Monday, April 2, 2007

THAMANI YA PESA KATIKA MADUKA YA KUUZA NA KUNUNUA CHENJI

Na Mobini Sarya

Thamani ya Pesa katika Maduka ya Kuuza pesa Jijini Dar es Salaam, 1 April 2007.
DUKA LA JAMANI FOREX

AINA YA PESA KUNUNUA KUUZAA

BAHARAIN DNR 3100 3250
KUWAIT DNR 4200 4450
SAUD RYL 300 340
QUATAR RYL 320 335
NEWZEAL $ 800 850
HONG K $ 140 160
PAKSTAN KP 17 19
CYPRUS PND 2300 2500
EGPT PND 150 200
SINGAPORE 750 800
THAILA BT 29 30
TAIWANI $ 29 30
CHINA 120 140

April 2, 2007 DUKA LA JAMANI FOREX

AINA YA PESA KUNUNUA KUUZA

USD $ 50,100 1230 1260
USD $ 5,10,20 1150 1260
US $ 1 1100 1260
UK.STERL.5,10,50 2350 2500
UK.1 2350 2500
EURO 1500 1680
CADS $ 950 1090
SWISS F. 900 1050
AUST.$ 850 1000
DHRS 320 355
D.KRNR 200 215
N.KRNR 180 200
S.KRNR 160 175
S.RAND 150 175
IND.RUP 26 29
KENYA SHS. 16 18.5
J.YEN 9 10.5
OMAN RYL 3100 3250
UGANDA SHS. 0.06 0.75


DUKA LA IMALASEKO 1 APRIL 2007

AINA YA PESA KUNUNUA KUUZA

US $ 50,100 1230 1260
US $ 5,10,20 1150 1260
US $ 1 1100 1260
UK.POUND 2350 2550
EURO 1400 1700
SWISS FRANC ---- -----

S.A.RAND 155 185
UAE. DH 300 370
K.SHS 17 19
OMAN RYL 3100 3400

GALAXY BUREAU DE CHANGE 1 April 2, 2007

AINA YA PESA KUNUNUA KUUZA

USD 50,100 1240 1265
UDD 5,10,20 1160 1265
AUST.$ 860 1010
STEARLING 2360 2550
EURO 1510 1710
OMAN RIAL 3150 3300
SWISS FRANC 920 1080
DIRHAMS 330 360
CANADIAN $ 1050 1130
S.A RANDS 162 185
JAPAN.YEN 9 11
DANISH KRNR 200 220
SWEEDISH KRNR 155 188
UGANDA 0.65 0.75
KENYA SHS 17 19

TAARIFA YA THMANI MFUKO WA UMOJA
KWA TAREHE 30 APRIL 2007

IDADI YA THAMANI THAMANI THAMANI BEI YA BEI YA
VIPANDE YA KIPAND YA KIPANDE YA MFUKO KUUZA KUNUNUA
VYA MFUKO TAREHE 29 TAREHE 30 KIPANDE KIPANDE
MACH 2007 MACHI 2007 (+ 1%) (-1%)
(EX-ID)* (EX-ID)*

TSHS. TSHS. TSHS TSHS TSHS

494,813,763.4958 116,7748 116.7641 57,771,535,624.5650 117.9216 115.5866

*(EX-ID) = PUGUFU KWA SHS 9/-GAWIO LILILOLIPWA TAREHE 29 September 2006.

Sunday, April 1, 2007

SERENGETI KILA MMOJA ANAWEZA KUHAMISHA MWENZAKE

Na Marco Shaweshi,Serengeti


CHAMA cha Walimu Mkoa wa Mara (CWT) kimewataka Maafisa Elimu wa Wilaya na wasaidizi wao kuhakikisha kuwa walimu wote WANATIMIZA wajibu wao sambamba na kupata haki zao kutoka kwa muwajili wao ambaye ni Serikali.

Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara Mwalimu Shadrack Tembe katika kikao chake alichofanya katika shule ya Msingi Nyamoko katika Kikao hicho alitumia fursa ya kuongea na walimu wa kata ya Nyamoko kwa niaba ya walimu wengine wa wilaya ya Serengeti.

Mwalimu tembe alisema baadhi ya migawanyiko ya walimu inasababisha Maafisa Elimu wengine kutokana na kujisahau kwao huwageuka walimu wenzao na kuanza kuwapinga wanapodai haki zao.

Mwenyekiti huyo aliwafananisha maafisa hao wanaowasaliti wenzao kama wafungwa waliopewa mikanda ya gerezani nakupewa madaraka kama nyampala anayejisahau na kuwapiga wenzake huku akiwatukana wafungwa tayari akiwa amesahau kuwa na yeye ni mfungwa.

Kauli ya Mwenyekiti huyo ilikuja baada ya walimu hao kwa niaba ya wenzao kumweleza kuwa walimu wa Serengeti, wamekata tama kwa mambo wanayofanyiwa katika wilaya hii, Mwalimu Julias Petro ngarawani alieleza adha aliyoipata alipouguliwa na Mke wake kuwa aliandikiwa Night Nne lakini alipomuona mkuu wake wa Idara ya Elimu alimuuliza huna akiba au hata rafiki akukopeshe hali iliyo msononesha baada ya kuambiwa hiyo na mtu aliyemtegemea.

Walimu hao walimueleza mwenyekiti huyo kuwa Serengeti uhamisho ni kama Biashara Mwalimun mmoja anaweza kuhama kwa kwa Mwaka mara Nne hadi tano ili mradi analipa teni ‘Percent’ kwa kila uhamisho anapewa.

Pia walisema kuwa Serengeti kila mmoja ofisi ya elimu anaouwezo wa kuandika nakutoa uhamisho hata mratibu anaweza kufanya hivyo kwa walimu katika kata na akapewa ruksa kuomba au kudai pesa ya uhamisho walimpa mfano uhamisho ulioandikwa na mratibu wa kata ya Kyambahi aliyetoa uhamisho kwa mwalimu kutokka Shule ya Nyichoka na kumpeleka shule ya Tumaini ambayo ni mpya ndani ya kata akadai huo ni uhamisho wa ndani.

WAZIRI ATEMBELEA TUME YA SAYANSI

Mobini Sarya

MAOMBI ya watu wanaotaka kuja kutafiti na kujifunza Satansi na Teknolojia hapa nchini kutoka nje imekuwa ikiongezeka kila Mwaka na kuipatia Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia Pesa za Kigeni.

hayo yalibainika kwenye Taarifa ialiyotolewaa kwa Waziri wa Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla alipokuwa akizindua Bodi mpya ya wajumbe wa Tathlitha ya saba ya tume hiyo, mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Tume jijini Dar es Salaam.

katika Taarifa hiyo Prof. Msolla aliambiwa na Tume hiyo kuwa wanafaunzi wanaotaka kuja kujifunza mambo ya Sayansi na Teknolojia hapa Nchini hulipa kiasi cha Dolla 100 na kwa wale wanaotaka kuja kufanya utafiti hapa nchini hutakaiwa kulipia dolla 500 kabla ya kupewa akibali na tume, pia katika hutakiwa akulipia Dolla 5o kwa ajili ya Maombi yao.

katika Hatua nayinaagine muombaji hutakiwa kutoa Taarifa kwenye kijiji alipofikia kufaanya utafiti na kila mwaka lazima atoe taarifa zake kwenye tume hiyo hadi siku anamaliza utafiti wake anatakiwa akupia kwenye tume kabla hajaondoka kwenda kwao.katika taarifa hiyo ilielezwa kuwa 60% ya watafiti wanalenga kutafiti katika Misitu na wanyama pori.

akizindua Bodi hiyo Profe.Msolla alisema kuwa Wizara yake inampango wa kuanzisha Mtandao mwingine Utakaojulikana kama Tanzania Education Network (TEN) utakaounganisha vyuo vyote nchini pamoja na Tafiti zote.

pia alaitaka tume hiyo kupitia vipengele mbalimbali kuona vilivyopitwa na wakati katika sheria namba saba ya Mwaka 1986 iliyoianzisha kwani ni miaka mingi mno imepita ili viondolewe.

Profesa Msolla alisema kuwa Wizara inaandaa Muswaada wa Sera ya utafiti wa Mendeleo ambao ukikamilika utapelekwa bungeni ili kupitishwa, "Maatumizi ya Sayansi na Teknolojia hayajajitokeza waziwazi katika kuleta Maendeleo ya watanzania, Tume hii ishauri Serikali iweze kuwasaaidia wanafunzi wanaojiunga na chuo kikuu wasomee Sayansi"alisema Msolla.

TLP MOTO KUWAKA TENA? LIPUMBA AALIKWA !

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama cha TLP unaotarajiwa akufanyika Kesho jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Agostine Lyatonga Mrema alilimbia Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Kwamba uamzi wa chama chake kumliaka Lipumba kuwa Mgeni rasmi kataiaka makutao huo ni muendelezo wa Mshikamano imara wa kisiasa kati ya vyama hivyo viwili.

Mrema alisema kuwa utafanyika kwa lengo la kujadili la kujadili hali ya kisiasa nje na ndani ya TLP chini ya uongozi wake halali unaotambulika katika ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ambao ni Yeye mwenyekiti ,Katibu mkuu John Komba na Makamau wawili ,Lumum Kasyupa kutoka Bara na Hamad Mkadam wa Zanzbar.

aidha katika hatua nyingine Mrema alaisema kuwa kama kuna wanachama wadai kuwa hakuna mkutano kwa sababu kesi ipo Mahakaamani, sio kweli kwani Mahakama haijawahi kuwazuia Vuiongozi wa TLP wasijishughulishe na shughuli za za kisiasa ndani ya chama hicho.

akizungumzia zaidi ugeni wa Lipumba katika mkutano huo utakaofanayaika kesho Mrema alisema kuwa hiyo ni njia moja ya kuimarisha Ushirikiano kuelekea kwenye umoja kamili kwani amekuwa akiunga mkono akampeni za Chama cha CUF, Mwaka jana alishikiana nao huko Zanzibar na Hivi karibuni aliwasaidia kupiga kampeni huko Tunduru kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge.

hali hiyo ndio imefanya kumwalika Lipumba kwenye mkutano wao wa kujadili maswala mbalimbali ya Chama hicho, ili kufanya wanaCUF kuwa karaibu na wanaTLP hali itakayowafanya kufikia malengo wanayotarajiwa kati ya vyama hivyo na kusisitiza kuwa mkutano huo lazima utafanayika bila kujali kuwa kunawatu wanataka kwenda Mahakamani kuupinga.

PESA ZIMEUWA HAKI NA UMAARUFU UMEZARAU MAHAKAMA

Sheria za nchi zinapotiwa kitanzi!

Na Mobini Sarya

SHERIA za nchi zimedharauliwa, Mahakama Kuu imebakwa na nchi imevuliwa nguo na kubaki uchi huku utawala wa sheria ukibaki na aibu kubwa isiyositiriwa, na iliyoweka historia katika taifa letu, huku watawala wakibaki na kigugumizi wasipate la kujibu baada ya kuonekana mtunga sheria ndiye mvunja sheria.
Hayo matukio yote yamekuja baada ya aliyekuwa kiongozi wa umma kushitakiwa kwa kosa la kuua kisha kuachiwa kwa dhamana ndani ya siku 120, kwa madai kuwa aliua bila kukusudia na kuwaacha watu wakijiuliza maswali mengi kuhusu jinsi kiongozi huyu alivyoshughulikiwa haraka na kutoka kama kweli taratibu zilifuatwa.
Aibu imekuwa kubwa zaidi na isiyofutika baada ya kiongozi huyo aliyewahi kuwa mbunge na mtunga sheria za nchi kupitia Jimbo la Ilala na baadaye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kupitishwa kwenye mlango wa majaji wakati anaingizwa Mahakama Kuu kupewa dhamana, kitu ambacho hakijawahi kutokea, huku akipewa ulinzi sawa na rais.
Katika kuonyeha kuwa ‘mtunga sheria ndiye mvunja sheria’ na sheria za hapa Tanzania hutungiwa ‘wendawazimu’ tu huku wenye akili wakizivunja, ndugu wa mtuhumiwa wa mauaji waliwageuza waandishi wa habari waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo kuwa ndio watuhumiwa na kuanza kuwaadhibu mithili ya vibaka, wakisaidiana na askari polisi!
Matukio hayo waliyoyafanya si mara yao ya kwanza, ilikuwa ni kuendeleza ufedhuli waliokuwa wameanza nao tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, pale walipoanza kuwazuia waandishi wa habari wasifanye kazi zao, kwa kuwatukana na kuwamwagia maji ya upupu, na siku zingine kumfunika mtuhumiwa kanga au kumletea kofia aina ya ‘pama’ ili ajifunike kuepuka aibu ya jamii, baada ya ‘kumuua bila kukusudia’ dereva wa daladala, Hassan Mbonde, ambaye uhai wake ulikatishwa na risasi zilizotua kichwani.
Katika kesi hii inayomkabili kiongozi wa umma, tusingependa kuijadili kutokana na kuwa ipo mahakamani, lakini jinsi mwenendo wake unavyokwenda na matukio yaliyoambatana nayo, hiyo kesi hakuna kizuizi chochote kinachoweza kuzuia isiandikwe wala kuzungumzwa mitaani, kwani hadi sasa kila mmoja anayeifuatilia anajua kinachofanyika au kuendelea.
Mwenendo mzima wa kesi umekuwa ukiacha maswali mengi kuliko majibu, huku kila kukicha haki na sheria vikikiukwa kwa uwazi bila kuhojiwa, na hali ilianza kushangaza katika Mahakama ya Kisutu pale ndugu wa mtuhumiwa walipofanikiwa kumfunika kanga ili asipigwe picha huku polisi wakichekelea, maswali yaliyoibuka hapa ni kwamba ndugu zake walipataje nafasi ya kumkaribia mtuhumiwa wa mauaji kiasi hicho ikiwa mahabusu wa kawaida tu ndugu zao wanazuiliwa kuwasogelea pale wanapofikishwa mahakamani?
Je, katika hili polisi walikuwa wanajua wajibu wao kwa kuwaruhusu ndugu wa mtuhumiwa wa mauaji kumsogelea, wangewezaje kumzuia mtu mwingine ambaye angejipenyeza kama ndugu wa mtuhumiwa kumbe akiwa na lengo la kumchoma kisu mtuhumiwa, ilikuwaje polisi katika Mahakama ya Kisutu waendele kuwashuhudia ndugu wa mtuhumiwa wakiwafanyia waandishi vitendo vya dharau hadi pale hakimu alipoingilia kati na kusema wazi kuwa polisi walikuwa wamezembea kupita kiasi?
Kama kuna mkono wa mtu unatumika katika kesi hii, basi ulianza kutumika kikamilifu katika Mahakama ya Kisutu na polisi walilishwa limbwata wakawa kama chatu aliyemeza mzoga na kulala asijue la kufanya huku wakiangalia bila aibu vitendo vya uvunjwaji wa sheria za nchi.
