Saturday, August 11, 2007

शेह्जेना ZAKAMATWA

VITA YA KUPAMBANA NA BIASHARA YA MADWA YA KULEVYA NI NGUMU

Na Mobini Sarya

VITA ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya inazidi kuwa ngumu baada ya watu wanaojihusha na biashara hiyo kuzidi kubuni njia za kukwepa kutiwa mbaroni.

hali hiyo imebainika baada ya Polisi jijini Dar es Salaam,kugundua njia mpya inayotumiwa na watu hao ambapo wamefanikiwa kukamata Madawa ya zaidi ya shilingi milioni 36 wiki hii, Mtwara na Dar es Salaam.

akizungumza na wanadishi wa habari Ofisini kwake jana Mkuu wa Kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya nchini(OC) Kamishna Msaidizi wa Polisi alitaja njia hiyo ni Ruti ubayoanzia nchini Komoro kwa kumia ndege za Shirika la Air Tanzania (ATC)
Godfrey Nzowa alisema kuwa Agoust 6 Mwaka huu 9:30 alisiri watu wawili walikamatwa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Mmoja wao akiwa na kete 90 za Heroin tumboni baada ya kuwashuku.

Kamanda Nzowa aliwataja vijana hao kuwa ni George Renatus au Bulegi Mkazi wa Magomeni Mwenye umri wa miaka 38, kabila msukuma kwa mjibu wa mama yake lakini kwenye Pasporti yake inaonyesha anaumri wa miaka 39.

mwingine ni Hussein Ali Mbwana (25) lakini mwenyewe anajiita Hessein Mbwana Alii kabila lake msambaa, mfanyabiashara na Mkazi wa Kariakomo na Magomeni.

vijana hao walikamatwa na Kikosi cha kupambana na Madawa hayo wakitokea Komoro ambapo baada ya kuhojiwa walikana kuwa na madawa hayo lakini baada ya kushikiriwa kwa siku mbili Agost 8, saa 10 jioni George alitoa Pipi 2 za madawa hayo aina ya heroini, lakini alishindwa kusukuma pipi zingine ikabidi apelekwe Hospitali ya Taifa Mhimbili (MNH).

Baada ya madakitari kumpiga X-lay walibaini kuwa alikuwa na Pipi nyingine lakini ziliwa zimekaa vibaya kwa hiyo asingeweza kuzitoa kwa njia ya kawaida ikabidi afanyiwe upasuaji na kutolewa pipi 88 na zile mbili ikawa jumla 90.na sasa amelazwa Hospitalini katika hodi ya Sewaji Mhimbili akiwa chini ya ulinzi.

Aidha Nzowa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo umeonyesha kuwa Hussein aliondoka hapa nchini Julai 24 Mwaka huu kuelekea Mumbai India kupitia Nairobi nchini Kenya na Baadaye alielekea Yemeni, Agousti 2 alikwenda Komoro akiwa tayari na madawa hayo ndipo wakakutana na George na kumpatia.

na katika Pasi ya Georgi inaonyesha kuwa alitoka hapa nchini Julai 3 ili kumpokea Georgi ambapo aliyatema Komoro baada ya na mwenzake kumeza madawa hayo wakarejea hapa nchini Agousti 6 kwa kutumia usafiri wa Ndege za ATC.

Katika uchunguzi huo imeonyesha kuwa watuhumiwa wengi wamekuwa wakitumia njia hiyo kwa kusafiri na Ndege za ATC hadi Mtwara kisha hupanda mabasi kuja Dar es Salaam.

Kamanda Nzowa amesema kuwa kiasi cha madawa yaliyokamatwa jijini Dar es Salaam kikizalishwa katika kete kila pipi moja inatoa kete 1000 ambapo kila kete moja inauzwa shilingi 1200 hadi 1500 na jumla ya kete zote 90 zinakadiliwa kuwa na thamani ya zaidi shilingi milioni 18

aidha katika tukio lingine kama hilo Agoust 8 Mwaka huu, Hamza Mohamed Sultani(38) Mkazi wa Karikoo kabila lake Mzaramo alikatwa Mkoani Mtwara akitokea nchini Komoro akiwa na kiasi kikubwa cha madawa aina ya Heroini Gram 900 zenye thamani inayokisiwa kuwa shilingi Milioni 18 , akiwa ameweka katika viatu vyake.

Nzowa alisema kuwa Mtuhumiwa huyo alikatwa saa saba machana Uwanja wa Ndege wa Mtwara na kwa mjibu wa Pasi yake ya kusafiria inaonyesha kuwa alitoka hapa nchini Julai 31 mwaka huu akaelekea Dubai kisha Comoro akiwa tayari na madawa hayo ambapo alipanda ndege ya shirika la ATC kuelekea mtwara ili apande basi hadi Dar es Salaam madawa yakiwa kwenye viatu ndani ya Begi lake.

watuhumiwa wote wanashikiriwa ili kukamilisha upelelezi kisha kupandishwa kizimbani ambapo thamani ya madawa hayo itajulikana rasmi.
MWISHO