Thursday, January 31, 2013
TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2013 LIMEIVA
Na Mwandishi wetu,Tanpress
ZAIDI ya maombi 560 ya wasanii kutoka ndani na nje ya nchi wanaotaka
kutumbuiza katika tamasha la sauti
za Busara Zanzibar yamewasilishwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara ,Sima Mohamedi akizungumza na Shirika la habari, Tanpress leo jijini Dar ee Slaam kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo.Picha na Tanpress
Hata hivyo ni vikundi 25 tu kutoka kila pande ya dunia ndio
watakaotumbuiza katika tamasha hilo litakalofanyika mwezi huu,Mjini Zanzibar kusherekea miaka 10
tangua kuanzishwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za busara, Sima Mohamedi amewambia wandishi
wa habari jijini Dar es Salaam, kuwa Tamasha hili litaanza tarehe 14 mpaka 17 Februari 2013 ndani ya Ngome
Kongwe Zanzibar.
Mohamed amesema kuwa licha ya
kwmaba tamasha hilo litavutia idadi kubwa ya wenyeji na wageni kutoka mataifa
mbali mbali kwa mwaka 2013, lakini wanakabiliwa na gharama za udhamini.
“Wachumi wanatumbia kuwa kila unapotumia dola moja kuandaa tamasha dola
15 inaingia kwenye mzunguko wa uchumi, hivyo tungewaomba wafanyabishara
wajitokeze kutudhamini kwani bila hili tamasha hakuna biashara”amaenukuliwa
Tamasha la mwaka huu litajumuisha wasanii 200: zaidi ya vikundi ishirini na tano kutoka Afrika
mashariki na kwingineko; utaalamu wa kutumia vyombo vya umeme na asilia
vyote hivi vitaonekana moja kwa moja kwenye jukwaa la Sauti za Busara.
Ndani ya Ngome Kongwe itakuwa ni
siku tatu mfululizo kwa muziki wa moja kwa moja, ratiba hii itaendelea kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili ikiambatana na
shoo kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa saba usiku
.
Tamasha pia litajumuisha filamu za miziki ya kiafrika: kumbukumbu, video za muziki na maonyesho ya moja kwa moja ya onyesho, yote haya tumelenga kukuza utajiri na utofauti wa muziki wa kiafrika hii itaonyeshwa ndani ya ukumbi wa Amphitheatre Ngome Kongwe.
Orodha ya wasanii wa kimataifa watakao shiriki Tamasha la 10 la Sauti za Busara ni Cheikh Lo kutoka Senegal, ni mwimbaji, mwandishi, mpiga Gitaa, Kora, ngoma na ni kivutio Afrika magharibi na kati, aliunda aina yake ya kipekee.

Cheikh Lô alizaliwa mwaka 1955, wazazi wake ni watu wa Senegal mji wa
Bobo Dioulasso, Burkina Faso, sio mbali na mpaka wa Mali,mahali alipokulia
wanaongea Bambara (Lugha ya Mali), Wolof (Lugha ya Senegal) na kifaransa.
Wakati wa utotoni alikuwa anasikiliza aina zote za muziki hususani miziki
ya Congo ijulikanayo kama rumba ni muziki unaojulikana sana Afrika. Miaka 21
alianza kuimba na kupiga kora na Orchestra Volta Jazz mjini Bobo
Dioulasso.
Youssou N'Dour aliitambua sauti yake ndipo alipomsaidia
kukuza kipaji chake baada kukutananaye kwa mara ya kwanza mwaka
1989. "Kila alipokuwa akiimba vibwagizo nilivutiwa na sauti yake,"
N'Dour alisema, " lakini nilitokea kumfahamu kupitia nakala yake
'Doxandeme'. Niliisikiliza sauti yake "wow" – Niliona kitu
kupitia sauti yake ambayo ilikuwa safari kutoka Burkina, Niger, Mali".
Katika Tamasha la miaka 10 ya Sauti za Busara itakutanisha bendi bora (Best of the Best) ambazo zilipendwa na mashabiki wa muziki kwa miaka tisa iliyopita ikiwemo bendi Mama na kiongozi wa rumba Tanzania wanaojulikana kama DDC Mlimani Park Orchestre (Sikinde)

Nao wakati wa Taarab asilia Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla
wajulikanao kama Culture Musical Club wataonyesha cheche zao kwenye Tamasha la
kumi la Sauti za Busara, kundi hili lililojizolea umaarufu sehemu mbalimbali
ndani na nje ya nchi kama Marekani, Japan na kwingineko.
Wasanii wengine ni Khaira Arby (Mali), Comrade Fatso na Chabvondoka (Zimbabwe), Atongo Zimba (Ghana), N'Faly Kouyaté (Guinea), Nathalie Natiembe (Reunion), Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros /
Mayotte), Wazimbo (Mozambique), The Moreira Project (Mozambique / Afrika Kusini), Owiny Sigoma Band (Kenya / UK), Mokoomba (Zimbabwe), Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania), Mani Martin (Rwanda), Burkina Electric (Burkina Faso / USA), Lumumba Theatre Group (Tanzania), Sousou & Maher Cissoko (Senegal /
Sweden), Super Maya Baikoko (Tanzania), Peter Msechu (Tanzania) na wengineo
wengi.
Sauti za Busara itaandaa Movers & Shakers networking forum kwa wenyeji na wageni wataalam katika sanaa. Mtandao huu utachukuwa nafasi katika kujadil maendeleo, kubadilishana mawazo na ubunifu katika kiwanda cha sanaa kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko.
It’s not just the festival that puts on a show; the local community is encouraged to take part by hosting Busara Xtra fringe events. These includetraditional ngoma drum and dance, fashion shows, dhow races, open-mic sessions, after-parties and performances of Zanzibar’s oldest taarab orchestras as arranged by the local community.
Si tamasha pekee linalofanya maonyesho: wenyeji nao wanapewa moyo wa kuhodhi matukio mbalimbali yajulikanayo kama Busara Xtra. Matukio hayo yanajumuisha ngoma za asili, maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa, taarabu asilia na mengineyo mengi ambayo yanaandaliwa na wenyeji.

Labels: BURUDANI