Kama hiyo haitoshi, inafahamika wazi kuwa mbele ya pesa hakuna kinachoshindikana, hali ilikuwa mbaya zaidi walipomfikisha mtuhumiwa Mahakama Kuu, kwani waliamua kutumia mlango unaotumiwa na majaji pekee kwa kumpitisha mtuhumiwa, wakati wanajua kuwa huo mlango hata mfanyakazi wa mahakama hiyo haruhusiwi kupita, mlinzi wa mahakama alipojaribu kuwazuia wakamnyanyasa kwa kumsukuma, hadi wakafanikiwa kutizima azima yao.
Kitendo kilichowakasirisha majaji wa mahakama hiyo na kuamua kumtaka Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, atoe maelezo, ndani ya muda ambao mtuhumiwa alipewa dhamana katika Mahakama Kuu na ndugu zake waligeuza eneo hilo kuwa uwanja wa masumbwi kwa kuwaadhibu waandishi mbele ya Mahakama ya haki huku wakiimba kuwa nchi hii ni yao, kama waandishi walikuwa hawawajui watajua sasa, na kuwajeruhi waandishi kadhaa.
Baada ya kuangalia mwenendo mzima wa hii kesi, wananchi wameingiwa na hofu kama kweli haki itatendeka kuhusiana na kesi hii.
Siku chache tu baada ya Ditopile kushikiliwa na polisi kwa kuua dereva Novemba 8 mwaka jana, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Rais Kikwete amekiri kuwa Dito alikuwa mwanamtandao wa kuaminika, amesononeshwa kwa tukio hilo, na hajui afanye nini, akasema anaachia sheria ifanye kazi yake.
Kutokana na Tanzania kuwa na mfumo mbaya wa sheria za kulindana kumesababisha mtuhumiwa wa mauaji kubadilishiwa kesi nje ya Mahakama Kuu kupitia dirisha la nyuma na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia kwa muda wa siku 120 tu.
Huku watu waliokamatwa kwa kuhisiwa tu wengine kwa makosa madogo madogo wamesota jela na wengine kufia mahabusu bila kesi yao kusikilizwa wakiambiwa kuwa upepelezi bado haujakamilika, na kunyimwa dhamana bila maelezo ya msingi huku wakinyimwa nafasi ya kuonana na ndugu zao, wapo wanaolalamika kunyimwa huduma ya matibabu kutoka kwa ndugu zao.
Kuachiwa kwa dhamana kwa mtuhumiwa wa mauaji kwa upande wa pili kumefungua njia ya ukombozi na mapinduzi kutokea magereza, tukio hilo limehitimisha yale manung’uniko ya muda mrefu kuwa magereza Tanzania ni sehemu ya kuwatunzia walalahoi huku wenye nguvu wakiachiwa bila kutiwa hatiani hata kama kuna ushahidi wa wazi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa kwa kukusudia.
Hapa Tanzania imekuwa ni kawaida kwa tajiri anayetenda kosa, mfano la kuua kuambiwa kajeruhi, lakini mlalahoi akijeruhi anaambiwa kaua, kibaka anauawa, mzururaji anaandikiwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kunyimwa dhamana wengine kubambikiziwa kesi wasizozijua huku wakiambulia kipigo cha maumivu ili wakubali makosa bandia.
Mgomo wa siku kadhaa wa mahabusu uliotawala katika magereza ya maeneo mbalimbali nchini, umeashiria mwanzo mpya wa mapinduzi ya haki na ni mwanzo wa aibu kubwa kwa taifa kama letu linalojivunia utawala bora wa sheria na kulinda haki za binadamu.
Wiki za hivi karibuni zimegubikwa na aibu kubwa kwa taifa, mahabusu wakitaka haki ambayo wameikosa siku nyingi, wapo waliokamatwa kwa kuiba kuku wamekaa rumande kwa muda mrefu wakiambiwa upelelezi bado haujakamilika, lakini wengine wanakamatwa kesho yake kwa mauaji au kulawiti watoto wanadhaminiwa.
