Sunday, August 19, 2007

Jamii

Na Mobini Sarya

JAMII imetakiwa kutumia njia ya uzazi wa mpango kwani inaokoa sana vifo vingi vya akina mama na watoto ambavyo hutokea kutokana na uzazi usio na mpango.

Ushauri huo ummetolewa kwenye Semina iliyoandaliwa na Chama cha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake (AGOTA) na kuwakutanisha wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kujifunza namna ya kutumia uzazi wa mpango katika mpango unaokilikana kama Familya Planningi (FP).

Katika semina hiyo wandishi walipata nafasi ya kujifunza njia mbalimbali za kutumia kwa mwanamke na mwanaume ili kuepuka mimba na kupanga uzazi, ambapo miongoni mwa njia ambazo zilitajwa ni kutumia vidonge vya majira,kuchomwa sindanom,

kuwekewa njiti ambazo zinaziba mirija ya uzazi au kuwekewa kijiti ndani ya mkono sehemu zenye mafutamafuta kwa mwanamke na kwa mwanaume njia ni moja tu ya kukata mrija wa uzazi unaotumika kupitisha mayai ya uzazi.

Pamoja na kuwa njia zote zilionekana kuwa zinafaa lakini pia wataalamu wanasema kila njia ina madhara yake kwa mfano mtu aliyefunga kuzaa anaweza kufika kipindi akahitaji kufunguliwa ili azae ikashindikana.

DK.Ridhard Lema wa AGOTA ambaye ni Daktari katika hospitali ya Massana alisema kuwa kati ya akinamama wanaopaswa kutumia uzazi wa mpango ni asilimia 20 tu hutumia njia hiyo, ingawa wanahakikisha kuwa kila mteja anayefika katika vituo vyao vya Quality of Care anachagua njia nzuri ya kufunga ambayo haitamletea matatizo makubwa.

Katika semina hiyo ilibainika kwamba sababu ya wanahabari wengi kuacha kuandika habari za Afya na kukimbilia kuandika za kisiasa sana ni kwasababu madaktari wengi wamejiweka mbali na waandishi, mara nyingi wanapofuatwa ili watoe ripoti ya kitabibu huanza kumzungusha mwandishi kuwa sio wasemaji.

Kutokana na hali hiyo wajumbe wa Semina waliunda kamati ya watu sita itakaojumuisha Madaktari na wandishi ili waweze kutafuta sababu ya utengano uliopo kati ya wataalam wa Afya na waandishi ili waweze kufanyakazi pamoja ya kuelemisha jamii kuhusu afya ya mpango.

nbmkkjkjuodn/mc तिझू rczh, .m

Je ujio wa the comedy ni kiama cha wasanii w a maigizo?
Na Mobini Sarya

KAMA ilivyo ndivyo inavyoonekana kuwa kwamba kila jambo lenye mwanzo halikosi kuwa na Mwisho na Ngoma ikilia saana inakaribia kupasuka.

Hivi ndivyo ilivyo katika sanaa na wasanii wa Bongo kwamba sanaa yao inadumu kwa muda tu japo inawashika watu kisha inaibuka sanaa nyingine inameza ile ya kwanza.

Zamani zilikuwepo Bendi maarufu na wanamziki Mahiri wakiokuwa wakilitikisa anga la Mziki wa Afrika Mashariki na kati miongoni mwao ni kama Super Matimila ya Remmey Wangara , Tabota Jazz na Magereza Las Wanyika na Simba Wanyika zilikuwa zikiongozwa na wasanii mahiri kama Marehemu marjan Rajabu.

Hizo bendi nyakati zake zilipokuwa zikipiga kwenye ukumbi fulani kila mtu alihitaji kufika huko ili ajionee na kuburudika lakini kadri miaka ilivyo kwenda bendi za wakongo man zilitoa ushindani mkali na kutishia mziki wa Bongo baada ya kuja na mtindo wa Disco dansi.

Upinzani mkali uliibuka miaka ya tisini wakati wa enzi za Rais wa Kongo zamani Zaire, Mabutu SeSseko Kuku Wazabanga ambapo vijana wenye Elimu ya chuo kikuu waligeukia mziki akina Koffi Olomide waliokuwa na staili ya Ndombolo ya Solo.

