Friday, November 30, 2007

WIKI YA MAMLAKA YA ANGA NA VIWANJA

Na Mobini Sarya

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege na Anga imetangaza wiki ya Usafiri wa Anga na Maadhimisho ya usafiri wa Anga Duniani itakayoanza jumatatu ijayo.

akizungumza na waandishi wa habari jan katika ukumbi wa idara habari MAELEZO mkurugenzi wa mamlaka hiyo nchini Margaret Munyangi alisema kuwa maadhimisho hayo yatakuwa ya sita tangu yaanzishwe hapa nchini.

" kuanzia Disemba mosi ya kila Mwaka tunaadhimisha wiki ya usafiri wa anga ili kwenda sambamba na maadhimisho ya usafiri wa anga Duniani yanayofanyika kila Disemba saba ya Kila Mwaka"alisema Munyangi



Munyangi alisema kuwa wanatumia wiki hiyo kwa kutoa elimu kwa wananchi na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa watu wanaofika kutembelea mabanda ya maonyesho yanakayokuwepo uwanjani.

kauli mbiu ya usafiri wa anga mwaka huu ni 'usafiri wa anga- kichocheo cha maendeleo'

aidha aliwaambia waandishi kuwa wanatarajia kuboresha viwanja 18 vya ndege hapa nchini ili kurahisha usafiri kwa wananchi hasa baada ya makampuni mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kuwekeza.



Na Mobini Sarya

SHIRIKA la uendeshaji Treni ya Reli ya Kati (TRL) limetoa Taarifa ya chanzo kilichosababisha kukwama kwa Treni mbili njiani kwa siku kadhaa.

katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Jayaram
ambaye Mkurugenzi Mtendaji wa TRL ilisema kuwa,imesababishwa na Kutokea ajali ya treni ya mizigo iliyotokea saa 7.30 usiku wa Novemba 27 Mwaka huu katika eneo la reli kati ya stesheni za Kaliua na Kigoma.

taarifa hiyo ilibainisha kuwa ajali iliyohusisha mabehewa sita yaliyokuwa yamebeba mbolea kuacha njia ambapo yaliharibu njia ya reli yenye urefu wa mita 300.

kutokana na hali hiyo Maafisa wa Reli na wafanyakazi wa kawaida wakiwemo Wakuu wa Usafirishaji wa Reli(DTM), Mhandisi Mitambo(DME), Mhandisi Ujenzi(DCE) wakishirikiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Tabora wamefika katika eneo la tukio ambako wameanza kazi ya ukarabati.

Njia hiyo ya reli ilitarajiwa kufunguliwa jana saa nne usiku.

Kutokana na ajali hiyo treni ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambayo iliwasili saa moja asubuhi Novemba 27, 2007 ilizuiwa hapo kwa vile njia ya reli ilikuwa haipitiki.


aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa hadi sasa Chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na jopo maalum la maofisa waandamizi wa TRL wakiwemo walioko Tabora.

taarifa hiyo imetolewa Wakati treni ya abiria kwenda Kigoma ikiwa imekwama kusafiri kwa siku ya nne mfululizo katika mji mdogo wa Kaliua, wilayani Urambo, huku treni nyingine ya abiria kutoka Dar es Salaam, iliyowasili Tabora kwenda Kigoma, nayo imekwama kwa siku mbili.



Habari toka Kaliua, wilayani Urambo, ilikokwama treni, zinasema kuwa baadhi ya abiria tayari wameishiwa fedha za kujikimu na vyakula, hata kulazimika kuuza baadhi ya vitu vyao, huku vibaka ambao inadaiwa kuwa wamefungua `kambi` ya muda ndani ya treni wakikwapua baadhi ya vifaa vya abiria hao na hivyo kuwazidishia machungu.

Treni ya abiria iliyoondoka Dar es salaam Jumapili Novemba 25, mwaka huu, imekwama kuendelea na safari zake katika mji mdogo wa Kaliua, wilayani Urambo kufuatia ajali ya gari la mizigo lililokuwa linakwenda Kigoma kutokea Tabora kuacha njia na behewa moja kupinduka huku mabehewa sita yakiacha njia. Hakuna mtu aliyejeruhiwa au kufa katika tukio hilo.

Treni ya abiria iliyokwama Tabora iliondoka Dar es salaam, Jumanne iliyopita, ikiwa na msongamano wa abiria, hasa wa daraja wa tatu.

hivi karibuni Serikali imeingia Mkataba na Kampuni ya RITES kutoka India kwa matumaini kuwa kampuni hiyo itawekeza mtaji wa kuboresha usafiri tafauti hivyo tangu ianze Novemba Mosi matatizo yamezidi kuongezeka.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

Kumetokea ajali ya treni ya mizigo mnamo saa 7.30 usiku wa wa Novemba 27, 2007 katika eneo la reli kati ya stesheni za Kaliua na Kigoma. Yaliyohusisha mabehewa sita (6) yaliyokuwa yamebeba mbolea kuacha njia ambapo yaliharibu njia ya reli yenye urefu wa mita 300.

Maafisa wa Reli na wafanyakazi wa kawaida wakiwemo Wakuu wa Usafirishaji wa Reli(DTM), Mhandisi Mitambo(DME), Mhandisi Ujenzi(DCE) na Mhandisi wa Mawasiliano na Ishara(DSTE) wakishirikiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Tabora walifika katika eneo la tukio haraka bila ya kujali mvua kubwa na mazingira magumu na ambako walianza kazi ya ukarabati wakitumia jeki na kreni iliyoletwa kutoka Tabora.
Njia hiyo ya reli inatarajiwa kufunguliwa leo saa nne usiku huu.

Kutokana na ajali hiyo treni ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambayo iliwasili saa moja asubuhi Novemba 27, 2007 ilizuiwa hapo kwa vile njia ya reli ilikuwa haipitiki.

Hata hivyo utaratibu umefanywa na TRL wa kuwapatia abiria chakula na maji.

Chanzo cha ajali hivi sasa kinachunguzwa na jopo maalum la maofisa waandamizi wa TRL wakiwemo DME, DTM, DCE na DSTE walioko Tabora.

Imesainiwa na: N. Jayaram
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Novemba 29, 2007 DAR ES SALAAM

Wednesday, November 28, 2007

Katika Dunia hii kuna Watu hawaoni Mchana wanahitaji msaada wa Tochi: TREN INAWEZA KUPATA AJALI

Katika Dunia hii kuna Watu hawaoni Mchana wanahitaji msaada wa Tochi: TREN INAWEZA KUPATA AJALINa Mobini Sarya

ABIRIA wanaotumia usafiri wa Treni ya Kati (TRL) wameonyesha wasiwasi wao juu ya usafiri huo kuwa umezidi kuwa wa mashaka hali inayoweza kusababisha ajali wakati wowote kutokana na kuendelea kuzorota na ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kurekebisha hali hiyo.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa Nyakati tofauti abiria wanaotumia usafiri huo kutoka mikoa ya Kigoma Tabora na Mwanza walisema kuwa hali ya usafiri huo sio ya kuridhisha kabisa na ni hatari kwa afya na usalama wao kutokana na hali ya mabehewa ya Treni hiyo kuwa machavu na machafu .

Abiria hao wanasema kuwa hata makochi wanayokalia yamechaa na kuchanika,
“mabehewa yamechakaa,harufu mbaya vitanda vibovu hakuna huduma nzuri zinazoridhisha, lakini hatari kubwa kuliko vyote ni uchakavu au uwezo wa vichwa (Injini) za Treni hiyo zilivyochoka hali inayoweza kusababisha ajali wakati wowote kutokana na kuzimika ghafla njiani” alisema abiria mmoja.
kampuni hiyo tangu ianzishe usafiri huo Novemba Mosi Mwaka huu imedaiwa kuendelea kutumia mabehewa na injini zilezile bila kufanya mabadiliko wala ukarabati wake.
Ingawa Kampuni inayosimamia Treni hiyo kwa muda mrefu imegoma kutoa ushirikiano wa wandishi lakini Mkurugenzi wa Reli upande wa Sumatra Alfred Nalitolela alisema kuwa tangu Mwekezaji huyo akabidhiwe Treni alichoongeza tu ni treni kufika Dar es Salaam.


Hata hivyo imedaiwa kuwa Injini hizo awali zilionekana kushindwa kuhimili usafiri pamoja na mabehewa yake nakulazimu Shirika la zamani (TRC) lililokuwa linaimiliki kukatisha huduma ya usafiri huo na kuishia Dodoma.



“hii treni ni ileile na mabehewa ni yale yaliyokuwepo zamani kilibadilika hapa tu nim kuongeza safari kufika Dar es Salaam, hakuna kipya zaidi ya hapo”alisema Nalitolela

Alisema kuwa kinawachowanyima usinginzi kama Sumatra ni jinsi hali ya usalama huo ulivyo kwani kwa sasa miondombinu kama ya simu hakuna sehemu nyingi jambo linaloweza kusababisha Treni kugongana wakati wowote kwa kukosa mawasiliano hali hiyo imefanya wamtake Mwekezaji kutengeneza hiyo simu.

aidha akizungumzia uimara wa Mabehewa na injini alisema kuwa wamewasialiana naye amewambia kuvikia Mwezi Disemba RITES watakuwa wamefufua vichwa vitano na kufikia Februari mwakani atakuwa amekarabati mahewa 25 nakuyaweka barabarani ili kupunguza msongamano wa abiria.

Nalitolela alisema kuwa usalama kwa Abiria ni jambo wanalolizingatia lakini kama wangeamua kuisimamisha hadi kila kitu kikamilike ingechukua muda mrefu nakusababisha adha ya usafiri kwa abiria, kwani hata kuboresha mabehewa na kuyafanyia usafiri ingechukua zaidi ya miezi minne.




Kutokana na hali hiyo imeripotiwa na abiria hao kuwa Treni hiyo imekuwa ikizimika njiani kufanya usalama wa abiria kuwa mashakani kwa kuhofiwa kuwa inaweza kuzimika kwenye mpando au mtelemko mkali na kuisababisha ianze kuserereka na mwishowe kuanguka kama ilivyowahi kutokea na kuuwa watu mwaka juzi Dodoma.
Aidha imedaiwa kuwa wakati treni hiyo inaelekea Tabora mwanzoni mwa wiki hii ilipoteza nguvu ya umeme na kuanza kutembea kwenye giza torore nakusababisha hofu kwa abiria waliokuwa wanaporwa na Vibaka waliogeuza treni hiyo kuwa hifadhi ya muda.
Kufuatia hali hiyo Tanzania Daima hivi karibuni iliwasiliana na Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) na Mwenyekiti wake Peter Cleverly Bakilana alisema kuwa hata wao wanataarifa hizo na tayari wamekwisha wajulisha (TRL) ili waboreshe hali hiyo haraka.

Hata hivyo alipoulizwa kwanini SUMATRA waliiruhusu Treni hiyo kabla ya kuangalia usalama wake alisema kuwa wasingeweza kuizuia kwani tayari Serikali ilikuwa imebaliki kwa kuewekeana saini na Mwekezaji na kama wangeizuia wangesababisha usafiri huo kuchelewa.
“Sisi pamoja na kutambua mapungufu hayo tusingeweza kuzuia treni isiondoke hadi wakamilishe kila kitu ikiwemo usafi kufanya hivyo kungechukua z aidi ya miezi minne, hata hivyo tunachojali ni usalama wa abiria tumekwishawandikia instruction kuwaomba warekebishe hali hiyo”alisema Bakilana.

Pamoja na majibu hayo alisema kuwa hawezi kuisimamisha hiyo treni kwani bado haijasababisha ajali yoyote na kama ni ajali hata zikinunuliwa injini mpya bado itakuwepo tu,

habari zingine zilizopatikana kutokana Sumatra zinadai kuwa tangu mwekezaji huyo Kampuni ya Rites aliyeanza kuongoza shirika hilo Novemba mosi Mwaka huu ameshindwa kutumia pesa zake kuboresha huduma hiyo na baadala yake amekuwa akiujaribu kupandisha nauli ya abiria ili avune pesa haraka hali ambayo imekataliwa na Sumatra.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la kusimamia watumiaji wa usafiri wanchi kavu na Majini (SUMATRACCC) Oscar Kikoyo alipozungumza na gazeti hili alisema kuwa usafiri huo ni wa mashaka unapaswa kusimamishwa hadi utengemae,

hata hivyo wasemaji wa TRL walipotafutwa w alishindwa kutoa ushirikiano na mara kadhaa wamekuwa w akisema waandikiwe maswali walipoandikiwa zaidi ya mwezi sasa hawajatoa majibu.

TREN INAWEZA KUPATA AJALI

Sunday, November 25, 2007

Benedicto Mutungirehi: Mimi ni mbunge likizoni

Mobini Sarya




UKIANZA kuzungumza naye mara moja unagundua kuwa ni mwanasiasa mwenye mtazamo wa kidini zaidi kuliko siasa yenyewe. Anapokuwa katika jukwaa la siasa anakuwa tofauti na anavyoonekana.




Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza tukiwa safarini Kigoma, nilidhani anasumbuliwa na jambo fulani la kusikitisha, kwani mara nyingi alikuwa kimya, hali iliyonilazimu kuchukua hatua ya kumfahamu zaidi.


Huyo si mwingine bali ni mbunge wa zamani wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Jimbo la Kyerwa, Benedicto Mutungirehi (40). Anasema kuwa hakushindwa ubunge bali amepumzika kwa muda yaani sawa na ‘mbunge aliyeko likizoni.’

Tangu ajiunge na siasa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na kugombea ubunge kupitia TLP Jimbo la Kyerwa, mkoani Kagera, amejipatia umaarufu nje na ndani ya jimbo lake, hasa baada ya kupata ushindi uliowashangaza wengi alipomwangusha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Eustace Katagira (CCM).

Umahiri wake wa kujenga hoja na kukwepa mtego wa kufungiwa ubunge, ulimjengea sifa nje na ndani ya Bunge hata kusababisha aliyekuwa Spika wakati huo, Pius Msekwa, kumpenda na kumpa nafasi kila wakati ya kusimama na kuchangia au kutoa hoja zenye ‘afya’ bungeni.

Lakini pia anasema umahiri wake wa kujenga hoja ulimwezesha kukwepa misukosuko wanayoipata wabunge wa upinzani, hadi kupendwa na Spika Msekwa na akawa anapewa mialiko ya nje.

Mutungirehi ametokea wapi?

Alizaliwa Mwaka 1967 katika kijiji cha Kitwe, wilayani Karagwe, akiwa mtoto wa nane katika familia ya mzee Mutungirehi.

Akiwa anasoma Darasa la Nne mwaka 1980, karama ya uongozi ilianza kujionyesha kuwa ni kiongozi alipogombea ukiranja mkuu alipopambana na mwanafunzi wa Darasa la Sita aliyekuwa amerudia shule. Alimshinda kwa kura nyingi.

Hapo ndipo karama ya uongozi ilipoanza kwani akiwa katika Shule ya Sekondari Kihororo Mwaka 1985 akiwa kidato cha pili, alichaguliwa kuwa mwenyekiti (Kaka Mkuu) wa serikali ya wanafunzi. Alipokuwa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Mirambo, Tabora, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa nidhamu.

Unaweza kusema ni mtu aliyezaliwa akiwa na karama ya uongozi, kwani alipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, akiwa mwaka wa pili mwaka 1994, alichaguliwa kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO). Ndiye aliyekomesha tabia ya mapinduzi ya uongozi chuoni hapo.

Hata hivyo Mutungirehi anasema hatasahau jinsi alivyotaka kuuawa wakati anajaribu kuzima mapinduzi chuoni hapo. Anasema wapinduaji walikuwa wamejipanga kuitisha mkutano haramu na kumwekea mtego kuwa akifika tu ukumbini, waanzishe vurumai wapate nafasi ya kumuua.

Lakini alibahatika na kudokezwa na mtu asihudhurie huo mkutano atauawa. Alikini alifanya ukaidi, akaenda, kweli vijana wa Mlimani wakataka kumshambulia.

Anasema wakati wanataka kumpiga, alianguka chini akawa anarusha mateke. Kuona vile wale vijana wakakimbia wakidhani amekufa.

Chanzo cha mgogoro huo kilitokana na msimamo wake wa kutaka serikali iwakopeshe wanafunzi pesa za matumizi badala ya mzigo huo kukabidhiwa wazazi, lakini wanafunzi wao wakataka serikali ilipe gharama zote bila masharti, jambo analosema lisingewezekana na utaratibu wake ndio unaotumika hadi leo.

Kutokana na mgogoro huo, wakamtaka aondoke madarakani, uongozi wa chuo ukaingilia kati ukiwataka waitishe mkutano wamtoe kwa njia ya kidemokrasia ikashindikana. Chuo kikafungwa kwa miezi miwili huku wanafunzi wa kitengo cha uhandisi waliokuwa vinara wa mapinduzi wakasimamishwa mwaka mmoja.

Hata hivyo anajivunia kuwa wakati wake aliweza kufanya mambo makubwa ambayo leo hii yanatumika baada ya kufanikiwa kuingia Ikulu kuonana na Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa na madai sita. Yote yalikubaliwa.

Moja ya madai hayo ilikuwa kama mtu ameajiriwa serikalini na akitaka kwenda kuongeza elimu chuo kikuu, alipwe mshahara badala ya utaratibu wa serikali uliokuwa unamzuia kulipwa bila kujali kama ana familia.

Pia alitaka sh 50,000 za kununulia vitabu wanafunzi zilizokuwa zinatumwa moja kwa moja kwenye duka la vitabu la chuo, wapewe pesa hizo wanunue wenyewe mitaani.

Tatu ilikuwa imetangazwa kuwa kwa mwanafunzi ambaye haendi likizo akibaki chuoni alipie chumba, wakapinga madai hayo wakataka akae bure. Pia serikali ilibadili mitaala ghafla ikasema anayesomea ualimu atakuwa anasoma miaka minne baadala ya mitatu, wakasema lazima ibaki mitatu. Pia waliiomba serikali ibadili matazamo ifungue milango ya majadiliano linapotokea tatizo la wanafunzi badala ya kufunga chuo.

Madai yote yalikubaliwa na serikali baada ya Rais Mwinyi akiwa na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, wakati huo, Benjamin Mkapa, kuyapitia madai yao kwa kina.

Hayo ndiyo mafanikio anayojivunia kuyaacha Mlimani na uzoefu wa kiuongozi. Anasema kutokana na hayo, ameweza kujua namna ya kukabili tatizo anapokuwa anaongoza jumuiya ya watu wengi na kutoa maamuzi magumu.

Itikadi yake ilikuwa nini?




Wakati akiwa chuo kikuu akichukua shahada ya Sanaa na Lugha, alikuwa mfuasi mzuri wa Siasa za Karl Max na Lenin. Hakuwahi kuamini kama Mungu alikuwapo pamoja na kwamba alipokuwa mdogo alikuwa akipelekwa kanisani (Roman Catholic) na kaka yake alikobatizwa. Lakini jambo la kushangaza hakurudi tena kanisani.

Alikuwa haamini kama kuna shetani au nguvu yoyote ya giza. Alikuwa miongoni mwa wale wanaoamini kuwa historia ndiyo inayoongoza dunia na mtu huwa maskini kwa sababu mwenzake anamiliki mali zote, jambo lililomweka mbali na imani za kidini.

Mutungirehi alihitimu masomo yake ya chuo kikuu mwaka 1995 na kuamua kurudi kijijini kwao kulima badala ya kutafuta ajira nyingine akihofia kutoa au kupokea rushwa.

Pamoja na kuwa alitunukiwa Shahada ya Sanaa na Lugha mwaka 1995, lakini alikataa kuomba ajira kwa madai kuwa alihofia hangekwepa kupokea rushwa kutokana na mishahara ya wafanyakazi kipindi kile kuwa midogo kuweza kukidhi mahitaji.

