Tuesday, December 4, 2007

Ukaguzi viwanja vya ndege kuimarishwa


WIKI YA USAFIRI WA ANGA


na Mobini Sarya



Banda lililokuwa katika kiwanja cha Ndege Julias Nyerere, siku ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya usafiri wa Anga

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imetakiwa kulipa kipaumbele suala la usalama wa viwanja kwa hakikisha wanawakagua abiria wote bila kujali uraia wala wadhifa ili kukabiliana na ugaidi.
Aidha, wamiliki wa makampuni ya ndege wametakiwa kushirikiana na TAA katika suala la ukaguzi kwa kuwa usalama unapokosekana kiwanjani waathirika ni wananchi.



hilo ni moja ya mabanda yalikuwa uwanjani hapo kwa ajili ya maonyesho ya nane yaliyoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi Viwanja vya ndege TCAA
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Miundombinu, Aron Kachema, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa anga.



HAPO MGENI RASMI katika maadhimisho hayo ARON KACHEMA ambaye ni mkurugenzi wa utawala Miundombinu akikata keki ya ndege kuasherehekea siku ya kuzaliwa TAA MIAKA 8 ILIYOPITA

Akihutubia katika maadhimisho hayo, Kachema aliwaambia wamiliki wa makampuni ya ndege kuwaelimisha abiria na wafanyakazi wao kuhusu ukaguzi kuwa ni sehemu ya maisha na shughuli za anga duniani kote.



JAMAA akipokea Keki baada ya kukatwa ,huyo ni mkuu wa Viwanja wa MR.Tesha

“Waelimisheni abiria na wafanyakazi wenu kwamba kukaguliwa si adhabu au kudhalilishwa, bali ni sehemu ya maisha ya kila siku katika shughuli za anga duniani kote,” alisema Kachema.


Katika maadhimisho hayo Kachema alizindua rasmi kamera za usalama (CCTV) na njia mpya ya kupita abiria wanaounganisha safari.




Naye Mkurugenzi wa TAA, Prosper Tesha, alisema mamlaka hiyo inatimiza miaka minane tangu kuanzishwa na kukabidhiwa majukumu ya kuendesha na kusimamia viwanja vya ndege.



baadhi ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo

TAFITI ZA WATAFITI: Teknolojia

kutoka angani


Na Mobini Sarya,
Mashirika ya habari

kama ulikuwa unapenda kuwasiliana na

ndugu yako kwa njia ya simu ukiwa

angani lakini inashindikana kutokana

na tahadhari iliyowekwa kuwa inaweza

kuingilina na mawasiliano ya ndege

kwasasa haitakuwa tatizo.

kwani Dunia imeendelea kupiga hatua

kubwa katika suala la teknolojia na

mawasiliano baada ya wanasayansi

kugundua namna ya kuepusha mawimbi ya

sauti wakati abiria wa ndege anaongea

na simu kuingiliana na mawasiliano ya

ndege.

Wataalam hao wameweza kufanya

Mabadiliko ya teknolojia yatawezesha

abiria kutumia simu za mkononi wakati

ndege ikiwa angani.


Tekinlojia mpya Simu sasa kupigwa


Hivi sasa abiria wa ndege wanaweza

kutumia simu zao za mikononi

wanaposafiri katika anga za Ulaya kwa

majaribio.

Mipango imeandaliwa na nchi wanachama

wa Umoja wa Ulaya kwa kutumia

teknolojia inayowezesha simu za

mkononi kupigwa bila kusababisha

athari zozote za mawasiliano ya ndege.

kutokana na hatua hiyo ya kiteknolojia

Wasimamizi kote barani Ulaya

wameanzisha mjadala kuhusu uwezekano

wa kutumia kwa teknolojia hiyo dunia

kote bila kuleta madhara.

Endapo teknolojia hiyo itaidhinishwa,

abiria wanaosafiri katika ndege

wataweza kuwasiliana na ndugu zao

kutokea angani wakati ndege ikiwa

umbali wa mita 3000 juu.

hata hivyo Mashirika ya ndege

yatahitaji kuamua endapo yanataka

kutumia teknolojia hiyo na endapo

kibali kitatolewa na idara za

usimamizi katika nchi husika.


Je Teknolojia hii inafanyaje kazi?


Kiwango cha ushirikiano kati ya nchi

za Ulaya itakuwa na maana kwamba simu

za mkononi zinaweza kupigwa wakati

ndege zikiruka katika anga za mataifa

ambayo bado hayajaidhinisha

utekelezaji wa teknolojia hiyo.

Kwa wakati huu matumizi ya simu za

mkononi yamepigwa marufuku kwenye

ndege kwasababu ya kuwepo kwa ushahidi

kwamba zinaweza kuingilia na kuvuruga

mawasiliano na mifumo ya kuongozea

ndege.

Utafiti uliochatangazwa mwaka 2003 na

CAA ulipata matokeo kwamba mawimbi ya

simu za mkononi yanavuruga uongozaji

wa ndege kwa takriban nyuzi tano.

Hatua tofauti

Msemaji wa taasisi ya usimamizi wa

mawasiliano nchini Uingereza ya Ofcom,

ameeleza kwamba bado kuna mambo

kadhaa yanatakiwa kurekebishwa kabla

ya idhini ya mwisho haijatolewa

kuwezesha mpango huo kusambazwa

Duniani.

Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa

anga ya Uingereza (CAA), na ile ya

Ulaya, European Aviation Safety

Agency, yanafanya kazi kwa pamoja

kuhakikisha kwamba usalama wa ndege na

abiria unazingatiwa kabla ya mifumo

hiyo kuanza kutumika.


kwa muda mrefu Mawasiliano ya simu za

mkononi katika ndege imekuwa kikwazo

kwa abiria wengi hatua ambayo ilikuwa

ikilalalamikiwa.


Taasisi ya usimamizi wa ndege imesema

kwamba teknolojia hiyo inaweza kuanza

kutumika mwaka ujao wa 2008.

Mfumo unaopendekezwa unatumia kituo

cha ndani ya ndege ambacho kinarusha

mawimbi kwenda simu za mkononi za

abiria.

Vituo vya kurushia mawimbi vya simu za

mkononi vilivyoko ardhini vitapokea na

kusambaza mawasiliano kwa njia ya

satellite kuunganisha na vile vya

ndani ya ndege.Simu zitatozwa kupitia

mitandao ya kawaida ya abiria.

Kwa kuanzia mfumo wa simu utakaotumika

ni 2G pekee, japokuwa Ofcom imesema

endapo kutakuwa na mafanikio, kutakuwa

na uwezekano wa kuzindua kwa mfumo wa

kisasa zaidi wa 3G na mingineyo mipya

itakayoundwa siku za usoni.


Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa

internet. mobinsons@yahoo.com

Labels:

Monday, December 3, 2007

Simu sasa kupigwa kutoka angani

ndege ikiwa angani.
Hivi sasa abiria wa ndege wanaweza

kutumia simu zao za mikononi

wanaposafiri katika anga za Ulaya.
Mipango imeandaliwa na nchi wanachama

wa Umoja wa Ulaya kutumia teknolojia

inayowezesha simu za mkononi kupigwa

bila kusababisha athari zozote za

mawasiliano ya ndege.



mfumo huo wa simu jinsi utakavyokuwa ikiwa BINADAMU ataruhusiwa kupiga simu ndge ikiwa angani

Mabadiliko ya teknolojia yatawezesha

abiria kutumia simu za mkononi wakati
Wasimamizi kote barani Ulaya

wameitisha mashauriano kuhusu

uwezekano wa kutumika kwa teknolojia

hiyo.

Endapo itaidhinishwa, huduma hiyo

itawezesha simu kupigwa tokea angani

wakati ndege ikiwa umbali wa mita 3000

juu.

Mashirika ya ndege yatahitaji kuamua

endapo yanataka kutumia teknolojia,

endapo ruksa itatolewa na idara za

usimamizi za nchi husika.

Je mfumo huu unafanyeje kazi?

Kiwango cha ushirikiano kati ya nchi

za Ulaya itakuwa na maana kwamba simu

za mkononi zinaweza kupigwa wakati

ndege zikiruka katika anga za mataifa

ambayo bado hayajaidhinisha

utekelezaji wa teknolojia hiyo.

Kwa wakati huu matumizi ya simu za

mkononi yamepigwa marufuku kwenye

ndege kwasababu ya kuwepo kwa ushahidi

kwamba zinaweza kuingilia na kuvuruga

mawasiliano na mifumo ya kuongozea

ndege.

Utafiti uliochatangazwa mwaka 2003 na

CAA ulipata matokeo kwamba mawimbi ya

simu za mkononi yanavuruga uongozaji

wa ndege kwa takriban nyuzi tano.

Hatua tofauti

Msemaji wa taasisi ya usimamizi wa

mawasiliano nchini Uingereza ya Ofcom,

ameeleza kwamba bado kuna hatua kadhaa

kabla ya idhini ya mwisho haijatolewa

kuwezesha mpango huo kusambazwa

kikamilifu.

Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa

anga ya Uingereza (CAA), na ile ya

Ulaya, European Aviation Safety

Agency, yanafanya kazi kwa pamoja

kuhakikisha kwamba usalama wa ndege na

abiria unazingatiwa kabla ya mifumo

hiyo kuanza kutumika.


Mawasiliano ya simu za mkononi katika

ndege imekuwa kikwazo kwa abiria

wengi.


Taasisi ya usimamizi wa ndege imesema

kwamba teknolojia hiyo inaweza kuanza

kutumika mwaka ujao wa 2008.

Mfumo unaopendekezwa unatumia kituo

cha ndani ya ndege ambacho kinarusha

mawimbi kwenda simu za mkononi za

abiria.

Vituo vya kurushia mawimbi vya simu za

mkononi vilivyoko ardhini vitapokea na

kusambaza mawasiliano kwa njia ya

satellite kuunganisha na vile vya

ndani ya ndege.Simu zitatozwa kupitia

mitandao ya kawaida ya abiria.

Kwa kuanzia mfumo wa simu utakaotumika

ni 2G pekee, japokuwa Ofcom imesema

endapo kutakuwa na mafanikio, kutakuwa

na uwezekano wa kuzindua kwa mfumo wa

kisasa zaidi wa 3G na mingineyo mipya

itakayoundwa siku za usoni.


taarifa hii imeandaliwa kwa msaada wa

bbc

Laana ya wataafu (EAC) kulitafuna Taifa

Meghji awaambia wastaafu EAC: Wazee tulieni bado tunahakiki mafao yenu


watia kambi Stesheni ya TRL hadi
kieleweke

Na Mobini Sarya.


KWA miaka kadhaa sasa Wazee wastaafu
wa Shirika la Reli lililokuwa chini ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki wanalala
katika stesheni ya Treni Dar es Salaam
wakisubiri rehema za Mwenyezi Mungu
ili waweze kulipwa mafao yao.


wastaafu hao zaidi ya 40 ambao
wanatokea mikoa mbalimbali wakionekana
wamechoka na umri wao kwenda wamesema
walikuja Dar es Salaam miaka mitatu
iliyopita baada ya kuona majina ya
wastaafu yao yakichapishwa kwenye
magazeti kwa ajili ya kulipwa mafao
yao.

Wamesema baada ya kufika Dar es Salaam
walishangaa kuona majina yao hayapo
kwenye orodha ya malipo na
walipofuatilia wakaambiwa wasubiri
ndipo wakaamua kuweka kambi Stesheni
kusubiri Serikali ishughulikie suala
lao.

Ingawa walikuja na vielelezo kamili
baada ya kuona majina yao lakini hata
hivyo waliishia kupigwa kalenda
mwishowe nauli imewashia wameamua
kuishi hapo.

baada ya kuwatembelea katika makazi yao wazee hao
waliniambia kuwa zaidi ya miaka mitatu
sasa wamekuwa wakiishi mahali hapo
huku wakitumia maboksi kama matandiko
ya kulalia wakati wa usiku.

katika mazungumzo yao imebainika kuwa
Wazee hao wanakabiliwa na njaa kali
kwa kukosa chakula na maji ya kuoga na
wala hakuna kikundi chochote cha
watetezi w a haki za binadamu au
wanasiasa waliofika hapo kwa ajili ya
kutoa musaada.

Kero kubwa inayowakabili ni sehemu ya kujisaidia
haja kubwa ambapo wanalazimika kwenda
choo cha kulipia na kutozwa
Sh. 100 kwa kujisaidia mara moja

"Mwanangu tunapoishi hapa matatizo
yetu ni mengi, hatuna chakula wala
maji ya kuoga"Anasema mzee mmoja kwa
uchovu

hata hivyo kinachosikitisha zaidi ni
kuona kwamba wakati serikali ya awamu
ya nne imekuwa ikihubiri kuwa maisha
bora kwa kila mtanzania kwa wazee hao
imekuwa ikivaa miwani ya mbao.

hiyo inatokana na kuwa pamoja na mvua
inakuwa inanyesha wazee hao vikongwe
hubaki kwenye kuta za
majengo ya stesheni bila hata nguo ya
kujifunika wala neti ya kujikinga na
mbu wa malaria.

hapo ndipo yanapozuka maswali je hao
wazee sio binadamu wanaostahili kinga
na maisha bora? serikali na
wanaharakati hawawaoni?

kwa mjibu wa maelezo yao wanasubiri
malipo kamili kutokana na kiasi cha
shilingi bilioni 404/ zilizotolewa na
Malkia wa Uingereza Mwaka
2004.

Fedha hizo zilitangazwa na Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa, kwenye kilele
cha sherehe za Meimosi zilizofanyika
mkoani Mtwara mwaka huo.

wakati nikizungumza nao nilibaini kuwa
wazee hao wamekuwa wakiokota makopo ya
maji majalalani na kuuza ili wapate pesa ya
kununulia sahani moja ya wali.

Mzee Plasdi Marugu(64)kutoka Dodoma
mabaye amepiga kambi hapo kwa miezi
sita sasa anasema awali walikuwa
wanauza makopo hayo kwa kilo shilingi
300 na sasa bei yake imeshuka hadi
shilingi 150 wakati sahani ya chakula
imepanda kutoka shingi 500 hadi 700.

kutokana na mateso wanayoyapata wazee
hao wameanza kufa mmoja mmoja kama
ilivyotokea kwa Laston Mwakabana,
mkazi wa Kyela, Mbeya, ambaye alikuwa
Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia
mafao yake,
hadi amefariki dunia mwezi uliopita
mzee Mwakabana alikuwa analala nje kwa
miaka minne bila msaada wowote. .


wazee hao walisema marehemu alianza
kutapika na kuharisha damu na
walimpeleka Hospitali ambako
aliongezwa damu.

wamesema kuwa marehemu amekuwa
akifuatilia mafao yake jijini kwa
miaka minne bila mafanikio huku akiwa
ameweka makazi yake katika stesheni ya
treni.

wazee hao pamoja na kupata matatizo ya
kulala nje pia wamekuwa kuwa
wakidhulumia haki zao kama John
Herbert ambaye amedai mafao yake
yamepotelea Hazina katika mazingira ya
kutatanisha.

hiyo ni baada ya kukuta hundi yake
imesainiwa na mtu asiyemfahamu.

Herbert ambaye wakati wa EAC alikuwa
akifanya kazi Shirika la Reli Tanzania
(TRC), anadai alifika Hazina, lakini
alishangaa kuona nyaraka zinaonesha
kuwa ameshasaini na kuchukua hundi
wakati hajafanya hivyo.

mstaafu huyo alidai baada ya
kukamilisha taratibu zote za
ufuatiliaji mafao Februari mwaka jana
alitakiwa kwenda kuchukua hundi yake,
lakini baada ya kufika Hazina ndogo
iliyopo eneo la Posta ya Zamani, Dar
es Salaam, aliambiwa kuwa tayari
imeshachukuliwa.

hata alipojaribu kufuatilia hatima
yake ili kujua haki yake ya malipo ya
mafao katika ofisi ndogo ya Hazina
alifukuzwa na wafanyakazi.

Herbert ambaye namba yake ya kazi
ilikuwa ni 668859 alianza kazi mwaka
1968 na kustaafu mwaka 1979 mkoani
Tabora.

pamoja na kilio hicho cha wazee Hazina
imekuwa ngumu kutoa ufafanuzi wa
kinachokuamisha wazee hao wasilipwe
maafao yao yaliyotolewa na Malkia wa
Uingereza.


Tatizo lingine ni kwamba hapa
Tanzania, bado hakuna sera maalum
ambazo zinaelekeza jinsi ambavyo wazee
wanavyoweza kuhudumiwa inapofika
vipindi ambapo wanakosa misaada
mbalimbali ya kibinadamu kutoka kwa
familia zao.

Tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo
wazee wengi wakibaki kunyanyasika na
kutelekezwa hata na familia zao, jambo
ambalo baadhi yao hulazimika kuingia
mitaani na kuwa ombaomba.


Serikali itakuwa inakumbuka vema
Oktoba 18, mwaka 2005 ambapo mamia ya
wasimamizi wa mirathi na wajane
waliandamana na kuvamia ofisi za
Hazina jijini Dar es Salaam wakidai
kupigwa danadana katika mafao ya ndugu
zao waliokuwa watumishi wa Jumuiya
hiyo ambayo ilivunjika mwaka 1977.

familia hizo kipindi hicho zilidai
kwamba, wakati mahakama za mwanzo
zinazosimamia mirathi yao,
ziliwaelekeza kwenda kuchukua madai
yao Hazina, ofisi hiyo ilikuwa
ikiwapiga chenga na kuwasababishia
usumbufu bila kujali kuwa walikuwa
wanatokea mikoani.

watu wamekuwa wakijiuliza kuwa ni
lini Tanzania itafikia hatua kuweka
makambi maalum kwa watu wenye umri
mkubwa na kuwahudumia kwa kila hali
hadi wanapokufa kama mateso yenyewe
ndio hayo.





Wazee hao wameitaka serikali
iwape haki zao sasa badala ya kuendelea
kuwazungusha.

wanasema malipo hayo si
hisani ya serikali bali jasho lao
ambalo kuendelea kulizulia ni dhulma.

wakati Jumuiya hiyo inavunjika baada ya viongozi wakuu wa
nchi husika kutofautiana kisiasa iliacha Mashirika yaliyokuwa chini yake kuwa ni ni pamoja na Reli, Bandari na
Ndege.

jumuiya hiyo ambayo makao yake
makuu yalikuwa Nairobi wenzao
wa Kenya na Uganda walishalipwa mara
tu baada ya kuvunjika.





kadri siku zinavyozidi wazee hao
wanaingiwa na
wasiwasi juu ya uwezekano wa kulipwa
haki zao.


Wakati akihojiwa na chombo kimoja cha
habari cha nje, msemaji wa Hazina
alisema mpaka sasa ofisi yake
imeshawalipa wastaafu wasiopungua 700
na kwamba zoezi hilo linaendelea.


kutokana na kelele kuzidi Waziri wa Fedha Zakia Meghji,hivi karibuni
aliwataka wastaafu hao
kutulia wakati Serikali ikihakiki
malipo yao.

Waziri Meghji anasema hadi sasa
uhakiki unaendelea ili kuhakikisha
kila mstaafu wa Jumuiya hiyo, analipwa
stahili zake kama inavyotakiwa.

anakili kuwa tangu aingie wizarani,
amekutana na malalamiko mengi kuhusu
mafao ya wastaafu hao, wapo wanaodai
kutolipwa kabisa, wapo wanaodai
wamelipwa kidogo na matatizo mengine lukuki.


"Bado uhakiki unaendelea, ili
kuhakikisha kwamba kila mtu anapata
stahili yake kulingana na sheria na
tunaendelea kuwalipa, hivyo basi yafaa
wakawa watulivu wakati uhakiki
ukiendelea," alisisitiza Bi. Meghji.

Akizungumzia kiasi ambacho Serikali
inatakiwa kukilipa, Bi. Meghji alisema
awali Serikali ilitenga sh. bilioni 50
fedha ambazo katika majadiliano
zilionekana ni ndogo, hivyo
zikaongezwa sh. bilioni 67 na kufikia
sh. bilioni 117.


Wastaafu hao wanapozungumzia juu ya tukio
la kifo cha marehemu Mwakabana,
kilichoshangaza katika vyombo vya
habari, wameshangaa kuwa Waziri Basil
Mramba, aliishia kuchangia shilingi
20,000/ tu kwenye tukio hilo kama
rambirambi na kusafirisha mwili wa
marehemu.


"Nafikiri, kutokana na hali ya tukio
hilo kusababishwa na uzembe wa
serikali walau angekuwa makini
kuonyesha jinsi gani anasikitishwa na
tukio hilo, kama vile angemchangia
Mbunge mwenzake", alidai.


Hata hivyo wazee hao kwa pamoja
wamejumuika kutoa masikitiko yao kwa
jamaa wa marehemu Mwakabana, na
kuikumbusha serikali kutekeleza ahadi
zinazoendelea za kuwalipa mafao yao
yasije yakawafika yaliyomfika mwenzao
ya kufia kwenye jalala la mabehewa
chakavu.