Tuesday, December 5, 2023

Mikopo ya Kausha damu riba yake ni asilimia 3.5 tu

Ukikopa laki unalipa riba 3500

Na Mobini Sarya, Tanpresstz

Waziri wa Fedha,Mwingulu

AJABU na kweli imeelezwa kuwa ile mikopo ya haraka ambayo inatolewa kwenye vibanda maarufu kama kausha damu au mikopo umiza riba yake ni asilimia 3.5 tofauti wanavyo fanya kwasasa.

Akitoa elimu kwenye kongamano la akinamama Women Talk Chalinze, Afisa Maendeleo Wilaya ya Chalinze, Ramadhani Mumba, alisema kuwa hiyo ni kwa mjibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya Mwaka 2020 na kanuni zake.

“wale wakopeshaji wadogo mnaowaita kausha damu riba yake inapaswa kuwa asilimia 3.5 kwa mwezi yaani ukikopa laki moja unalipa 3500 kwa mwezi sio vingenevyo, atakayekiuka mkataba huo faini yake inafikia milioni 20”alisema Mumba

Aliwashauri wajasiriamali kabla ya kuchukua mkopo huo kuomba kwanza mkataba na kuusoma vizuri kabla ya kutia saini, kama upo kinyume wajulishwe maafisa maendeleo wa jamii waliopo kata za jirani ili wachukue hatua za kisheria.

Ukikutwa unafundisha 'vicoba' bila leseni faini Mil.1

 Ukikutwa unafundisha 'vicoba' bila leseni faini Mil.1

Na Mobini Sarya,Chalinze

Waziri wa Fedha Mwingulu Nchemba
Kwa mjibu wa Sheria ya huduma ndogo za kifedha wale wanaojiita walimu wa vikundi zamani Vicoba wanapaswa kusajiliwa halamashauri na kupewa leseni kama mapromota.

Kwa mjibu wa sheria hiyo ya Mwaka 2019/20 endapo mwalimu atakutwa akifanya hivyo bila kibali atapigwa faini ya shilingi milioni 1 au kwenda jela fasta.

Afisa Maendeleo Wilaya ya Chalinze,Ramadhani Mumba, tayari wamesajili mapromota watano ambao wameitikia sheria hiyo ambapo gharama ya leseni ni shil.50,000 wengine zaidi ya 20 wanasubiri kupatiwa leseni.

Vicoba vimefutwa rasmi, ukishiriki bila kibali mil.20 faini

Walimu wa vikundi nao kupewa leseni kama mapromota.

Na Mobini Sarya, Tanpresstz

Wazari wa Fedha Mwingulu Nchemba
 SHERIA imefuta rasmi vikundi vinavyoitwa,Village Community Bank maarufu kama Vicoba, sasa vinaitwa Community Microfinance Group kifupi (C.M.G) ukikutwa unashiriki ambacho hakijasajiliwa jela au faini.

Akitoa elimu kwenye kongamano la akinamama Women Talk Chalinze, Afisa Maendeleo Wilaya ya Chalinze,Ramadhani Mumba, alisema kuwa hiyo ni kwa mjibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya Mwaka 2020 na kanuni zake.

“Vikundi vya vicoba vimebadilishwa jina kutokana Village Community Bank na sasa vinajulikana kama vikundi vya kijamii vinavyotoa huduma ndogo za kifedha CMG na uendeshaji wake unafuata sheria kwahiyo lazima visajiliwe,

….. vicoba ni kitu kikubwa, kwa mjibu wa sheria hiyo ukikutwa unashiriki kikundi ambacho hakijasajiliwa faini kuanzia mil.3 hadi 20 au jela miezi 6”alisema Mumba.

Aidha wale wanaohamasisha, au walimu wa vikundi wanapaswa kusajiliwa sheria inawatambua kama mapromota wanapewa leseni kwa shilingi 50,000 ukikutwa unafanya kazi hiyo bila leseni faini yake milioni 1.

        

Monday, December 4, 2023

Mtoto wa miaka 4 adaiwa kubakwa Mogo, Kipawa

Njama za kupotosha ukweli zapangwa atoroshwe.

Na Tanpresstz,Kipawa

mtoto wa miaka 4 anayedaiwa kubakwa
VITA ya ukatili wa kijinsia inazidi kuwa ngumu kutokana na matukio ubakaji kufichwa na familia za wahanga likiwemo lililotokea mtaa wa Mogo kata ya Kipawa kwa mtoto wa miaka 4 kubakwa.

Taarifa zilizofikia shirika la habari  vijijini,Tanpresstz zinahabarisha kwamba kumekuwepo na njama kubwa za kutaka kufifisha tukio hilo lililotokea Disemba mosi 2023 kuripotiwa kituo cha Polisi Staki shari Disemba 2.

taarifa ya kitabibu iliyopelekwa kituo cha Polisi sitaki Shari ambayo inadai alichezwa tu kwa maelezo aliyopewa mlezi na Polisi.

Akizungumza na Tanpresstz Katibu Elimu,Malezi na Mazingira (EMAU) Tawi la Mogo kupitia Jumuiya ya Wazazi (CCM) Forget Chakupewa anasema kuwa tukio hilo walilipata siku zikiwa zimepita huku muathirika akiwa ndani.

“Sisi kama viongozi wa Jumuiya tulipokea taarifa siku ikiwa imepita tulipofuatilia tukakuta huyo mtoto anaugulia maumivu huku walezi wake wakiendelea kumkanda na maji ya moto tukachukua jukumu la kumpeleka Polisi akapatiwe matibabu”anasema Forgeti.

 
Hata hivyo juhudi za kupotosha ukweli zilianza baada ya Polisi kutoa fomu namba 3, PF3 kwa lengo la kwenda kumpima hospitali ambapo mjumbe wa shinda alitakiwa kuongoza msafara lakini aliyenda peke yake mlezi wa mtoto ambaye sasa anakanusha mtoto wake kubakwa,

“Mtoto wangu hajawahi kubakwa, nashangaa anayevumisha hayo mambo nikimjua atanilipa anatupa presha mimi na mama yangu kwani watu wanazidi kumiminika hapa, nimeenda hospitali wamesema alichezewa tu na watoto wenzake”alifoka Cesilia Philipo ambaye anadai ni mlezi wa mtoto huyo.

Wakati akiwatuhumu viongozi wa jumuiya ya wazazi kwamba ndio wanasambaza taarifa hizo, katibu wa shina namba 9 lilipofanyikia tukio hilo, Geofrey Rugeye anasema baada ya kupata taarifa hiyo alifika kwenye familia hiyo siku ya Ijumaa jioni akakuta mtoto amelala kwenye mkeka, akawaambia wampeleke kituoni akatibiwe.

“Leo wanakana ,wanajaribu kuficha ukweli Jumamosi iliyopita tulipokuja hapa walikuwa wanasema bibi yake alipoamka usiku alikuta mtoto amelala akajiachia huku mbegu za kiume zinatoka sehemu za siri akamuita mpangaji jirani akaja akadhibitisha kwamba ni kweli kesho nyake wakaanza kumkanda na maji ya moto”amesema mjumbe kwa masikitiko

Aidha katibu wa Jumuiya ya wazazi tawi la Mogo yeye anasema alikuwa amesafiri aliporudi Ijumaa jioni akaambiwa hiyo familia na mhanga walifika kwake wanataka huyo mtoto awaonyeshe aliyembaka na kumharibu sehemu za siri.

“Mimi nashangaa wanasema kwamba mimi ndio natangaza, wakati wenyewe ndio waliyatoa nje wanaona yameanza kushughulikiwa wanataka kuficha ukweli huku wakipanga kumtorosha muathirika,..hata hiyo ripoti ya daktari hatujui kama ina usahihi”alisema Katibu wazazi.

Sesilia Philipo Mlezi wa muathirika anayekanusha mwanae kubakwa

Tanpresstz imefanikiwa kuona taarifa ya uchunguzi kutoka kituo cha Buguruni ambayo daktari ameandika kwamba hakuona damu ikitoka kwenye sehemu za siri bila kujali kwamba huyo mtoto ameogeshwa tangu Disemba Mosi hadi leo Disemba 4 damu haiwezi kuonnekana.  

katibu wa Jumuiya ya Wazazi anasema kwamba "Wanasema amechezewa tu na watoto wenzake hivi hii inaruhusiwa, ..watoto wenzake wangemchezea akandwe na maji ya moto, au kwasababu mtoto huyo ni wa kambo hana mtetezi? na kuna taarifaa kwamba anataka kutoroshwa"analalama  

baadhi ya watu waliozungumza na Tanpresstz bila kutaja majina yao wameomba wadau wa haki za binadamu wamchukue mtoto wampeleke kwenye vipimo zaidi kwani anaonekana kuugulia ndani bila msaada wowote, huku walezi wake wakikanusha taarifa za kubakwa.

Labels:

Sunday, December 3, 2023

Arafa Kikwete kuibeba Taasisi ya Women Talk Chalinze

Mke wa mbunge wa Chalinze ajitosa vita ya ukatili wa kijinsia, Women Talk Group wamkaribisha awe mshauri wao.

Na Mobini Sarya,Tanpresstz

Bi Arafa Kikwete ambaye ni mke wa Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma, Ridhiwan


TAASISI ya umoja wa wanawake (WOMEN TALK CHALINZE) imemuomba Arafa Ridhiwani Kikwete, eneo kwa ajili ya kuweka makazi ya watoto wenye uhitaji maalum, ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti wa taasisi hiyo,Kulwa Mwakapande kwenye kongamano la wanawake linaloandaliwa na taasisi hiyo kila Mwaka maeneo ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Bi, Arafa Ridhiwan Kikwete

“Tunayo ombi kwako na kwa mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,ili tuweze kutimiza malengo yetu tunaomba kupatiwa eneo maalum ,kwa ajili ya kuweka makazi ya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kutimiza ndoto zao”alisema maadam Mwakapande

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo lililofanyika Disemba 2,2023,Lugoba alikuwa ni Bi.Arafa Ridhiwani Kikwete ambaye ameipongeza taasisi hiyo kwa shughuli zake za kusaidia makundi maalumu wakiwemo watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

“Nileeteni mahitaji yenu, ni vitu gani mnataka mkatoe msaada na mimi nitawasaidia kwa kushirikiana na mme wangu (mbunge wa Chalinze) kipindi hiki shule zinaelekea kufungwa na nyie mnasema mnasaidia wanafunzi ni vyema nikapata mahitaji yenu mapema ili tuweze kuwasaidia”alisema Bi.Arafa Kikwete.

Aliwaasa akinamama hao kuzingatia kikamilifu malezi ya watoto yanayostahili ili kupunguza ukatili wa kijinsia ‘tusiache jukumu letu, msingi wa kulea watoto tusimuachie mtu mwingine’aliwaasa.

Akisoma risala mwenyekiti wa kongamano hilo, Kulwa Mwakapande kuwa umoja wao ulianzishwa Mwaka 2021 ukiwa  na wanawake 50 wakiwa na lengo la kuwakutanisha wanawake ili kujadili mambo yao na kuwagusa akina mama na watoto wenye mazingira magumu kwa kuwapatia misaada mbalimbali.

“Tulikuwa na lengo la kuwakutanisha akina mama ili kujadili mamabo yetu na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na sasa hivi wanawake wameongezeka na kufikia 200 huku tukiendelea kusambaa kata zote za Chalinze”alisema Maadam Mwakapande.

 Aidha katika kutekeleza malengo yao wamefanikiwa kutembelea vituo vya watoto yatima kama vile Hope Disability na KULEANA kinachosimamiwa na Askof.Rommy, huku wakifanikiwa kuandaa maadhimisho ya Mtoto wa AFRIKA yaliyofanyika Juni 14,2023 Halmashauri ya Chalinze.

“Pia tumeweza kufanya makongamano ya wanawake kwa miaka miwili mfululizo yaani 2021 na 2023 na kuwapatia wanawake 15 tuzo kutokana na kujituma kwao huku tukianzisha kundi dogo ndani ya kundi kubwa linalojulikana kama  ACTIVE MAMAZ ambalo limesajiliwa na kufungua akaunti kwa lengo la kujiwekea akiba ya 50,000 kila mwezi”alisema Maadam Mwakapande.

 

Labels: