wabunge wamshangaa mpakanjia
Wabunge wamshangaa Mpakanjia kudai kuibiwa msibani
na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa zamani wa Njombe Kaskazini, Jackson Makwetta, aliyekuwa miongoni mwa wabunge 13 waliohudhuria mazishi ya mbunge mwenzao, Amina Chifupa, amekerwa na hatua ya Mohammed Mpakanjia, kutangaza hadharani kwamba ameibiwa simu yake ya mkononi.
Tangazo la kupotea kwa simu hiyo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Darry Rwegasira, hali iliyolazimu kusitishwa kwa muda shughuli za mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Ihanjo, Tarafa ya Lupembe mkoani Iringa.
“Wananchi wa jimbo langu wamedhalilishwa, sina hakika kama huyu jamaa alikuwa na nia njema nao, kudai kuibiwa simu, wakati mara zote alionekana akiwa pweke,” alisema Makwetta.
Makwetta, alisema Mpakanjia alipaswa kutambua kuwa mahala pale ni msibani na aliyefariki alikuwa mke wake na kwamba si vyema kutoa taarifa hiyo, vinginevyo itaeleweka walioiba ni wakwe zake.
“Ni kama amekuja hapa kutudhalilisha, haiwezekani suala la simu yake binafsi linasimamisha shughuli muhimu, kuna mambo ya msingi kitaifa na kimkoa yalipaswa kuelezwa, lakini tumechukua muda kuelezwa suala la simu,” alisema Makwetta.
Mbali na Makwetta, wabunge wengine walilalamikia kauli nzito iliyotolewa na DC huyo, kwamba watu walioiba simu hiyo si waungwana kutokana na uamuzi wa kumfanyia jambo hilo mfiwa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wabunge hao walisema kauli ya DC huyo ililenga kuwadhalilisha wananchi waliohudhuria kwenye msiba huo.
Mary Kasembe, Mbunge wa Viti Maalum, alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Mpakanjia kulifikisha kwa DC suala la kuibwa au kupotea simu, lakini baadhi ya watu wakisema yawezekana imedondoka kaburini.
“Kwa ujumla, hatua yake ya kutangaza kwamba ameibiwa simu tena kudai wakati akipokea mwili wa marehemu, tayari kwa maziko ni kukosa uungwana machoni mwa waliohudhuria mazishi hayo pamoja na waombolezaji wengine kutoka karibu kila mkoa nchini,” alisema Kasembe.
Kwa upande wake, Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango, alilalamikia suala hilo na kusema limeonyesha ni kwa kiasi gani Mpakanjia asivyoweza kuthamini maisha ya mtu na mali alizonazo.
“Kweli simu ni muhimu, lakini sisi kama wawakilishi wa Bunge na mheshimiwa Spika, tumeshangazwa kusikia kwamba simu imeibiwa wakati akiwa kaburini, kupokea mwili wa marehemu mbunge mwenzetu,” alisema Malecela.
Aidha, mbunge wa viti maalum, Janeth Massaburi, alisema pamoja na kulalamikia hatua ya Mpakanjia kudai kupoteza simu, alipaswa kutulia na kufikiria umuhimu wa Amina aliyefariki na kupata idadi kubwa ya waombolezaji kuanzia jijini Dar es Salaam, Iringa, Njombe mpaka kijijini Lupembe.
“Nchi nzima inamlilia Amina, inasikitishwa kusikia Mpakanjia akitangaza kuibiwa simu, kuna wabunge wenzetu wameibiwa simu siku ya mkesha wa msiba huu, hawakulalamika kiasi hiki, inakuwaje kama kweli alikuwa akimpenda hakutakiwa kutoa matamshi kama hayo kwa wakati ule,” alisema Massaburi.
Mbunge mwingine Aziza Ally, alisema amesikitishwa kwa kiasi kikubwa kusikia Mpakanjia akiomba msaada wa dola na kulalalamikia kupotea kwa simu yake.
Lakini pia mbunge huyo, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, alisema kuwa hatua ya DC wa Njombe kutoa matamshi mazito bila kuzingatia kama kweli simu imeibiwa ni dalili tosha kwamba aliamua kutaka kuwadhalilisha wananchi wengi waliohudhuria msiba huo.
Amina, alifariki dunia Juni 26 saa 2:45 usiku katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam, akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na homa kali na kuzikwa juzi.

Labels: je kasi aliyoanza nayo JK bado anayo na watumishi je?