Akiwa kijijini kwao, alichaguliwa kuongoza Chama cha Wakulima wa Kahawa cha chama cha ushirika - Karagwe Development Co-operative Union (KDCU) akiwa makamu mwenyekiti.

Hata hivyo hakudumu katika uongozi huo. Alilazimika kujiuzulu baada ya kuwashauri wanaushirika wa KDCU kuwa hafurahishwi na jinsi wanavyokiendesha chama hicho kwani kitawaletea wakulima hasara. Ukweli ulikuja kudhihirika baada ya kujiuzulu. Chama kilipata hasara kubwa aliyokuja kuitetea bungeni baada ya kuwa mbunge.

Anasema uongozi ndani wa chama hicho cha ushirika ulimsaidia sana wakati anagombea ubunge. Hakupata shida ya kushinda. Wanakaragwe walikuwa wanaufahamu mchango wake katika kuinua na kutetea soko la kahawa akiwa na kaulimbiu yake ‘Wakulima waachiwe wachague wenyewe soko la kuuzia kahawa.’

Alianza lini siasa?

Mwaka 2000 aliibuka ghafla kwenye siasa akijitokeza kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kyerwa kupitia chama cha TLP. Chama hicho hakikuwa na umaarufu wala wafuasi wengi katika eneo hilo, lakini aliwashangaza wengi alipomwangusha aliyekuwa mbunge wa siku nyingi, Eustace Kataragira (CCM).

Alikuwa mbunge wa jimbo lake kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano, mwaka 2005 alipokujashindwa na Katagira kwa tofauti ya kura 2,800 uchaguzi anaosema ulijaa udanganyifu na wizi wa kura.

Lakini hakukata rufaa kwa sababu kesi nyingi huchelewa kuamuliwa.

“Mimi ninaamini uongozi hutoka kwa Mungu na Mungu anasema usiibe, sasa aliyeiba kura akakalia kiti kisicho chake atapata adhabu pamoja na waliomsaidia. Adhabu hiyo haiko mbali. Itakuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia hiyo,” anaonya Mutungirehi, sasa muumini wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God (TAG).

Anasema alianza kwenda kanisani Oktoba 2006 katika Kanisa la Katoliki baada ya kuuasi ukomunisti, lakini Desemba mwaka huo alibadili madhehebu ghafla na kuhamia TAG kwa madai kuwa alipokea wito wa kumtaka abadili imani.

Mutungirehi anasema kwa kipindi alichokaa nje ya Bunge, amepata muda wa kupumzika na kufanya kazi yake vema ya ukatibu mwenezi wa TLP, nafasi aliyoipata Machi, mwaka huu.

Amewezaje kudumu TLP?

Anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakimhoji amewezaje kuvumilia kuwako TLP ambako wengine wamekimbia.

Anaasema “Migogoro mingi katika vyama vya siasa inatokana na tamaa ya madaraka. Viongozi wengi wamekuwa wakishinikizwa kuachia madaraka wakati wao wanakuwa hawajaamua”.

Anasema hali hiyo husababisha vurugu na ndicho kisa cha wanachama wengi kuikimbia TLP, kwani walikuwa wanataka kumwondoa Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema, bila kufuata utaratibu.

Yeye anasema yupo TLP kwa raha kwa vile hana haja ya kugombea madaraka na ndiyo maana watu wengi wamekuwa wakishindwa kumwelewa, kwani pamoja na kuwa na uwezo mkubwa kisiasa na kielimu ameendelea kubaki TLP pamoja na kwamba makada wa vyama vingine wamekuwa wakimshawishi ajiunge navyo.

“Kutaka aliyepo madarakani atoke ili wewe uingie ndiyo chanzo cha migogoro mingi inayosababishwa na tamaa ya madaraka. Mimi siwezi kufanya kosa la kuzurura kwenye vyama,” anasema na kuongeza kuwa anachoamini si kwa utashi wake, kama ambavyo wanasiasa wengine wanavyojiapisha kuwa hawawezi kuhama chama halafu baada ya muda mfupi wanahama.

Mutungirehi na ubunge

Akiwa mbunge alitetea bei ya soko la kahawa hadi serikali ikasikia kilio chake na kupandisha bei kwa asilimia 100. Alitumia muda mwingi baada ya Bunge kutembelea wapiga kura wake akiwaambia haki zao. Jambo hilo lilimjengea umaarufu mkubwa.

Wananchi wa Karagwe walikuwa wamedhulumiwa sh. bilioni 2 za baada ya kuuza kahawa. Akawapigania kwa kujenga hoja hadi wakapewa na amekuwa akitumia muda mwingi kuwaelimisha wakulima jinsi ya kuondokana na umasikini.

Anamzungumziaje Rais Kikwete?

Katika maoni yake kuhusu utawala wa Rais Jakaya Kikwete, anaonekana kuungana na Mchungaji Christopher Mtikila pale anaposema kuwa Rais Kikwete aliingia madarakani ‘kiharamu’ ingawa kwa macho ya kibindamu na kidemokrasia anaonekana kuwa alishinda.

“Kikwete alitumia njia mbaya kuingia Ikulu, amemchukiza Mwenyezi Mungu. Jambo hili atakuja kulijutia wakati atakapokuwa anapokea malipo yake muda si mrefu,” anasema mwanasiasa huyo, kama vile anatabiri kuwa katika nafasi nzuri ya kumrithi Mrema mara atakapostaafu.

Mutungirehi anasema kuwa hata hili vuguvugu la kisiasa linaloendelea hapa nchini, ni sababu ya hizo hizo kama dalili na ishara za mambo makubwa yanayokuja. “Ukimwona mbunge anayewakilisha wananchi amechomewa nyumba yake, vibaka wanauawa hovyo…ujue uongozi wa CCM unakwenda kuvunjika na mfumo mpya unaojali wananchi utasimama punde si punde,” anasema.

Mutungirehi anasema kuwa mfumo huo anaoutabiri utawekwa kwa makusudi na Mwenyezi Mungu ili kuondoa rushwa na kulinda maliasili za taifa hili zitumike kikamilifu na ufisadi uishe kabisa nchini.

Anaendelea kusisitiza kuwa Kikwete aliingia kwa njia mbaya, sasa ameanza kulipa gharama ndiyo maana anazurura nje badala ya kukaa ajenge uchumi wa nchi unaoporomoka kila siku.

Kuhusu uchumi, Mutungirehi anahoji uhalali wa serikali kuuza kila kitu - viwanda na mabenki - badala ya kujenga kama alivyokuwa anafanya mwasisi wa taifa hili, Mwalimu Julias Nyerere.

“Kama Nyerere asingejenga mabenki, reli na viwanda leo hawa wangekuwa wanauza nini? Hata ranchi ambazo Mwalimu Nyerere alikuwa anatengeneza wameuza, sasa vya kwao wanavyojenga viko wapi?” anahoji mwanasiasa huyo.

Anasema kuwa ili nchi iimarike kiuchumi, lazima mfumo wa ‘home-grown’ uimarike na ikitokea uchumi wa dunia umeharibika tujitegemee. Lakini hapa kwetu hakuna kitu kama hicho.

“Vipo vitu ambavyo serikali inapaswa kuwekeza ili kulinda uchumi wa nchi,” anashauri.

Anasema serikali imekuwa ikijinadi kuwa makusanyo ya kodi yanaongezeka, lakini bila kuangalia kuwa vyanzo vya mapato navyo vimeongezeka au ni mzigo unaongezeka kwenye vyanzo vilivyoopo.

“Serikali inaongeza kodi wao wanasema kwamba kodi imeongezeka na uchumi lakini hatuoni vitegauchumi vinaongezeka bali wanazidi kudidimiza vilivyopo, kwani kuongeza kodi ni uharibifu unaodidimiza kipato cha wananchi.

“Tatizo ni kwamba wanapenda kufanya mambo yao kisiasa, wakitaja mapato mengi wanapigiwa makofi lakini hawaangalii je, mwaka huu tumezalisha kama bidhaa tani ngapi na mwaka kesho itakuwa ngapi?” anahoji.

