Mikopo ya Kausha damu riba yake ni asilimia 3.5 tu
Ukikopa laki unalipa riba 3500
Na
Mobini Sarya, TanpresstzWaziri wa Fedha,Mwingulu
AJABU na kweli imeelezwa kuwa ile mikopo ya haraka ambayo inatolewa kwenye vibanda maarufu kama kausha damu au mikopo umiza riba yake ni asilimia 3.5 tofauti wanavyo fanya kwasasa.
Akitoa elimu kwenye kongamano la akinamama Women Talk Chalinze, Afisa Maendeleo Wilaya ya Chalinze, Ramadhani Mumba, alisema kuwa hiyo ni kwa mjibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya Mwaka 2020 na kanuni zake.
“wale wakopeshaji wadogo mnaowaita kausha damu riba yake inapaswa kuwa asilimia 3.5 kwa mwezi yaani ukikopa laki moja unalipa 3500 kwa mwezi sio vingenevyo, atakayekiuka mkataba huo faini yake inafikia milioni 20”alisema Mumba
Aliwashauri wajasiriamali kabla ya kuchukua mkopo huo kuomba kwanza mkataba na kuusoma vizuri kabla ya kutia saini, kama upo kinyume wajulishwe maafisa maendeleo wa jamii waliopo kata za jirani ili wachukue hatua za kisheria.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home