Tasisi ya ocean Road isaidiwe haraka, Serikali imetia aibu imeombwa Bilion 1.4 imetoa 300.
Baadhi ya wananchi wakitoka kuwatazama wagonjwa katika tasisi ya Ocean Road hapo ni njia panda
TASISI ya Ocean Road inayotibu magonjwa ya kansa ambayo ndio pekee tegemeo la wanyonge hapa nchini kutokana na kutoa huduma zake nyingi bure inakabiliwa na hali mabaya inayoweza kuongeza maafa kwa wagonjwa ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa ili kutatua matatizo yake.
JENGO la utawala katika tasisi ya Ocean Road
Madaktari wa Tasisi hiyo wametoa kilio chao kuwa pamoja na umhimu wa kitengo hicho kwenye jamii bado a Serikali imekuwa mabali nacho kwa kukitengea kiasi kidogo cha bajeti ambayo haikidhi uwezo wa kutoa huduma ikiwemo kununua Madawa.
Kilio chao kimejulikana ambacho wanasema ni cha siku nyingi baada mgonjwa mmoja miongoni mwa walalahoi wengi kukutwa akilalama baada ya kuwa amezunguka jiji zima la Dar es Salaam akitafuta dawa za kansa bila kuzipata, kwani Ocean Road walimaliza miaka mingi iliyopita.
Mama huyo Maseke Daniel kutoka Mwanza aliyekuwa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kipindi cha Mwaka mzima alibainika kuwa ana Kansa ya Damu na aliandikiwa dawa aina ya Chlorambucil 2mg Tabs 25P ambazo zilikuwa zinamsaidia kupunguza chembe nyekundu za damu lakini tangu Septemba hadi Disemba Mwaka huu ameshindwa kuzipata huku ugonjwa ukizidi.
Huyo mama ni miongoni mwa wagonjwa waokufa kwa kukosa dawa huku madaktari wakiwatazama bila kuweza kuwasaidia kwa kukosa dawa za kuwapa.
Baada ya mgonjwa huyo kuwa ameniwasilishia kilio chake niliamua kuunga naye kwa kumsaia kutafuta dawa hizo kwa kutumia Taaluma ya habari kwa kuanza na Tasisi hiyo ya Ocean Road lakini baada ya kufika huko nilibaini kuwa Hali ya Tasisi hiyo inazidi kuwa mbaya mwaka hadi Mwaka huku idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na Maradhi hayo ikizidi kuongezaka na kupelekea wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu.
Baadhi ya Madaktari niliohojiana nao walisema kuwa hali hiyo inasababishwa na Serikali kubana zaidi bajeti ya fedha inayokuwa imekusudiwa kununulia dawa ambazo kutokana na ughali wake ni wachache wanaoweza kumudu kuzinunua katika maduka binafsi.
Nilipomuuliza Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ,katika tasisi hiyo Dk.Richard Lyamo alisema kuwa hali ni mbaya katika kitengo hicho na kuomba mwandishi asihangaikie dawa hiyo moja kwani wanaupungufu mkubwa wa aina nyingi za madawa ambayo kwa kipindi kirefu yamekosekana hapa nchini.
Lyamo alisema kuwa ingawa Ocen Road inatoa matibabu bure na ndio imekuwa na kawaida ya kuagiza dawa zinazotegemewa na wagonjwa wengi hapa nchini lakini imekuwa haisaidiwi kikamilifu na serikali na kama wafadhili wasingekuwa wanaisaidia kidogo kidogo hali ingekuwa mbaya zaidi.
“Tatizo ni kubwa hapa kuliko unavyofikiria,kuna madawa mengi yamekosekana kwa muda mrefu bila kupatikana unaposema unatoa huduma bure inabidi uwezeshe vitengo husika kikamilifu, unaweza kwenda bohari kuomba dawa ukaambiwa hazipo kumbe zipo sasa ufanyeje na mgonjwa anahitaji”alisema Dk.Lyamo kwa masikitiko.
Dk Lyamo alisema kuwa matatizo ya kitengo hicho ni makubwa ingawa hayajawekwa wazi na wamejaribu kuiambia Serikali hadi wamechoka, kwani hata wagonjwa kwa sasa wanalala chini kwa kuzidi huku Wizara ya afya ikifunga baadhi ya Wodi nakusababisha mlundikano wa wagonjwa.
alisema kuwa zamani walikuwa wanalaza wagonjwa 100 au 110 lakini kwa sasa wanalala zaidi ya 170 na 180 , huku wadi zilizotakiwa kukamilika kufukia mwezi Septemba zikiwa bado.
Wakati Lyamo akilalaniliomuona mkuu wa kitengo cha manunuzi ya dawa Jerome Mponda ili kupata ufafanuzi zaidi wa ugumu uliopo wakati wa kuagiza dawa hizo.
Mponda alisema kuwa wakati nchi ikakabiliwa na upungufu mkubwa wa Dawa hizo, katika bajeti ya Mwaka 2007 na 2008 ziliombwa shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya kununulia dawa hizo kutokana na matumizi yake kuongezeka lakini katika hali ya kushangaza serikali imewaidhinishia shilingi Milioni 300 tu jambo ambalo limewashangaza hata wataalam wa magonjwa hayo kwani walikuwa wamekusudia kununua aina 122 za madawa ya shilingi Bilion 1,381,811,249.36.
Bajeti iliyokuwa imeombwa ni kwa ajili ya kununua dawa za kutibu magonjwa ya saratani na nyingine za kuwasidia waathirika wa VVU na Saratani.
Kutokana na hali hiyo Wataalam wa Tasisi hiyo ambayo ndio pekee yenye uwezo wa kuagiza dawa hizo kupitia bohari kuu ya Madawa, wameonya kuwa kwa sasa nchi itazidi kukumbwa na upungufu mkubwa wa dawa hizo hali inayoweza kupelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za kununua dawa hizo katika maduka machache yanayoziuza.
Hata hivyo maduka yanayouza dawa hizo ni machache mno na mengi yakiwa Dar es Salaam kutokana na uchunguzi uliofanywa katika maduka hayo ilibainika kuwa dawa zinazouzwa hapo ni aina chache sana kati ya nyingi zinazohitajika kwa watumiaji kwani ugonjwa wa kansa sio aina moja.
wamiliki wa maduka hayo jijini Dar es Salaam, walipooulizwa kuhusiana kukosekana madawa walisema kuwa hawapendi kuwaagiza madawa hayo kwa kuwa ni ya gharama kubwa huku wakihofia kupata hasara kwani wanaamini kuwa hutolewa bure katika hospitali za Serikali kwa hiyo watamuuzia nani.
Baadhi ya madaktari wa Tasisi hiyo waliozungumza na Tanzania Daima wameliambia kuwa kwa muda sasa hali ya matibabu hospitali hapo imekuwa ngumu kutokana na kukosekana dawa zinazokidhi matibabu kwa wagonjwa.
wanakabiliwa na upungufu wa Madawa mengi kutokana na kiasi kidogo kinachotengwa na Serikali bila kujali mahitaji ya wagonjwa ambao wamezidi kuongezeka katika tasisi hiyo.
Mbali na kiasi kidogo wanachopewa hata utaratibu unaotumiwa kupata madawa nao unalalamikiwa kuwa ni mbovu kwani Mgonjwa anaweza kufa akisubiri dawa.
kwa mfano tasisi hiyo iliagiza aina 122 za dawa hayo Mwezi Disemba mwaka jana lakini kutokana na kuwa na kiasi kidogo cha Pesa katika akaunti yao Bohari ikawapa jibu Mwezi Februari kuwa akaunti yao haina pesa za kutosha kwa hiyo wapunguze dawa.
Ikabidi wapunguze Mwezi machi wakapeleka Orodha ya dawa 33 lakini tangu mwezi huo wamekuja kupokea dawa sita mwezi Oktoba kati ya hizo ambapo wameendelea kupata zingine taratibu huku wagonjwa wakiendelea kuumia.
Ucheleweshaji huo unatokana na mchakato uliokuwa unaendeshwa na Bohari kuu kwa kutangaza tenda hadi kumpata mnunuzi atakaye agiza dawa hizo.
Utaratibu umekuwa ukilalamikiwa na madaktari pamoja na w agonjwa kuwa unasababisha wagonjwa wengi kuendelea kupoteza maisha kwa kukosa Dawa.
Baadhi ya Madaktari waliohojiwa hapo walisema kuwa kuna wagonjwa waofika hapo kwa ajili ya kupewa dawa hizo baada ya kuwa wamepimwa na kudhibitika lakini wamekuwa wakiambulia patupu hali inayopelekea wenye uwezo kuzitafuta mitaani lakini wasio na uwezo kubaki majumbani mwao wakiugulia.
“unajua tatizo ni kwamba Kansa sio malaria ambayo mgonjwa unaweza kumpa dawa hii isipokuwepo utampa nyingine hata kwa kumchanganyia lakini Kansa zipo aina nyingi ipo ya damu, Ngozi na nyinginezo na ujue kila moja inadawa yake unaweza kukuta dawa hiyo imekosekana kwa miezi sita unafikiri mgonjwa atasubiri huyo sikufa tu”alisema mmoja wa Madkitari wa Ocean Road.
Aidha uongozi wa Tasisi hiyo ulisema kwamba kutokana na mlolongo mrefu Dawa zinaweza kukaa zaidi ya miezi sita jazijafika hali ambayo hufanya hali ya wagonjwa kuwa mbaya na wengine hata kupoteza maisha hali hiyo imewafaya kuagiza zile mhimu tu ambazo zinatumiwa na wagonjwa wengi.
Mponda alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo wamekuwa w akiagiza kwa wingi dawa za kupunguza maumivu na maji ya kuwaongezea wagonjwa ili kusukuma siku pale w anapokuwa wamekosa dawa husika kwani wanaamini ni wagonjwa wachache wenye uwezo wa kuzinunua.