Ni nani ambaye anapenda mziki kama angesikia Mziki wa Awilo Longomba asingeruka juu na kucheza ilifikia kipindi mwanamziki wa Kongo akija kufanya onyesho lake hapa anapokelewa kama mfalame na kingilio siku huyo kinakuwa juu tafauti na wanamziki wetu wanyumbani.

Lakini kila jambo lina mwisho wake kwani Vijana wa hapa nyumbani Tanzania waliamua nao kufanya mapinduzi kwa kuanzisha bendi zilikuwa zinaimba kama Ndombolo ya wakongo lakini kwa kutafsiri kwa Kiswahili ‘bongo ndansi wakajikuta wanaliteka anga la bongo na kuanza kutoa upinzani kwa wakongo.

Wanamziki wa kitanzania walifanikiwa kujizolea umaarufu baada ya kuimba mtindo wa ndombolo lakini kwa staili ya Bongo Dansi yaani kwa Kiswahili, bendi kama Twanga Pepeta wakati zinaibuka zilionyesha upinzani mkali kwa wanamziki wa kikongo na kulitikisa Anga la Bongo.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa bendi za hapa nyumbani kupiga mziki wa aina ya kongo lakini kwa lugha ya kiswahi jambo lililowafurahisha wapenzi wa burudani hapa nyumbani na kufanya bendi myingi kuzawaliwa hapa na kuzika kabisa bendi za zamani zikabaki zinaitwa zilipendwa au zilizovuma.

Ujio wa wanamziki wetu wa kizazi kipya ambao waliamua kufanya mapinduzi ulikwenda sambamba na wasanii wa sanaa ya maigizo katika anga la Bongo, waliokuwa na mtindo walioupachika jina la Bongo Fleva baasi lilikuwa ni hitimisho la Ngoma ya wakongo na Filamu za kigeni kupendwa hapa nchini.

Wakati vijana kama Joseph Mbilinyi almaarufu kama Mr.two wanaingia kwenye anga la Bongo Fleva walikua wanabezwa na wanaopenda miziki ya Dansi na kuwaona hawa vijana wa kizazi kipya wanaoimba kwa kufoka foka kuwa ni wahuni.

Na nyimbo zao zilikuwa zinaonekana kuwa zenye kubeba ujumbe wa matusi hasa Mr. alipotoka na wimbo wake wa ‘Nipo mikononi mwa Polisi, Afande’
Hata hivyo kubezwa kwao hakukuchukuwa muda.

Wakati vijana zaidi akina Dudubaya walipoibuka na nyimbo zao kama ‘Mwanangu huna nidhamu’ Hard Blasta na wakiongozwa na Joseph Haule a.k.a Profesa Jay ‘Ee Mkozi nitoe Roho niepukane na hili balaa’.

Wakati vijana hao wakiibuka walianza kuwateka makundi ya vijana, kabla ya kuwanza kateka rika zote za nmakundi ya jamii, mapinduzi yalizidi kuwa makubwa baada ya vijana hao kuanza kurekiodi video za picha na kurushwa katika televisheni mbalimbali , vijana kwa wakubwa walishinda wakitazama luninga.

Kutokana na hali hiyo hali ya wanamziki kutoka kongo ilikuwa imefikia kikomo kwani ile jeuri ya kufika hapa wana jikusanyia kipato kikubwa na vingirio kuwa juu zilikoma baada ya wananziki fulani kufika hapa nchini na kukupanishwa katika kumbi tafauti wakajikuta wabongo wengi wanakwenda penye kizazi kipya.

Lakini hizo zama sasa zinaonekana kupitwa na wakati kwani baada ya vijana wengi kuufanya mziki huo kuwa ajira kila mmoja aliyeshindwa kuendelea na na masomo kuugeukia ummekuwa sio dili tena ,sasa hata bendi za kina msondo zimeanza kurudi kwenye chati.

