Nyamango/Soswa visiwa vyenye frusa tele za uwekezaji
·
zinahitajika
zahanati,shule na kumbi za starehe.
Na Tanpress,Nyamango
NYAMANGO na Chembaya ni visiwa viliopo
maili 46 Mgharibi mwa jijini Mwanza ingawa vinahesabiwa kuwa vipo wilayani
Sengerema Mkoa wa Mwanza.
Vinakisiwa kuwa na wakazi zaidi ya
10,000 ambao wanategemea shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki wanaopatikana
katika ziwa viktoria.
Usafiri unaotumika kwenda kwenye
visiwa hivyo ni boti au meli za watu binafsi,ambazo hutumia masaa 12 kutoka jijini mwanza eneo hilo na
mara nyingi boti ya mwendo kasi huingia saa mbili usiku.
Aidha kutoka katika visiwa hivi hadi
kwenye mwalo wa Kanyara ambayo ni nchi kavu ya wilaya ya Sengerema boti hutumia
masaa manne hadi masaa matatu kufika nchi kavu.
Pia kutoka eneo la kitongoji cha
Kanyara usafiri ni wa shida Km.80 hadi kufika Sengerema mjini zilipo huduma
zote za kijamii.
Eneo hilo lina vitongoji viwili
vinavyoundwa na visiwa vine ambavyo ni Soswa/Chembaya na Nyamango/Chamagati ni
katika eneo hilo lenye makazi ya kudumu ya watu ndipo frusa za uwekezaji
zipojitokeza.
Hivi karibuni Mwandishi wa Shirika
lahabari Tanpress alifika kwenye visiwa hivyo kwa lengo la kukusanya habari na
matukio ndipo alipojionea frusanyingi za uwekezaji.
Kwanza licha ya kwamba wavuvi wengi ni
watu wanaopenda starehe hasa za ulevi lakini ‘viwanja vyakujirusha’kuburudika
ni kama havitoshi.
Maeneo mbalimbali ambayo mwandishi
waTanpress alitembelea alikuta wenyeji wakipata vinywaji kwenye baa
zinazofanana na vilabu vya Pombe za kienyeji jambo linaloonyesha kuwa maeneo
hayo yanahitajika uwekezaji wa baa na mahoteli ya kisasa.
Aidha nishati ya umeme kwenye eneo
hilo inahitajika kwa haraka kwani wengi wanatumia jeneretor ambazo hawamudu
kununua mafuta hivyo hata wale wachache waliojitolea kujenga nyumba za kulala
wageni wanawasha vibatari wasijue lakufanya.
Hivyo anahitajika ,mwekezaji mkubwa
aweke mashine inayotumia mafuta ya diseli kwa ajili ya kuzalisha umeme wa
kutosha katika eneo hilo,ambalo kwasasa lipo gizani ingawa wenyeji wanahitaji
huduma hiyo.
Baadhi ya maeneo ,mengine au hata
visiwa vingine mashine za kufua umeme
kwa kutumia mafuta ya diseli ndio zinatumika kusambaza umeme jambo ambalo
halijafanyika kwenye visiwa vya Nyamango.
Frusa nyingine uwekeza ambayo
inalipa ni kituo cha afya au
zahanati,licha ya kwamba wavuvi wanafamilia zinazohitaji huduma ya afya
wanapougua au akinamama wanapotaka kujifungua huduma hiyo haipo kabisa kwenye
visiwa hivyo.
Kwa hiyo akitokea mwekezaji akafungua
zahanati yenye uwezo wa kuzalisha akinamama wajawazito anaweza akanufaika kwa
haraka kwasababu inavyoonekana serikali imeamua kutelekeza wakazi hao na haina
mpango wowote wa kuwajengea zahanati.
Kwasasa zahanati sio jambo la
mjadalainahitajika kwaharaka kuweza kuokoa maisha ya akinamama wajawazito na
watu wa kawaida wanao umizana kwenye starehe zikiwemo ulevi.
Ni vyema kamamwekezaji anavutiwa na
uwekezaji huo akajenga kabisa kituo kikubwa cha afya kwasababu hakuna kituo
karibu hata kwenye visiwa vya jirani kama zilagula na Yozwa bado huduma hiyo
wanakwenda kuitafuta mbali.
Elimu ni frusa nyingine ya uwekezaji
inayohitaji watu wenye mitaji kwani pamoja na kwamba wavuvi hao wanafamilia zao
eneo hilo lakini kuna shule moja ya umma ambayo hata hivyo haitoshi mahitaji.
Shule hiyo ya msingi inajulikana kama
Soswa shule ya Msingi bado haijaweza kutoa elimu bora kutokana na kukosekana
kwa walimu wa kutosha eneo lavisiwa hivyo.
Kwa hiyo zinahitajika shule za awali
kwa kila kisiwa ambapo kuna visiwa vinne
pia zinatakiwa shule binafsi za
sekondari na msingi au hata vyuo vya michezo ya majini kwa ajili ya wagoeleaji.
Frusa zingine niliziona ni kuweka boti
za mwendo kasi kwa ajili ya kuwakimbiza wagonjwa hospitalini na kuanzisha
kampuni za ulinzi kwani hivi sasa baada ya uvamizi kuwepo sasa wakazi wa pale
wameanza kukodi walinzi kutoka Mwanza ambapo ni mbali zaidi.
Zipo frusa nyingi za uwekezaji hata
kwenye soko lachakula cha kuku na wanyama wengine lakini kama wewe ni mwekezaji
unaweza kufikahukoukajionea mwenyewe.
www.mobinday.blogsopot.com
0753399 579 mobinsons@yahoo.com

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home