Thursday, December 27, 2012

Mambo ya Ex mass 2012

Aha pozi la  siku kuu ya X-Mass 2012. picha na Tanpress

Mkazi wa Bagamoyo akijenga nyumba yake

Mama mmoja wa kimasai akijenga nyumba eneo la Rugoba kitongoji cha Sekondari wilayani Bagamoyo  wakati vijana wake wakiendelea kupiga stori ndani, sio utamaduni wa kabila hilo kumkuta kijana anajenga nyumba kwani yeye huesabika kama ni mtafutaji na mchungaji. Picha na Tanpress.

Lumbesa ya Kora Kisalawe

Ni majuzi tu Disemba 2012. nilitembelea Kitongoji cha Kora wilayani Sengerema kamera ya TanPress ikanasa mzinga huu, ulikuwa umekamatwa na kupakiwa kwewnye ofisi ya mwenyekiti wa kitongoji hicho.picha na Tanpress

Wednesday, December 26, 2012

Zahanati ya Lushamba hufungwa jumapili na Jmosi

Nyamango/Soswa visiwa vyenye frusa tele za uwekezaji
·          
zinahitajika zahanati,shule na kumbi za starehe.

Na Tanpress,Nyamango

NYAMANGO na Chembaya ni visiwa viliopo maili 46 Mgharibi mwa jijini Mwanza ingawa vinahesabiwa kuwa vipo wilayani Sengerema  Mkoa wa Mwanza.
Vinakisiwa kuwa na wakazi zaidi ya 10,000 ambao wanategemea shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki wanaopatikana katika ziwa viktoria.
Usafiri unaotumika kwenda kwenye visiwa hivyo ni boti au meli za watu binafsi,ambazo hutumia  masaa 12 kutoka jijini mwanza eneo hilo na mara nyingi boti ya mwendo kasi huingia saa mbili usiku.
Aidha kutoka katika visiwa hivi hadi kwenye mwalo wa Kanyara ambayo ni nchi kavu ya wilaya ya Sengerema boti hutumia masaa manne hadi masaa matatu kufika nchi kavu.
Pia kutoka eneo la kitongoji cha Kanyara usafiri ni wa shida Km.80 hadi kufika Sengerema mjini zilipo huduma zote za kijamii.  
Eneo hilo lina vitongoji viwili vinavyoundwa na visiwa vine ambavyo ni Soswa/Chembaya na Nyamango/Chamagati ni katika eneo hilo lenye makazi ya kudumu ya watu ndipo frusa za uwekezaji zipojitokeza.
Hivi karibuni Mwandishi wa Shirika lahabari Tanpress alifika kwenye visiwa hivyo kwa lengo la kukusanya habari na matukio ndipo alipojionea frusanyingi za uwekezaji.
Kwanza licha ya kwamba wavuvi wengi ni watu wanaopenda starehe hasa za ulevi lakini ‘viwanja vyakujirusha’kuburudika ni kama havitoshi.
Maeneo mbalimbali ambayo mwandishi waTanpress alitembelea alikuta wenyeji wakipata vinywaji kwenye baa zinazofanana na vilabu vya Pombe za kienyeji jambo linaloonyesha kuwa maeneo hayo yanahitajika uwekezaji wa baa na mahoteli ya kisasa.
Aidha nishati ya umeme kwenye eneo hilo inahitajika kwa haraka kwani wengi wanatumia jeneretor ambazo hawamudu kununua mafuta hivyo hata wale wachache waliojitolea kujenga nyumba za kulala wageni wanawasha vibatari wasijue lakufanya.
Hivyo anahitajika ,mwekezaji mkubwa aweke mashine inayotumia mafuta ya diseli kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosha katika eneo hilo,ambalo kwasasa lipo gizani ingawa wenyeji wanahitaji huduma hiyo.
Baadhi ya maeneo ,mengine au hata visiwa vingine  mashine za kufua umeme kwa kutumia mafuta ya diseli ndio zinatumika kusambaza umeme jambo ambalo halijafanyika kwenye visiwa vya Nyamango.
Frusa nyingine uwekeza ambayo inalipa  ni kituo cha afya au zahanati,licha ya kwamba wavuvi wanafamilia zinazohitaji huduma ya afya wanapougua au akinamama wanapotaka kujifungua huduma hiyo haipo kabisa kwenye visiwa hivyo.
Kwa hiyo akitokea mwekezaji akafungua zahanati yenye uwezo wa kuzalisha akinamama wajawazito anaweza akanufaika kwa haraka kwasababu inavyoonekana serikali imeamua kutelekeza wakazi hao na haina mpango wowote wa kuwajengea zahanati.
Kwasasa zahanati sio jambo la mjadalainahitajika kwaharaka kuweza kuokoa maisha ya akinamama wajawazito na watu wa kawaida wanao umizana kwenye starehe zikiwemo ulevi.
Ni vyema kamamwekezaji anavutiwa na uwekezaji huo akajenga kabisa kituo kikubwa cha afya kwasababu hakuna kituo karibu hata kwenye visiwa vya jirani kama zilagula na Yozwa bado huduma hiyo wanakwenda kuitafuta mbali.
Elimu ni frusa nyingine ya uwekezaji inayohitaji watu wenye mitaji kwani pamoja na kwamba wavuvi hao wanafamilia zao eneo hilo lakini kuna shule moja ya umma ambayo hata hivyo haitoshi mahitaji.
Shule hiyo ya msingi inajulikana kama Soswa shule ya Msingi bado haijaweza kutoa elimu bora kutokana na kukosekana kwa walimu wa kutosha eneo lavisiwa hivyo.
Kwa hiyo zinahitajika shule za awali kwa kila kisiwa ambapo  kuna visiwa vinne pia zinatakiwa  shule binafsi za sekondari na msingi au hata vyuo vya michezo ya majini kwa ajili ya wagoeleaji.
Frusa zingine niliziona ni kuweka boti za mwendo kasi kwa ajili ya kuwakimbiza wagonjwa hospitalini na kuanzisha kampuni za ulinzi kwani hivi sasa baada ya uvamizi kuwepo sasa wakazi wa pale wameanza kukodi walinzi kutoka Mwanza ambapo ni mbali zaidi.
Zipo frusa nyingi za uwekezaji hata kwenye soko lachakula cha kuku na wanyama wengine lakini kama wewe ni mwekezaji unaweza kufikahukoukajionea mwenyewe.
www.mobinday.blogsopot.com 0753399 579 mobinsons@yahoo.com   
         
Nyamango/Soswa visiwa vyenye frusa tele za uwekezaji

·         zinahitajika zahanati,shule na kumbi za starehe.

Monday, December 24, 2012

Nyamango;visiwa vilivyotelekezwa na serikali

Ripoti maalumu.

·         Hawana zahanati wala maji safi

·         Tangu uhuru serikali haijawahi kufanya lolote
·         Kikongwe ajitosa kuokoa roho za wajawazito

Na Mobini Sarya, Nyamango,Mwanza

WAKATI Serikali ya Tanzania na wananchi wake wakisherehekea miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara,wakazi wa visiwa vya Sengerema ,mkoa wa Mwanza wapo katika huzunika kubwa baada ya serikali kutelekeza visiwa hivyo tangu uhuru.
Visiwa hivyo ni Soswa/Chembaya,Nyamango Chamagati,Kasalazi naGembale,Yozwa na Busenge ambavyo vinahesabiwa kuwa vipo kijiji cha Lushamba Kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa ingawa vipo mbali. 

Wakazi hao wameliambia shirika la habari (Tanpress) kwamba hawana cha kujivunia tangu nchi hii imepata uhuru zaidi ya kushurutishwa na serikali ya Tanzania kulipa kodi na michango mingine bila kupewa  maendeleo yoyote.
“Kama unavyoona Mwandishi katika eneo hili ambalo lina visiwa vinne vyenye kuundwa na vitongoji viwili hatujawahi kuletewa amaendeleo yoyote yale wanayopata watanzania wengine”anasema  George Rwezaula …ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamango na Chamagati
Hivi ni visiwa viwili tafauti lakini kwa makusudi serikali imeviacha kuwa kitongoji kimoja chanye wakazi  zaidi ya 3500 na kaya 75 wakati kitongoji kinatakiwa kisizidi kaya 50,lakini pia kuna visiwa zaidi ya 7 eneo hilo ambavyo vilipaswa kuundiwa kijiji ili kusogeza hudumakaribu.

Mwenyekiti huyo kwa niaba ya wananchi wake amemwambia Mwandishi wa Tanpress aliyetebelea  maeneo hayo kuwa visiwa hivyo vina ukosefu wa huduma mhimu za kijamii ikiwemo vituo vya afya,shule, maji safi na kituo cha Polisi.
Akizungumza na TanPress katika kisiwa cha Nyamango , Rwezaula alishukru kutembelewa na Mwandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu historia  ya uhuru jambo lililosababisha kuchelewa kwa maendeleo eneo hilo.
“Mwandishi kwanza tunakushukru kuweza kufika katika kisiwa chetu,hakuna mwandishi ambaye amewahi kuja hapa,licha ya kwamba kuna  matukio makubwa  na kutisha  ambayo hufaanyika hapa kamaujambazi wa kutisha  lakini taarifa hazifiki kwenye vyombo vya habari”anasema Mwenyekiti huyo.
Katika kuonyesha tatizo la ukosefu wa kituo cha Polisi , Rwezaula amekumbushia kwamba kati ya Mwezi Septemba hadi November Mwaka huu wavuvi  visiwa hivyo waliporwa zaidi ya mashine 100 za mitumbwi na maharamia usiku,lakini walipojulisha jeshi la polisi ilichukua siku tano kufika kwenye tukio.
“Sisi hapa visiwani hatuna huduma ya Polisi ndio maana majambazi huingia kila wakati kwasababu kituo kinacho tuhudimia kipo Nchi kavu kilomita 60,ukiwapigia simu Polisi wanasema hawana mafuta hadi wachangishane”anasema Mwenyekiti huyo.
Akizungmza na Tanpress Kamanda Polisi Mkoa wa Mwanza anasema “wambie wananchi wapeleke malalamiko yao Halmashauri…mbona  wanalipa kodi kwanini wasijegewe vituo kama njia ya kuletewa maendeleo  ……ujue mazingira yao ni tofauti unakuta kisiwa kina watu wachache labda wabuni njia nyingine ya kujilinda kamaulinzi shirikishi kwasababu usafiri kwenda kwao ni taabu ….mazingira yao ni magumu”anasema RPC Erenest  Mangu.
  Anaongeza kuwa  Vituo vyote ni mali ya jamii “wakijenga tu hata kesho….. ungewashauri wajenge kituo cha poli sisi tuwapelekea askari,………kama magari yenyewe ni taabu kufanyia doria nchi kavu,usafiri wa boti tutapataje tufike kwenye visiwa hivyo..tutawapelekea askari kama wakijenga vituo……..,wabunge wa maeneo yao wangekuwa wanapiga kelele za namna hiyo hata magari na usafiri wa boti ungekuwa umepatikana.anasema Ernest Mangu ambaye amehamia Mwanza akitokea Pwani.
Licha ya kwamba visiwa hivyo vipo Maili 45 kutoka jijini Mwanza na Kilmeta 120 kutoka wilayani sengerema havina huduma yoyote ya afya wala usafiri wa uhakika kuweza kuwafikisha wagonjwa na wajawazito kwenye kituo cha afya.
Kukosekana kwa kituo cha afya wala zahanati karibu kumesababisha ongezeko la vifo vya akinama wajawazito licha ya kwamba kila Mwaka serikali hutenga bajeti ya afya iliyopaswa kugawanywa katika maeneo yote.
Mwandishi wa habari hizi alilazimika kukodi usafiri nakutembea kutwa kwenye visiwa saba kutafuta huduma ya kituo cha afya hakauweza kukipata badala yake aliambiwa aende nchi kavu ilipo zahanati ya kijiji Kmeta 40 ambapo hata hivyo baada ya kufika alikuta imefungwa kwa amelezo kuwa jumapili haiendeshi shughuli zozote za afya. 
 Akizungumza kwenye kibanda chake cha kuuzia madwa mganga muuguzi wa zahanati hiyo,Yasinta Midale alsiema kuwa Zahanati hiyo licha ya kuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wa visiwani lakini haina huduma mhimu.
“Kwamfano hapa tuna muda mrefu hatupimi maambukizi ya ukimwi kwa akinamama wajawazito kwasababu hakuna vipimo hata vya malaria hivyo ingawa tunapokea wajawazito 78 hadi 85 kwa mwezi wanahitaji huduma ya kliniki”anasema Muuguzi huyo
Hata hivyo alipoulizwa kamamjamzito angefika hapo siku ya jumamosi aujumapili kutaka  kujifungua angepataje  msaada wakati zahanati imefungwa alidai  kuwa kuna kituo cha afya kijiji cha jirani ambacho kina,milikiwa na kanisa ndicho hutoa huduma siku  kama  hizo .
 Kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo ya afya kumemsukuma kikongwe mmoja mwenye miaka 55 kuanza rasmi shughuli ya kuzalisha akimama kwenye visiwa vinavyomzunguka.
Mama Madewa akizungumza kwenye kibanda chake anachotumia  kutoa  madawa ameliambia Tanpress kwamba alianza huduma hiyo Mwaka 2007 baada ya kuona serikali imeshindwa kuwasaidia akinamama wanateseka na kupoteza maisha.
“wakati huo akinamama walipokuwa wanaona wamekaribia kujifungua walikuwa wanasafiri kwenda nchi kavu kusubiria ,lakini kuna wale ambao waliendelea kutafuta pesa na kukuta muda wakujifungua umefika hao ndio walikuwa wanapata taabu hadi nilipoanza hii kazi”anasema Bi.Madewa
Licha ya huyo mkunga kujitahidi kuhudumia akimama wa visiwa vya Chamagati,Nyamango,Chembaya na zilagula vyenye wakazi zaidi ya 10000 bado serikali haijawahi kumpatia mafunzo yoyote hata ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamango, George Rwezaula aliyempeleka Mwandishi kwenye banda la mkunga huyo amedai kwamba mara kadhaa aliwahi kupeleka ombi la mkunga huyo kwenye vikao vya kata ili apatiwe  mafunzo lakini serikali ya wilaya ilidai kuwa bajeti imefika kikomo.
Mwenyekiti huyo anashangaa serikali kupitia Mamlaka  ya mapato TRA kufika hapo mara kwa mara kukusanya kodi,halmashauri nayo kukusanya ushuru lukuki lakini  wameshindwa kupewa hudumayoyote ya kijamii ikiwemo maji safi.
Ametaja baadhi ya ushuru unaokusanywa na serikali kuwa ni shilingi 90,000 za kusajili mtumbwi kwa  namba MSR,leseni kila Mwaka 35000 huku mitumbwi kwenye kisiwa kimoja ikiwa zaidi ya 300,wavuvi kutakiwa na halmashauri kulipia  shilingi 7000 kila mwezi (parking fees).
Aidha TRA hukusanya kwa wavuvi wa dagaa shilingi 2000 kila debe huku boti zinazonunua au kupakia samaki kwenye eneo hilo kulazimika kulipia  mapato ya shilingi laki.2 hadi tatu kutegemeana na ukubwa wa boti kila inapojaza samaki.      
Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Magumba alipoulizwa kukosekana kwa huduma ya afya visiwani alidai kuwa hilo hawezi kulizungumzia kwasababu nayeye amelikuta ingawa kipaumbele chao kwasasa ni kujenga shule ya Msingi eneo la katika Kitongoji cha Kanyara.
“Aha hata mimi niliwahi kuuliza nikaambiwa na Halmashauri kwamba wanataka tufanye ili wao wamalizie ,sasa ukimwambia mwananchi achangie ujenzi ili Serikali ituunge mkono anaona kama anaibiwa  ukizingatia kuwa sasa hivi tunataka kuchangia shule mpya”anasema…
Hata hivyo juhudi za kumtaafuta diwani wa Kata ya Bulyaheke,Bageti Ngere Nyuki zimegonga Mwamba baada ya kukwepa kukutana  na Mwandishi wa habari mara kadhaa alipopigiwa simu huku akitoa visingizio vingi wakati mwingine akidai yupo mbali au kwenye kelele hawezi kuzungumza.
Naye Mbunge wa Jimbo la  Buchosa,Charles Tzeba , alipoulizwa kuhusiana na kukosekana kwa huduma mhimu za kijamii katika visiwa hivyo alidai  kuwa yeye ni mbunge wa kitaifa anayesimamia bajeti kuu mengine hayo waulizwe viongozi wa Halamashauri.
“kwani wee mwandishi nani amekutuma ukachunguze hayo? Kwanza ujue kuwa mimi nimechaguliwa kama mbunge kipindi hiki hivyo hali nimeikuta kama ilivyo labda uwasiliane na viongozi wa  Halmashauri wakueleze wana mpango gani na maeneo hayo kwasababu wanabajeti zao”AlisemaTzeba 
Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Uchukuzi alisema kuwa kazi yake nikusimamia bajeti ya kitaifa namna inavyotekelezwa na serikali na maswala ya jimbo  wanaopaswa kuyashughulikia ni Diwani pamoja na mwenyekiti wa halmashauri kwa kushirikiana na mkurugenzi.
Hata hivyo juhudi za kuwapata viongozi hao zinaendelea kwani mwandishi amefika mara kadhaa kwenye ofisi za  Halmashauri hiyo na kushindwa kuwaona viongozi wa Halmashauri wala kupata  mawasiliano yao.

Asnnat Mtasingwa;Kikongwe pekee anayetegemewa na wajawazito visiwani.

*alikuwa mpishi wa kambi za dagaa sasa ategemewa kama daktari bingwa.
*anazalisha bila oparesheni,wala ganzi

 Na ,Tanpress

“WAKATI mwingine naweza kumzalisha mjamzito akatokwa damu nyingi hivyo nakimbilia duka la madawa namuomba muuzaji anaakuja na dawa anamchoma huyo mama anayevuja damu zinasimama”kauli ya masikitikokutoka kwamkunga wa jadi visiwani Sengerema,bi.Mtasiwa
Aliingia katika visiwa vya wilaya ya Sengerema mkoa  wa Mwanza katika ziwa viktoria akiwa kama mpishi wa chakula cha wavuvi kwenye kambi za dagaa, miaka 20 iliyopita.
Wakati huo hakujua kwamba baada ya mda angekuja kuwa mtu mhimu ambaye sasa anategemewa na jamii yenye wakazi 25000 wanaoishi kwenye visiwa saba vinavyolazimishwa kuwa chini ya kijiji kimoja cha Lushamba.
Huyo ni bi Annat  Mtasingwa (55) ambaye ni mkazi wa kisiwa cha Nyamango kinacho unganishwa na kisiwa jirani cha chamagati na kujulikana kama kitongoji cha Nyamango/Chamagati mali ya kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa.
Kwa mjibu wa takwimu zilizotolewa na Mwenyekiti wa kitongoji cha visiwa hivyo,George Rwezaula alisema kuwa kitongoji chake kina kaya 80 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka kitongoji kiwe na kaya 50.
Akiwa anaendelea na shughuli za upishi mama huyo wa kabila la wahaya kutoka mkoa wa Kagera alibaini kuwa eneo alilokuwa anaishi lilikuwa halina huduma ya afya kwa ajili ya kujifungulia wala Mkunga aliyefunzwa,kwa ajili ya kuokoa akinama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
“Mara ya kwanza nakumbuka ilikuwa Mwaka 2007 wakati wifi yangu niliyekuwa naishi naye alipohitaji huduma ya  kujifungua ikakosekana ikabidi mimi nimzalishe ndipo watu wakajua wakaanza kuja.”anasema Annat Mtasingwa nyumbani kwake.
Anasema baada ya wifi yake kujifungua salama walikuja akimama watatu nao akawazalisha hapo ndipo habari zilienea akaanza kwenye visiwa vingine 7 ambavyo baadaye alikuja kugundua kuwa havina zahanati wala kiliniki kwa ajili ya akinamama kujifungulia.
Ni hapo ndipo bibi huyo anayejulikana sasa kama mkunga wa jadi licha ya kwamba hana mafunzo yoyote alipoanza kupokea akinamama wenye mimba wakiwemo wagonjwa mbalimbali na kulazimika kuacha shughuli za upishi ili apate muda wa kuwahudumia.
 Mtasingwa (55) anasema kuwa licha ya kuanza kubobea kwenye magonjwa ya akinamama na kuwazalisha hivi sasa amegudua dawa za kutibu hata wanaume hususani wale wanaougua magonjwa ya Gono.
“ukiachana na akinamama wanaokuja kujifungua ambao wakati mwingine kama mtoto amekaa vibaya hulazimika kutumia dawa aina ya ukingura kumugeuza akae vizuri…lakini pia wateja wangu wengi ni wanaume wanaogua kisonono na Kaswende”anasema Mtasingwa (55)
Magonjwa ya zinaa yametajwa kuwa ndio yanaogoza katika kisiwa hiki na vingine vinavyozunguka maeneo hayo,hata wamiliki wa maduka ya dawa wamedhibisha hili.
Hata hivyo kikongwe huyo anasema kuwa changamoto kubwa inayomkabili ni kukosekana kwa sehemu ya kuwalaza akinamama wanaotaka kujifunga kwani anakitanda kimoja wakati hupokea hadi akinamama watatu kwa siku.
Ingawa anasema hakuna mjamzito aliyefariki mikononi mwake lakini anasema wapo ambao huvuja damu nyingi nakumtia wasiwasi hadikumkimbilia dada mmoja anayeuza dawa za kisasa Rebecca Jafety(28) amabaye huwachoma  dawa  ya kuzuia damu. 
“Wakati mwingine naweza kumzalisha mjamzito akatokwa damu nyingi hivyo nakimbilia duka la madawa namuomba muuzaji anaakuja na dawa anamchoma huyo mama anayevuja damu zinasimama”kauli ya masikitikokutoka kwamkunga wa jadi visiwani Sengerema,bi.Mtasiwa
 Ni hapo ndipo ilipobainika kuwa zaidi ya wakazi 25,000 ambao wanaishi kwa kutegemea shughuli za  uvuvi katika visiwa hivyo ambavyo vimetajwa kuwa ni Kasalazi,Gembale ,Nyamango/Chamagati,chembaya/Soswa na Mwalo wa Kanyara kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke hawana kituo cha afya kabisa.  
Lakini hiyo sio hoja wala sababu kwa watawala bora mambo yanaenda,linalotakiwa kujulikana kwa msomaji ni kwamba licha ya serikali kudai kuwa akinamama wajawazito na wale wanaaojifua wapate huduma hiyo bure lakini kwa akinamama wa visiwani hulipia gharama kwa mkunga.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, George Rwezaula amesema kuwa kuwepo kwa mama huyo kumewasaidia wakazi wa kitongoji chake kupunguza michango iliyokuwa inawakabili kila mara kulazimika kuchangia usafiri wa kukodi boti kumpeleka mjamzito kwenye zahanati ya Kanyara.
“Kama unavyoona hapa akinamama wengi wanafanya kazi ya kusomba dagaa ili wapate pesa,wakati mwingine anaweza kuwa hana pesa na uchungu umemshika anataka kujifungua tunachangishana….angalia madaftari ambayo huorodhesha michango ili kuokoa akinama wajawazito kuwahi hospitalini”anasema George Rwezaula
Pamoja kuwa wakazi wa visiwa hivi wamejenga tabia ya kuchangia kwa maisha yote ili kuwakimbiza wajawazito kwenye zahanati ya kijiji cha Lushamba pale inaposhindikana kuzalishwa na mkunga,lakini bado zahanati hiyo ambayo ipo mwendo wa masaa manne hadi matani kwenye maji haina huduma mhimu.
Mwandishi wa Shirika la habari alitembelea zahanati hiyo siku ya jumapili na kukuta ipo Km.6 kutoka zinaposimama boti zinazowatoa wagonjwa visiwani,baada ya kukodi pikipiki na kwenda hadi ilipo aliambulia kukuta milango imefungwa kwa maelezo kuwa siku za  wikendi haitoi huduma.
 Akizungumza kwenye kibanda chake cha kuuzia madawa katika kijiwe cha Lushamba Mkunga  muuguzi wa zahanati hiyo,Yasinta Midale alisema kuwa Zahanati hiyo licha ya kuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wa visiwani lakini haina huduma mhimu.
“Kwamfano hapa tuna muda mrefu hatupimi maambukizi ya ukimwi kwa akinamama wajawazito kwasababu hakuna vipimo hata vya malaria hivyo ingawa tunapokea wajawazito 78 hadi 85 kwa mwezi wanaohitaji huduma ya kliniki  hatuwapimi” anasema  Muuguzi huyo
Hata hivyo anapoulizwa kama  mjamzito angefika hapo siku ya jumamosi au jumapili kutaka  kujifungua angepataje  msaada wakati zahanati imefungwa alidai  kuwa kuna kituo cha afya kijiji cha jirani ambacho kina,milikiwa na kanisa ndicho hutoa huduma siku  kama  hizo.
 “Kwanza kiukweli kabisa hapa ni kama hakuna huduma ya afya ya uhakika kwasababu kisheria sisi zahanati kutibu hadi saa tisa alasiri tunafunga maana baada ya hapo hatulipwi chochote halafu wikendi sisi tunapumzika labda itokee dharura mgonjwa atutafute vingenevyo inabidi wampeleke zahanati ya kakobe inayomilikiwa na dini”anasema Mkunga Midale.
Pia imebainika kuwa zahanati hiyo haina hata umeme wala sola hivyo kuwapatia shida nyingine ya kutoahuduma ya kujifungua kwa akinamama wanaotaka kufanya hivyo nyakati za usiku.
  Baada ya wananchi kuona hali imekuwa taabu aidha hukodi gari kumpeleka mgonjwa Km 80 katika hospitali teule ya Halamsuri ya wilaya ya sengerema na kama hakuna pesa za kutosha gari ya wagonjwa huitwa kutoka mjini sengerema masaa 3 kufika na kugeuza masaa mengine matatu hivyo mamahupoteza maisha au kujifungulia njiani.
Mzee Jonathani Kamiga Lukazoha amewahi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho chenye visiwa saba tangu Mwaka 2005 hadi 2010,alipotakiwa na tanpress kueleza juhudi zilizowekezwa na serikali katika kutatua tatizo lakituo kikubwa cha afya maeneo ya visiwani alisema.
 ‘Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba pesa zimekuwa zikitengwa kwa ajili ya kujenga zahanati eneo la Soswa kwa miaka mingi lakini zimekuwa zikiyeyuka mifukoni mwa wajanja kwani kila nilipokuwa nikifuatilia sikuweza kupata ushirikiano kutoka kwa diwani aliyekuwepo”Anasema Lukazoha
Madai ya mstaafu huyo yanaungwa mkono na mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamango/Chamagati, Bw.Rwezaula ambaye ametoa nyaraka za Halmashauri ya Sengerema zikionyesha kuwa bajeti ya Mwaka huu 2011/2011 halmashauri imetenga pesa za kumalizia ujenzi wa zahanati ya Soswa wakati ukweli ni kwamba hakuna hata msingi.
“Ukamilishaji wa zahanati Soswa/Nyantakubwa,Nyashana na Kabaganga..kutoka Halmashauri ni milioni 600 na serikali kuu ni milioni 180”linasomeka kablasha la halmashauri kuonyesha kuwa ujenzi wa zahanati unaelekea  kukamilika.
Baada ya Mwenyekiti wa kitongoji hicho kulisoma akawasiliana haraka  na Diwani wa kata yaBulyaheke ,Bageti Ngere Nyuki ambaye alijibu kwa kifupi kuwa anasubiri ramani kutoka halmashauri ili wananchi waanze kujenga msingi na ukuta halmashauri ipaue.      
Mbunge wa Jimbo la Buchosa alipoulizwa kuhusiana na kukosekana kwa huduma hiyo naye alionyesha kituko cha Mwaka baada yakudai kuwa majukumu yake ni kusimamia bajeti ya taifa sio maeneo kama hayo.
“kwani wee mwandishi nani amekutuma ukachunguze hayo? Kwanza ujue kuwa mimi nimechaguliwa kama mbunge kipindi hiki hivyo hali nimeikuta kama ilivyo labda uwasiliane na viongozi wa  Halmashauri wakueleze wanampango gani na maeneo hayo kwasababu wanabajeti zao”AlisemaTzeba 
Nakuongeza kuwa ‘bwana wewe mwandishi umetumwa na nani kuniuliza  hayo maswali hujui kwamba hata kabla ya  mimi kuingia madarakani  nilikuta maisha yanaendelea na viongozi walikuwepo na nilikuta matatizo ya ukosefu wa huduma za kijamii”?
Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Magumba alipoulizwa kukosekana kwa huduma ya afya visiwani alidai kuwa hilo hawezi kulizungumzia kwasababu nayeye amelikuta ingawa kipaumbele chao kwasasa ni kujenga shule ya Msingi eneo la katika Kitongoji cha Kanyara.
“Aha hata mimi niliwahi kuuliza nikaambiwa na Halmashauri kwamba wanataka tufanye ili wao wamalizie ,sasa ukimwambia mwananchi achangie ujenzi ili Serikali ituunge mkono anaona kama anaibiwa  ukizingatia kuwa sasa hivi tunataka kuchangia shule mpya”anasema Bugumba

Msemaji wa wizara ya Afya Bw.Mwamaja amweka wazi kuwa wizara yake haina taarifa kutoka maeneo hayo,kwani wao hushughulika na mambo ya kitaifa na kuachia viongozi wa maeneo majukumu mengine. 
www.mobinday.blogspot.com.0753399579 mobinsons@yahoo.com