Tumesikia katika gereza la Isanga, Dodoma wafungwa waliokamatwa kwa kosa la unyang’anyi baada ya kukaa rumande bila dhamana sasa wamebadilishiwa kesi na kuwa ya kuua na kule Serengeti Polisi walikamata madumu ya maji wakadhani ni mafuta ya dizeli wakambambikizia mwananchi mmoja wakakaa naye kituo kikuu cha polisi kuanzia asubuhi hadi jioni bila dhamana wakitaka rushwa hadi mwenye madumu alipojitokeza jioni na kuomba madumu yake, polisi wakashtuka kuwa kumbe ndani kulikuwa na maji.
Kesi hii ya Ditopile imetufanya tufahamu kuwa kumbe kuna wananchi na ‘walanchi’, tumefahamu kwamba kuna watu wameua lakini hata mahabusu wengine hawakufika, miongoni mwao ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoani Dar es Salaam (RCO), Abdallah Zombe, upelelezi wake ulikamilika ndani ya siku 150 yeye yupo rumande.
Mwingine ni mtoto wa Balozi Rupia aliyetuhumiwa kwa kosa la mauaji na kuachiwa baada ya siku tisa.
Aidha, mtoto wa Kingunge Ngombale-Mwiru pia inadaiwa aliwahi kuua, lakini hata hakufika mahakamani, na mtoto wa Sumaye naye alituhumiwa kwa mauaji lakini wote hawa wanatesa uraiani.
Kutokana na mwenendo usiofaa wa kuendesha kesi nchini, wananchi wote wanapaswa kuungana kupinga haki kutolewa kwa kubaguana, pia tunapaswa kuungana na mwanaharakati Christopher Mtikila, kuiomba mahakama kufuta nafasi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, kwani inaonekana ipo kwa ajili ya kuwalinda vigogo wachafu, kama kuna sheria mbaya ya nchi hii inapaswa kulaaniwa ni sheria inayomtambua Mwendesha Mashitaka (DPP).
Mwendesha Mashitaka ni mtu anayebaka haki za majaji kutokana na kupewa uwezo wa kuruhusu kesi iende mahakamani au isiende na kupewa uwezo wa kuibadili kama anavyopenda, na hii nafasi ilianzishwa na wakoloni ili kujilinda dhidi na ufedhuri waliokuwa wanawafanyia Waafrika, hata walipokabidhi madaraka, wamewaachia watawala wetu ndio wanaitumia kujilinda wakituhumiwa kuwa wamekula rushwa, wanamkimbilia mwendesha mashitaka anawabadilishia kesi.
Mkurugenzi wa Mashitaka anaingilia uhuru wa mahakama na kuwafanya majaji wawe vibaraka wake kama yeye alivyo kibaraka wa viongozi wa serikali, haiwezekani abadilishe mashitaka yawe ya kuua bila kukusudia nje ya mahakama halafu anawapelekea majaji wa Mahakama Kuu wagonge muhuri wa kumpa dhamana mtuhumiwa bila kuona kesi yake kwanza kama ni hivyo basi hata dhamana angetoa yeye.
Sheria hii anayoitumia DPP kama angekuwa anaitumia kwa wananchi wote kusingekuwapo msongamano wa wananchi mahabusu, kwani wengi wametenda makosa bila kukukusudia, tangu waandishi wamepigwa na kuharibiwa vifaa vyao polisi wameshindwa kuwachukulia hatua wale waliohusika, kitu kinachotushawishi tuamini kuwa lile tukio liliratibiwa kikamilifu na polisi.
Kesi hii imetufundisha mambo mengi, imetuonyesha jinsi ndugu wa watawala wanavyotenda makosa kwa makusudi wakitegemea kuwa watasaidiwa na wakubwa wao, na jinsi walivyoweza kuidhalilisha serikali ambayo imechaguliwa na wananchi, lakini hii haitavumilika siku zote, waandishi wameonyesha nia ya mapambano, pia mahabusu wamebipu, tunawasubiri wananchi waungane na wanaharakati kufanya maandamano ya kupinga kubaguliwa wanyonge na kukandamizwa haki zao.
Wiki ijayo nitaeleza jinsi mwendo mbaya huu wa kesi ulivyoanza kujionyesha kuwa mnyonge hana haki, nitaonyesha jinsi kiongozi wa nchi anavyotakiwa awe asiyekuwa na ubia na mtu kwenye madaraka yake.
Kwa mara ya kwanza historia ya taifa letu imetiwa doa kubwa na viongozi wenyewe serikalini, watuhumiwa wahukumiwe kulingana na sheria si utashi wetu kisiasa!

Web.www.mobinday.blogspot.com email.mobinsons@yahoo.com

Mwisho