Anasema Rais Kikwete anakwepa kusoma takwimu za uchumi ili apate nafasi ya kukaa na wasomi, wamshauri namna ya kujenga uchumi, lakini badala yake amekuwa akitumia muda mwingi kutafakari safari za nje na namna atakavyoenda kuzungumza huko.

Mutungirehi anamsifu Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa uwezo wake wa kujieleza, na upana wa mawazo anapokuwa anafanya jambo bila kujali kama anasifiwa au la.

Anatabiri kuwa hali hii ikiachwa iendelee maisha ya watu yatakuwa magumu na mfumo wa uzalishaji utasimama, kila mmoja atashindwa kununua wala kuuza.

Wapinzani watamsaidiaje?

Hata hivyo anasema kambi ya upinzani itamsaidia Kikwete kwa kuwaeleza Watanzania matatizo yanayoikabili nchi, ili wachukue hatua, kwani serikali ya sasa haisikilizi matatizo yao. Anawasifu wananchi jinsi walivyoamka na kuwaunga mkono katika harakati zao za kuelekea ukombozi kamili.

Mtungirehi anatoa wito iundwe tume huru ya kuchunguza ufisadi uliuokithiri nchini hadi kufikia hatua wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakawataja hadharani.

Anasema ikiwa tume huru itaundwa kuchunguza ufisadi na kubaini kuwa walidanganya kwa kutaja watuhumiwa, wao ndio watakaowajibishwa. Anashangaa ni kwa nini serikali haiundi tume hiyo kama madai yao ni ya uongo.

Anamtaka Rais Kikwete aunde tume ya kuchunguza ufisadi huo ili kuonyesha ushupavu na ujasiri hadi nje ya nchi. Na kama angetekeleza hilo tangu zamani watu kama Joseph Butiku wasingeibuka na kuwaunga mkono wapinzani. Anatahadharisha kuwa bila kuunda tume hiyo wapinzani watatangaza mgogoro mkubwa utakaoweza kumwondoa madarakani.

Kuhusu muungano wa vyama, kwanza anakiri kuwa muungano wa ushirikiano wa vyama vinne umewasaidia sana kupata nguvu mpya ya kuweza kulisukuma jahazi la siasa nchini. Anamaliza kwa kutoa wito kwa Watanzania sasa waamke wachunguze mwenendo au uendeshaji wa nchi hii chini ya CCM.

Iwapo watabaini hauwaridhishi kama yeye asivyoamini, wachukue hatua ili kuweza kuing’oa CCM kwa maana kama iking’oka na kukaa pembeni itajifunza kutoka kwa atakayekuwa ameingia madarakani.

Anasema atakayeingia madarakani atakuwa makini kwani atakuwa amejifunza kuanguka kwa CCM. huyo Ndiye Mtungurehi Mwanasiasa Kijana anayelilia Tume ya Uchaguzi amezaliwa wilaya ya Karagwe ni Benedekto Mtungurehi anamke Mmoja na watoto watano.



juu

Jengo la Wagonjwa wa nje na Kliniki (OPD/MCH)



Jengo la Wagonjwa wa nje na Kliniki (OPD/MCH) la Zahanati ya Zingiziwa iliyopo kata ya Chanika ambalo limejengwa kwa ufadhili wa TASAFII liliwekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.


Mratibu wa TASAF wa Manispaa ya Ilala ndugu Renatus Kihongo (wanne kulia), Mkaguzi wa Mifumo wa TASAF Ndugu Anna Chande (wa pili kulia), pamoja na wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi Mtaa wa Lukooni wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya madarasa 6 ya Shule ya Masingi Lukooni yaliyojengwa kwa mchango wa TASAF II.

MANISPAA YA ILALA



Mratibu wa TASAF wa Manispaa ya Ilala bwana Renatus Kihongo akiwa katika shughuli za kila siku za mipango ya TASAF ofisini kwake alipotembelewa na mwandishi na mwandishi wetu hivi karibuni.