Nyamango;visiwa vilivyotelekezwa na serikali
Ripoti
maalumu.
·
Hawana
zahanati wala maji safi
·
Tangu
uhuru serikali haijawahi kufanya lolote
·
Kikongwe
ajitosa kuokoa roho za wajawazito
Na
Mobini Sarya, Nyamango,Mwanza
WAKATI
Serikali ya Tanzania na wananchi wake wakisherehekea miaka 51 ya uhuru wa
Tanzania Bara,wakazi wa visiwa vya Sengerema ,mkoa wa Mwanza wapo katika
huzunika kubwa baada ya serikali kutelekeza visiwa hivyo tangu uhuru.
Visiwa
hivyo ni Soswa/Chembaya,Nyamango Chamagati,Kasalazi naGembale,Yozwa na Busenge
ambavyo vinahesabiwa kuwa vipo kijiji cha Lushamba Kata ya Bulyaheke jimbo la
Buchosa ingawa vipo mbali.
Wakazi
hao wameliambia shirika la habari (Tanpress) kwamba hawana cha kujivunia tangu
nchi hii imepata uhuru zaidi ya kushurutishwa na serikali ya Tanzania kulipa
kodi na michango mingine bila kupewa
maendeleo yoyote.
“Kama
unavyoona Mwandishi katika eneo hili ambalo lina visiwa vinne vyenye kuundwa na
vitongoji viwili hatujawahi kuletewa amaendeleo yoyote yale wanayopata
watanzania wengine”anasema George
Rwezaula …ambaye
ni mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamango na Chamagati
Hivi
ni visiwa viwili tafauti lakini kwa makusudi serikali imeviacha kuwa kitongoji
kimoja chanye wakazi zaidi ya 3500 na
kaya 75 wakati kitongoji kinatakiwa kisizidi kaya 50,lakini pia kuna visiwa
zaidi ya 7 eneo hilo ambavyo vilipaswa kuundiwa kijiji ili kusogeza
hudumakaribu.
Mwenyekiti
huyo kwa niaba ya wananchi wake amemwambia Mwandishi wa Tanpress
aliyetebelea maeneo hayo kuwa visiwa
hivyo vina ukosefu wa huduma mhimu za kijamii ikiwemo vituo vya afya,shule,
maji safi na kituo cha Polisi.
Akizungumza
na TanPress katika kisiwa cha Nyamango ,
Rwezaula
alishukru kutembelewa na Mwandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu
historia ya uhuru jambo lililosababisha
kuchelewa kwa maendeleo eneo hilo.
“Mwandishi
kwanza tunakushukru kuweza kufika katika kisiwa chetu,hakuna mwandishi ambaye
amewahi kuja hapa,licha ya kwamba kuna
matukio makubwa na kutisha ambayo hufaanyika hapa kamaujambazi wa
kutisha lakini taarifa hazifiki kwenye
vyombo vya habari”anasema Mwenyekiti huyo.
Katika
kuonyesha tatizo la ukosefu wa kituo cha Polisi , Rwezaula amekumbushia kwamba
kati ya Mwezi Septemba hadi November Mwaka huu wavuvi visiwa hivyo waliporwa zaidi ya mashine 100
za mitumbwi na maharamia usiku,lakini walipojulisha jeshi la polisi ilichukua
siku tano kufika kwenye tukio.
“Sisi
hapa visiwani hatuna huduma ya Polisi ndio maana majambazi huingia kila wakati
kwasababu kituo kinacho tuhudimia kipo Nchi kavu kilomita 60,ukiwapigia simu
Polisi wanasema hawana mafuta hadi wachangishane”anasema Mwenyekiti huyo.
Akizungmza na Tanpress Kamanda Polisi
Mkoa wa Mwanza anasema “wambie wananchi wapeleke malalamiko yao
Halmashauri…mbona wanalipa kodi kwanini
wasijegewe vituo kama njia ya kuletewa maendeleo ……ujue mazingira yao ni tofauti unakuta
kisiwa kina watu wachache labda wabuni njia nyingine ya kujilinda kamaulinzi
shirikishi kwasababu usafiri kwenda kwao ni taabu ….mazingira yao ni
magumu”anasema RPC Erenest Mangu.
Anaongeza kuwa Vituo vyote ni
mali ya jamii “wakijenga tu hata kesho….. ungewashauri wajenge kituo cha poli
sisi tuwapelekea askari,………kama magari yenyewe ni taabu kufanyia doria nchi
kavu,usafiri wa boti tutapataje tufike kwenye visiwa hivyo..tutawapelekea
askari kama wakijenga vituo……..,wabunge wa maeneo yao wangekuwa wanapiga kelele
za namna hiyo hata magari na usafiri wa boti ungekuwa umepatikana.anasema
Ernest Mangu ambaye amehamia Mwanza akitokea Pwani.
Licha
ya kwamba visiwa hivyo vipo Maili 45 kutoka jijini Mwanza na Kilmeta 120 kutoka
wilayani sengerema havina huduma yoyote ya afya wala usafiri wa uhakika kuweza
kuwafikisha wagonjwa na wajawazito kwenye kituo cha afya.
Kukosekana
kwa kituo cha afya wala zahanati karibu kumesababisha ongezeko la vifo vya
akinama wajawazito licha ya kwamba kila Mwaka serikali hutenga bajeti ya afya
iliyopaswa kugawanywa katika maeneo yote.
Mwandishi
wa habari hizi alilazimika kukodi usafiri nakutembea kutwa kwenye visiwa saba
kutafuta huduma ya kituo cha afya hakauweza kukipata badala yake aliambiwa
aende nchi kavu ilipo zahanati ya kijiji Kmeta 40 ambapo hata hivyo baada ya
kufika alikuta imefungwa kwa amelezo kuwa jumapili haiendeshi shughuli zozote
za afya.
Akizungumza kwenye kibanda chake cha kuuzia madwa
mganga muuguzi wa zahanati hiyo,Yasinta Midale alsiema kuwa Zahanati hiyo licha
ya kuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wa visiwani lakini haina huduma mhimu.
“Kwamfano
hapa tuna muda mrefu hatupimi maambukizi ya ukimwi kwa akinamama wajawazito
kwasababu hakuna vipimo hata vya malaria hivyo ingawa tunapokea wajawazito 78
hadi 85 kwa mwezi wanahitaji huduma ya kliniki”anasema Muuguzi huyo
Hata
hivyo alipoulizwa kamamjamzito angefika hapo siku ya jumamosi aujumapili
kutaka kujifungua angepataje msaada wakati zahanati imefungwa alidai kuwa kuna kituo cha afya kijiji cha jirani
ambacho kina,milikiwa na kanisa ndicho hutoa huduma siku kama
hizo .
Kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo ya afya
kumemsukuma kikongwe mmoja mwenye miaka 55 kuanza rasmi shughuli ya kuzalisha
akimama kwenye visiwa vinavyomzunguka.
Mama
Madewa akizungumza kwenye kibanda chake anachotumia kutoa
madawa ameliambia Tanpress kwamba alianza huduma hiyo Mwaka 2007 baada
ya kuona serikali imeshindwa kuwasaidia akinamama wanateseka na kupoteza
maisha.
“wakati
huo akinamama walipokuwa wanaona wamekaribia kujifungua walikuwa wanasafiri
kwenda nchi kavu kusubiria ,lakini kuna wale ambao waliendelea kutafuta pesa na
kukuta muda wakujifungua umefika hao ndio walikuwa wanapata taabu hadi
nilipoanza hii kazi”anasema Bi.Madewa
Licha
ya huyo mkunga kujitahidi kuhudumia akimama wa visiwa vya
Chamagati,Nyamango,Chembaya na zilagula vyenye wakazi zaidi ya 10000 bado
serikali haijawahi kumpatia mafunzo yoyote hata ya kujikinga na maambukizi ya
ukimwi.
Mwenyekiti
wa kitongoji cha Nyamango, George Rwezaula aliyempeleka Mwandishi kwenye banda
la mkunga huyo amedai kwamba mara kadhaa aliwahi kupeleka ombi la mkunga huyo
kwenye vikao vya kata ili apatiwe
mafunzo lakini serikali ya wilaya ilidai kuwa bajeti imefika kikomo.
Mwenyekiti
huyo anashangaa serikali kupitia Mamlaka
ya mapato TRA kufika hapo mara kwa mara kukusanya kodi,halmashauri nayo
kukusanya ushuru lukuki lakini
wameshindwa kupewa hudumayoyote ya kijamii ikiwemo maji safi.
Ametaja
baadhi ya ushuru unaokusanywa na serikali kuwa ni shilingi 90,000 za kusajili
mtumbwi kwa namba MSR,leseni kila Mwaka
35000 huku mitumbwi kwenye kisiwa kimoja ikiwa zaidi ya 300,wavuvi kutakiwa na
halmashauri kulipia shilingi 7000 kila
mwezi (parking fees).
Aidha
TRA hukusanya kwa wavuvi wa dagaa shilingi 2000 kila debe huku boti zinazonunua
au kupakia samaki kwenye eneo hilo kulazimika kulipia mapato ya shilingi laki.2 hadi tatu
kutegemeana na ukubwa wa boti kila inapojaza samaki.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Lushamba, Deus Magumba alipoulizwa kukosekana kwa huduma ya afya
visiwani alidai kuwa hilo hawezi kulizungumzia kwasababu nayeye amelikuta
ingawa kipaumbele chao kwasasa ni kujenga shule ya Msingi eneo la katika
Kitongoji cha Kanyara.
“Aha
hata mimi niliwahi kuuliza nikaambiwa na Halmashauri kwamba wanataka tufanye
ili wao wamalizie ,sasa ukimwambia mwananchi achangie ujenzi ili Serikali
ituunge mkono anaona kama anaibiwa
ukizingatia kuwa sasa hivi tunataka kuchangia shule mpya”anasema…
Hata
hivyo juhudi za kumtaafuta diwani wa Kata ya Bulyaheke,Bageti Ngere Nyuki
zimegonga Mwamba baada ya kukwepa kukutana
na Mwandishi wa habari mara kadhaa alipopigiwa simu huku akitoa
visingizio vingi wakati mwingine akidai yupo mbali au kwenye kelele hawezi
kuzungumza.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Buchosa,Charles Tzeba
, alipoulizwa kuhusiana na kukosekana kwa huduma mhimu za kijamii katika visiwa
hivyo alidai kuwa yeye ni mbunge wa
kitaifa anayesimamia bajeti kuu mengine hayo waulizwe viongozi wa Halamashauri.
“kwani
wee mwandishi nani amekutuma ukachunguze hayo? Kwanza ujue kuwa mimi
nimechaguliwa kama mbunge kipindi hiki hivyo hali nimeikuta kama ilivyo labda
uwasiliane na viongozi wa Halmashauri
wakueleze wana mpango gani na maeneo hayo kwasababu wanabajeti
zao”AlisemaTzeba
Mbunge
huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Uchukuzi alisema kuwa kazi yake nikusimamia
bajeti ya kitaifa namna inavyotekelezwa na serikali na maswala ya jimbo wanaopaswa kuyashughulikia ni Diwani pamoja
na mwenyekiti wa halmashauri kwa kushirikiana na mkurugenzi.
Hata
hivyo juhudi za kuwapata viongozi hao zinaendelea kwani mwandishi amefika mara
kadhaa kwenye ofisi za Halmashauri hiyo
na kushindwa kuwaona viongozi wa Halmashauri wala kupata mawasiliano yao.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home