Swali ambalo limeibuka tena kwenye sanaa ya Bongo ni je Ujio wa Ze Komedi ni kiama cha wasanii hasa wa maigizo hapa nchini?

Imekuwa ni kwaida kila Alhamisi kinaponza kipindi cha Ze Comedy kinachoendeshwa na vijana wa kundi hilo akina Masanja Mkandamizaji ambaye ni msoma taarifa ya habari, Joti au Hamejei anayebonyeza Kizenji katika habari za biashara ,

Mpoki na wakuvanga wanaocheza katika sehemu mbalimbali kukuta watu wamerundikana na katika mabaa na majumani kwa watu wakitaza kipindi hicho katika Televishion ya chanel 5.

Kipindi hicho ambacho katika taaluma ya uandishi wa habari kinaonekana kuwakilisha katuni kimeonekana kuwateka watu wa matabaka mabalimbali wakubwa kwa wadogo ,waheshimiwa kwa wastaarabu kila mmoja inapofika saa moja jioni alhamisi hujipumzisha kwenye TV yake akikitazama.

Ni jambo la kwaida kukuta hata kwenye chumba cha habari wakati kama huo wandishi wakiwa wamesimamisha shughuli zao na ili kukitazama kipindi hicho lakini kinapokuwepo kipindi cha Bunge utakuta kila mmoja anaendelea na shughuli zake.

Baada ya kuwa vijana hao wa The Comedy wamewakamata vilivyo watazamaji , sanaa ya bongo immeanza kuwa mashakani, wasanii wa kuanza kulia njaa ni w ale wanaoigiza ambao awali walikuwa wanapambana na wasanii wenzao kutoka Nigeria sasa wanaona soko lao limeathiliwa.

Zamani ilikuwa ni jambo la kwaida kukuta siku kama za jumamosi watu wamejazana kwenye majumba ya senema na majumbani kwao wakitazama maigizo au miziki ya kibongo lakini sasa hilo sio kivutio tena kila mmoja anataka kumuona Ze Comedy kama wanavyojulikana.

Kutokana na watu wengi kuvutiwa na kupindi hicho lakini watoto wadogo wanaonekana kuwathirika nacho wataalamu wa Saikolojia wanaonya kuwa ikiwa wazazi wengi hawataangalia watoto wao wenye umri wa miaka chini ya kumi watakuwa vilema.

Hiyo imetokana na w atoto wengi kuanza kutembea kwa kukunja miguu kama anavyotembea Hamijei haali hiyo inaelezwa na wataalam kuwa ni rahisi mtoto kuzoea hata akiwa mkubwa.

Wasanii wa maigizo sasa nao wanaona kama muda wao umepitwa na wakati kwani katika sanaa ya uigizaji hasa ucheshi walikuwepo akina Bambo na kingwendo ambao katika kipindi chao kila mtazamani alipenda kuwaona wakiburudisha lakini leo wako wapi? Hiyo ndio inazidisha mashaka je kiama chao kimefika kama mitindo ya mziki ilivyofikia kikomo?

Pia inaelezwa kuwa kutokana na kipindi hicho kuwa na watazamaji wengi hata matangazo ya televisheni yanayorishwa hapo yemekuwa ni ghari kuliko vindi vingine na makampuni mbalimbali yamekuwa yakiwania nafasi ya kurusha matanagazo yake hapo.

Ni wakati mwafaka sasa kwa vijana hao kuwaandaa maisha ikiwemo kujenga na kumarisha familia zao na kuweza kujiwekea akiba ya uzeeni kutokana na sanaa ya bongo kutokuwa na uhakika wa kudumu kama zilivyo nchi za wenzetu.

Baada ya vijana hao kuonyesha utundu hasa katika saa ya mziki kuna uvumi kuwa mwana Asha Baraka anatamani kuwachukua katika bendi yake wawe wanenguaji wake, jambo ambalo halijathibitishwa, ingawa inaweza kuwa ngumu kutokana na mikataba ya kazi kubana ,swali linalobaki ni je ujio wa Ze Comeidy ni kiama cha wasanii?.

www.mobinday.blogspot.com ..,0753399579,mobinsons@yahoo.com.