Thursday, December 15, 2022

Afisa Elimu Kata ya Nyamswa awapeleka walimu Kutalii Senapa

 

Afisa Elimu Kata ya Nyamswa awapeleka walimu Kutalii Senapa

Na Mobini Sarya, Bunda

ZAIDI ya walimu 78 wakiwemo wanafunzi waliofaulu vizuri mitihani yao katika kata ya Nyamuswa wilayani Bunda,mkoani Mara, wamepelekwa na Afisa Elimu Kata hiyo Andrew Matogoro, kutalii kwenye hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA) kama njia ya kuwapa motisha ya kazi yao. 

AFISA ELIMU KATA YA NYAMUSWA WATATU KUTOKA KUSHOTO ANDREW MATOGORO AKIWA NA WALIMU WENZAKE KWENYE ZIARA HIYO
 

 Akizungumza na mtandao huu, Matogoro amesema kuwa aliandaa ziara hiyo ya siku mbili akishirikiana na viongozi wa kata, nakuwajumuisha Wazee maarufu wa kata hiyo, mtendaji kata ,Diwani na Afisa Elimu Wilaya ya Bunda  kama chachu ya kuinua elimu na kuwapa motisha walimu wa shule ya Msingi na Sekondari waliofanya vizuri ili   kutambua kazi waliofanya Mwaka mzima wa 2022.


          baadhi ya walimu wa shule mbalimbali za Msingi na Sekondari katika kata hiyo


“Tulianzia kwenye geti la Ndabaka,lengo ni kutambua juhudi za walimu hawa na kuwapa motisha namna wanavyofanya kazi, mwaka jana tulienda kisiwa cha saa nane Mwanza, tuna lengo la kuwaunganisha walimu na jamii ndio maana tumekuja na wazee marufu wa kata hiyo wafahamiane ili walimu waweze kufanyakazi katika mazingira mazuri”alisema Matogoro

 Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa  Chama cha Walimu Bunda Emmanuel Majura aliwapongeza viongozi wa kata hiyo kwa kutumia frusa hiyo kuunganisha walimu na kuwapa nafasi ya kwenda kutalii kupumzisha akili hivyo akashauri na viongozi wengine kuiga mfano huo kuandaa ziara za ndani na nje ya wilaya ambazo zinasaidia kujenga akili za walimu.

“Nitoe wito kwa walimu na viongozi wa maeneo mengine kwa maana ya kata za bunda na wilaya tuone namna ya kufanya ili kuwamotisha walimu wetu ziara za namna hii ni mhimu, viongozi wengine wakafanya na sisi kama chama tunaangalia namna gani tutawaunga mkono wakituomba msaada  pamoja na kuwa walimu ni wengi tutakuwa tayari kuwaunga mkono ili kuwamotisha walimu”alisema Majura

 

Baadhi ya walimu waliojumuika kwenye ziara hiyo wamepongeza mratibu kwa kwa kuwapeleka bila kuchagia gharama kutazama wanyama wakubwa maarufu kama BIG FIVE kwenye hifadhi ya Senapa ambayo inatajwa kuwa na vivutio vingi ikilinganishwa na hifadhi zingine hapa nchini.

Elika Bukumbi ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamswa A, alisema katika ziara hiyo amejifunza namna wanyama wanavyoishi na kuzaliana pia alifurahishwa na motisha aliyopata baada ya kutangazwa kufanya vizuri katika somo la Kiswahili ambayo anafundisha kwani wanafunzi walioongoza kwa kupata ufaulu wa A.

“Nimeweza kujifuza vitu vingi ikiwa ni kushudia namna wanyama wale wanavyoishi pamoja na kufurahishwa tulivyokaa pamoja na kufahamiana na walimu wenzangu lakini kepekee nilifurahi mno nilipotangazwa kama mwalimu niliofanya vizuri katika somo la kiswahili kwa kuwafanya wanafunzi kupata alama za A, hii ni kama deni kwangu kwa mwaka kesho” alisema Gidion

Naye Diwani wa Kata hiyo Ibrahim  Mganga Igai aliyeongozana nao aliwapongeza walimu hao namna wanavyojituma katika majukumu yao ya kuinua elimu nakuahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katiaka  kutatua kero zao zote kwa haraka wanapo mpelekea.

“Kwanza niwapongeze walimu wa kata yangu namna wanavyojituma kuhakikisha ufaulu unaongezeka  nina ahidi kutoa ushirikiano kwa walimu wote na nitatua kero zote zinazowakabili walimu wa kata yote”alisema Igai

Labels: