwa kukamilisha majukumu yake kwa Naibu wake Bw.Shaibu Akwilombe lakini ajabu ni kwamba anayekaimu nafasi ya Slaa ni John Mnyika ambae ni mkurugenzi wa vijana”wameeleza wajumbe hao na kuendelea :

“Mbaya zaidi kuna katibu mtendaji, Bw.Victor Kimesera,yeye sasa amefanywa kama tairi la akiba hata makabrashaanayoandika huwa yanachanwa na kutupwa katika pipa la takataka.Wengine waliotengwa na Slaa ni Mtemelwa na Shija”

waajumbe hao wanao taka mikoa ya Lindi ,Mtwara,Kigoma, Shinyanga,Iringa na Zanzibar wamesisitiza kwamba mambo ya ndani ya chama hicho sio shwari kwani hata Dk.Kabourou hana maelewano ya dhati na Mbowe na kundi lake lote linalomuunga mkono.

Hivyo ,wameapa kwamba mapinduzi lazima yafanyike na Dk.Kabourou kukalia kiti cha uongoziwa chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwang’oa baadhi ya watendaji akiwemo mbunge wa Kigoma kaskazini,Bw.Zitto Kabwe anayeelezwa kuwa spika ya Mbowe na uteuzi wa wabunge wa viti maalum utenguliwe na Mbowe katu asithubutu kuwania tena urais kwa tiketi ya chama hicho 2010.

“Yote haya yataibuka katika kikao cha mwezi April.Tutataka misaada ya chamacha Conservative cha Uingereza ambayo imefanywa siri ibainike wazi ikiwa ni pamoja na kuunda kamati ya kuchunguza fedha zilizotolewa na wafadhili mbalimbali wa chama hiki,michango ambayo haifahamiki,”wameeleza wajumbe hao.

Aidha wanataka Mbowe atoe maelezo ya magari sita ,matano yakiwa ni Suzuki Escudo na moja Toyota Hiace linalodaiwa kuwa linatumika katika biashara binafsi ya Mbowe.

Ijumaa, Januari 20- 26
Makala ya Siasa ukuruasa wa 5
Kichwa cha Habari: HARUFU YA UKABILA YATISHIA HATMA YA CHADEMA
Makala hiyo imeandikwa na mwandishi Juvenalis Lesia

UPO msemo wa waswahili unaosema kwamba “Mvuta kamba huvutia kwake. Msemo huo na mingine una maana kubwa sana katika mazingira na Tamaduni hususan Waafrika.


Kumbukumbu zinaonyesha kwamba CHADEMA iliasisiwa mwaka 1993 na Mzee Edwin Mtei ambaye aliwahi kuwa Gavana waBenki Kuu ya Tanzania (BoT) na Waziri wa Fedha katika seriakli ya awamu ya Kwanza.

Wazee wa Mkoa wa Kilimanjaro walioshiriki kuasisi CHADEMA wapo wengi na miongoni mwao ni Mbunge wa sasa wa jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya chama hicho Bw. Philemon Ndesamburo.

Uteuzi wa Lucy Owenya ambaye ni binti wa Freeman Mbowe aliyegombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu CHADEMA limezua lawama na mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho ambacho kimeshika nafasi ya tatu kwa kupata kura nyingi za urais wa viti vya ubunge.

Baadhi ya mashabiki wa CHADEMA wanadai kwamba mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliopita uliendeshwa kwa mizengwe ndiyo maana jina la Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Profesa Mwesiga Baregu likatupwa kapuni.

Wanadai walipachikwa watu wa kuchuana na Mwenyekiti Mbowe ambao hawana ubavu wakisiasa na siku ya uchaguzi waliondoa majina yao wote ili Mbowe asipate mpinzani katika kinyang’anyiro cha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.

Wafurukutwa wa CHADEMA wanaendelea kudai kuwa Bi Chiku Abwao na wenzake waliojiunga kwenye chama hicho wakitokea NCCR-Mageuzi ambako walivurunda , wamepewa madaraka makubwa na ndiyo maana jina na Bi Chiku lilikuwa miongoni mwa majina yaliyopelekwa NEC ateuliwe kuwa mbunge wa viti maalum.

Mashabiki wengine wa kisiasa wanamtuhumu mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Mbowe kwa kutowapa msaada wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliopita na kwamba fedha za chama hicho alizitumia kukodisha helkopta aliyokuwa anaitumnia kwaenye kampeni za kusaka urais.

Kwa upande wa uteuzi wa wabunge wa viti maalum, hali siyo shwari kwani kuana madai kwamba wanachama walioteuliwa ni kutoka Mkoa wa Kilimanjaro tofauti na mapendekexzo ya kmati kuu.

Wabunge hao wanadaiwa kupenyezwa kwa upendeleo wa ukabila fadhila baadhi ya vigogo ambao ni wafadhili wa chama hicho.

Kutokana na sakata hilo, kundi la wanawake kuitokea jasho CHADEMA Kwa muda mrefu lakini wameachwa ,wameamua kuanika hadharani maovu ya vigogo wa chama ambao wanashutumiwa kuwa madikteta.

Ijumaa, Machi 17-23, 2006
Toleo namba 335, ukurasa wa kwanza

Kichwa cha habari:

Wakata CHADEMA inakutana Dar
MBOWE ASOMEWA RASMI MASHTAKA 15
*Adaiwa kuhamisha Ofisi Kuu Billicanas
*Wazanzibari walinyimwa Viti Maalum
*Yadaiwa alinyanyapaa wagombea ubunge
*Mikoa yasutwa kwa kumkosoa waziwazi

Na Mwandishi Wetu
IDADI kubwa ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wiki hii walichachamaa na kutaka Mwenyekiti wao, Bw. Freeman Mbowe asimamishwe uongozi ili kujibu mashataka 15 yanayomkabili katika uongozi wake.

Habari zilizonaswa kutoka ndani ya kikao hicho kilichoanza wiki hii kwenye Hoteli ya Land Mark Dar es Salaam, zilieleza kwamba wajumbe wamechukizwa na tabia ya Bw. Mbowe kuburuza chama badala ya kutekeleza maagizo ya Kamati kutokana na ubabe huo wajumbe waliona njia sahihi ya kunusuru chama na kurejesha hadhi mahali pake, waliunda mshikamano kwa kuorodhesha tuhuma zipatazo 15 na kumeweka ktimoto aandae majibu bila kubabaisha.

Baadhi ya mashitaka hayo ambayo yaliwasisimua wajumbe yalipowekwa ubaoni ni Bw. Mbowe kupangua majina ya wabunge 6 wa viti maalum waliopendekezwa na waasisi wa CHADEMA.

Waasisi hao walipendekeza wanachama wafurukutwa ndio wateuliwe kujaza nafasi hizo lakini bila sababu za msingi wala ridhaa rasni. Wapambe wengine walikutana kwenye hoteli ya Bilcanas na kupitisha majina mengine.

Aidha uteuzi huo uligusa wajumbe wa Zanzibar ambao wamedai katika shitaka la pili kwamba hakuna mwanachama wa CHADEMA aliyeteuliwa viti hivyo maalum kutoka upande wa Zanzibar ingawa sheria ya vyama vya Siasa inasisitiza uwakilishi kutoka pande mbilo za muungano.

“Uongozi gani huu wa kutufanya Wazanzibari ni busati la kupangusia viatu kutakatishia nyumba kheri tugawane ambao kama mwenyekiti hawezi kuondoka,”alifoka mjumbe mmoja.

Nalo suala la Bwana Mbowe kukodi helikopta lilizua malumbano na kumtaka asitafune maneno.kati ya wagombea ubunge 30 waliokuwa tishio mikoani,hakuna aliyepata msaada wa Bw,Mbowe (kama mwenyekiti) isipokuwa wateule wachache (majina tunayo) wa kambi yake.

Nukta hiyo imekolezwa na tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wa Makao Makuu walifunga ofisi na kuandaa tafrija nzito katika ukumbi wa Rose Garden,Mikocheni Dar es Salaam kushangilia mwereka aliopigwa Makamu mwenyekiti wao Dk, Aman Walid Kaborou katika kugombea ubunge Kigoma Mjini Uchaguzi uliopita bali aeleze kwa maandishi ni kikao gani kilimpa idhini ya kukodi Helkopta kutoka Kenya na kutimulia vumbi Wananchi?

Hasira ziliongezeka na kutaka maelezo kutaka kuhusu amri inayodaiwa kutolewa na bwana Mbowe kwamba ruzzuku inayopokewa kila mwezi kutoka Serikalini megwe kwa asilimia kubwa kumpa huyo aliyegombea Urais (akabwagwa) ili kurejesha fedha alizotumia kuzunguka nchi nzima.

Tuhuma nyingine iliyotawala kikao ni madai ya uhakika kwamba bwana Mbowe alitokwa jasho jembamba liliposomwa shitaka jingine kwamba anadaiwa kutoa shilingi milioni 5 tasilimu kwa mmoja wa wanachama wengine ambao wanahangaika kukopa pesa za kuendesha kesi kama huyo aliyependelewa.

Kuhusu ubadhilifu na kutuma vibaya madaraka,ilidaiwa kuwa kiongozi Fulani aliyetoka CUF na kutafuta hifadhi ndani CHADEMA ametafuna shilingi milioni 9 za chama, lakini hakuna anayethubutu kumtikisa anadai ni mshauri anayeelewana na Bw,Mbowe.

Shitaka la kuvunja hadhi ya ofisi lilisisimua masikio ya wajumbe ilipodaiwa kuwa kuna warembo watatu (majina tunayo) wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro lakini wanahangaikia maisha chuo kikuu wamepewa nafasi za maana makao makuu ya chama bila ya kupewa idhini ya kamati kuu na wanatamba kwa kutumia magari. Compyuta na vifaa vilivyopo kuliko watendaj wakuu.

Gumzo la kuhamisha shughuli za ofisi Bilicanas liliwashawishi wajumbe kutaka maelezo rasmi hususani mbunge wa Kigoma Kaskazini Bwa, Zito Kabwe kuhamisha hata mafaili na nyaraka kwa maelezo ya Bw, Mbowe na anajitangaza kuwa ndiye Kiongozi wa Sekretarieti iliyoweka kambi hoterini humo, badala ya Kinondoni.

Mmoja wa Waasisi Bw,Bob Nyakanga Makani alionyesha busara na hekima wakati mashitaka hayo yakisomwa kuelekezwa kwa mrithi ake,na kufanya amuonee huruma jinsi mpangilio wa hoja ulivyowekwa.

Inadaiwa Bw, Mbowe amekuwa akikwepa kuidhinisha sherehe za kumuaga rasmi mwenyekiti huyo mstaafu Bw,Makani, kama chama kilivyowahi kufanya kwa mtangulizi wake Bwana Edwin Mtei.

Baadhi ya wajumbe walitishia kujitoa chama hicho kwa vile inaonekana kuwa ni chama cha Wachaga na ndio wanathaminiwa kuliko wote lakini Bw, Makni ambaye ni Msukuma hana thamani tena, na Mbowe mwenyewe hujifanya ana majukumu mengi kila akikumbukwa na wakubwa wenzie.

Katika sherehe za kumuaga Bw, Mtei anaelezwa Mheshimiwa Mbowe alichangia shlingi nusu Milioni taslimu loakini akikumbushwa la mzee Makani huibua wimbo wa hali ngumu.

Katibu Mkuu Bwana Willboard Slaa,amerushiwa tuhuma kwamba ni mwanachama mtiifu wa CCM tangu 1993 na ndio maana hajawahi kuchangia shughuli za CHADEMA kwenye hafla yeyote ingawa ana mapesa ya kutosha.

Naye bwana Victor Kimesera ambaye ndiye mtendaji wa Mako Makuu ameporwa madaraka na Mh, Kabwe,kiasi cha kubakia kusoma magazeti kutwa nzima wakati kazi zake zinafanyiwa jengo la Bilicanas linalomilikiwa na Bw, Mbowe.

Bw,Mbowe ameshutumiwa pia kwa kuandaa mabadiliko ya kuvunja ofisi za mkoa na badala yake kutaka wilaya ndizo zipewe nguvu chini ya mako makuu.

Mjumbe aliyedaiwa maelezo kuhusu hilo alichachamaa kwamba mwenyekiti anaamini kwamba mikoa mingi haina imani naye hivyo dawa ni kufuta mawasiliano na makao makuu ya mikoani.

Mjumbe aliyedai maelezo kuhusu hilo alichachamaa kwamba mwenyekiti anaamini kwamba mikoa mingi haina imani naye hivyo dawa ni kufuta mawasiliano na ofisi za mikoa ili wenyeviti jeuri waanze kubangaiza mitaani au kujibanza wilayani.

Mjadala huo wa vigogo kubinafsisha chama bila kufuata vikao halali wala nidhamu,wajumbe wengi walipendekeza mwenyekiti Mbowe na katibu Mkuu Bwana Slaa wakae pembeni ili maovu zaidi yachimbwe.

Washauri Makamu Mwenyekiti Bwana Kabourou ashikilie milingoti ya CHADEMA ama sivyo wajumbe wakirudi mikoani wataanzisha mawasiliano ya kupitia viongoz ili kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa kutimua kundi linalovuruga ustawi a chama na kunufaisha wachache.

Kikao hicho ambacho kilipangwa kuwa cha siku moja kiliendelea bila ukomo kutokana na hoja nzito kuibuliwa huku wajumbe wakipenyezeana vikaratasi chini kwa chini,na wengine kuwasiliana kwa meseji za simu ndani ya ukumbi.


HOJA, Ijumaa, Februari 25- Machi 3 mwaka 2005
Makala ya Siasa
Kichwa cha Habari: SAUTI YA UMMA WAPANIA KUGAWANA WANACHAMA NA CHADEMA
Na Mwandishi Wetu
JASHO la mtu haliliwi. Kazi kubwa iliyopo mbele yetu sisi viongozi wa kitaifa wa Sauti ya Umma (SAU) ni kugawana mtaji (Wanachama) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho tumekitumikia kwa muda mrefu, hivyo tayari tumekamilisha mipango ya kusimamisha wagombea ubunge na madiwani katika majimbo yote yanayoongozwa na CHADEMA ambayo ni Kigoma Mjini, Karatu, Arusha na Hai mkoani Kilimanjaro.

Aya iliyotangulia hapo juu ni kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa SAU, Paul Kyara na Katibu Mkuu wake, Jacob Nkomola katika mahojiano na HOJA juzi ambapo walizungumzia mikakati mbalimbali ya chama hicho.

“Tulikuwa watendaji ndani ya CHADEMA, tunafahamu uwezo na udhaifu wa viongozi wake wakuu, hivyo CHADEMA ihakikishe kwamba inapata upinzani mkubwa kutoka chama cha SAU kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani tumepania kuchukua jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ambalo linaongozwa na Freeman Mbowe, Kigoma Mjini la Dk. Amaan Kabourou na lile la Karatu linaloongozwa na Dk. Wilbroad Slaa,” Wamejigamba viongozi hao.

Nkomola maarufu kwa jina la Kaka Kuona, amemchambua Mbowe na kudai kwamba hana uwezo mkubwa wa kisiasa kwani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, alibwagwa jimboni Hai na mgombea wa Chama cha NCCR-Mageuzi, jambo ambalo lilimfanya akate tamaa na kususa kabisa shughuli za chama hicho hadi alipoibuka tena mwaka 2000 na kufanikiwa kunyakua wadhifa wa ubunge katika jimbo hilo baada ya vigogo wa CHADEMA kufanya kazi ya ziada.

Anasema alivyobwagwa na NCCR-Mageuzi kwenye jimbo la Hai mwaka 1995, alikuwa amepanga kujiunga na CCM mwaka 2000 ili afanikiwe kunyakua wadhifa wa ubunge katika jimbo hilo, lakini ilimwia vigumu kwani alikwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CHADEMA na kwamba angekuwa amemuasi Baba Mkwe wake, Edwin Mtei ambaye ndiye muasisi wa CHADEMA.

“Mkutano mkuu wa uchaguzi wa CHADEMA uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu ambao ulimweka madarakani Freeman Mbowe, ulijaa mizengwe kwani mbunge wa jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philimon Ndesamburo ndiye aliyetegemewa kuwa Mwenyekiti wa chama kutokana na hekima na busara zake kwani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 alibwagwa kwenye jimbo lake na mgombea wa NCCR-Mageuzi, lakini hakukata tamaa ya kujishughulisha na shughuli za CHADEMA kama alivyofanya Mbowe ambaye aliibuka tena kwenye shughuli za chama baada ya kupata ubunge wa jimbo la Hai mwaka 2000,” alisema Nkomola.



HOJA, Ijumaa Februali18 -24 -2005

Habari za Kitaifa, ukurasa wa 3

Kichwa cha habari

Maandamano yapangwa kutimua watendaji CHADEMA

*Yadaiwa wanahujumu sera za Chama
*Fedha za ruzuku zaishia Kanda ya Kaskazini
*Vyombo vya misaada ya Wazungu vyakodishwa


Na mwandishi wetu

MIVUTANO ya ndani inaendelea kufukuta ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo safari hii wanachama 600 wameandaliwa kuandamana hadi makao Makuu YA Chama hicho jijini kuwatimua watendaji wote wa kuajiriwa na chama hicho imethibitika.

Habari za uhakuka kutoka katika kikao cha maandalizi hayo zimebainisha kuwa,wanachama hao watakaoandamana watatoka katika wilaya ya Kinondoni,Ilala na Temeke, mkoaniDar es Salaam na mikoa ya jirani hasa ya Pwani.

Inaelezwa kuwa waandamanaji hao watakwenda Makao Makuu ya chama hicho Mtaa wa Ufipa Kinondoni wakiwa na mabango na watashinikiza watendaji waliowekwa kwenye ofisi hiyo,Mbowe na Katibu Mkuu Dk,Slaa waondoke

Maofisa wanaomulikwa ili watimuliwe kutoka maofisini mwao bila simile ni pamoja na Bw, Shaibu Akwilombe,Antony Komu,Msafiri Abdurahman Mtetemelwa, Sofia Kiwangwa na ndugu Shija.

Imebainika kwamba wanachama hao wakifanikiwa kuwaondoa watendaji hao baadae wataungana na wajumbe wa Baraza kuu la CHADEMA Kushinikiza mapinduzi yatakayowang’oa Mbowe na Slaa katika nyazfa zao.

“nina hakika tutafanikiwa kwani kamati Kuu ya CHADEMA Tayari imeshapasuka na hivi sasa Mwenyekiti (Mbowe) amebak anaungwa mkono na wajumbe watatu tu,”ameeleza mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya CHADEMA aliyeomba jina lake lisitajwe lihifadhiwe.

Mjumbe huyo amesema chama hicho sasa hivi kimekuwa kikiendeshwa kikanda,hivyo wanataka wawang’oe Mbowe na Slaa ili kufutilia mbali mazingira hayo machafu ndani ya CHADEMA.

CHADEMA imekuwa na mivutano ya ndani kwa ndani ya kiongozi na habari za uhakika zinasema Mwenyekiti,Bw, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu,Dk,Wilbord Slaa hawana maelewano na Makamu Mwnyekiti Dk, Kaborou.

Mambo mabaya yanayosukuma wanachama hao kumshikia bango Mh,Mbowe ,Dk,Slaa na wapiga debe wao kukataa kumuaga rasmi Mwenyekiti mstaafu Bw,Bob Nyakanga Makani tofauti na ilivyoenziwa mtangulizi wake Bw, Edwin Mtei.

Inaelezwa kwamba fikra ya kuandaa hafla ya kumuaga Bob Makani inaleta zogo ndani ya CHADEMA akielezwa kuwa Msukuma hawezi kutukuzwa kiasi hicho ndani ya CHADEMA hata kama aliitendea wema kila mtu.

Pia wafurukutwa wanadai kuwa fedha za ruzuku zinaelekezwa jimbo la Hai na mikoa mingine watendaji wanakosa hati kodi ya pango.

Kuhusu majungu wanachama hao wanadai majungu imekuwa ni kama uji na mgonjwa hayabanduki ofisini kiasi cha kuathiri nidhamu na usikivu unaostahili tofauti na enzi za bw, Makani.

Kuhusu ubadhilifu na hujuma, wanachama hao ambao wana mtandao mkubwa wa mawasiliano wanasdai kwamba vyombo vya kutumia kwenye mikutano vilivyotolewa kwa Chadema na Chama cha Conservative cha Uingereza vimegeuzwa mali ya watu binafsi,kuvigusa sawa na kuchezea umeme.

Wanadai hakuna ofisa yeyote wa CHADEMA anayeruhusiwa kutumia vyombo hivyo kikazi mpaka aweke dahamana ya nyumba au shamba ndipo agues kipaza sauti.

Mmoja wa wajumbe hao kutoka Mtwara alilalamika kudhalilishwa kwa kuambiwa
“kama huna dhamana ya nyumba au shamba nenda kapande juu ya mkorosho utangaze sera za chama maana Wazugu watauliza vikiaribika.”.


Hoja Oktoba 14-20 mwaka 2004 Toleo namba 317
Katika ukurasa wa kwanza liliandika habari yenye kichwa cha habari cha
VIONGOZI SAU WAMSHAMBULIA MBOWE, MREMA
*Ni kwa kutumia helkopta katika kampeni
Na Juvenalis Lesia
CHAMA cha Sauti ya UMMA (SAU), kimemponda mgombea urais wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kutumia mamilioni ya fedha kukodi helkopta kwa ajili ya kampeni za kuisaka Ikulu na kuwataka watanzania wajihadhari na mgombea huyo.

Tahadhali hiyo ilitolewa na mgombea urais wa chama hicho,Paul Kyara katika mahojaino yake na HOJA, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema kiongozi mzuri huchaguliwa kwa haiba na sera na siyo kwa mabavu kama navyotamba Mbowe na CHADEMA, anayetumia helkopta katika mikutano yake ya kampeni kuwavuta walalahoi.

Alisema kama watanzania watabweteka na kumchangua Mbowe wa CHADEMA kwa ajili ya mbwembwe zake za kutumia helkopta au Mrema kwa kupanda farasi wakati wa kuchukua na kurejesha fomu tume ya uchaguzi, wajue wana deni la kulipa fadhila ambalo CHADEMA na TLP wanadaiwa na wafadhili.

HOJA la Ijumaa, Novemba 4-10 mwaka 2005, toleo namba 319, uk 1
Kicha cha Habari: MBOWE KUHOJIWA KUHUSU HELKOPTA
*Vigogo CHADEMA wasema ang’oke
Na Mwandishi Wetu
MCHAKATO wa kumpata mgombea Mwenza ndani ya CHADEMA, huenda ukaingia dosari baada ya baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho kushinikiza ziwepo agenda za mbili badala ya moja katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Habari za ndani ya chama hicho zinasema wajumbe wa mkutano huo wanataka agenda ziongezwe kutoka moja ambayo ni ya kumteua mgombea mwenza iwepo nyingine ya kumjadili mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na matumizi ya fedha za wafadhili zilizotolewa kwa ajili ya kuwasadia wagombea wa ubunge na udiwani.

Wajumbe wa mkutano huo wanataka waelezwe sababu za Mbowe kuamua kutumia kiasi cha karibu shilingi milioni 300 kukodi helkopta wakati wagombea wa ubunge katika majimbo na madiwani kwenye kata wakihaha kwa kukosa fedha.

Mbowe anadaiwa pia kuwapatia fedha kwa upendeleo baadhi ya wagombea wa majimbo 10 majina tunayo, lakini wagombea wengine imeelezwa wamekuwa wakitaabika kwa kufanya kampeni katika mazingira magumu licha ya Mbowe kuzuru katika majimbo hayo kwa kutumia helkopta, hakuweza kupata muda wa kuongea na kujua matatizo wanayokabiliana nayo katika kampeni zao.

Wajumbe hao wanataka, kama itathibitika kuwa Mbowe ametumia udikteta kuhodhi fedha hizo na kuwanyima wagombea wake kwenye majimbo, ajiuzuru nafasi ya Uenyekiti mara moja.

HOJA la Ijumaa, Februari 18-24 mwaka 2005
Makala ya Siasa, pg 5
CHAMA CHA SAUTI YA UMMA KUPANGUA KARATA ZA CHADEMA
KATIKA mikutano kadhaa na waandishi wa habari, ilielezwa kwamba matarajio ya mkutano mkuu wa taifa wa CHADEMA uliofanyika mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu ilikuwa ni kumchagua Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya chama hicho Philemon Ndesamburo kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho na siyo Free Man Mbowe ambaye ni Mbunge chama hicho jimboni Hai Mkoani Kilimanjaro.

Yalikuwepo madai kwamba wiki mbili kabla ya mkutano Mkuu huo baadhi ya vigogo wa chama hicho walikutana kwenye kijiji Fulani jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro kumtangaza Free Man Mbowe kuwa mdiye mgombea pekee wa wadhifa wa uenyekiti jambo ambalo linadaiwa lilizua kutokuelewana na kusababisha chama hicho kumeguka.

Wa chama hicho walikuwa wamegawana vyeo vya juu ndani ya chama hicho bila kusubiri kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba.

Walidai kuwa CHADEMA imepoteza mwelekeo, sifa na heshima kutokana na kiongozi kuendesha chama kama kampuni yake binafsi huku akiahidi kuendesha siasa za ubabe na umwamba.kuwatukana viongozi wa kitaifa wananchi na kwamba tangu Mbowe aliposhika wadhifa huo, chama hicho kimegubikwa na wageni wanaodharau viongozi na wanachama kiasi cha kuingilia hata uendeshaji wa chama.

Jacob Nkomola alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akilalama kamba siasa ndani ya chama hicho kilichoasisiwa na Edwin Mtei mwaka 1993 ambaye pia ni baba mkwe wa Freeman Mbowe imenunuliwa na matajiri wanaotaka kuabudiwa kama miungu kutokana na fedha zao na kwamba Mwenyekiti aliyeng’atuka madarakani Bob Makani alivumilia mengi kwani alikuwa anadharauliwa kwa kiwangocha hali ya juu na matajiri ndani ya CHADEMA ambao hakuwataja.

Mbowe ndiye aliyetumia ubabe na kushinikiza kamati kuu kumwondoa kwenye wadhifa wake aliyekuwa Katibu Mkuu kwenye uongozi uliopita Mbunge wa Kigoma Mjini D.k Aman Walid Kabourou na kupendekeza nafasi hiyo akaimu Victor Kimesera alizidi kufichua Nkomola.

Aidha ilidaiwa kwamba haukupita muda Mbowe akaibuka na hoja nyingine kwenye mkutano wa kamati kuu uliofuata kwamba Kimesera naye hafai na kutaka wadhifa huo akaimu Dk. Wilbrod Slaa ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho wakati huo na Mbunge wa jimbo la Karatu Mkoani Manyara.



HOJA, Ijumaa, Desemba 2-8 2005
Ukurasa wa 5
Makala ya Siasa

SAU yafichua siri za Freeman Mbowe

*Ni mgombea urais wa CCM ‘B’ kwa gharama za CHADEMA
*Jukumu lake ni kuibomoa CUF, TLP na NCCR
*Bingwa wa kuhubiri ukabila, udini na majimbo

Na Jacob Nkomola
CHAMA cha Sauti ya Umma (SAU), tumesikitishwa sana na tabia chafu ya Mbowe, mgombea urais wa CHADEMA, kwa kauli anazozitoa mara kwa mara kwa kuwadharau wagombea pamoja na vyama vyao eti ni vidogo na havifai.

Mbowe katika hotuba yake ya kampeni aliyoitoa mjini Iringa, katika viwanja vya Mbwembetogwa, alisema yeye ana uwezo wa kufanya kampeni hata miaka mitano ijayo mpaka kieleweke. Pia alidai kuwa wagombea wenzake wamechemsha , eti yeye ndiye tajiri anayeweza kukodi ndege hata miaka mitano. Je, kweli kwa kauli kama hizi, Mbowe anafaa kuwa Rais wa Tanzania?

Sisi tunafahamu kuwa Mbowe anafaa kuwa Rais wa Marekani au Uingereza kwani huko wanatakiwa matajiri.

Kama Mbowe anapesa nyingi kuliko CCM, je, anaweza kuwaambia hata wana CHADEMA wenzake kwamba utajiri na mapesa anayotamba nayo, kayapata wapi?

Mbowe kama ana uwezo wa kuendesha kampeni hata kwa miaka mitano ijayo, je, Mbona utajiri huo hajawapa wagombea wenzake wa CHADEMA wa Ubunge na udiwani ambao wako hoi bin taabani?

Mbowe aache kelele za disco la Billicanas, hazina maana kwa watanzania kwani wanahitaji maendeleo sio disco analoliendesha Billicanas, Cassino ambako watoto wa watanzania wanaharibikia kimaandili.

Mbowe ungekuwa unaitakia mema nchi hii dhidi ya utajiri wako, watanzania wangekupeleka Ikulu kama ungejenga hospitali, shule, visima, kupiga vita UKIMWI kwa vitendo, ungejenga barabara .nk. Hizo mbwembwe zako za ujana na Ikulu utaisikia kwenye vyombo vya habari tu.

Mbowe sisi tunafahamu kwamba wewe, hupambani na CCM, acha kudang’anya . Wewe ni bomu dhidi ya upinzani ambaye umepania kuua upinzani na hasa CUF.

Mikakati yako ya kuibomoa CUF ilianza muda mrefu sana na ndio maana uling’ang’ania kumchukua Shaibu Akwilombe aliyekuwa CUF ili atoe siri za CUF na CHADEMA iiteke Dar es Salaam na ulishindwa.

Mbowe ni adui mkubwa wa upinzani, wewe ulizunguka mikoa yote ya Tanzania, kuwarubuni viongozi na wanachama wa vyama vya CUF, TLP, NCCR-Mageuzi, UDP eti wajitoe kwenye vyama vyao na wajiunge na CHADEMA. Je wewe ni mpinzani?

Sisi tunajue wewe Mbowe ni CCM ‘B’ ndiye uliyesababisha vyama vya upinzani vishindwe kushirikiana.

Mbowe hata hizo fedha unazolipia helkopta, ni fedha unazopewa ili kuumaliza upinzani. Wewe mchana ni CHADEMA usiku Mbowe ni CCM damu.

Tena wana CHADEMA wangejua wewe una wasaliti, wangekufukuza uenyekiti mara moja.Hat hivyo sasa wenzako wamekushtukia na wanakususubiri uchaguzi uishe ili wakutimue kwenye chama.

Mbowe ubabe wako wa kusemsema ovyo mwisho wake ni Desemba 2005.Baada ya hapo utalijua jiji la Makamba.

Tunawaomba Watanzania msichague mgombea eti kwa vile ni tajiri ana helikopta.Kiongozi bora hana makeke,majivuno,kutaka sifa na jazba.

Kumchagua Mbowe atatulete mfumo wa utawala ambao utapeleka nchi yetu kugawanyika kikabila,kidini nk.

Sera ya Mbowe y majimbo ni ushahidi tosha kwamba Mbowe ni mbaguzi kama Kaburu na ni mtu wa kumwogopa kama homa ya mafua ya ndege.Msimpe kura hafai kuwa hata katibu kata.

Mbowe wagombea wenzako wananadi sera na ilani ya uchaguzi za vyama vyao,wewe unanadi nini?Tunachokiona kwake ni magwanda anayovaa na helikopta yako,ndio maana watu wengi wanamiminika kushangaa magwanda anayovaa na helikopta yako ndio maana watu wengi wanamiminika kushangaa magwanda yako na helikopta kwa maana hawaamini mgombea urais.

Mtanzania mwenye maadili mema anaweza kuruka angani na wapiga kura wanakanyaga miba na nawe umati unafuata sio kwamba qwatakupigia kura ila hawaamini kwamba wewe una uchungu na nci hii ila wanakuona kama mcheza shoo wa Twanga pepeta au unaonyesha promotion Mr. Mbowe and Conpany.

Mbowe utaambulia kura chache na wabunge wachacha na madiwani wachache na utapata ruzuku kidogo na hii ndio dhamira yako. Kama ungetaka kwenda Ikulu, utajiri wako ungewawezesha wagombea wako wa ubunge na madiwani. Pole sana Mbowe siasa wewe bado.

Mbowe ni mtu mpenda sifa, anapenda asifiwe kama Yesu Kristo au Mtume Muhamad, akiingia Ikulu, atateua siku maalum ya kumwabudu yeye Mbowe kama mfalme.

Mbowe mara kwa mara anapenda kuishambulia serikali kwamba ilinunua ndege kwa gharama kubwa, yeye mbona anatumia fedha nyingi kukodi helkopta? Je huyo mtu anachoongea majukwaani anakielewa?

Mbowe ananishangaza sana. Mimi Nkomola ndiye niliyemfundisha siasa, lakini namshangaa sana amesahau elimu yote niliyompa ya kujenga hoja kwa vielelezo.

Mbowe nilimfundisha kutaala jukwaa kwa kutumia nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu. Sasa Mbowe hana sera, wananchi hawamwelewi anataka kuwafanyia nini?

Mbowe, mimi Nkomola nipo tayari kukufundisha tena upya namna ya kujenga hoja ili angalau ubaki mwenyekiti wa CHADEMA mwenye busara na hekima.

Watanzania chagueni Sauti ya Umma (SAU),CHADEMA ni CCM ‘B’ kupitia kwa Mbowe
Jacob Nkomola
Katibu Mkuu SAU
Dar es Salaam.

HOJA, Ijumaa, April 15-21, 2005.
Ukurasa wa kwanza Na. 296.

MBOWE ‘AMZUIA’ PROF. BAREGU KUCHUKUA FOMU YA URAIS CHADEMA.

*Shughuli yaahirishwa kimya kimya.

Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe, amehairisha hafla ya kumkabidhisha fomu mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho ambyo ilipangwa kufanyika juzi bila kutoa sababu kwa wageni na waandishi wa habari waliokuwa wamealikwa katika hafla hiyo.Mgombea aliyekuwa amejiandaa kuchukua fomu ni mhadhili wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu.

Haikuweza kufahamika mar moja ni kwanini Mbowe amehairisha hafla hiyo ya kumkabidhisha Prof. Baregu fomu ambayo ilikuwa imegongana wakati mmoja na nyingine ya NCCR-Mageuzi ambao walikuwa wanamkabidhi fomu majira ya saa tano mchana Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Edmund Adrian Sengondo Mvungi katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi mtaa wa Kilosa Ilala Jijini Dar es Salaam.

Freeman Mbowe ambaye kwa muda mrefu ambaye alikuwa anapima ‘upepo’ wa kisiasa unavyovuma ili aweze kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea wadhifa wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, tayari ameshachukua fomu kwa ajili ya kutetea kiti chake cha ubunge jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.


HOJA, Ijumaa, februri 25-Machi 3, 2005
Ukurasa wa kwanza Na. 290

MBOWE ATAKIWA KUIVUNJA CHADEMA

Na Mwandishi Wetu.
Chama cha Sauti ya Umma (SAU), kimemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuvunja chama chake kwanza kama mfano ili vyama vingine viigekwa lengo la kuwa na chama kimoja cha upinzani kitakachochuana na CCM katika uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu.

Mwenyekiti wa chama hicho, mwenyekiti wa chama hicho, Kyara na Katibu Mkuu wake, Jacob Nkomola wameliambia Hoja juzi katika mhojiano juzi kwamba kauli ya Mbowe ya kuwaambia wapinzani wavunje vyama na kuunganisha inaonyesha jinsi kiongozi huyo alivyo mchyanga katika siasa kwani Sheria za nchi haziruhusu Muungano kama huo na muda uliobakia kufikia uchaguzi Mkuu ni mdogo.

Kyara na Nkomola wamezidi kusema kwamba propaganda ambazo zimekuwa zinaenezwa na viongozi wa CHADEMA kwamba wanasubili viongozi wa safi watakaofanyiwa mizengwe wakati wa mchujo wa mgombea urais katika chama tawala wajiunge na CHADEMA ni za ‘kitoto’ kwani hakuna kiongozi ndani ya CCM anayeweza kutoka kwenye chama hicho akaenda upinzani mwenye uwezo wa kutwaa madaraka ya kuongoza dola katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Viongozi hao wa Sauti ya Umma wamebainisha kwamba Mbowe anayumba kisiasa katika chama chake ndiyo maana anatoa kauli hadharani ambazo hajazifanyia utafiti ambazo kama vyama vya upinzani havitakuwa makini vitawagonganisha mashabiki na wafurukutwa wao kwani wataamioni ubinafsi na unafiki ndani ya vyama hivyo ndiyo unaokwamisha vyama hivyo kuungana na kuing’oa CCM madarakani.



Falsafa ya mgombea Urais na magwanda ya ‘Kijeshi’
Ijumaa,Oktoba 7-13,2005

Na Juvenalis Lesia

WAHENGA walisema, ukitaka kujua tabia ya mtu tazama rafiki zake na kisha tabia na mienendo yake,utaweza kumjua vizuri ni mtu mwenye uelekeo wa aina gani.

Kwa mujibu wa ilani na Haki za Binadaamu za Kimataifa mtu hakatazwi kutumia wazi analoona linaamsitiri,lakin hatakiwi kutembea uchi.Miongozo mingine ya taifa inakataza kuvaa sare zinazofanana na za vyombo vya ulinzi na Usalama ambaavyo ni Jeshi la Wanaanchi wa Tanzania (JWTZ),Jeshi la Poliosi,Magereza na Jeshi la kujenga Taifa.

Katika kipindi hiki ambacho wanasiasa wanaendelea kunadi sera na ilani zao kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 30,baadhi ya wanasiasa,wanaonekana kwenye majukwaa ya kisiasa na mavazi yanayofanana nay a wanamgambo,jambo ambalo limewatia shaka baadhi ya wafurukutwa na mashabiki wake.

Mashabiki wa chama hico na baadhi ya wananchi wana hofu kuwa kama Mbowe atatwaa madaraka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kifungu cha 33 (2) kinamtaka kwamba,Rais atakuwa mkuu wa nchi,Kiongozi wa seriksli ns amiri jeshi Mkuu,atavaa magwanda ya Jeshi na kuongoza taifa kwa amri za kijeshi kama alivyoonekana kwenye mikutano ya Kampeni.

Viongozi hao, waliwahamasisha wafanyabiashara ndogondogo maarfufu ‘wamachinga’ kwamba wanataabika kila siku kutimuliwa kwenye maeneo yao ya biashara ,mama lishe vyakula vyao vinamwagwa na baadhi ya raia kubambikiwa kesi za uzururaji.Hivyo CHADEMA itawaelimisha kuhusu haki zao hata hivyo baadhi ya wananchi walitafsiri kitendo hicho kilikusudia kuwachonganisha na serikali.

Ingefaa wanasiasa kunadi sera na malengo yao bila majigambo na jazba kwenye majukwaa hususan CHADEMA na CUF ambavyo vinawatia hofu wananchi.

Yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbowe ambaye amefikia daraja la kuitwa ‘Castro’ Kasoro hana ndevu nyingi,amewahi kukaririwa akisema kuwa atavaa magwanda hayo mpaka aingie Ikulu, na mwenye wivu au kuchukia na ajinyonge.

Kumbe ndio mana hata mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (saau),Bwana Paul Kyara Handry,wakati akizindua sera na ilani ya chama chake aliaonya wananchi kuwa macho na wanasiasa wenye mavazi aliyodai ni ya wanamgambo maana kama watapewa ridhaa ya kuongoza nchi wanaweza kupangua katiba.


HOJA
Ijumaa,julai 22-28,2005

Magari ya Wafadhili yapata mkosi CHADEMA

*Moja limeibwa nyumbani kwa Mbowe
*Jingine limepinduka Shinyanga,halifai
*Mkurugenzi naye kagonga moja Mlimani Kitonga

Na Mwandishi wetu

MAGARI yote matano yaliyotolea na wahisani wa Uholanzi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kiweze kufanikisha kampeni za uchaguzi yaamepata mikosi na hayafai tena kukanyaga barabarani,imebainika.

Gari la kwanzakukumbana na mkosi huo ni aina ya Suzuki Scudo ambalo inadaiwa liliibiwa likiwa limeegeshwa nyumbani kwa Mwenyekiti a Chama hico,Freeman Mbowe.

Wakati mkuu wa usafirishaji anaendelea kutafakari hilo,gari jingine jipya kabisa (namba tunazo) limepinduka huko Shinyanga wakati wa Ziara ya katibu Mkuu wa CHADEMA,Dk,Wilbord Slaa mkoani humo.

Mzimu wa kutafuna magari ya chama umeendelea kuenea na kutua kwenye gari jingine lililoshuka injini yake likipanda mlima wa Kitonga mkoa wa Iringa likiwa linaendeshwa na mmoja wa wakurugenzi wa CHADEMA (Jina tunalo)

Mkurugenzi huyo ambaye alikimbia sera za CUF mwaka jana hajaguswa wala kuhojiwa na kamati ya nidhamu kuhusu kisa cha kufanya mbwembwe mlimani na gari la wafurukutwa.

Sasa hivi limeegeshwa ofisi za chama hicho zilizoko Kinondoni,Dar es Salaa,halifai tena.
Nalo gari aina ya Land Cruiser analotumia Mwenyekiti Mbowe anadaiwa lilipata ajali kubwa mkoani Singida alipotembelea huko kuhamasisha uhai wa chama ili kupanda mbegu za fitina dhidi ya chama tawala na wapinzani wengine.

Wakaguzi wa magari kwa taarifa tulizonazo wametathmini majaliwa ya gari hilo na kueleza kwamba halifai kabisa kutumika labda baadhi ya vyama vitumike katika kutengeneza majiko ya mkaa.

Aidha, kuna taarifa za uhakika kwamba gari moja jingine nalo limeng’olewa vipuri vijulikanavyo kama controller Box na kupachikwa kwenye gari la hotel ya kigogo mmoja wa Makao Makuu ya chama hicho iliyoko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kutokana na hatua hiyo, gari hilo nalo limetelekezwa halifai tena kufanya shughuli yeyote.

Baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA wamemshutumu Mbowe kwa kushindwa kudhibiti mali za chama.

Wakati anaendelea kuhubiri uadilfu thabiti kama atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Labels:

Mbowe anaandaliwa kumrithi Kikwete?

Uchaguzi


Mbowe kuandaliwa au anajiandaa kumrithi kikwete ?


Na Mobini Sarya

Kwa miaka ya nyuma kwenye siasa zetu za Afrika Mashariki ilikuwa vigumu kutabili nani ataongoza baada ya kiongozi alieyeko madarakani kusitaafu lakini kwa miaka ya hivi karibuni inakuwa rahisi kufahamu ninani atayeshika dola baada ya aliyeko madarakani kutoka.

Hata kwa wenzetu Kenya kwa sasa bila shaka ukiuliza ninani atakekuwa raisi wa Jamhuri ya Kenya baadala ya Mwai Kibaki atakuambia hata kosa kukuambia ninani.

Hivyo hivyo kwa hapa kwetu Tanzania chaguzi ulipokaribia vyama vya siasa vikaanza kuitisha kura za maoni kutamtafuta mgombea kwa chama tawala watu walianza kusema bila kutafuna maneno kuwa kikwete ndiye atashinda na kweli ikawa hivyo pia ulipoanza uchaguzi mkuu walisema kwamba kikwete atakuwa Raisi na kweli ikawa.

Ndio maana na mimi na uliza kama sio kubashiri kuwa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA anaandaliwa kumrithi kikwete baada ya muda wa serikali ya awamu ya nne kufikia kikomo mwaka 2015 kama sio 2010 ?

Ninazo sababu kadhaa zinazo nifanya nihoji ambazo nafikiri hata msomaji atapaswa achangie kupata changamoto nimeamua kuhoji kwa kulingana na mfululizo wa matukio yanayo mweka Mbowe kwenye kumbukumbu ya historia.

Binafsi mimi simweelewi wapi alipoanzia siasa na sikupenda nianze kutafiti historia yake kwa sababu sielezei maisha yake wala historia yake binafsi, ila naeleza kitu kitakachotokana na masilahi ya taifa na kubadili kabisa siasa za Taifa hapo badae na Afrika nzima.

Kwa wale wanaomfahamu wanasema Mbowe kama walivyo viongozi wa vyama vingi alikuwa CCM akiwa kijana na kada wa chama alitaka atumie nafasi yake kutumikia wananchi kama Mbunge ingawa aliongoza kwenye kura za maoni lakini alienguliwa na akatangazwa aliyekuwa ameshindwa.

Kitendo hicho kilimfanya atafute chama makini ahamie ili aweze kupata nafasi ya kutumikia wananchi wa jimbo lake bila shaka chaguo lake lilikuwa Chadema na kweli alipogombea akashinda akawa mbunge wa jimbo la Hai kwa vipindi viwili mfululizo hadi alipoacha mwenyewe.

Ingawa aliacha akitaka kugombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini wananchi wake walimfuata wakitaka aendelee kugombea ubunge kwani bila yeye Jimbo litarudi mikononi mwa CCM na kweli ndivyo matokeo yalivyokuwa.

Kwani Mbowe alibaki na msimamo wake ule wa awali wa kugombea urais nafasi ambayo sasa ilimtambulisha nchi nzima na kupata umarufu wa ghafla na kutishia wanasiasa wenzake kutoka vyama mbalimbali vya siasa kikiwemo chama tawala hadi ikafikia wakati wakamvumishia kwamba amerejea CCM ilikuwavunja nguvu wafuasi wake.

Hatua ya kutumia usafiri wa anga kupiga kampeni nchi nzima ilikuwa ni hatua nyingine ya kuwatia wasiwasi mkubwa sio wapinzani wake tu hata wachunguzi wa masuala ya siasa walifikia hatua wakashindwa kufahamu ninani atakuwa wapili baada ya Kikwete na idadi ya kura atakazopata.

Kwani aliweza kwenda hadi vijijini ambako wagoimbea wengine hawakuweza kufika na kuteka makundi mbalimbali kwenye mikutano yake ya kampeni na kuzidi kuwachanganya wengi pale alipokuwa anafika kwenye jimbo ambalo mgombea ubunge kutoka chama cha upinzani ananguvu na kuamua kunadi.

Hatua hiyo ya kishujaa ambayo nilisifiwa na wasomi mbalimbali na kusema anaonyesha ukomavu wa kisiasa aliifikia kwa lengo la kuongeza idadi ya wabunge kutoka kambi ya upinzani Bungeni bila kujali itikadi.

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa alishika nafasi ya tatu lakini alishangaza watu akiwa mpinzani alipojitokeza na katika tume ya uchaguzi kisha kumkumbatia mgombea wa CCMaliyekuwa ameshinda.

Hali iliyoacha maswali mengi mitaani na kuweka histori toka uchaguzi wa vyama vingi uanze mwaka 1995 ni vigumu ilikuwa ndoto mpinzani kukaa mezani moja hasa kipindi cha uchaguzi kwani maneno yasingeisha kusema kwamba ni wakala wa CCM ameletwa ili auwe upinzani.

Pamoja na shutuma lakini pia wanasiasa nchi nyingi za Afrika hawariziki na matokeo ya uchaguzi yanapotangazwa na ukakuta aliyeshinda anatoka chama tawala kwa hiyo kitendo cha Mbowe kumkumbatia Kikwete kiliacha maswali mengi.

Wengine wakihoji na kumpongeza kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa unaoelekea kubadili mfumo wa siasa ya nchi yetu na kuleta umoja na kusahau uhasama lakini wakosoaji wake walibaki wakisema anaoonekana kutaka kujionyesha kwa kikwete ili apewe madaraka.s

Labels: