Magreath Sitta;Mafunzo ya Jeshi la Wokovu yamenisadia nisitende maovu
Maadhimisho ya miaka 90 ya Jeshi la Wokovu Territory ya Tanzania yakamilika
Na Nashoni Shadrack, Tanpresstz
![]() |
| Gwaride la maadhimisho ya miaka 90 ya Jeshi la Wokovu |
Akizungumza kwenye kongamano la Maadhimisho ya Miaka 90 tangu jeshi la Wokovu
kuingia hapa nchini Tanzania, Mwaka 1933, Bi Sitta ambaye ni mjane wa Spika wa
zamani, marehemu Samweli Sitta, alisema kabla ya kuolewa na mshirika wa
Moravian, wazazi wake walikuwa Salvation Army hivyo alilelewa kwenye kanisa hilo.
“Kwa kweli nisema kwamba mafunzo na malezi
niliyopatiwa katika kanisa hili yamenisaidia sana nisitende maovu…..
yamenisaidia sana hata sasa , ingawa niliolewa Moravian baadaye tulipohamia Dar
es Salaam, tukajiunga na kanisa la KKKT nikiwa mtu mzima lakini najivunia
kulelewa jeshi la Wokovu”alaisema na Kushangiliwa
Mbunge BI,Samweli Sitta baada ya kukabidhi mchango wa shilingi milioni moja jukwaani katika kongamano la miaka 90 ya SALVATION ARMY
Katika maadhimisho hayo ambayo yamefikia tamati Jumapili Disemba 10,2023 makao makuu ,Mgulani Dar es Salaam, yakihudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, Bi Sitta alitoa Shilingii Milioni moja Tasilimu kusaidia shughuli za maadhimisho.
Katika maadhimisho hayo ambayo yalianza Disemba 5 hadi 10 Mwaka 2023, takriban Makadeti 30 waliapishwa kuwa wachungaji na akupewa aagizo rasmi kwenda kwenye vikao (makanisa) mbalimbali kuongoza waumini na kutangaza injili.


0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home