Friday, August 8, 2008

Hatari inayolikabili taifa

JK na Serengeti Anko Ben na Kiwira


Na mbunge mtarajiwa

“JAMANI muacheni mzee Mkapa apumzike ….tumuache mzee apumzike sasa” hiyo ili kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa siku chache baada ya kuingia Ikulu, akiwaomba wananchi waache kumshambulia Mtangulizi wake Rais Benjamin Mkapa kwa tuhuma za kufanya biashara ikulu ikiwemo kuliingizia taifa hasara.

Kauli ya Rais Kikwete ninaiunga mkono kwa moyo mkunjufu kabisa bila kuhoji sababu ya Rais kusema hivyo, wakati akijua kuwa mtangulizi wake alikwenda kinyume cha katiba akafanya biashara ikulu

Alishindwa kusimamia miiko ya uongozi akaliingizia taifa hasara wakati akijua kuwa alichaguliwa na wanachi ili aliongoze taifa lipige hatua ya maendeleo. Pichani RAIS JAKAYA KIKWETE akiwa katika soko moja mjini Iringa katika sikukuu ya nanenane mwaka huu

Bila kuzingatia makosa hayo Wananchi tuunge tu mkono kauli hiyo ya Kikwete tumuache Mkapa apumzike hata kama alifanya makosa Ikulu kwani yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo kama nitakavyoyaeleza katika Makala hii.

Inawezekana Rais Mkapa hakufanya makosa makubwa ya kujiingiza kwenye biashara ya ujasilimali alipokuwa ikulu labda alikuwa na lengo mahususi ya kubuni ajira za kuwapa vijana ambao wangemtembezea ‘mitumba’ mitaani.

Huo utakuwa ni mfano mzuri kama itabainika kuwa alikuwa akitoa mfano kwa viongozi waliopo serikalini kuacha kutegemea pesa kidogo zinazopatikana kwa njia ya mishahara kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao na kukidhi mahitaji ya familia bali watafute njia zingine bora.

Ikiwa ndio hivyo ni vizuri kabisa Anko Ben (jina la utani kutokana na kampuni yake ya ANBEN) kuanzisha biashara Ikulu ili kuwapatia vijana ajira na hakuna sababu ya kumhoji wala kumalalamikia mzee wa watu tumuache apumzike.

Lakini kinachotuuma hata tunashindwa kutulia na ambacho Rais Kikwete labda hakijui ni kuhusiana na taarifa kwamba mzee huyo alitumia Pango la ikulu kufanya biashara kwa kipindi cha miaka mitano ya mwisho katika utawala wake bila kulipa kodi ya pango.

Hicho ndio kunatuuma na tungependa Kikwete atuambie ukweli kama mzee Ben alilipa kodi ili tumwache na kama hakulipa atuambie tutazipataje hizo pesa huo ndio ugomvi ubao hata katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa alinukuliwa akipiga kelele na sio vingenevyo.

Lakini kama alilipa kodi ya pango mzee anaweza kupumzika kwani hata huo mgodi wa kiwira wanao seme kwamba amejinyakulia na familia yake haiwezi kutuathiri sana licha ya kuambiwa alijipangia hata bei.

kwamba mgondi wa kiwira ulikuwa na thamani ya Dolla Milion 7 yeye akalipa shilingi Milioni 70 tu, lakini ni bora mzawa kuchukua kuliko ambavyo angechukua mgeni kama wafanyavyo katika sekta nyingine.

Kwa kuwa mgodi huo upo hapa nchini na vijana wetu wanaendelea kupata ajira huku faida akichuma yeye tumwache apumzike hayo ndio malipo ya uzeeni kwani mzee kwasasa si hawezi kushika jembe na makosa yalishafanyika.

Watanzania tunapaswa kuacha kupiga kelele ambazo hazisaidii za kumtaka Mkapa arudishe kiwira huku tukisaahau kuwa licha ya kwamba alikuwa Rais lakini aliupata kwa njia za Kisheria na mikataba anayo jambo ambalo haiwezikani kuirudisha.

Tunapaswa sasa kuelekeza nguvu zetu kumkabili Rais Kikwete ambaye yupo ikulu ache kufanyabiashara akiwa Ikulu tusimwache hadi aondoke ndio tuanze kumpigia kelele wakati tunajua fika kuwa sheria zetu hazirihusu kumtia hatiani Rais Mstaafu.

Ikiwa ndio hivyo tumbane Kikwete akiwa madarakani atueleze biashara anayofanya katika mbuga ya Serengeti akiwa na maswahiba wake kutoka marekani.

Jk kama alivyo mtangulizi wake Anko Ben Mkapa, nayeye amekiuka maadili ya Ikulu amehodhi mbuga ya Serengeti nakuanza kujenga mahoteli makubwa akishirikiana na wafanyabaishara kutoka marekani.

Hadi sasa sehemu kubwa ya mbuga hiyo imekwisha angukia mikononi mwao hasa katika eneo la Mkoa wa Mara kutoka Bunda hadi Serengeti wamejiwekea walinzi wanaolinda wananchi w asijitafutie kitoweo.

Tumuhoji Rais nay eye atoe maelezo bila kumng’unya kilichomkosa Ikulu hadi ahangaikie biashara kwani anakula na kuvaa kwa kodi za wananchi.

Tuambiwe amelipa kiasi gani serikali kama kodi za kuendesha buiashara ya ujenzi wa mahoteli mbugani licha ya kutambua kuwa ni kunyume cha maadili ya uongozi kufanya hivyo.

Kwa watu ambao hawajafika wilaya ya Serengeti mkoani Mara ni kwamba ukifika katika wilaya hiyo inaweza kufikiri upo katika nchi nyingine kwani tayari kuna jamhuri ya wamarekani ambao wana majeshi yao huku.

Kila siku katika mahakama ya wilaya hiyo kesi nyingi zinazosikilizwa ni wananchi waliokamatwa na askari wa kampuni moja ya kimarekani ambayo inalinda mbuga hiyo kwa kosa la kuingia mbugani

Leo wazawa hawana chao kwenye mbuga hiyo Rais amehodhi kupitia mgongo wa mwekezaji sasa wameanzisha harakati za kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kwa mgongo wa Halmashauri ya Serengeti.

Halimashauri inayotajwa kujenga uwanja ni ile ambayo imo kwenye kundi la halmashauri masikini lakini cha ajabu serikali inasisitiza kuwa ndio inajenga uwanja huo wakati inafahamika kuwa hatua za kuwalipa wananchi fidia zilishakamilika licha ya kwamba hakuna bajeti yoyote iliyowahi kutengwa.

Taarifa za serikali kudai bungeni Mwaka jana kuwa ndio inampango wa kujenga uwanja huo zinapingana na zile zilizopo Serengeti ambazo zinadai kuwa Mwekezaji mmoja ambaye ni swahiba wa Kikwete ndiye anajenga uwanja huo kwa mkataba na wilaya hiyo.

Lakini pamoja na kwamba taratibu za kuwanza kujenga uwanja huo zimekamilika hakuna mkataba wowote uliosainiwa baina ya halmashauri hiyo na mwekezaji.

Wakati ulaghai huo ukitendeka Rais Kikwete amekuwa akifika mara kwa mara katika mapumziko yake Serengeti kwa ajili ya kumalizia hoteli yake itakayokuwa na hadhi afrika ambayo ameijenga katika kijiji cha bilia Sadeco Km chache kutoka mjini.

Huyu ndiye kiongozi tunayetakiwa kumshughulikia sio Mkapa kwani amekwishapita tusimwachie huyu naye apite ndio tuanze kupiga kelele kwamba alifanya biashara ikulu mara alipora Mbuga tumwmabie sasa hivi akiwa madarakani.

Tumweleze kuwa mchezo unaofanya Serengeti na wamarekani kwa mgongo wa wawekezaji tumeujua ache kuendesha biashara ya utalii akiwa ikulu, tunaambiwa hoteli hiyo inawahi michuano ya Kombe la Dunia ili wageni na timu kubwa zipige kambi hapo wakati zitakapokuwa zinafanya mazoezi kwenye uwanja wa taifa.

Rais Kikwete ameamua kuchagua biashara ya utalii katika mbuga ya Serengeti wakati mtangulizi wake anko Ben alichagua kufa na kiwira ndio maana tunasema yaliyopita sio ndwele tumdhiti JK haraka tukichelewe tutakuja kuambiwa tumwache kijana apumzike!

Toa maoni yako; mobinsons@yahoo.com

Labels: